
SEHEMU YA 09
Mama akaniuliza we Mbona unanukia sana, Si nikakumbuka ule muda mussa alikuwa ananishika shika
Ndio akanikumbusha niliondoka mbio bila hata kumuaga hivyo 😔😔😔 nikamwambia mama Si yule Vidia amekuja na pafyum yake ndio nikajipulizia mama akasema embu muulize inauzwa shingap nzuri kweli na sie tuwe tunanukia mwanangu,Muulize jina nitamuagiza Muha 😅😅😅 nikamwambia mama sawaaa nikimuona kesho nitamuulizaaa
Nikaingia ndani fasta nikamtext mussa
Umeondoka??🤗🤗 akanambia umeniacha Njia panda naelekea wapiii nipo naangalia tu njia labda utatokea hapa au kulee
Nikamwambia we nenda mie nishaingia kulala,,akasema Oooh umelala hata sijakukisi jamani vibaya hivyo
Nikamwambia nenda siku ingine akanambia unaniahidi eeh nikacheka nikakata simu😀 nikaikumbatia simu🥰🥰🥰🥰
Yaan nasikia et Rahaaaa😅😅😅walai sijawahi kuwa mpuuzi kiasi hichi
Ikaingia text Nimefika Dina nimefurahi sana kukuona asante
Nikamwambia shukrani pia
Akanambia Dinaa ujue mie nakupenda sanaaaa yaan siwezi kuendelea kukuficha
🙄🙄🙄 mwili ukaanza kutetemekaa sasa najibu nini akatext Haloo
Nilikuwa kimyaa hata kujibu tena nashindwa niandike nini
Kweli mie nimetongozwa sanaa yaan sanaa kwa siku naweza tongozwa na vijana kibao na kesho wakarudia bila kuchoka lakini sijawahi hata kufikiria wala kuwahisi ni wanaume
Lakini huyu mwanaume huyuuu Halooo siwezi hata kuelezea The way navyo Feel kwa huyu mukaka mpya nina Vibee hatari kuna kama mdudu ananitekenya tekenya mwilini mpaka ndani ya moyo🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰
Akanambia naomba nikupigie , kabla sijajibu simu ikaita yeye ndie alikuwa anapiga nikajitupa kwanza kitandani nikagala gala nacheka mwenyewe baada ya kutengeneza koo ndio nikapokea
Hapo nipo chini ya shuka n
Ndio nikapokea simu naongelea Tumboni yaani kisauti achaaaa🤗🤗🤗🤗
“Haloo!”
“Dinaa”
“Abee”
“Nimekumiss mama yangu”
Uwiiii😂😂😂😂😂😂Nilisikia mwili kama umepigwa na shoti nikajibu “asante” yaan hiyo sauti kwanzaaaa unaweza sema nina vimafua kwa mbaliiii🥰🥰🥰🥰
“Kwani we hujanimiss??”
“Nimekuona sasa hivi tu”
“Mmmh kwelii mie basi nimeona kama vile tumeonana mwaka jana et”
😂😂😂ila wanaumeeee🙌🙌🙌Vichwa vyenuuuu
Kabla sijamjubu simu ikakata hata sijui kwanini😅😅😅 Roho ikaniuma nikusubiri nipigiwe wapii subiri na kusubiri wapiii🙌🙌
Nina hamu ya kuongea nae hatari mpaka roho inaniuma wee nikasema hapana nikaenda kwa mama hapo ilikuwa usiku umeenda lakini sikuweza kuvumilia hata nikamwambia mama embu naomba simu yako akasema ya nini huku anafoka hata sikumjibu niliichukua nikakimbia nikaenda kujifungia chumbani kwangu
Akabaki ananichamba mie hata sisikii nikaweka ile namba ya mussa kuipiga nikabaki najishauri sasa namwambia ninii??🤔🤔
Akipokea nitasema ninii?? Si ndio nitaonekana mie rahisi, Mana hata kutongozwa sijatongozwa hivyoo😥😥Lakini mie nampenda huyu sijui mbaba sijui mkaka atajua yeye mie nampenda kichwa kuuma na vile alinambia ananipenda ndio basi tenaaaa🙌🙌🤗🤗😫🤗
Nikajikaza baada ya kujifikiria zaidi ya nusu saa nikapata pa kumuanzia nikapiga ikaita kidogo ikapokelewa haloo sauti nzito nzito moyo ukafanya paa mussa wangu huyoo kapokea🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU