CONNECTION YA BALTASAR (20)

SEHEMU YA 20

 nilifika nyumbani  kwa shemu, nikaingia ndani hata sikubisha hodi na hiyo ni kawaida yangu .. 

Nilimkuta mke wangu  mule ndani akiwa juu ya kifua cha kaka yake wamelala jui ya kochi wanachezeana😥😥😥 sikuamini nachokiona nilimuita mama Fai zaidi ya mara kumiii

Mwili wangu ulikuwa unatetemeka sanaa nilishindwa kusimama kabisa mke wangu yaan anatembea na kaka yake auu??

  Nilianguka nimekuja kuamka nipo hospital  Sule akaniuliza shida nini nilimuomba nataka kuongea na mama Fai akanambia  hajamuona tangu alipo mpigia simu kuwa nipo hospital akamuelekeza hospital  nilipo na hawakuonana wala hajamwambia shida ninii!!!

Nilijikuta nalia sana nilishindwa kuficha machozi yangu kama wanavyosema mwanaume hutakiwi et kulia aah hapana nililia ili kutoa kitu kilichokuwa moyoni mwangu

  Nikaomba niongee na Mama fai lakini sikumpata zilipita siku nne mie nimetoka hospital  ndio mama fai alikuja na familia yake akiwa mama yake yeye pamoja na kaka zake ambao ndio nilikuwa nawajua tangu namuoa 

Mama fai alikuja kukiri kuwa yule hakuwa kaka yake , ni ukweli ambao niliomba uwe uongo ,ni ukweli ambao nilitamani nisinge ujua mpaka nakufa , ulikuwa Ukweli mchungu sana mie kuupokea 
 
Alisema kuwa  ni mwanaume aliekuwa na mahusiano nae tangu alipo fika tu dar alimpa maisha hakumuacha atange tange hivyo baada ya kukutana na mimi alikubali kwa sababu bwana wake alimlazimisha akubali ili wapate hela kupitia mimi , akanambia yote alifanya kwa kulazimishwa lakini hakuwa na hisia nae tena ananipenda mimi   , alinielezea vitu vingi aisee nilikuwa nimechanganyikiwa sanaaa nilikuwa naona kama anapiga  kelele 

Nilimwambia nataka mtoto wangu yeye aendelee na maisha yake simuhitaji tena

Ndugu zake waliomba sana nirudiane nae nimsamehe , hata sule aliniomba pia nimsamehe tu 

Nikachukua mwanangu nikamwambia aende nitamfata kwao ila mtoto aniachiee

Unajua nini Dinaa??
  Hili ndio jambo  lilifanya niwe chizi kabisa  hata kuvaa nilisahau kula wala kunywa
.  Fai hakuwa mwanangu kabisa fai alikuwa mtoto wa yule jamaa

Nilikaaa nae siku moja tu na siku unayofata yule mwanaume alikuja kudai mtoto tena kwa fujo sanaaa , matusi  na kejeli et mie sina uwezo wa kuzalisha kwahiyo.alikuwa ananisaidia majukumu ya ndani sikuwa nayaweza😥😥

Sikuwa hata na nguvu ya kuita police au kumpigia simu mtu aje , mwanangu niliempenda kuliko kitu chochote kilee alichukuliwa huku namtazama ..

  Hapo ndio nilipo poteza mwelekeo kabisa sikujua usiku wala mchana sikujua njaa wala kiu, Uwezo wangu wa kufanya kazi nilipoteza pia

Nilikuwa nashinda nalia usiku kucha naliaa
  Ndio sule aliamua kuja kuishi nyumbani kwangu unamuona mpaka leo anaishi na mimi

Ukweli sijawahi kumuweka karibu mwanamke  hata kwa sec moja yeyote yule ,

  Dinaaa Naapa ipo tofaut kabisa kwako  japo siwezi kusema et nakuamini sana , naogopa kuzama lakin nakupenda sanaa”

   🤔🤔🤔Nilishusha pumzi baada ya kusikia yote hayooo , nikasema huyu mama fai popote alipo mungu amuathibu mbona hakuwa hata na uoga jamani

Akanambia  ndio.hivyoo sipendi sanaa kuongelea hili lakini wewe unaenda kuwa familia yangu lazima ujue hili pia

  Ni matukio ambayo bado yanaishi ndani ya moyo wangu 

  Nikamwambia” mussa mie nakupenda kiukweli nimekuona  hizi siku chache tu lakini nakupenda sanaa kama utanikubali nikubali siwezi kufanya ujingaa wowote ulee “

:nakuelewa sana Dina pia nakupenda na nitakuoa haraka sanaa “
 
.oiii😅😅😅🤗🤗🤗hii ndoa kama.upepo jamani si nitaachika pia kama upepo mieee

   Akanambia  jiandae nakuja kukuoa kesho kutwaa , nataka nitulie na katoto kangu  kadogo dogo ka Dina kangu

Kanaenda kunizalia mtoto wangu🥰🥰🥰🥰🥰

Akashika tumbo langu “kwahiyo mwanangu  amelala humoo ,,hayaa kula basiii mana anasikia njaaa”😅😅

“Nimeshibaa jamani”

“Wakati ulikuwa umenunaaa kula bwana🤗🤗🤗”
   
  Namie mood ikarudi kula kama koteee

MWISHO WA SEASON ONE

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata