CONNECTION YA BALTASAR (10)

SEHEMU YA 10

Nikajishaua na kile kisauti changu cha maangamizi hata sijui kilitokea wapi kwa maana sijawahi kuwa nacho hata mara moja

“Haloo” nikaitikia huku hata sijiamini

  “Dinnna!!!????” Akaniita yaan ile kama hakutarajia mie kumpigia au haamini nikasema ndio akasema hee jamani nilipoona umekata simu nikajua umelala  au mama ameingia ndio mana nimeogopa hata kupiga tena ….

Moyo ukafanya  uhppsss  ,nikasema mie sikukata simu nilijua wewe ndie umekata akasema hapanaa kwanini nikate wakati natamani kuong……..”

Kabla hajamaliza kuongea salio si likakata😂😂😂😂nilitamani kuliaaaa aisee nikasema  hivi hapa ndio hapigi tena yaan aah ,

Nikasikia mpaka hasira , lakini akapiga muda huo huo kwenye namba yangu akanambia  vipi huu mtandao hautaki leo mie niongee ma mrembo wanguu,,,,
😂😂hiyo mrembo wangu mie li kichwa paaaa🤗🤗🤗🤗🤗
 

Nikamwambia salio limeisha tu akanambia  asante kunipigia unajua ningelala hovyoo …

Sasa mie kuzuga ili asinione nimemtafuta nikamwambia nilikuwa nataka kukuuliza hiviii et pafyum yako inaitwajee ulinunua shingap??

Akanambia  umeipenda nikasema ndio naitaka nambie jina akanambia basi nitakuletea hata usijali  
Nilifurahi nikamwambia asantee kama zotee akanambia  basi nitakutumia vocha ujiunge nikasema iwe vocha sitaki helaaa😂😂😂yaan mie et nakataa hela yaan helaa Mussa alikuwa ananishangaa akanambia we upoje mbona vi bint vya lika lako huviambii kitu kuhusu hela yaan wewe kama sio mtoto wa afumbili et😅😂😂😂😂🤣

Akanambia  unaishi kizamaniii kwelii😂😂😂nikamwambia mbona unanichamba jamani akasema basi nisemehe mke wangu ….

“Heee🙄🙄Mke tenaaaaaa????”  Nilishtuka

Akasema  et ooh Noo nimekosema Type error 😂😂😂😂😂😂😂 nikasema afu weweee

Akanambia  ila wewe kazuri sanaaa yaan upo kama wa kula kula hivii mhu unajua”

😂😂Ila mussa🙌🙌🙌🙌 huyu kaka amekuwa ananifurahisha sana aisee …

  Nililala baada ya kuongea nae muda mrefuuu hatari ..

Asubuhi  nikaamka na kichambo cha mama simu yake alinichamba huyo ananiuliza kwanini nilichukua simu yake majibu sina …

Mchana mussa akanitafuta akanambia  amenimiss kweli anataka kuniona 😜😜
Ujanja wa kumkatalia ninao sasa nikamwambia mie sasa utaniona wapi njoo kwetu😜😂hapo nilikuwa nazuga tu aka akanambia Mhhh unataka bi mkubwa anitoe kichwa eeh

Nikamwambia kwahiyo unataka kunichezea tu sio akanambia  Noo Dina mbona we sio wa kuchezewa jamani nikasema haya bwanaaa

Akanambia leo sijatoka hata kwenda kibaruani nipo tayari hata kufukuzwa kwa ajili yako naomba uje unitembelee🤗

😂😂😂😂Ila Mussaaa 🤣🤣 nilicheka sana nikamwambia  toka hapaa we sema una yako sio kwa ajili yangu

Et akanambia  mama yangu Dinaa naomba uje pleaseeee😘

Nikamwambia  mie sa mbona sijapaju akanambia nitakuelekeza ndio maana simu zipo njoo basi babyyy🥰🥰🥰 nikasema sawa nakuja

Sasa unafikiri uwezo wa kukataa ninao🤣🤣mie nishampenda huyu mtu tayari hata nakumbuka basi heka heka za mama sasaaa …hata sikuwaza tena habar za mama ananilinda

   Nilioga zangu nikatafuta kijora changu pambee , nikamwambia mama mie naenda kwa shoga angu tulisoma nae nikamwambia  naenda kuwasalimia akanambia  mbona gafla sanaa nikamwambia  nimepata hamu ya gafla kwenda

Mama yangu anavyoniamini hakuwa na shida sana nikaondoka zangu kudandia dala dala huyooo njiani mussa akanipigia et  nikuandalie niniii🥰🥰🥰 nikamwambia chochote tu mie nakula akasema kwahiyo hata busu nisiandae🤣🤣nilicheka  kwa nguvu kwenye dala dalaa hatari  mpaka watu walinitazama


  Nikafika kituoni  nikamwambia nimefika akanambia  mpe boda hapo nimuelekeze nikasema sawa nikampa boda sijui akaelekezwa nini mie kwenye Boda  huyoo

Wakati nipo njiani ndio nikaanza sasa kujiuliza hivi je nikienda kuchunwa ngozi huko nitafanyaje mie ,mana sijaaga kwa mtu kama naenda kwa bwana

Nimeaga naenda kwa shoga angu tu , boda ikasimama nje ya Geti moja kubwaa sanaa jeusi nyumba kubwa juu kuna waya za umeme

Mmh nikasema si Lodge hii🙄🙄🙄🙄 sema zile Lodge za helaa ,
Uwiii  Nimeishaa miee 🙆‍♀️🙆‍♀️🙆‍♀️🙆‍♀️

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata