
SEHEMU YA 03
“Eh.ehee nipokee ili iweje hela umetoa wapii,Huna kazi huna badhi kazi yako kulala tu nakula hayaa nambie hiyo hela umetoa wapi Dinaa kama umeanza michezo michafu Dina nakukata hilo kojoleo lako mbwa wewe hivi unanielewa??’
“Jamani mamaaaa!!!”
“Jamani Ng’ong’oooo ,Nyooo!!!”
😔😔Niliamua kuingia zangu tu ndani kwa hasira yaan mama yangu hana hata shukrani kila siku ananitukana mie kazi yangu kula na kulala nimeferi Form four, ananiita mie mmbea naweza hiyo kazi tu
Mtaa mzima wanajua mie nilipata zero mama yangu hajui kuongea taratibu hapo penyewe mtaa mzima wamejua kama mie nimeleo nimenunua mihogo kwa hela ya kuhongwa mama akaikataa ile mihogo ..
Nikajitupa zangu kitandani nikachukua simu nikawasha data , vimeseji vijaingia kwa kuongozana nilipo fungua ni yule Kaka wa jana alie nitumia video anatumia jina la Mussa shango
(Hujaamka tu mrembo)
(Uko poa)
(Siku njema)
Mmmh🙄nikasema huyu kaka nae vipi mbona kama ananishaukia, nikaingia kutazama Profile yake , hakukua na picha hata mojaa
Mmh nikasema hapa si ndio watu wanakutanaga na majini jamani naskiaga story za majini hivi hivi
Nikaachana nae nikaendelea kusaka habari za Mr Mianne , mama akaingia ndani
“We Dina ,Umetoa wapi hela ??”
Yaan mama yanguuu😟😟😟khaaa!!
“Mi nikajua yameshakwishaa?? Daaah ?”
“Yanaishajee??”
Yaan huyu mama yangu Amekuwa ananikagua mie tangu mdogo mpaka najielewa , kila siku kunipachua chupi ananikagua kama nimeanza wanaume mama yangu ni mkaliii , sijawahi kumzoea japo mimi ndio kipenzi chake lakini nikileta ujinga weeh nafumulia mie kama hanijuii , Yaan hapa huwezi amini tunagombania mihogo ya elfu mbili na sukari robo jamanii🙌🙌🙌
Mama yangu ana maisha magumu sana lakini sio wa kutegemea mtoto wake wa kike zaidi wa kiume , kaka yangu ndio huwa anatutetea nyumbani kwa vitu vyote kula hata mimi shule ,japokuwa na yeye bado anajitafuta huko …
Mama katuzaa wawili tu mimi na kaka yangu yeye yupo mkoa mwingine anajitafuta
Elfu tatu tu na chench inarudi lakini imekuwa kesi ya jinai , hapa mama kawa mbogo mie nilijua atafurahi mana hatukuwa na ratiba ya tunakula nini asubuhi nina uhakika mama amelala na hela yake ya mtaji tu wa mkaa na sio ya kulaa lakini ona anavyonichamba …
“Bwana mama me sijapewa na mwanaume wala sina huyo mwanaume??”
“Enhee umetoa wapi, Au tuvuane chupi unataka??”
“Mamaaaa!!!”
“Nyokooo!!”
.”vua hiyo chupii”
“Mamaaaaa!!! Kwahiyo mimi kukusaidia kununua chakula imekuwa shida??”
“Sio kununua chakula shida hela umetoa wapi Dina, hela hizo miambili zisikudanganye mwanangu hivi unanielewa vizuri , kufeli shule sio kufeli maisha sio ujirahisi kwa hawa wavuta bangi wa hapa mtaani Dina hivi unanielewa??”
“Maaamaaaaa aah Nakuelewa wala mie siwezi siwezi mama siweziii aaah”
“Hayaa kalete mihogo “
“Saaa mama unanipa hela ya mihogo wakati nimenunua mihogo hii hapa mama sijahongwa hii hela jamani wala sina bwana”
Mama yangu aligoma kabisa kula hiyo mihogo asojua imetoka wapii namie kumwambia nilipo toa nilikuwa nashindwa
Ilibdi nimwambia mama nilikuwa na 3000 nilimuibia ibia kwenye mkaa wake yaan niliikusanya kidogo kidogo
Mama angu huwa ananiamini sana tu mana ananipenda mno na anajua mie siwezi kwelii kugeuka mashart yake na kila siku najitunza mie
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU