CONNECTION YA BALTASAR (08)

SEHEMU YA 08

 Shuhuri ikaisha tukabeba mke ,  muoaji Alikuwa  wa huko huko mtaani kwetu kwahiyo harusi tulikuwa  tunapeleka mtaani kwetu

 
  Kukawa na ngoma usiku zinakesha unajua mie ni dada wa mtaa na mama anajua vizuri mie kwa shuhuri sijambo kwahiyo hakunizuia kabisa 🤗🤗🤗🤗 

  Akanipigia simu mussa kwenye ile  namba aliyonipigia ile mchana kuacha ile mama aliibrock
 
“”Babyy ushalala??” Akaniuliza yaan mie  nacheka  tu 😀😀
 
“Nilale wapi nipo jirani  hapa kuna ngoma”

“Mmm mama hakukatazi ??”

“Ameniruhusu “

“Naweza kuja kukuona “

Mmmhhhh🤗🤗🤗🤗Nikamuuliza unaweza huku moyoni natamani ajee🤣🤣 yaan tangu nimuone ile mchana oiii nashindwa kumsahau natamani nimuone tena na tenaaa
Akanambia  we sema su mie dakika kumi nyingi nipo hapo😀😀  nikasema Su akanambia kwahiyo ndio Ameniruhusu hivyoo?? Nikamwambia  Zisizidi dakika Kumi zikizidi usije

Akasema oyyyyy😀😀😀 usitake nipae we bint nipunguzie tatu sawa nipo hapo

Akakata simu mie nikabaki nacheka tu yaan huyu kaka mh🤗🤗🤗🤗🤗

Huwezi amini nilikuwa natizama tu njia  huyu mtu anakuja au hadi nahesabu dakika , muda unaenda mtu hata haji nikawa  natamani kumtext 😀😀😀

Moyo unanambia we mtoto shika adabu yako khaa😫😫😫

Karibu li saa zima likapita nakwambia nilikasirika et 😀😀kama mpumbavu nikatamani kumtumia li sms usije tu lakini sina hayo mazoea nae sasaaa

Nimekaribia kukata tamaa ndio simu inaita akanambia  nipo karibu nielekeze nikamuelekeza mtaani kwetu nikamwambia sehemu ya kusubiri asije huku maama asije pelekewa umbea buree😜

Nikaenda nikawakuta wawili yeye amevaa Track kulikuwa na baridi baridi hiyo siku , na mwenzie amevaa Kawaida kwanza  hata sikumfatilia mie

Akanambia  nimechelewa eeh ?? Mie nikacheka aibuu  kama zoteee 🙈 nipo tu nainama inama akanambia  yule aliekuja nae sule huyu ndio Dina nilikwambiaa
  Yule mwenzie akanambia  et nashukuru kukufahamu shemu

🙄🙄heee Shemmmmmm??? Nilishtukaaa musa akacheka akasema embu acha utani bwana  Sulee 

Akanambia  huyu ndugu yangu anapenda sana utani achana nae , nikacheka

Akanambia  Dina huyu ndugu yangu anaitwa Suleiman ni mdogo wangu kabisaaa nimemwambia anisindikize mana huku mitaa ya watu naogopa nisije kuvunjwa mguu buree 

Kama kawaida yangu nacheka tu ,yule sule akasema Bro nakuja mara moja ngoja nicheck check mazingira 

Kumbe ndio anatuacha hivyo wawili  ila mwanzo sikuwa nimeelewa kabisaaa🤗🤗🤗🤗 alivyoondoka tu

Mussa akanishika mikono yangu mie hata kuitoa siwezi  nilijikuta kama ndezi akinipeleka hivi nipo naenda tu ujanja ule kwa wanaume ninao kuwa nao leo sina pyeeee kimekwishaa

  “Dina we ni mrembo sanaa hivi unajijua”

🙈🙈🙈🙈”Hapana”

“Boyfriend wako ndio hajawahi kukuambia kwani??”

Huyu kaka mnafika et boyfriend wangu hapo yupo ananipapasa mikono yangu🙈🙈 hako ka fillings  najisikia sijawahi jisikia kabisaaa 

Nikamwambia mie sina Boyfriend 🤗🤗🤗akanambia  haya Ex wako
Nikasema mie sina Ex…. mmmh kwahiyi hujawahi jiingiza kwenye mahusiano….ndio…..aaaah ya kweli hayo Dina….. ndio… kwahiyo wewe badooo mwalii eeh…….🙈🙈mi sijui…..embu nitazame kama unasema kweli …..🙈🙈Sitaki bwanaa….embu nitazameeeee….


  Ananilazimisha kumtazama bado ananivuta vuta ile  nageuza Tu uso upande wake akani kiss😘🥰🥰🥰🥰Mdomoni ile ya pap pap😅😅😅 haina kuganda lakini lips zake zikabaki kwenye lips zangu  nikawa nasikia kiubaridi flan hivii   ,,,,mama nae  si ndio wacha apige simu aliogopa hatari akanambia weee hajatuona kweli  mie natetemekaaa hata sikumjibu nilikimbia mbio z hatari 

Sikupokea simu ya mama nikaenda kwenye ngoma kwanza kumtazama sikumkuta nikaenda nyumbani  natetemeka 

Nikamkuta hana hata habar anataka zake kulala akanambia  haya muda wa  ngoma umeisha funga mlango kulala huko

Nikasema sawa nikampita kwenda chumbani kwangu akaniita we Dina nikaitika kwa kujiamini abee mama akanambia  mbona unanikia hivyo umetoa wapi hayo marashii??

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata