CHAGUO LA MOYO (27) MWISHO

sehemu ya 27FINAL

“Kwanza kabisa kabla sijaanza kuongea naomba mnijibu swali moja, nikweli mnapendana?”

“Ndio” tulijibu wote

“Nikweli unaujauzito”

“Hapana mama”

“Ndio anao “

sasa mbona Kila mtu anaongea lake hapa nikweli au sio kweli” nilimwagalia Berat nikashindwa kujibu maana mimi najua kuwa Sina sasa anaposema ninayo ana maana gani
So nikamuacha ajibu yeye

“Ndio nimjazito”

“Hongereni na mna mpango gani”

“Wiki ujayo ni ndoa yetu”nilimwagalia kwa mshangao wiki ijayo au ana maanisha mwaka ujao

“Mbona haraka hivyo”

‘yeah ndio tumeamua iwe hivyo hata hivyo hatuna chakusubiri” 😏Sema umeamua sio tumeamua umeamua na nani

“Okay Sonia kwakuwa huna wazazi vp mahari yako atapokea mama yako mdogo au utapokea mwenyewe “………heee amejuaje kama Sina wazazi wakati sikuwahi kumwambia mtu yoyote maisha yangu

“Usiwaze tunafahamu kila kitu kuhusu wewe” nyie kumbe mnajua alafu hamsemi😏

“Nitapokea mwenyewe ila nitaitoa sadaka yote sitochukua hata Senti “

“Sawa vizuri “

Basi mama aliinuka na kuondoka

“Alafu unamaanisha nini Kila mda kusema nina mimba wakati Sina “

“Usinimbie hadi mda huu hujajua kuwa unamtoto wangu tumboni mwako”

“Huyo mtoto ameingia lini ‘”

“Amka twende hospital “

“Niende hospital kwani naumwa “

“Twende ukathibitishe maana naweza kukuacha mwenyewe ukanywa vitu vya ajabu unaniulia mtoto wangu”

Tulitoka na kwenda hospital tulifika akasema nichukuliwe vipimo vyote yaani hadi nywele natania bhn😅

Nikachukuliwa na Baada ya mda majibu yakatoka Kweli nilikuwa na ujauzito wa mwezi mmoja inaonekana iliingia ile siku ya kwanza

“Ulifanya kusudie “nilimuuliza wakati tukiwa kwenye gari kurudi nyumbani hakujibu ila alitabasamu tu nakuendelea kuendesha

Tulifika nyumbani nikamkuta Nicole amekaa seblen alivyotuona aliamka na kuondoka alionesha hakutaka kuongea na sisi

“Naomba nikaongee nae”
“Okay utanikuta chumbani”

Nilienda chumbani kwake nikagonga

“Sitaki kuongea na wewe unaweza kwenda”

Aliongea wala sikumsikiliza nikaingia

Anachukua mto na kujifunika usoni

“Nicole please naomba unisikilize basi” hakujibu

“Nicole, nisamehe najua nimekukosea”

“Umenikosea nin wakati ni maisha yako so fanya unachojisikia”

“Okay naomba tuongee basi'”

“Sina chakuongea na ww “

“Nina mimba “

“Hongera “

“Nisamehe kwakua nilikuficha ila nilitaka nikwambie ukirudi “

“Alafu niliporudi uliniambia”

“Hapana nilishindwa kwasababu aliniblock na nikaona nikikwambia utanisema kwakuwa ukikuwa umeshanionya mda “

“Sikia Sonia sio kwamba nilitaka utoke na mtu ninaemtaka mimi hapana ila nilitaka kuona unakuwa na mtu ambae angekupa furaha hivyo kama uliona Berat ndio anakupa furaha haikuwa na sababu ya kunificha kingine ulichonikwaza kwann uliendeleza ukaribu na Rahul wakat unajua uko na Berat na unafahamu ni jinsi gani Rahu anavyokupenda ona ulichosababisha kaishia kuumia wakati ungemuweka wazi mapema asinge umia”

“Nisamehe Nicole ila sikuchua kua Rahul ananipenda mimi Nilijua ni rafiki tu”

“Rafiki,ni mtu gani anaweza kuwa na urafiki wa aina ile okay najua hakuwahi kukutamkia lakin matendo yake yalionesha wazi kuwa anakupenda na Kila mtu aliliona hilo alafu wewe unataka kusema ulikuwa urafiki anyway yameisha kwakuwa umeshapata chaguo la moyo wako hakikisha ule ukaribu hauendelei na mtafute Rahul uongee nae hili jambo aelewe “

“Sawa asante “

“So nikweli unaujauzito “

“Yeah “

“Hivi umewezaje kumpenda mtu kama Berat yaani ukimuangalia tu anatisha Hana story na mtu yeye mda wote sura ameikunja tu na maneno yake ni ndio hapana kamaliza alafu mwenzetu umeshapewa vitu hadi mimba juu”

Nilicheka sana

“Ulishasikia watu wanasema kipenda roho hula nyama mbichi basi ndio hii najua kuwa yuko tofauti na nimependa huo huo utofauti wake “

“Una moyo shoga yangu ‘” basi urafiki ukarudi tena tukapiga story kama zote mr alipoona nimekaa mda mrefu akapiga na kuambia niende

“Sasa ngoja niende tutaongea baadae”

“Poa”

Nilifika chumbani na kukuta amekaa huku kashika sahani ya matunda

“Kaa hapo nimda wa kula matunda “

“Saizi ? Mbona mapema sana”

“Una mtoto tumboni hivyo hutakiwi kukaa mda mrefu bila kula sawa”

“Ndio nile Kila baada ya masaa mawili jamani”

“Hata baada ya dakika kumi sawa tu kikubwa sitaki ukae na njaa utamuumiza mtoto n wewe pia utaumia”

Kazi ninayo
Basi kama kawaida yake akanilisha pale nilipomaliza akaniambia nikae hapo hamn kutoka natakiwa kupumzika

Mimi ninani nimbishie nikakaa akawa ananifanyia masaji ya miguu 🥰

Huyu ndio mr romantic wangu bhn

Jion ilifika nikatoka ili niongee na Rahul nilienda chumbani kwake nikagonga hakuwepo nikauliza Wang akaniambia yuko nje kwenye bustani bas nikamfuata huko

“Rahul ” aliposikia namuita alinigeukia na kuniagalia Kisha akainuka na kunishika mkono alanisogeza alipokaa kanikalisha na yeye akakaa

“Unajisikiaje ” aliniuliza baada ya kukaa

“Niko poa vp wew”

“Siko sawa”

“Rahul naomba unisamehe kwani mimi ndio nimesababisha wewe kuwa hivyo”

“Hapana Sonia haujanikosea ila naomba nikuulize na unijibu ukweli kutoka ndani ya moyo wako”

“Sawa niulize “

“Umeshawahi kunipenda “

“No siwahi” nilipomjibu hivyo alitabasamu kwa uchungu 😓

“So nikweli unampenda Berat?”

“Ndio nampenda”

“Unafuraha ukiwa na yeye na unafikili anaweza kukupa furaha maisha yako yote”

“Yeah nifuraha na Nina amini kuwa atanipa furaha siku zote”

“Are sure “

“Yeah asimia mia”

“Good”

“I’m sorry “

“Hapana hujakosea maisha ndio yalivyo ila nashindwa kuzuia moyo wangu kuumia kwakua nilikupenda na ninakupenda hadi sasa hivyo kitendo ch kukukosa ni maumivu kwangu japo ninafuraha kuwa umepata yule unaempenda na yeye anakupenda hiyo inatosha kwangu naumia ila nitakuwa sawa na ikitokea mnakuwa tofauti usisite kuja kwangu kwani imeshindikana kuwa na wewe ila ahadi yangu iko pale pale nitahakikisha kuwa unafuraha so ikiwa na chochote njoo nipo kwaajili yako “

Aliongea huku machozi yakimlenga

“Sawa asante kwa Kila kitu “

“Asante pia kwakuwa sehemu ya maisha yangu “

“Okay “

“Sonia “..
“Abee”

“Naweza kukukumbata kwa mara ya mwisho please “

Sikumjibu Bali niliinuka na kumkumbatia alishindwa kujizua akaanza kulia mimi mwenyewe nililia 😭…….

“I will miss you” aliongea huku akinifuta machozi

“I will miss you too Rahul”

“Okay thanks and byee”

Aliniachia na kuondoka huku akifuta machozi. Nilijisikia vibaya sana nikainamisha kichwa kwenye meza na kubaki nikilia nilishtuka kusikia mtu akinipiga piga mgongoni

Niligeuka nikakuta ni mama alitoa kitambaa akanipa nijifute machozi Kisha akasema

” Hutakiwi kulia ukiwa kwenye hali hiyo “

“Ooo! Sawa ” nilijibu huku nilijifuta machozi vizuri


“Mapenzi nikitu kimoja Cha ajabu sana ni kizuri pale unapopata yule unae mpenda na yeye akawa anakupenda lakin ukipenda alafu unaempenda asikupende huwa inatupa maumivu Sana ila nibora kujua. Mapema kuwa hakupendi kuliko kuwa nae alafu ukaja kujua yuko nawewe kwa mpito tu na hakupendi huwa inakuwa maumivu zaidi

Najua wakati unaingiza hapa kwangu na kuona watoto wangu jinsi Kila mmoja ana baba yake tena wanatokea mataifa tofauti tofauti utakuwa ulisema kitu moyoni mwako

Ngoja leo nikwambie kidogo kuhusu maisha yangu

Nilizaliwa katika familia yenye uwezo mkubwa sana kifedha wazazi wangu walinipenda mno na familia yetu ilikuwa maarufu sana
Siku zote niliishi maisha maisha mazuri kama mtoto wamfalme nikisomeshwa kwenye shule za ghalama sana tena nchi za nje …….. lakin nilikosa kitu kimoja sikuwahi kuwa na bahati ya kupendwa yaani kila mwanaume niliekutana nae hakuwa na mapenzi ya dhati na mimi bali walifata mali na wengine walitaka kupita tu. ……… nakumbuka nilikuwa najiambia Kila siku kuwa hata nikikutana na matapeli wangap ila naamini iko siku nitapata anaenipenda kweli hivyo hata nikiachwa nilikuwa nalia baadae naamka na kusahau nampata mwingine

Nakumbuka Kuna mwanaume ambae alikuja kwenye maisha yangu nilimpenda kuliko wanaume wote niliwahi kuwa nao huyo mwanaume alinifanya nikaona kuwa mapenzi yake yapo ………….alinionesha upendo usio wa kawaida nakumbuka tulipanga kuoana akatoa mahari siku ya ndoa ikafika nikiwa salon alikuja kijana mmoja akaomba kuongea na mim sikuwa na shaka nikakongea nae 😄 Acha nicheke kama mazuri vile iko hivi yule kaka likuja kunionesha kitu ambacho sikukijua ilikuwa ni video mambayo ikimuonesha mume wangu mtarajiwa akiongea na wazee wa tatu ambao walikua wakijadili ni namna gani wataweza kumuangusha baba yangu kiuchumi waliongea mengi Kila mtu akitoa wazo lake yule mume wangu akiwaambia kuwa yeye ataifanya hiyo kazi na atafanikiwa aliulizwa utafanya nn’ ahadi ufanikishe alijibu “nitaingia kwenye mahusiano na binti yake wakwanza na nitamuoa alafu nikishamuoa tutatekeleza Kila tunachotaka kwani nitakuwa karibu na nae hivyo nitajua baadhi ya mambo ambayo yatatusaidia” wazo hulo likapata kibari kwa wote alitoa na kunionesha nyingine apambapo walikuwa mume wangu na huyo kijana aliyekuwa akinionesha video hiza. Kwenye ile video alikuwa akiongea tofauti na ile ya mwanzo alikuwa akisema yeye lengo lake ni kutafuta ukaribu na baba ili aweze kupata nafasi za juu serikalini hivyo yuko taofauti na wale Baada ya kuona vile siku amini Bali nilimfukuza yule kaka na nikalipuzia kabisa ndoa ilifungwa tukaanza kuishi rasmi kama wanandoa matendo yake yalianza kunionesha kuwa zile video ni zakweli japo niliendalea kuwa mbishi siku moja nilimfuma kwa macho yangu na masikio yangu akiongea na wale wazee na kupanga mbinu tena walikuwa tayari hata kuiangamiza familia yangu yote. Niliumia kupita maelezo nilitachukia mapenzi na sikutaka kusikia kitu kinachiitwa mapenzi kwenye masikio yangu. Ndipo niliamua kuwa nitazaa watoto wangu na mwanaume yoyote nitake mtaka na ndicho nilichokifanya ………likan kuna kitu nilikuja kuambiwa na mtu mtumishi wamungu kuhusu maisha yangu nilibaki nimechoka unajua nikitu gani hicho” nilitikisa kichwa kuwa sijui

“Siku hiyo nilikuwa kwenye Ibada tu yakawaida tena zile Ibada za kati kati ya wiki na sikuwa na mazoea ya kwenda kanisani maana maisha niliyokuwa nimechagua kuishi nilikiona sifai hata kuingia kanisani lakin siku hiyo nilipata makumo hadi nikaenda

Nilikaa kitu Cha nyuma kabisa kiongozi wa Ibada aliingia ile anapita mbele yangu kama hatua mbili tu aligeuka na kuniangalia kwa sekunde kadhaa Kisha akaenda madhabahuni na kuanza Ibada baada ya Ibada alinifata na kuniambia nimfuate ofisini kwake. Sikuwa na hiana nikamfuata

Nilipofika Aliniambia nikae nikaa Kisha akasema

“Pole sana mama kwa maisha uliyo ishi Jana nikiwa kwenye maombi Mungu alinionesha kitu kuhusu wewe na akaniambia kuwa utakuj leo kanisani na utakaa nyuma”.

Nilishtuka aliposema hivyo Kisha akaendelea kusema

“Kwann hujawahi kupata mtu wakukupenda hadi umefika umri huu”

Lile swali lilikuwa gumu kujibu kwanza nijiuliza kajuaje yaani nimeshasahau kama amesema ameoneshwa na Mungu

“Okay haina jibu ngoja nikupe jibu, jibu ni kwamba unaishi katika kifungo Cha maneno aliyo tamkiwa na baba yako kipindi akiwa kijana wamiaka 20”. Nilishtuka sana aliposema hivyo

“Samahani kifungo Cha maneno ? Una maanisha ninj unaposema hivyo”

“Ni hivi baba yako kipindi yuko kijana aliwahi kuwa na mahusiano na binti wakazi pale nyumbani kwao na yeye ndio aliemtoa usichana yule Binti ……..yule alikuja kupata ujauzito akamwambia baba yako na baba yako aka kataa na kumtaka atoe ila binti alikataa baba alimwambia kuwa kama hatatoa basi atajua mwenyewe yeye hahusiki kabisa. Yule binti alihisi anataniwa hivyo akapuuzia siku zilienda mama yake na baba yako alipogundua kuwa binti ni mjamzito akataka kumfukuza lakin binti akasema mimba ni ya mtoto wako jambo ambalo yule mama alipingana nalo na Kumtetea mwanae kuwa hawezi kulala na kijakazi kama yeye baba yake baba yako alimuita baba yako na kumuuliza kama nikweli binti anaongea ukweli au laa baba yako alikataa na kusema hajawahi kuwa nae

Yule binti akafukuzwa ila kabla hajaondoka aliongea neno ambalo ndio lime funga maisha yako. Na usipo omba watoto wako nao watapita hiyo njia,…….alisema “Sam leo umekataa kuwa hukuwahi kuwa na mimi hata siku moja sawa lakin nataka ujue kama wewe ndio uliekuwa mwanaume wangu wa kwanza na ukanipa huu ujauzito nakwambia hautokaa kamwe kwenye maisha yako kupata mtu atakae kupenda na wewe utapata wa kucheza na maisha yako kama ulivyo cheza na yakwangu mbingu na zisikie aridhi na ipokee” hili ndio neno aliloongea yule binti Kisha akaondoka baba yako hakuwai kumtafuta wala kujisumbua kuwaza kuhusu yeye yule msichana alikuja kufariki yeye na mtoto wakati akijifungua kwaiyo hiii dhambi ndio ilimekuwa ikikutafuna maisha yako yote “

Ilikuwa ngumu kuamini na kukubari lakin alinipa maneno kadhaa katika biblia na nikatoka moja kwa moja nilienda kwa baba nikamuuliza habari ile kwanza alishtuka Kisha akakiri kuwa ndio alifanya vile kwaiyo toka hapo nimekuwa nikiomba Sana Mungu awaepushe wanangu na hiyo dhambi na nilikaa na wanangu wa kiume nikawaambia ikitokea mtu yoyote akampa mimba Dada wakazi huyo atakuwa mke wake atake asi take “””””


Alimaliza kunieleza nikasema nyie maisha yana vitu vingi sana

Basi siku zilienda hatimae nikafunga ndoa na Berat wangu ……..mda wa kujifungua ulifika nikajifunga mtoto wa kike hii ni copy ya mama mkwe 😅 yaani hakufanana na sisi hata ukucha Kila kitu bibi yake hadi kuongea ……….mama alifurahi sana

Baada ya mtoto kufunga mwaka nikabeba mimba nyingine tukapata mtoto wakiume ………. baada ya miaka mitatu tukapata tena mtoto mwingine na hivi ninavyokupa story hii Nina mimba ya mtoto wa nne

Rahul akuja kupata mpenzi wake akaoa saizi Wana watoto wawili. Johar aliondokaga mda sana hata sijui yuko wapi

Nicole aliolewa na yeye saizi anamtoto mmoja na yeye pia ana mimba ya mtoto wapili

Kuhusu mama yangu mdogo
Aliachana na mumewe mwaka mmoja baada ya mimi kutoroka alifukuzwa kazi enzi zile za anko magu kwey tumbua tumbua na alikuwa na mikopo bank akashindwa kulipa kwasababu hakuwa na kazi hivyo nyumba ikauzwa
Sasaivi anuza dagaa mwanza huko mwanza vijijini

joy alipata mzungu akaenda ulaya hajawahi kurudi hadi leo hamna mawasiliano yake Wala ya yule mzungu wake sasa hatujui kama yuko hai au wameshamnywa supu

Na huu ndio mwisho wa story yangu nashukuru sana kwa wote milio soma kisa hiki najua Kuna mahari umeokota kitu byee love all

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!