
SEHEMU YA 16
Mama alinigongea hata niende kula hakujua kama nishakula huko niko ndii nikamwambia hata chakula chenu siliii🤔🤔😔
Basi kaka ndio anazidi kubebeshwa lawamaaa😅😅yaan mama na alimuita yeye mwenyewe hapo ..
Nikalala zangu mie hata sikujua wamemaliza vipii
Asubuhi sikutoka nje mama ananiita njoo unywe chai nasema sitaki kaka atanipiga mama ananiambia we Dina embu njoo hawezi kukupiga mie nipo hai hawezi njoo namie nimekaza sijiii alinambia nifie humuu😔😔 ngoja nife mlizike 😅😅😅
Mama anasema jana umelala njaa Dina na hiyo hali yako embu njoo we Dina wewe
Mie kimyaaaa
Mara nikasikia li sauti la kaka
“We mpumbavu wewe haraka toka humo ndani hakuna wa kukubembeleza, nikivunja hichi kitasa dina mama yako hatoweza kunizuia hivi unanielewa”
Mmmh 😅😅😅alivyoongea sauti ya kiume aaah weeee nikajua hapa navunjwa mguu wallah 😂nikafungua mlango mwenyewe
Kaka akanisonya tu wala hakuongeza neno , mie nikachukua chai nikanywa zangu kaka baada ya chai akaondoka zake et akamwambia mama kila akiniona anasikia hasira hawezi kukaa na mie karibu😟😟😟😟
Mama akamwambia we nenda tu mie nitamaliza na mwanangu mwenyewe kaka akaondoka analalamika et mama ananiendekeza ..
Kaka alipoondoka mama akanambia haya we nae njoo unifatie vocha hapaa nikatoka kufata vocha
Wakati natoka dukani nikasikia naitwa
“Babyyy Dinaa” kamoyo puu💗 nikageuka fasta sikuamini namuona baby daddy wangu mtarajiwa 🥰🥰
Tena ananitazama kwa tabasam kama sio yule alienipa stress wiki mbili zotee
Nilikimbia mwenzangu nae akatanua mikono yake nikajichomeka chap akani hug🤗🤗🤗
Akanibusu mpaka basi
“Dinaa mamaaa et una mtoto wangu ???”
🙄🙄🙄Hee huyu shemu si alinambia hata mwambia nimwambie mwenyewe imekuwajeee??
“Umejuajee”
“Dinaaaa embu njoo kwanzaaa”🥰🥰🥰akanibeba juu juu yaan hapo ni asubuhi mtaani watu kibaooo halafu mussa analeta mahaba ya kitajiri yale ya kwenye Tv😅😅😅😅
“Sitaki wewe si ulisha nikataa”😔😔😔😔 nikajitoa hapo tayar nishanunaaa ila sio Serious
Zuchu alisema hivi kuna wimbo wake flani hivi (nikinuna mie ndio nadeka usije dhani kiburi ukanacha nije kuchekwa) 😂😂😂
Sasa mie ndio nilinuna ule mnuno wa kudeka😅😅😅
Akanivuta nikaangukia kifuani kwake
“Mama mtoto wangu naweza kukuelezea tafadhali “
“Sitaki hata maelezo yako”
“Noo!!!Dinaa” si akanipiga busu la mdomo🤗🤗
Sasa mie ndio akili ikaja nikagundua kuwa robo tatu ya watu wote wanatutazama sisi nageuza macho ili kutazama vizuri mamaaa🤔🤔🤔
Nakutana uso na macho na mama yangu salaleee ameshika kiuno anatazama jicho kalioi🤦♀️🤦♀️🤦♀️
Nikajitoa fasta kwa mussa “mamaaa!!!?”
Mussa kusikia mama aloo😅😅😅aliruka nyumba kama hatua 7 za gafla mnooo
“Nimekuja kuongea na mama naomba unipeleke nyumbani ” akabadilisha na sauti kawa mwema sana
“Twende” na mie nikajibu kama wa maana vileee
Mama hakuongea kitu akarudi zake nyumbani basi tulikuwa tunatembea kimyaa kama tumejisaidia kwenye nguo kila mtu ana haya kivyake
Nikamfikisha nyumbani mama alikuwa amenunaaaaa kama anamjua mussa vile kumbe hata hajawahi kumuona
“Hiyo mimba haitoshi umeanza na kunitia aibu mtaani kufanya mapenzi hadharani sio”
“Mamaaaa!!!”
“Mpumbavu weweee mbona unanudharirisha sana Dina”
Daah😔😔😔😔 Ilibdi tu nikae kimya tusibishane mbele ya mgeni
Nikamwambia mussa karibu huku nampa kiti mama hata hakumkaribisha alikuwa anamtazama kama amejisaidia mbele yake bila kutoa nguo
“Mama huyu ndio mussa yule tulienda kwake juzi”
Mama alimtazamaa yaan kuanzia chini mpaka juu kwa sauti ya kuchoka akamwambia
“Karibu, haya kimekuleta nini hapa??”
Hee mamaaa😔😔 Nilijisikia vibaya kweli hata hamkaribishi vizuri angejua mimi huyu kaka bila yeye siwezi kuishi basi tu
Angemtetemekea kwa ajili ya uhai wangu
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU