INGIZA (20)

INGIZA 20 🔞

Niliondoka pale hospitalini kwa kutoroka, nilifika hadi nje ya geti nikiwa nimeshika simu yangu mkononi.

Nilitembea taratibu mpaka nikafika karibia na nyumbani ndipo nilipoiwasha ile simu

Kitendo cha kuiwasha tu hivi haikupita hata dakika nzima nikasikia imeita, kuitazama hivi ni namba mpya ikabidi nipokee na kuisikilza sauti

“hallow” ilitoka sauti kwa huyo mtu aliyepiga

“hallow” niljibu

“samahani mimi ni Madam Zai, baada ya mume wangu kutufuma aliamua kuniacha, sa hivi niko Dodoma nimeacha hadi kazi ninataka nije nifungue ofisi nyingine huku kama ile ya tanga, kama hautojali upande gari ukuje Dodoma uendelee na kazi yako

“mh” niliguna na kukata simu kwa hasira maana alikuwa ameshaniua lakini nilipokata nilikaa kama dakika mbili tu akanitumia SMS ndefu

“Nimekaa hapo tanga kwa muda wa miaka mitatu nimewaambukiza vijana wengi sana waliopagawa na hili kalio langu, sa hivi nimeamua kuhamia Dodoma karibu na chuo cha Udom nitawakomesha, na wewe kama unataka uje tuwamalize niambie nikutumie nauli usikubali ufe peke yako, UKIMWI hujaumbiwa wewe”

Ile message ilinisikitisha sana, niliwaza kwanini anafanya hivyo, ilichukua takribani siku nzima kuielewa kwamba ana maana gani ndipo name nilijikuta nikishawishika na kumuandikia SMS

“kweli kaka yangu Nick ulimuacha salama”

“hahahaa tena Nick ashanifir….. mara kibao tuko naye huku tunamaliza watu”

“ok sawa nitakuambia”

Sikupenda kwenda Dodoma kama alivyoniambia yule mwanamke nilirudi kwa mage nikamkuta analia sana yuko nje

“Mage” nilimuita kwa huzuni

“usilitaje jina langu muuwaji mkubwa wewe” alisema na kuchukua udongo akanirushia

“mbona unaniita hivyo mpenzi” nilimuuliza lakini nilikuwa nishahisi kwamba ameshashtuka kwamba ameshaambukizwa kitu

“wewe ni wa kuniua na ukimwi mimi?” aliniuliza

Ilibidi nipige magoti na kumuomba msamaha huku nikimtia moyo kwamba ni mambo ya kawaida, japo ilichukua muda kunielewa lakini mwisho alinielewa tukaanza kuishi kwa pamoja na tukaweza kupata mtoto wetu wa kiume sasa hivi ana miaka miwili kasoro, nimeshazoea na ninatumia kuelimisha

Kwa wale wanaosoma udom sa hivi yule Madam Zai yupo pale chuoni anauza Cafeteria anajiita Mama Manka, angalieni atawamaliza

MWISHO

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!