
SEHEMU YA 24
👇
Nilishtuka kutoka usingizini kumbe nilikuwa naota
“No Inamaana Berat anamwanamke mwingine hapana hii haiwezi kuwa kweli ananipenda mimi tu “
Nilishuka kitandani na kwenda chumbani kwa Lee nikamuukuze maana yeye ndio mtu pekee humu ndani mwenye mazoea na Berat na lengo langu ni kudhibitisha kweli anamtu au laa
“Mambo Lee”
“Unataka nn”
“Aam Kuna dada amenipa huu mzigo amesema nimpe Berat akitoka kazn”
Nilivyosema hivyo akafunika kitabu alichokuwa anasoma akaniangali
“Mtu gani”
“Simjui ila nahisi anaweza kuwa mpenzi wake”
“Mpenzi wake?”
“Ndio”
Kwann “
“Nahisi hivyo tu “
“Aaa sawa unaweza kwenda “
“Kwani Hana mpenzi “
“Ndio Hana vp unataka kuwa mpenzi wake”. Aliposema hivyo nilifurahi moyoni 🤗
“Aaa nimeuliza tu”
“Ili iweje”
“Aaa nijue tu”
“Haya umeshajua sasa unaweza kutoka chumbani kwangu”
Niligeuka huku uso ukiwa na tabasamu na kuondoka nilipofika mlangoni tu akanistopsha
“Wait, ona hii ‘”
😳Nilitoa macho baada ya kuona picha ya Berat akiwa na msichana anamvisha pete akanionesha nyingine wakiwa kenye pozi la mahaba huku wanacheka
“Subiri nikuoneshe nyingine”
Akanionesha ya mdada mwengine walikuwa wameshikana mikono huku wakionesha kufurahi
Nyingine walikuwa kama vile wanatembea alafu yule dada ameweka kichwa begani
“Huyu wakwanza ndio wife na huyu wapili ni mchepuko so hili ndio jibu la swali lako,
Vp mbona unalia “
Sikujua hata kama machozi yanatoka
“Unampenda?” Wala sikujibu nilikuwa nimesimama kama Sanamu tu huku machozi yakitoka kama Bomba
“Hahahahahaha so unampenda Berat haa😮 kweli umejua kunifurahisha
Kwani wakati ulikuwa unampenda uliona ni wahadhi yako kuwa nayeye ata kupenda mh au kwa akili yako mbovu ambayo haijui hata mlango wa shule ukoje ulifiki kuwa yuko single at that age kwamba sio mzima au
Sikia kama ulikuwa unahuo upumbavu nibora uache sasaiv maana Berat hawezi kamwe kuwa na mwanamke kama wewe ambae huna mbele Wala nyuma unategemea akupeleke wapi ila subiri huenda ukawa umeshaliwa hahahahaha hii inafurahisha Sana kama ameshakula pole atakuwa alitaka kumwaga akakosa dustbin so akaona amwage kwako hivyo usichukulie kumaanisha sawaee”
Aliongea bila hata kujali nitajiskiaje alinitoa chumbani kwake na kufunga mlango
Nilitoka na kwenda chumbani kwangu. Ile nafika namkuta Johar anacheka balaa
“Sonia Sonia Sonia nimekuita mara tatu tena kwa kumaanisha hivi nimesikia au nilikuwa naota inamaana unampenda Berat
Oh! Lord hivi hujioni ulivyo unaona nisawa wewe kuwa nae kikaragosi kama wewe mhu kweli hiki nikituko Cha mwaka heee makubwa haya tena yanatisha lbda nikwambie wewe bidada kamwe haitakaa itokee wewe kuwa na yeye hivi hutumii hata akili kwanzia lini ardhi na mbingu vinakaa pamoja jibu ni hapana ndio
Sasa wewe jilize hapo alafua nimeambiwa kuwa anakuja na mgeni hivyo ukienda kupika uongeze kachuka huyo akaondoka
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU