
SEHEMU YA 07
basi nikaendela na shuhuri huku namsubiri huyo mtu sijui ni mkaka au mbaba mie hata sijui haikupita hata muda akanipigia simu nimuelekeze nilipo mana yupo tayari alikuwa amefika nikamwambia akanambia basi ngoja nikupe boda umuelekeze nikasema poa
Mana yeye alikuwa yupo kituoni kabisa na sie tulikuwa ndani ndani huko uswahilini
Akanipigia nikamuelekeza huyo Boda haikupita muda akanipigia simu amefika ila amesimama mbali kidogo na kwenye shuhuri
Sasa mie nikatafuta nafasi ya kuchomoka sikutaka gazeti likauzwe kwa mama na waswahili buree mama anitoe kichwa akhaaa
Nikatazama tazama watu wapo bize nikachomoka kama nipo vilee , nikamtext kumuuliza amevaa aje akanambia we ukimuona mtu kavaa kama chizi chizi hivi ni mimi but Tshirt ni Blue ndo mimi huyoo 😀😀 nikacheka kwa emoj moyoni nikasema ngoja nikutane na muokota makopo walai nitazimia kihele hele kitaniisha mieee kilanga choteee🤣🤣
Nikaanza kuwaza nikikutana na muokota makopo namkwepajee?? Nikasema mie sijitambulishi nikimuona kwa mbali yupo hovyo namkwepa shwaaa🤣🤣 mie mwenyewe nilivyo pisi kalii aah halafu anizingue akhaa hata sitaki
Basi nikatembea kidogo nikawaona watu wawili mmoja boda na mwingine ni mkaka yupo pembeni ya Boda amevaa Tshirt ya Blue lakini anaonekana ni Expensive hatari 🙄🙄 mpaka nikaogopa kumsogelea
. Nikawa bado sijawafikia ila nikatoa simu kumpigia nisije bure kuchanganya na file
Akanambia babyy ni mimii jamaniiii “
🤣🤣🤣akaongea sauti ya kutia huruna ile na utani hapo hakupokea simu yaan alinambia kwa mdomo nikawaza huyu kanijua mie jamani nilitaka kumpita mama niliona hata siendani nae
Basi nikasogea kwa aibu najichekesha chekesha akanambia mambooooo
Mie nacheka tu aibuu hatari nikajibu poa huku nimeinama chini
Akanambia Waooh mzuri kama ka tootoo 😀😀 nikacheka et waaohh so Cuteee😘 akachumu ile yas, mbali yaani mwaah
Mi naona aibu mana anaonekana ni mkubwa huyu miaka 30_36 Nilivyomkadilia hazidi hapo wala hapungui hapo , amevaa nguo nzurii mwenzangu sio kama za vijana wa mtaani kwetu.halafu sasa ananukia huyooo harufu nzurii imepoaaa mpaka rahaa
Sasa mie jamani nina jasho hatari na kile kigoma cha shuhirini ndio uwiii , lakini kwa Uzuri tu mashaallah mie ni kazuri mno
Ndio mana mama yangu ananilinda na mapanga ningekuwa mwamba angeniachia ili nipate yeyote tu🤣🤣🤣maana angejua hapa mwanangu hakuna mwanaume mwenye Tamaa kiasi hicho
Sema mie mrembo hata shule nilikuwa nasifika nilikuwa wa kwanza kwa urembo shule nzima lakini kichwani ndio sifurii kabisaa mie akili za shule Hata sikujaaliwa 😥😥😥😥😥😥
Akanambia nimefurahi kukuona sana sanaa Dina nikamwambia usijali akanambia twende basi tukale hata kidogo mie nina njaaa nikasema wapii.? Akhaa mie siendi akasema ooooh jamani kwahiyo nife njaa ?
Nikamwambia walaa mie umeshaniona we nenda tu ,,,,,mmmmh vibaya hivyo Dina ujue …. hapana siku ingine….linii?? ….sijui…. umeniahidi mwenyewe si ndio… mie nikacheka hapo nikashindwa kujibu
Basi alinipigisha story nyingii kaka anaongea huyuu🙌🙌🙌lakini haboi hata kidogo anachekeshaa yaan una enjoy sio wale wanaume anaongea yeye kero unaona wewe akhaa
Tulikaa hapo mpaka nilipoona shuhuri inakaribia kuisha nikaondoka akasikitikaaa et nimemshindisha njaa🤣🤣🤣jamaniii🙌🙌🙌
Mie nikaondoka zangu akanivuta mkono akanambia Chukua basi hii utakunywa hata soda weee nikamwambia akhaaa sitaki nilikataa hela yake hapo huku natembea sikutaka hata kusimama mwenzangu mbeleeee😟😜
Nikamuacha ananitazama kwa nyuma na kijora changu basi najizuia kutembea mana mie nikitembea kwa kujiachia huku nyuma utasema yanaanguka 😜😜Siwapangi Serious kabisa nikawa nabana miguu ili kuzuia mitikisiko ya makalio
Sikugeuka nyuma mpaka nilipo sikia mlio wa piki piki unaondoka nikageuka ndiio inaishiaa nikabaki nakumbuka visa vya huyu kaka nacheka tu mwenyewe
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU