
JOGGING MASTER (04)

JOGGING MASTER ππ4
(Master of loveπ)
ππππππππ
“Yan Sina hata mia ,wewe kama una jero nunua vocha uweke alisema yule mdada…..
Nilitoka nje palikuwa na wakaka wengi wanauza vocha nikanunua na kurudi hostels ,yule mdada aliunga vocha na kunipatia simu nikampigia baba
Iliita na alipokea
” haloo baba ,
“hee Fanikiwa ulifika salama mama?
“nilifika baba za huko?
“Salama …mama yako hajala tangu ulipoondoka anakuwaza tu ongea nae
Alisema na kumpatia mama simu ambae alifurahi sana kunisikia na kunipa mawaidha mengi sana kuhusu maisha ya mjini ….
Walifurahi sana kunisikia na tuliagana
“Asante sana dada mzuri ,nilimwambia yule mwenye kasimu ……..
“Asante kushukuru alisema na kutabasam ……
“Unaitwa dada nani vile ? Nilimuuliza
” Naitwa dada Maombi” alisema
“Ooh Mimi naitwa Fanikiwa nilimwambia
“Asante kukufahamu natumia nimepata rafiki alisema na tulikumbatiana kwa furaha sana ….
Basi bwana nikawa nimepata rafiki wa chuo wote tukiwa washamba hatari π……
Maisha yalisonga ,niligundua ya kuwa maisha ya Maombi yalikuwa ni magumu kuliko hata yangu π’ …bora hata mm nililala lodge nilipofika yeye alifikia stend na kulala hapohapo alipigwa na mbu balaaa maskini alikuja na nauli na elfu 30 tu ya kula kutoka huko Geita ndani ndani π’π’
Alisema yeye amekuja kimiujiza tu Kwan hata hivyo kusoma kwake kote kulitegemea nguvu zake mwenyewe kwa maana hakuwa na baba wala mama …. bali bibi tu ambae alikuwa ni Mzee sana π’π’
Anasema alitumia muda mwingi kwenye vibarua vya hapa na pale Ili tu wasikose chochote kitu ndani pia alijisomesha kupitia vibarua hivyo π’π’π’π’
Nililia sana bada ya kujua historia yake niliumia sana mimi π’π’ ……..sasa mjini kule tulikuwa wageni na hamna mahali tungesema tutafanya kazi kupata pesa wakat tukingojea majina ya mikopo basi siku tatu tu Maombi aliishiwa pesa na ikabidi sasa mimi nifanye niwezavyo kumsaidia …..
Tulikuwa tunashrrikiana na Kusaidiana , lakini bei ya vyakula na gharama za maisha zilikuwa kubwa sana ,Yan matumizi yalizidi uwezo ….basi Hali ile sasa ikapelekea kale ka pesa ambako nilibakia nako taratiibu kakaanza kukatika ππ
Alooh mpaka kufikia ijumaa Nina buku jero tu π€£π€£
Hatuna pesa kabisa ,nilimpigia simu baba akasema Bado anatafuta mteja wa mbuzi Ili aweze kunitumia pesa nivumilie kidogo tu kila kitu kitakuwa sawa …….
Maombi alisema yeye ni lazima afanye kazi Ili Aishi lasivyo chuo kitamshinda na atarudi Geita kwa mguu π’ ijumaa hiyo tulikula mihogo na hatimaye tukabakia weupeee, tuko teee …yaani apeche alolo hata mia hatuna π€£π€£π€£
Usiku tulilala na njaa π€£π€£ daah sitasahau hakuna hata wa kusema akusaidie kila mtu amekuja kutoka kwao kama huna kitu ni utajijua …..usiku ulikuwa mrefu sana aisee tulipiga mihayo kama hatuna akili nzuri π’π’π€£
Alfajiri saa kumi na mojaaaaa haoooooo tukaamka …..
“Tunafanyaje ,tutoke tukazunguke huku na kule hatutakosa kitu chochote alisema Maombi ….
Tukaoga tukavaa zetu kama kawaida
magauni ya vitenge marefu sana haooo tukaingia mtaaniπ€£ …. Tulifuata uelekeo wa barabara iliyopita kwenye majumba mazuri ya kifahari ya watu huko kuko kimya sana ni matajiri tu na magari yao ndo hupita …..
basi tukiwa njiani tulipishana na mkaka mmoja hivi alikuwa kwenye mazoezi ya kukimbia (jogging) π, mmh tulivopishana nae tu alikuwa ananukia huyo balaaaππ ….
“mmmmh mtu yupo mazoezi na Bado ananukia hivi!”
“Hao ndo wale waliojipata sasa hawana stress na maisha alafu Kuna sisi wanakondoo mawakala wa lusifa walala hoi na walala njaa π€£π€£alisema Maombi ..nilicheka balaaa Yan nilivunja mbavu
itaendelea dears

