
SEHEMU YA 17
Mussa akaketi mpolee , akamwambia mama Samahani mama yangu naomba radhi dhati kabisa kwa makosa yote niliyofanya mlangoni kwako!”
“Haya sawa” mama akawa anajibu kifupi kifupi tu
“Nimekuja hapa kuomba nafasi ya kuwa na Dinaa kwa ajili ya mwanangu”
“Anhaa kwahiyo isingekuwa mimba ungekuwa umemuharibu mwanangu kisha kumtupa sio”
“Hapana mama hapana , sio hivyo ilikuwa tu kutokuelewana kati ya mimi na yeye lakini nipo tayari kumuoa”
“Embu mpigie mama ako mkubwa” mama akanambia nikachukua simu yake fasta kumpigia ma mkubwa salio hakuna akanambia vocha iko wapi
Nikakumbuka alinituma vocha 😅😅😅😅😅na nilinunua kabisa sa iko wapi nikaanza kuitafuta huku moyoni nina uhakika kabisaa ule mda nakumbatia umbatiana na Mussa nahisi ilianguka paleee
Mussa akanambia tumia hii ina salio ,mana mama alikuwa kashaanza kunitokomeza maneno yake 🙌
Nikachukua simu ya mussa simu ya kwenda, nasikiaga tu Et Aifoni nzitoo 😅😅 ile 15 afu nasikia hizi simu et ukiizama nayo kwenye maji haiharibiki mie nasikia sikia sijawahi kuishika kwanza naskia zina bei hatari
Mama akanambia muelezee kila kinachoendelea hapa na umwambie aje la sivyo hatokuja akaacha kazi zake
Ilibdi nitoke nje sikutaka kuongea mbele ya mussa kwakua alikuwa amenitolea lock
Nimempigia simu ma mkubwa mara mbili hakupokea nikawaza ngoja nimwandikie tu ujumbe akishika simu apige kwa mama kuna tatizo
Nilipo ingia kwenye msg juu kabisa nakutana na sms ya Sulee
(We nenda bro mbona Dina ni mwanamke mzuriii sanaa Bro shauri yaki)
Hiyo msg ndio ilikuwa juu kabisaa mmh habari ya kutuma kwa ma mkubwa ikaish kwanza nikawaza huyu Mussa hanipendi au haniamini?? Mbona simuelewi yaan hapa kaja kwa kusukumwa na Sule auu??
Mbona hata hafanani mimi anaejionesha kwangu ni tofauti kabisa na alivyo akija kwangu mcheshiii anajua kuigiza mbwa huyuu😔😔
Nilijikuta napata hasira nikafungua sms ili nisome walianzia wapii
Zilipo anzia kunihusu mie niliona sule anamwambia mussa
(Kwahiyo Bro Vipi kuhusu Dina)
(Aah sule najua nimemuharibia yule.bint lakini naamini atanisahau tu,acha nikae nae mbali)
(Lakini unampenda)
(Kupenda napenda lakini hawa wanawake aah aisee mie hata sitaki kuwa kwenye mahusiano Serious,laiti kama ningejua Dina ni Bikra walai nisinge muharibu nngemuacha na maisha yake )
(Basi tufanye iyo iwe tickets yake embu jaribu hapo ,sio wanawake wote wako sawa)
(Yule bado mdogo halafu hawajui wanaume siku akija kuzibuka atanipiga tukio la mama Fai likasome acha bwana nimalize uzee wangu kwa amani tena huyu anaweza hata kuniuwa mie kwa presha si unajua na umri ushaenda mimii)
(Kaka! kaka! kakaaa!! Embu mpe Nafasi Dina najua unampenda ila unajilazimisha embu jaribu tena basi kidogo tu baada ya hapa wala sintakuja tena kukuomba uwe kwenye mahusiano Serious )
(Hapana Sule)
(Basi fanya kwa ajili ya mwanao tu)
(Mwanangu yupii tena mzee)
(Dina ni mjamzito)
(Niniii weweee)
(Nilimwambia sintakwambia ,mpaka mkionana ndio akwambie yeye lakini naona huitaji kuonana nae tena so fanya kwa ajili ya mtoto tu please Mussa nakuomba sana)
(Sule una uhakika kama mtoto ni wangu)
(Wewe ndie uliemuanza kwahiyo wewe ndie baba)
(Ooooh mungu wangu siamini ujue Sule MY God hivi unaongea kweliii)
(Mtafute tena fanya haraka)
(Nitaenda lakini sule akiwa sio yasije kuwa ya mama Fai)
(Aaah bro mama fai mama fai sipendii)
(Embu ngoja nikupigie now tuongee vizuri dogo)
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU