
SEHEMU YA 05
Akanambia nikuache basi ulale nikasema sawa mana nasinzia hapa hatari ndio akakata simu mie usingizi ukanipitia
Nimekuja kushtuka asubuhi nakuta text et ulale salamaa mmmh huyuu nikatabasam tu bwana , nataka kuifuta kuna text ikaingia M pesa nimepokea 15000 kutoka kwa mussa mmh😞😞 jamani wakati bado nashangaa ikaingia text nunua Vocha bint et uwe na asubuhi njema
Hee hadi kujibu nikashindwa nijibu niniii??
Unajua Elfu kumi na tano kwangu ni kama milioni eeh nishazoea jero jero naa jero yaan mia tano ya Tanzania mie kuishika kwangu ni mtihani sana sasa hela kama hizi nawehuka
Nilimtumia sms Asante sanaaa lakini naomba usinitumie tena pesa mama yangu akijua anaweza hata nichunja hapendi mno , na simu yangu anaishika mara kwa maraa
Akanijibu muda huo huo akanambia mmh jamani I wish nimuone mama nimpe Hongera amekulea vyema mpaka raha umekuwa kama sio bint wa Dar
Mie nikacheka kwa emoji tu sikuandika kitu akanambia sijakuuliza hata jina mhu unaitwa nani cxx
Nikamwambia naitwa Dixfxnxxxa mie akasema Hata kajina kazuri sauti nzuri hivi huyu bint atakuwaje si atakuwa zaidi hata wa yule malkia wa uingeleza🤣🤣🤣🤣🤣
Ila wanaume jamani 🙌🙌🙌🙌🙌 hapanaaa Nilichekaaa sanaaa nikamwambia walaa mie wakawaida tu akasema Wish nikuone siku moja nikamwambia inshaallah tutaonana bwana Mussa
Akacheka kwa Emoji akanambia D mamaa nitakuchek mida nipo kibaruani hivyo nisije fukuzwa kazi bureee
Nikasema sawa kazi njema akasema sawa mamaa et akaweka na emoj ya kuchumu😘
Makubwa 🙌🙌🙌 sijawahi mie kuchat na Boy yeyote zaidi ya mashost kwahiyo haka ka moments nilijiona kama kiasi flani nimebadilika yaan nimependa😜😜
Mana muda wote nilikuwa nazipitia pitia Ile text😂😂 mtu mwenyewe hata simjui lakini basi tuuu anafurahisha
Mchana akanitex hello
mmh nikajibu fast hbr
Akajibu poa babyy umekula??
🙄🙄🙄Babyyy tenaaaa??? )Nikamuuliza kwa mshtuko akanambia
Baby I mean mtoto jamani we si unakisauti kama mtoto jamani hata hivyo hujatimiza miaka 18 so we ni Babyyy😀😀😀
. Ila huyu kaka 😂😂😂 nikaona aibu nikajichekesha kwa emoj kama zotee
Akambia Umeshakula babyy
😀😀😀nikajibu bado
Akanambia kwanini nikamwambia ni mapema sana sa hii sa sita hii jamani akanambia kwani chakula cha mchana wanakula sa ngapi?? Nikasema sa nane au Tisa
Akasema🙄🙄weee hicho mbona cha usiku nikamwambia basi tumetofautiana mie cha usiku sa nne kabisa akasema hee wewe unalala sa ngap nikamwambia muda wowote tu akanambia nakutumia hela basi ule hata viazi hapo mie sijiskii vizuri nakula wakati baby yupo njaa
😀😀😀Nikamwambia mie sisikii njaa bwana chai nimekunywa muda huu akasema hee basi mie nakutumia unywe hata soda😀😀
Nikawaza huyu mbona ameng’ang’ania sana kunitumia helaa?? Ujue ndio wanatolewa kafara watu hivi hivii hakiamungu nikamwambia mie hapana usinitumie mama yangu atajua na anaweza hata nitoa kichwa akacheka kwelii kwa Emoji akanambia nakutumia ndogoooo hata hawezi kujua ya soda tu please
Jamaniiii 🙄🙄nikabaki nina mtafakari huyu vipii hata bado sijamjibu ikaingia sms ya M pesa imethibishwa umepokea Elfu tano kutoka kwa Mussa Mmh🙄🙄 nimepatikana mie aisee
Akanambia nunua soda basi baby,mie narudi kibaruani kwani baadae bwana et
Hata sikumjibu aisee mie mbona naanza kuogopa jamani yaan naogopa kabisaa
Yaan ile kuongea kwangu kila habari ninayo lakini habari yangu nilikosa mtu wa kumsimulia kabisaaa
Niliona ngoja tu nimwambia mama lisije kuwa jini mie nikafa bure bila mama kujua lakini roho ingine inanambia nitaanzia wapi mie kumwambia mama yanguu??
Nikatoka chumbani kwangu ilikuwa usiku mama yupo ndani kwake , nikaenda kumwambia mama nashida ua kuongea na wewe akanambia enhee kwemaa nikasema hata sio kwema mama kuna huyo mkaka sijui mba…..”
“Amekubakaa??” Mama aliniwahiii hata sijamaliza
Yaan mama yangu bora mniue maiti mpelekeeeni lakini sio kunibandua aisee hilo ni kosa la jinai kabisaaa
“Mama bwana ndo mana mie sipendi kukuambia mambo yangu we hata husikilizi”
“Embu ongea sasa haraka haraka unajibana bana ninii??”
Nikamwambia mama kuna mtu mie nilikutana nae Fb tu akaniomba namba yangu nikampa si mjui wala hanijui ajabu ananitumia ma hela kila saa mie naogopa asije kuwa jambazii
Mama akasema ma helaa?? Yaan alikutumia kama milioni ngap?? Ni mzungu au ??
Milioni tena🙄🙄🙄 nikamwambia mama sio milioni embu angalia ile siku alinitumia elfu kumi……
ITAENDELEA……
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU