JOGGING MASTER (03)

JOGGING MASTER 💞💞3
(Master of Love💗)
💗💗💗💗💗💗💗💗

“Ndiyo unashangaa Nini sasa ? Mjini hapa
Alinijibu yule mdada ….
Dah sawa Sina namna itabidi nifuliwe gauni moja tu kwaajili ya kuvaa kesho nilichukua gauni moja chakavu tu nikampatia yule dada na pesa yake elfu tatu kisha nikarudi chumbani kulala …..

Nilihesabu kwanza pesa iliyobakia 81000 tu katika ile laki moja niliyopewa na baba 😢😢…pesa inazidi kukatika tu na sijafika hata hapo chuo …..

Kusema kweli nilikuwa nimechoka mnoooo, nilikuwa na usingizi wa viwangooooo nilijitupa kitandani na sikujua kumekucha sangapi hahahha

Niliamshwa na kelele za watu wakiwa wanatiana huko vyumbani kwao 🤣🤣…..
aii ongeza speed chomeka usitoe tamu aiii mamaa aiii….. Eeh jamani ndo makelele hivyo kha ,nililalamika nikiendelea kulala zangu …..

Ilifika saa nne nikaja kugongewa Ili niweze kutoka muda wangu umeisha ….

Niliamka na kuulizia gauni yangu yule dada akasema Bado haijakauka …. Daaah sa nitavaa nn jmn 😢😢nitaondoka vipi hapa ?

Ikanibidi nilipie Tena kwa siku nyingine Tena 😢 …..
Basi hapo ndo nikapata wasaa wa kulala vzr kabisa …nilichapa usingizi mpaka saa Tisa jioni Yan ……

Kilichoniamsha ilikuwa ni njaa tu …..niliamka na kukuta gauni yangu imeshakauka ….nilimuomba yule dada aniagizie ugali na mlenda

“Hakuna mama ntilie hapa kuna mabanda ya chips tu …alisema yule mdada

Nilikubali na kumwambia aniagizie chips na kuku nusu ….. Zililetwa aloo nilitafuna faster hatari na vile ni vitu adimu kuvipata hahahha……

Baada ya pale nilishushia na Maji ya bariiidi nikashibaa kitumbo ndiiiii ,nikamuuliza yule mdada eti chuo Cha (sitakitaja) Kiko wapi ….

Hee huko baharini huko ni mbali hatari Yan kama unataka kwenda jua tu unaanza upya safari 🙄 ,eeeh nilichoka kabisa Yan

Nilikusanya vitu vyangu vzr nikaviweka sawa kwaajili ya kesho asbh tu kukikucha naondoka zangu …..

Basi usiku sikula …wee kahela karibia kanaenda kuisha hata chuoni sijafika 🤣🤣

Nililala zangu usiku na kulivokucha tu saa kumi na mbili huyooo nikaaga na kuondoka …… Nilienda ampaka stend
Niliulizia ulizia kwa watu ambao nilijua tu ni watu na heshma zao wasingenidanganya wakanielekeza nikapanda gari kila mtu ananishangaa tu na mfuko wangu mpaka nikafika huko kilipo chuo 😂😂

Waao ni pazuri mnooo mnooo jmn amazing place pananivutia sana ,nilipokuwa nikishangaa shangaa Kuna baadhi ya wanafunzi walikuwa wakinitizama mnoo

“First year hili ona lishamba hatari ila nalipa miezi sita tu litakuwa liticha la makahaba 🙄🙄
Yalikuwa maneno ya moja wa kijana nilimtizama sana Tena kwa hasira Kwan amenionaje Mimi ? Shetwan mmoja huyu ashindwe kwa jina la Yesu…..

Niliulizia nikapelekwa hadi kwenye uongozi wa chuo ambapo palikuwa na wanafunzi wengi tu design kama yangu 😂 wengi walikuwa na magauni marefu ya vitenge na vitambaa na walikuwa na malemba vichwnani🤣🤣wamejikunyata sana kama vondege vimeloa hahahaha chezea ugeni wewe 🤣🤣🤣

Walinipokea vzr pale tukaandikishwa na tukapelekwa kupewa hostels ……Tuliambiwa
Usajili rasmi utaanza j tatu kwahyo malipo na kila kitu ni juma tatu ….Tulipelekwa huko ziliko hostels tukapewa room kila room watu wanne ….

Aah hatimaye nimefika Asante Mungu sasa naweza kuazima simu na kumpigia baba nimpe taarifa …….

Sikuwa na simu hata kiswaswadu nilitegemea nikipata mkopo nitanunua simu 😂 …..

Samahani dada naomba unigaie simu yako nimpigie baba yangu …….

Aah sawa ,alijibu yule.mdada na kutoa kisimu kidogo kimejaa rababend🤣🤣🤣 ila first year hahahah

Kisimu hata battan za kubonyeza hazionekani vzr yaan kimechoka kuliko hata maisha yangu 🤣🤣 hahahha lakini ana afadhali kuliko Mimi ambae hata hicho Sina ……
Namba ya baba ilikuwa kichwani nikampigia lkin haikuita
Ndugu mteja Salio lako halitoshi kwa sasa ,hahahah kumbe hakuna hata vocha 😂 maskini wakubwa sisi🤣

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata