
JOGGING MASTER (06)

JOGGING MASTER ππ6
(Amenipendea utoto wangu)
ππππππππ
Mida ni ilele…. njia ni ileile… upande wa barabara ni uleule na mkaka ni yule yule π tukakutana nae Tena kwa mara nyingine πYuko zake jogging π anafanya mazoezi
Safati hii ikabidi nimzingatie vizuri sasa ππ
Kumbe siyo mkaka actually kama tulivomuona alikuwa ni age flani hivi ya 35 au 40 ila sasa very smart and adorableπ …mzuri mnooo jamni kuna wanaume ni wazuri mpaka huwezi kuyazuia macho yako kuwatizama πππ …alikuwa na asili ya weupe flani mzuriii kama yule Pfunk Majani baba Paula ππSi mnajua Pfunk vile nili handsome lile libabaππ
Alafu ndevu zake zilikua kama na vimvi kidogo kwambaali…. kanyoa zake vzr mzuri Yuko very serious Yan jmn lizuri balaa ππ
Wakati Maombi akiwa anapiga mwendo kuwahi kazini Mimi nilisimama kumtizama yula mkaka mpaka alipopotea kwenye upeo wa macho yangu π π€£ π
“Vipi umelewa au ? Umeanza na wanaume mapema yote hii π π Maombi alinisanua hahah
“Maombi yule mkaka ni mzuri jamni duh sijawah kuona jitu zuri namna ile tangu kuzaliwa kwangu πππ
“Usione vyaelea vimeundwa huo uzuri wake ni kwasababu mkewake ameutengeneza sasa na wewe tuliza bichwa utafte mbuzi wako umshepuπ€£π€£π€£
Nilicheka jamni licha ya kuwa Maombi Yuko very smart lakin ana chembechembe za u comedian ndani yake hahaha π€£π€£π€£
“Umejuaje kama ana mke?
“Wewe huoni zile mvi? Kwamba zimetunzwa tu kumsubiri Fanikiwa ?πππ ule mvuto uliouona kwake umetengenezwa tulia utapata nyau wako utamtengeneza wacha kutamani Mali za watu πππ
Dah sikuwa na neno la kuongeza hapo ,Maombi aliongea ukweli mtupu …..
Basi tulifika kazini kwa yule dada etu Ukhty kama kawaida tulipiga chai kwanza alafu tukagawana majukumu ni kazi kazi ,hapa viazi pale vyombo ilikuwa ni kuchangamka tu π ndo kitu kilichotupeleka pale …..ila sasa siku yangu ni kama haikuwa sawa kabisa Leo
Sijazoea kuwa hivi ni kama moyo wangu unaniuma hivi!! Sijui kwann ila nikaona ni kawaida tu labda kwasababu ya njaa ππ napenda sana kula jmn Tena misosi ya huku mjini mitamu Ina mafuta na viungo vingi ππ …….tofaut na kule Namtumbo ni mwendo wa chukuchuku la kitunguu na chumvi tu Tena sometimes no kitunguu ni ndondo chuzi na chumvi tu Yana maharage yanaogelea tu kwenye mchuzi hahahaπ€£π€£ hatarious…..
Tulipiga kazi mpaka jion tukala na kuondoka ……basi hiyo siku ilikuwa tofauti na Jana na asubuhi ….tulipofika kwenye ile barabara
Nilikuwa makini sana kupepesa macho yangu π
Kuangaza huku kule ,sijui nilikuwa natafuta nn ila sijui macho yalitaka kuona Nini ππ, miguu iligoma kabisa kutembea kwa speed pale barabarani,Kuna kitu macho yalitamani kuona ila hayakuona π
Maombi alikuwa mbele yangu kama hatua saba hivi ila mm nilikuwa nyuma yake natembea kama bi harusi mpya π……
“Macho unataka kuona Nini kwani ?ππ niloyauliza macho yangu ila badlucky hayana mdomo yaksshindwa kunijibu π€£π€£π€£ Anyway unachotaka kukiona Leo hakipo kabisa naomba utulie sasa macho acha kupepeseka πππ mida ndo hii ila Leo unachotaka kuona hakipo, hakipo macho hakipoooo ππ
“Wewe endelea kujivuta kusubiri waume za watu wapite unuse harufu zao na kuangalia ndevu zao π€£π€£ ,alisema Maombi akiwa kulembaliπππ
niliwaambia Maombi Yuko very smart anaakili sana kuliko hata mm …alishajua Ninini kinanibabaisha pale njiani ππ ni waume za watu tu π π π
itaendelea dears

