
SEHEMU YA 13
Nikasema na hao ndio wanaume wenye maisha yao bora hata nngempa moyo hawa wahuni wa mtaani kwetu huenda ninge enjoy zanguuu
Basi mpaka panakucha hivii mie macho kodo sikulala kabisaa , mama akanigongea niende kunywa chai sina hamu hata ya chai nikamwambia tu mama nakuja akasema sawa
Nilipo toka nikam_mendea ameenda kuoga ile nikachukua simu yake , nikaweka namba ya mussa mana tayari nilikuwa nayo kichwani hapo wazo lilikuwa ni kumbembeleza tu nitafanyaje sasa nimeshindwa kabisa kumsahau
Nilipiga sana namba ya mussa haikuwa inapatikana
“Et nipo tayari kufukuzwa kazi kwa ajili yako”😫😫😫mfyuu niliyakumbuka haya maneno ila nyie wanaumee🙌🙌🙌
Nilipiga na namba yangu haikuwa inapatikana pia , ilikuwa ndio kazi yangu sasa kila siku kuipiga namba ya mussa na haikuwahi kupatikana mpaka nikawa najiuliza kwahiyo alisajili na laini ili tu anipate mie daah
Yaani ndani ya wiki moja tuu nilikuwa tayari nimekonda Uso hauna nuru kabisa mie mtu wa mawazo sanaa sanaa , mama aliniweka vikao na vikao alinisema mpaka basiii
Lakini sio mie ni moyo yaan moyo umeshindwa kabisa kuliacha hili swala kabisaaa , Wiki ya pili ndio hali ikazidi kuwa mbaya mpaka mama akaanza kuogopaaa sasa akawa anaongea analiaa
Mie nishakuwa mtu wa kujitenga tenaa mama akanambia unapakumbuka kwa huyo mtu nikasema ndio mama aka akanambia kesho twende huwezi kuteseka hivi bora akaniuwe nikasema sawaa mama
Asubuhi ile ndio ilikuwa siku ya kwenda niliamka naumwa sana yaan natapika tu natapika sanaa
Mama akanichukua safari ya kule ikafa tukaenda hospital mana mwili ulikuwa hauna nguvu kabisaa
Hospital ndio nilizidi kudata nyieee🙌🙌🙌Et mimi nina mimba uwiii😫😫😫 Nikajikuta namwambia mama nimeisha mie nimeishaaaaaa mama yanguuu
Nilihisi kuchanganyikiwa 😫😫😫🙌🙌 mama akanifokeaaa akanambia embu tulia unafikiri kuchanganyikiwa ndio kutatua tatizo au kulia ndio kutatua embu nyamazaaaa
Alifokaa mpaka watu wakageuka kututazama akanambia , huyo mtoto ni wako unataka kumuona ni mkosi??
Mungu ndio anajua kwanini amekupitisha hapo usijione unamkosi ilikuwa lazima upitee hapo
😔😔😔Daah yaan mama yangu alinilinda siku zote hichi ndio alikuwa hataki mimi nizae nyumbani lakini nimemuangusha vibaya sana
Hatukwenda nyumbani baada ya kutoka hospital tulienda kwa ma mkubwa , mama akamwadithia ma mkubwa kila kitu ma mkubwa alishauri kuwa mama anipeleke kwa mwenye mimba na akikataa twende police mana mie bado mdogo sina miaka 18
Mama akasema kesho asubuhi tutakwenda huko ilikuwa leo twende ma mkubwa akasema tutaenda wote mama akakataa akasema hata tusikusumbue wacha niende tu mimi …
Tulishinda kwa mama mkubwa hiyo siku mpaka usiku kabisa tukala na chakula cha usiku ndio tukaondika kurudi mida ya sa nne hivi usiku ..
Tumefika nyumbani jirani wa chumba cha nyuma akamwambia mama kuna mtu alikuja hapa kuwatafuta mlivyotoka tu na ameshinda hapa kuwasubiri ametoka muda sio mrefu yaani mmepishana hapaa
Mama akauliza ni nani yule dada akasema mie hata simjui ndio kwanza nimemuona ni mwanaume mkaka hivi
Mie moyo ukafanya paa sio mussa kweli nikawahi kumuuliza yupoje
Akanieleza huyo mtu alivyo , hakuwa hata anaendana na mussa wangu 😭😭,nikahisi maumivu kuanza upya tenaa
Alikuwa ameacha namba yake ya simu mama akaipiga iliita ya kwanza ikakata ikaita ya pili akapokea mdada akasema mwenyewe ametoka kidogo akija atampigia mama akakata bila hata kuongea akanambia nenda kalale …
Asubuhi kabla hata jua kutoka mama alikuja kuniamsha akanambia jiandae tunaenda
. Nilipata nguvu nimemkumbuka mussa nina hamu ya kumuonaaa🤗🤗🤗Nimemiss na kuwa na mimba yake nilikuwa na furaha mnoo sikujali atakataa au kukubali wacha niwe hata na mtoto wake tu inatosha
Tulienda mpaka hapo nikaikumbuka nyumba vizuri tu , yaan nilivyoona geti lilee miguu ikaanza kutetemekaa woga wa kukataliwa tena nikaanza kuuhisi upyaa
Nikakumbuka jinsi mussa alivyoniingiza kwa mahaba ya kubebwa juu juu na nikatoka kwa kilio hii nyumba siji kuisahau miee
Mama akanambia unauhakika ndio hapaa?? Nikasema ndio hapaa akagonga geti mara ya kwanza mara ya pili likafunguliwa
Uso kwa uso na Sulee alipo niona alishtukaa🤔🤔🤔
Akababaika mama akaniuliza ndio huyuuu?? Nikasema hapana mama akamwambia hayaa wewe huyo mzee wa kujaza watoto wa watu yupo wapiii ,mama akanigeukia akaniuliza anaitwa nanii?? Nikasema mussa huku nimeinamisha uso wangu chini
Mama akamgeukia Sule akamwambua hayaa umelisikia jina lake yupo wapii.?
Sule akasema mama naomba tuingie ndani tafadhali 🙏🙏🙏 mama akamwambia yupo hayupoo??
Sule akasema hayupo lakini tunaweza kuongea mie ni mdogo wake mama akamuuliza huyu unamjua wewe??
Huku ananinyooshea kidole
Sule akasema ndio ni Dina ninamjua vyema sana japo tulionana mara mojaa tu ..
Mama akasema haya tunakwenda tutarudi mwambie huyo mpuuzi nipo nayeye mpaka mwisho
Sule akasema hapana mama usiondoke naomba sana tuongee
Mama akamwambia mie sina cha kuongea na wewe namtaka aliemtia mwanangu😀😀😀yaan mama et nimetiwa 😂😂😂
Sule akasema mama naomba tuongee jana nilikuja mpaka nyumbani kwetu nilihangaika sana kupapata lakini sikuwakuta nilisubiri siku nzima hamkuja nikaacha namba yangu ya simu bado sikupata simu zenu
🙄🙄🙄🙄🙄🙄Kumbe huyu ndie alikuja nyumbani?? Sasa alikuja kufanya ninii??
Nikajikuta nina maswali kibao huku naombea mama akubali tumsikilize kwanini alikuja nyumbani jana
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU