JOGGING MASTER (02)

JOGGING MASTER πŸ’žπŸ’ž2
(Master of LoveπŸ’—)
πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—
Baba Alihifadhi mbuzi watano kwaajili ya elimu yangu ,baba na mama walishirikiana mno kulima kwaajili ya masomo yangu hawakutaka kusikia nakosa kitu chochote huko shuleni ,Kuna wakati walilala bila kula lkn walihakikisha wamenitumia chochote kitu na ninaishi na kujiona wa thamani kama walivyo wenzangu 😭😭😭

Aah nitawalipa Nini Mimi Wapenzi wa moyo wangu 😭😭😭 baba na mama yangu wa thamani kubwa 😭😭😭Mungu awaweke muishi maisha marefu mnoooo mnooooo mushangilie ushindi wangu na mafanikio makubwa mbele yangu kama lilivyo jina langu (Fanikiwa)……..hili ni ombi langu kuuu πŸ™….

Safari ya kwenda dar ilianza taratiiiibu na kwa uhakika ….nilikuwa natizama vile miti inarudi nyuma kila tulipo sogea mbele …..nikapata maana halisi ya earth rotation….kwamba ni kweli Dunia inazunguka na haijawahi kukoma kama tulivyosoma katika Geography ☺️☺️…..

kama ulikuwa unakula mafuta darasani backbencha huwezi kuelewa hili somo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Jiran niliyekaa nae alikuwa ni mama mtu mzima tu alikuwa bize na usingizi hakutaka maongezi yoyote yeye alitaka kulala tuπŸ˜‚πŸ˜‚….
Masaa mengi yalipita muda ulisonga na hatimaye tukaanza kuiacha Hali ya hewa ya Kijiji chetu na kuingia kwenye ulimwengu mpyaaa ….

Mida ya saa sita nilihisi njaa sana nikaona isiwe taabu mama yangu kanifungashia vitu vya asili πŸ˜‚nilifungua mfuko wangu nikatoa pande kubwa la gimbi nikatoa na lile dumu la maziwa nikaanza kutafuna pale …..basi Zima lilijaa harufu nzuri ya magimbi jamn yule mama jirani yangu alishindwa kuvumilia πŸ˜‚πŸ˜‚ aliamka kabisa

“Umeyatoa wapi haya….. nayapenda sana Naomba kipande kimoja mwananguπŸ˜‚πŸ˜‚ ” alinambia nikampa viwili kabisa hahahahaha

na Mimi mwanangu naomba …alikuwa mubaba mtu mzima tu upande wa pili ,nikampatia vipande viwili pia ….πŸ˜‚πŸ˜‚

Sikuwa na kikombe Cha maziwa sasa kila
nilipokabwa na gimbi niliinua dumu langu la maziwa la lita Tano juu na kuguda maziwa mazito ya njano mchambukoπŸ˜‹πŸ˜‹ ……aisee yalikuwa matamu balaaaaa watu wengi walikuwa wakinishangaa wengi walikuwa wanatamani vile namwz gidiii πŸ˜‚πŸ˜‚lkin waliogopa kuniomba …..yule mubaba kaona muuza juice nje akamuita akanunja yule tuvikombe twa plastic tutatu akaomba maziwa πŸ˜‚πŸ˜‚ nikampa ya kutosha ,akampa na yule mama jirani yangu kakikombe nae nikamiminja maziwa aloo waligigida 🀣🀣……watu wengne wananitizama wakidhani Sina akili timamu 🀣🀣🀣 oya wee mm mtoto wa masikini najali basi ?

Niliposhiba tu ndwiii usingizi huooo ukanibeba shwaaaa🀣 nilisinzia mule kwenye basi mpaka nikaskia haya jamani mwisho wa gari ndo huu hapa …aah tumefika dar My God nimefika kwenye city of my dream πŸ˜‚πŸ˜‚

Nilikuwaga naota tu lakin Leo live Niko kwenye ardhi ya Dar nilifurahi mnooooo ..
Pamoja na ushamba wangu lakin nilikuwa na akili sana ,nilijua tu dar lazima ni ngome ya vibaka na kila aina ya uhalifu

Sikushuka kwanza kwenye gari ,nilisubr watu wooote washuke na ndipo nilipomfuata dereva wa ile gari ……

“Shkamoo

“Marahabaaaa pole kwa safari

“Asante ,samahani naweza kulala wapi karibu hapa ambapo nitailipia elfu 15

“Oya Issa mpeleke mdogo angu hapo Rjs akalale alisema yule dereva na mara hiyo hyo alikuja bodaboda mmoja ambae ndo issa sasa akanibeba na kunipeleka huko alikoelekezwa sikuwa na wasiwasi kwamaana nilijua tu dereva hawezi kunichomesha hata kidogo …….

Alinifikisha na nikampatia buku lake ,ni kawaida kwa boda kulipwa buku hata kule Namtumbo Huwa wanatubeba kwa buku kama sehem siyo ya mbali …….

Aliniacha pale lodge na kuondoka zake …….nililipia chumba kwa usiku mmoja ule Huku nikishikilia vema furushi langu la nguo na magimbi nisiibiwe …

Nilioga na kutaka kubadilisha nguo …..nilizitoa kwenye mfuko Ili nivae
Aisee nguo zilikuwa zimeloa balaa πŸ™ zilimwagikia na mchuzi wa magimbi na mahindi 🀣Yan mahindi na magimbi yalichuja maji na kumwagikia kwenye nguo zooote zilikuwa zinanukia mahindi tu πŸ˜‚

Niliishiwa pozi ikanibidi nimrudie yule dada wa mapokezi ….samahani wapi nitafua nguo zangu ?.
Hairuhusiwi kufua hapa kama unataka kufuliwa nguo moja ni elfu tatu ,alisema

Elfu tatu? 😳
hii hii yenye sufuri tatu ?
itaendelea dears

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata