
SEHEMU YA 18
Kabla sijaendelea kusoma simu iliita ma mkubwa alikuwa anapiga nikakata fasta nikapokea simu
Nilijitambulisha nikamuelezea ma mkubwa kila alicho nambia mama akanambia haya nakuja
Nilikata simu nikarudi ndani mama akanambia we mbona umechukua muda mrefu hivyo nikasema alikuwa hata hapokei simu
Ila akilini nilikaa najua kabisa kuwa mussa kuja hapa nikwa sababu ya mdogo wake sio yeye 😔😔ile raha ya mwanzo yote ilipotea kwahiyo nisinge kuwa mjamzito mie nisinge mpata tena mussa
Ama yupo hapa ananionea huruma na sio kunipenda kwasababu amenitoa kauschana kangu tu kaka angenikuta gazeti la juzi basi labda angenifukuza kama mbwa ile siku 😔😔😔 Raha yote iliisha mpaka mama akaniuliza we mbona umekuwa mnyonge gaflaa nikasema mie nipo sawa nasema hivyo machozi kwa mbali yanataka kutoka ..
Ma mkubwa alifika wakanambia mie niondoke niwapishe maongezi yao mie nikawapisha wakati natoka nje ,kaka nae alikuwa anakuja sikujua ameitwa na nani hapo ..
Niliingia chumbani kwangu yaan aah hata mood ya kuwa na mussa iliisha nilikuwa nampenda sana mussa sanaaa lakini gafla tu nimeona kama najipendekeza sana kwake amaa nalazimisha tu
Sijui hata waliongea nini na mama mie ila walichukua muda mrefu sana mpaka mchana ndio muss akatoka akaniitaa akanambia ameomba leo atoke na mimii atanirudisha jioni
Nikasema haina shida kama umemuomba mama hata haina shida , tulienda taratibu anaongea anajichekesha na ule utani wake kama kawaida mie hata mood sikuwa nayo aisee hata ile support ya kucheka akhaa sikuwa nampa
Alinipeleka sehemu moja hivi sijui ni hotel ile mie hata sijui kulikuwa sehemu wanauza vinywaji kuna upande wa chakula kuna swimming kubwaaa
Miziki ya Lunc ile nasikilizaga Tbc mchana huwa inapigwa leo mie ndio naisikia live yaan wakati nakula Dj anatusindikiza taratibuuuuu 🥰🥰🥰🥰
Akanambia unataka kula nini Babyy, Nikasema chochote tu , nasema hapo nipo Serious hatari moyoni nina hasiraaaa😔😔😔
Akasema tuletee ngamia ya kuchoma na ugali kidogo usiache makange ya filigisi
🙄🙄moyoni nikasema hee kumbe kuna ngamia zinauzwa kwenye hotel ohoo makubwa
Ikaletwa nyama sahani Paaa😂😂😂nikisema sahani paaa yaan imajazwa nyamaa ki ugali kidogooooo😂😂
Ndo na hayo makange sasa mie si nasikiaga tu makange makange makange kwanza siku ya kwanza kusikia habari za makange nilijua mtu kakosea kusema badala ya makande akasema makange😂😂😂🙌🙌🙌
Ushamba bwanaaa hayaaa nyama ilikuja na umma na kisu aloo 😅😅😅😂😂yaan unakata ndio unakulaa mie sasa na lini??
Basi nikikata hivi kisu kinaenda upande manusura nivunje na sahani enyewe , ndio nikazidi kununaaa
Mussa akaivuta sahani yangu akaikata kata nyama yote ikawa vipande vidogo vidogo akanipa
Kama kuna mtu alikuwa anatufatiliaa naona alikuwa anacheka mwenyewe atajua yeye bwana
“Dinaa!!” Mussa akaniita huku ananitazama namie hata sikuitika niliknua tu uso nikamtazm bila hata kuitika
“Mbona hauna rahaa, sijakuzoea hivyo”
“Na lini mie nawewe tulizoeana”
“🙄dinaa haupo sawa eeh”
“Mie nipo sawa tule tu niende nyumbani “
“Noo Dinaa,embu nambie shida nini mpenzi wangu”
Akahama upande wake akaja kukaa pembeni yangu,niliskia uchungu huyu ananiigizia mie 😫😫😫 Kumbe hata hanipendiiii
Nimamuuliza hivi mussa wewe haunipendi au hauniamini??
Akatoa jicho akabaki kuitika itika nikamuuliza haunipendi au hauniamini?? Najua upo hapa kwa sababu ya hii mimba tu sasa mie sitaki kuonewa huruma na una uhakika gani kwamba hii ni mimba yako??”
“We Dina wewee🙄🙄Umeongea nini na Sulee??”
“Hakuusiani na Sule nipo nawewe hapa, kama upo hapa kwa ajili ya mtoto , kaa pembeni akizaliwa utakuja kumuona basii mie sitaki kuishi na mtu kwa sababu ananionea huruma “
Niliinuka zangu hata chakula unafikiri nilikiona utamu wake?? Pamoja na kuwa mie mshamba lakini aah wapiii
“Dinaa embu njoo” akaushika mkono wangu nisiondoke wacha machozi yaanze kunitoka
Nilijikuta naliaaa akanikumbatia acha basiii achaaaa😥Ndo nikazidi kuliaa huyu kaka kumpenda kote kuleee mieee
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU