CONNECTION YA BALTASAR (14)

SEHEMU YA 14

Sule akamuomba sana mama tuingie  ndani mie sikuwa na neno sikutaka kumkera mama yangu hata kidogo  mana hapa tu tayari nilishamkera na akisikia kaka yangu nimeisha mie kabisaaa 🙌🙌🙌

      Huku anasema sema mama lakini tukaingia ndani ,sule akamuuliza mama nikupe kinywaji gani mama akamjibu unafikiri tulikosa miasita ya maji sie au soda?? Au unafikiri huwa hatunywi et

😂😂😂😂Sule akamwambia mama naomba unisamehe,akaketi kwenye kochi mpoleee😀😀😀 mama ameweka uso wa mbuziii

“Hayaa huyo mpuuzi mwenzio yupo wapiii???” Mama akauliza kama kwenye shali na vile alimuona sule amepoa poa hee ndio akaona mbona anammudu kabisa

“Mussa ametoka mama”

“Naomba umpigie aje hapaa kabla sijaenda police ” 

“Yupo mbali mama lakini kabla hajaondoka aliniomba niweze kuliweka sawa  hili jambo mimi mwenyewe “

“Enhee kivipi??”

“Aahmm Dinna kwanza ulimuelewa vibaya bro ,sijui uliongea nae nini lakini anaomba radhi na amesema hakuwa anamaanisha et hakutaki bali alihitaji muda zaidi na wewe na sio haraka vile jambo ulilokuwa unataka”

Nilihisi kusonya mjinga kweli huyo.kaka mama akamuuliza enhee kwanini akutume wewe??”

“Bro amesafiri ile siku baada tu ya kuachana na Dina aliondoka ule ule usiku kwenda hispania kwenye biashara zake “

“Anhaa kwahiyo alijua kama kashamtia mimba mwanangu enhee unalishuhurikia vipi wewee??”

“Mama Dinaa ana mimbaa???”🙄🤔

Sule alishtka mpaka akainuka kwenye kochi mama akasema unashangaa ninii ??

“Ooh mungu wangu ,Dinaa ooh kwanza hongera lakini mie sina maamuzi juu ya hilo naomba tumsubiri bro , aje mie alinambia niwe karibu na Dina nimtazame mpaka atakapo kuja  lakini sikupata muda wa kukutafuta nilibanana sana na kazi mpaka jana na Leo pia nilihitaji kuja huko “

“Kwahiyo anarudi lini??”

“Sijajua lini ila atarudi mara moja atakapo kamilisha ratiba zake “

Mama akainuka akanambia inuka tuondokee 😫😫😫
Sule akasema hapana mama naomba umuache hapa Dina kwakua ana mtoto wetu🥰🥰🥰
  Moyoni nikapata amani mama akasema ili iweje huna hata adabu 🤔🤔Tuondoke Dina
   Tukaondoka  bila hata kuaga tena , Sule akabaki ananitazama nilivyogeuka kumtazama  akanikonyeza😀😀😀nikatabasam kidogo  nikapata amani moyoni 

   Tulipo toka kabisa nje ya geti sule akaja mbio et mama mkwee😀😀😀nilisahau kumpa Dina simu yake hii niliihifadhi
Daah nilicheka  kidogo yaan sikumbuki hata mara ya mwisho kucheka ilikuwa lini

Sura ilikuwa imeshakosa kabisa nuruu lakini leo nilihisi nina amani sanaaaa yaan kuna kama kitu nimekitua moyoni hiviii

Nikarudi kuchuka simu yangu akanipa kikaratasi kina namba akanambia  please  nipigie tuongee , sikujibu nilichukua simu na hiyo karatasi  nikaondoka zangu

Tumefika kituoni gari Zimejaa kweli  mie nikachukua simu yangu mana kitambo sina halafu nimeimiss kweliii

Ile nataka kuiwasha nikaona imekuwa nzito halafu imejaa kwenye cover  ikabidi nifunue enhee nakutana na hela kama elfu hamsini hiviii🥰🥰🥰nikamwambia mama ona kama akasema wajinga  kwahiyo wanataka kutuninua ??

Embu rudisha hizo helaaa🤔🤔🤔 mama nae vipiii😂😂😂 nina wiki mbili sijashika hata miaa halafu mie mama kijaa nikitamani miguu ya kuku jee😜😂😂 nikamwambia mama embu acha zako

Nikamwambia mama mbona hata hawajakataa mimba lakini  ,

Mama alinivuta sikiooo kwa hasira  hatari akanambia  na tukirudi hapa umwambie mwenyewe  kaka yako

🙄🙄kaka tenaaa yaan et nimwambie kaka mie nina mimba  naanzajeee

Mama akaichukua ile hela yote 😂😂akanambia  mpuuzi wewe hichi ki hela ndio kimekutoa imani …


   Jamani nyiee mie kwenda kwa kina mussa hata kama sikumkuta ilikuwa tiba kwangu sio kwamba nilitaka nilijikuta Automatically tu nimekuwa na furahaa yaan naongea  kidogo nacheka hatari

Hata kama nahisi alinijua akaenda na mimi vile vile mana nlimuona amechangamka sanaaa baada ya mimi  kurudi kwenye ule umcharuko wangu

Wakati mwanzo  nilikuwa najifungia tu ndani mwenyewe  ..

  Nilitafuta ka nteba Kangu(sehemu ya kujificha) nikampigia siku sule nikajitambulia akanambia  yaan Dinaa ujue siamini ??

“Huamini nini tena”

“Et kweli wewe ni mjamzito??”

“Ndio shemu ni kweli”


Waooooh hahaah Dina umeniita shemuu??, Kwahiyo  umemsamehe bro??”

“Kwani mie niliwahi kumkasirikia au yeye  ndio amenikasirikia ??”

“Unajua nini dinaa, Natamani sana uwe na bro yaan naomba usimchukie”

“Yeye mbona ananichukia??”

“Anachukia wanawake wote , siwezi kukuambia sana lakini hataki kuwa na mwanamke  permanent  huwa anatumia tu wanawake alivyokuona wewe akasema anataka kutulia na wewe lakini sio kuoa hataki tena kuoa mana mke wake wa mwanzo alimpitisha kwenye changamoto nyingi sanaa sanaa , Unajua mussa niliona amebadilika kidogo  tangu ameanza kuwasiliana na wewe that’s why  hata ile siku nilimlazimisha sana tuje huko nilitaka awe karibu zaidi nawewe niliona utamfaa na kweli anakupenda lakini anaogopa sana kuoa au kumuweka mwanamke karibu yake ,

Hata ulivyoondoka alinambia nikutafute nimuombee msamaha sikupata tu muda na hili la ujauzito  Dinaa I’m  happy mamaaa🥰🥰🥰”

  Nikabaki Gaa!! Kumbe kweli hataki kuoa🙄🙄

“Sasaa atanikubali kweli??”

“Mussa anakupenda mnoo  ni wewe kuwa yule mwanamke ambae atakuwa tofauti na wale wajinga alio wahi kuwa nao”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata