
SEHEMU YA 15
Shemu akanipanga sana akanipa mbinu za kuhakikisha bro wake namshika haswa
Sule akanambia mussa ndoto yake ilikuwa siku moja kuwa baba anatamani kuwa na mtoto ninafuraha kwa ajili yake mie wala sintamwambia kama wewe ni mjamzito nataka alisikie kutoka kwenye kinywa chako🥰🥰🥰🥰🥰
Akanambia shemu mtooto hakusumbui😂😂😂 jamani 🙌🙌 nikasema natapika tu
Akanambia basi jioni nitakuletea kitu kitamu ule huyo itakuwa amemiss bab yake🙌😂😂😂nikawa nachekaa huyu mtu na ndugu yake wote wanavituko akanambia jioni nakuja mke wetu nije nimuone mtoto wetu
Nikamuuliza et shemu kwani mke wake na musa alifanya nini, sule akanambia mmh embu atakwambia yeye akihitaji kukuambia lakini mie nisivuke mipaka
Jioni shemu alikuja 🥰🥰🥰Akaniita sehemu hakufika nyumbani alisema anamuogopa mama akaniletea ma pocho pocho nilikula hatari nikarudi nyumbani mzitoo
Nafika nyumbani si ndio namkuta kaka🙄🙄nikasema moyoni huyu nae usiku usiku anakuja nyumbani kwanza hata sijui kaja lini dar 🤔🤔 nikamwamkia shikamoo kaka akanambia embu kaa hapo yaan hata bila kuitikia salamu yangu
Nikasema moyoni kumekuchaaaa
Kaka akanambia we dina umeshindwa kabisaaa kujituliza yaan umeshindwa mpaka unatuletea mimba hapa nyumbani?? Mimba za utotoni??
“Kaka naomba unisamehee,Ni bahati mbayaa”
“Kwahiyo ulijikwaa ukadodokea mimba eeeh??……..wewe si nakuuliza …..naongea na wewe dinaa!!! …..kimya ndio kinamaanisha niniii??”
Kaka sijui alitaka jibu gani kutoka kwangu , anajua nilifanya nini nikapata mimba afu ananiuliza et nilidondokea😅😅😅kwahiyo nimjibu niliikalia auu?? 🤣🤣
Mie nilikuwa kimyaa nimejiinamia chini majibu sina
Akasimama akafungua mkanda wee nilipiga magoti fasta nikaanza kulia
Mama akamwambia Jose naomba usimpige huyo mtoto tena nitolee ujinga wako
Kaka akamwambia kwahiyo ulikuwa unaniambia ili iweje kama ulikuwa hutaki huyu mtoto akanywe angekuwa mtoto angeenda kujibinua huko abebe hiyo mimbaa
Mama akainuka akaja kusimama mbele yangu akamwambia hakuna maana kama kosa limeshafanyika hapa tuangalie jinsi ya kumtunza huyo mtoto basi kupiga na mtu yupo kwenye hali hiyo unataka kuniletea mie matatizo eeeh”
“Mama kaa pembeni sioni kazi huu mkanda kukufikia weweee”
“Kwahiyo unataka kunipiga si ndio”
“We Dina toka hapoo??”
Yaan et nitoke nyuma ya mama aah weee ndio kwanza nikajitengeneza vizuri kujificha🤣🤣🤣wenyewe wapigane tu si mtu na mama yake mie nifanyaje
Kaka akaanza kumsukuma mama ili anifikie mie wee na mie mama atakapo sukumwa ndio nafata huko huko kaka ananiambia dina nitakufumua nitakufumua weweee njoo hapa nikasema hata siji kaka
“Unasemaje wewee??”
Nikakimbia chumbani kwangu nikaenda kulala kaka akabaki anasema kwa jazba kweli yaan roho ilimuuma kwanini hajanifunza adabu🤣🤣embu anipishe mie asubiri watoto wake awafunze kwa kujinafasi
Nikalala zangu ndani kimyaa nikaacha mama na mtoto wanagombana mama akajuta kwa nini alimshirikisha kaka
Basi kaka akanambia haondoki hapo nyumbani na mie nijifungie ndanu maisha yangu yotee🤣nikamjibu sawa ngoja nifie humu ndani
Mama wacha aanze kulia et Dinaa usijiue mwanangu😅😅yaan mimi huyu nijiue mimiiiii?? Hee aah wapiii
Mama akabaki anamlaumu kaka nikifa atanila nyama analia mlangoni kwangu anagongaa mie kimyaa
Yaan hiyo siku tukawa kituko kwa majirani na bahati nzuri sie ndie mwenye nyumba ingekuwa tumepanga sijui ingekuwaje tuu
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU