CHAGUO LA MOYO (05)

SEHEMU YA 05

“Mmezaliwa wangapi”aliendelea kuuliza
“Niko mwenyewe”
“Duh pole, sisi tulizaliwa 7 Ila Sasa tuko 6 na wakike ni mimi tu last born wamama,. Kaka yangu wakwanza baba yake ni mkorea,wapili baba yake ni mturuki,watatu baba yake mchina,wanne baba yake ni muhindi,watano baba yake ni mwarabu,wasita ni mm baba yangu ni mzungu wa marekani yakusini na wamwisho Bab yake alikuwa mtanzania (mpare)….😳😳huyo mama alitaka kuzaa na kila nchi au ….”najua unawaza nn Mimi mwenyewe kila siku nilikuwa namuuliza hivyo hivyo”……..huyu dada anaongea hata hachoki Mambo mengine hata sioya kuyaongea ukitegemea tumeonana dakika chache tu huyu siwezi kukwambia Siri yangu anaonesha fliji lake bovu haligandishi😒

Yaani njia nzima alikuwa anaongea tu 😏 baada ya mda mrefu tulifika nje ya geti ….. Alipiga honi na geti lilifu nguliwa 😲nilitoa macho baada ya kuona jumba sio nyumba hili ni jumba palikuwa pazuri kama anaishi mfalme vile,…… Sonia..nilistuka baada ya kuitwa bhn …abee …….twende ….haraka nilimfuata huku nikishanga sangaa …….wow ndani nikuzuri balaa hembu subiri humu wanaishi watu au majini maana kulikuwa kumepambwa vitu vya thamani Sana ……. Karibu hapa ndio nyumban kuwa huru kabisa..alisema baada yakufika sebleni …Mara alikuja mmama na kusema mmefika ?…. hapana bado hatujafika …..😁alimjibu Nicole sijui ni Nani yake maana anamjibu Kama vile wanamatani….karibu binti … Asante shikamoo……

Marahabaa hujambo………. sijambo…… karibu sana, we johari njoo umpeleke mgeni chumbani kwake……😳 Johari Tena huyu siamesema yuko pekee yake Sasa inakuwaje”…
Alikuja huyo johari mwenyewe alikuwa mrefu mweusi alafu bongee

Shikamoo…. nifate
Hee mbona hajaitikia Sasa au ni mdogo Ila hapana mbona sura imekomaa hivyo…

Waooo chumba kilikuwa kizuri balaa “samahani dada johari hiki ndio chumba changu”

“Hapana Cha Bibi yako,alafu Mimi sio dada yako ukiniita Johari inatosha”

Alinionesha bafu na vitu ngine Kisha akaniambia namna ya kutumia
“Sasa ukatumie vitu tofauti na nilivyokwambia utarudi kijijini kwenu ukalime huko,alafu kingine hiyo minija huruhisiwi kuivaa humu ndani hatutaki uchulo sawae”

“Sawa” nilijibu Kisha akaondoka nilibaki niakuangalia chumba kilivyo kizuri ……… nikaenda kuoga nakushuka chini nilikuta johari anaangalia tv ……..

“Chakula Kiko hapo mezani “
” Haya Asante”
…………
Nisogea mezani nakufungua hotpot 😋mate yalinijaa baada ya kuona nyama ya kuku kitambo Sana sijala zaidi ya kula harufu yake

Nilipakua na kuanza kula wow chakula kitamu balaa…….. Sasa wakati niliendelea kula alipita mkaka mmoja hivi bonge la handsome hatari nilibakia nakijiko mdomoni nikimshangaa Hadi akaishia

Nilimaliza kula nikamshukuru akanielekeza jiko lilipo nikaenda na kuisha vyombo ……….Nyie hapa nipazuri kwanzia ndani hadi nje ………kutokana ni uchovu niliamua kwenda kulala ……. Wakati usingizi ikiwa unanipitia mlango wa mchumbani ulifunguliwa nilishtuka na kukaa ……… oooh kumbe ni Johari ……
“Unashtuka nn au unadhani Kuna wabakaji “

“Hapana “

“Sasa nimekuja kukwambia kitu kimoja kabla kesho haijafika ,humu ndani Kuna wanaume 5 saa unaruhusiwa kucheza na hao wa 4 Ila mmoja kaa nae mbali narudia tena kaa nae mbali “

“Samahani mbona sikuelewi”
“Usichoelewa nn hapo nakwambia kaa mbali na Rahul Ila hao wengine unaweza pita nao “

Alimaliza kuongea na kuondoka Mimi nilibaki nashangaaa tu

Sijui usingizi ulinipitia sangap Ila nilikuja kushituka kumekucha

Itaendelea…….

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!