JOGGING MASTER (07)

JOGGING MASTER πŸ’žπŸ’ž7
(Master of loveπŸ’—)
πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—

“Hamna bwana mi hata Sina time nae yule Mzee wanini Mimi πŸ˜•nimechoka tu miguu inaniuma si unaona kilima hiki ni kikali sana …nilisema uongo ila smart gal alishajua kuisoma akili yangu longtime ago 🀣🀣

“Mke wake akikukamata Sina msaada na wewe 🀣🀣alisema Tena Maombi akikaza mwendo jamani hahahahah

“Nilikaa chini kuvunja mbavu 🀣🀣🀣, licha ya kwamba Maombi ni rafiki yangu lakin aisee kanizidi mwaka mmoja Yan ananipa Raha mno huyu mwanamke πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Ni kweli akili yangu ilitamani Tena kumuona yule mwanaume 😌 ila sasa
Leo sijui kateguka mguu πŸ˜‚πŸ€£ mbona hapiti jamni au tayar ashajenga mwili kwa mazoezi πŸ˜‚

Nilijivuta wee mwisho nikaona ujinga huu nikakaza mwendo πŸƒ kumfikia Maombi ambae alikuwa zake bize kutembea Hana time na wanaume yeye ni kazi tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

“Vipi umemkosa mwanaume wa ndiyo zako πŸ˜‚? Maombi aliniuliza

“Hamna bwana mi nilichoka tu Sina muda na wanaume kwa maisha Gani hadi niwaze wanaume ,nilijitetea ila ilikuwa ni uongo mtupu πŸ˜‚πŸ˜‚

“Hahaha hutaki wanaume siyo πŸ˜‚ haya mtu wako Yule paleee πŸ‘‰ amekaa anakunywa maji …..

Alisema Maombi akinioneshea kwa kidole kwenye moja ya duka kubwa hilo la vinywaji la kitajiri lilikuwa upande wa pili wa barabara siyo ule upande wetu …..

“Paaaaaaaap” hivyo ndivyo moyo wangu ulilia 🀣baada ya kumuona yule mwanaume

Na kweli yule mkaka alikuwa pale nje na nguo zake za mazoezi , siyo zile nguo za asubuhi alikuwa kubadilisha πŸ˜‚..amekaa na pembeni yake alikuwepo na mdada mzuri huyo mweupe ni mrembo hatari 😒….. mdada kavaa kisuruali kimembana hicho balaa ….Yule mkaka alikaa kwenye kiti kizuri Cha bembea na alikuwa amekaa akinywa maji taratibuu huku wakipiga story na yule mdada ……. πŸ˜‚

nyie kamoyo kaliniuma nilipomuona yule mdada akicheka na mwaume wangu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜Œ ….nilitamani kumfata yule mkaka pale alipokaa nimsalimie tu alafu niondoke πŸ˜‚πŸ˜‚….


“Haya umemuona mke wake alivyo chombo ? sasa jimix wakukaange chips wakukule πŸ˜‚alisema Maombi

“Hamna bwana mimi wanini yule kwanza ni Mzee Mimi Bado mdogo Maombi siwez kupenda wanaume wakati nawaza chuo πŸ˜‚ ,uongo huoo uongooooo huoooooπŸ˜‚ nafsi yangu ilinisuta huko ndani ilijuwa tu ya kuwa nadanganya kabisaaaa…..

Tuliondoka zetu pale tukarudi hostels tulikula zetu vitu laini na kwenda kulalaaaaa …..usiku usingizi wangu haukuwa mzuri kabisa 😌😌

Akili haikuwa sawa …..sijawah kuvutiwa na mwanaume wa aina yoyote ile mm ila sasa mbona kama πŸ€”…… Aah ana mke yule na mkewake ni mzuri kuliko hata mm cheusi Mangala 😌


Basi akili yangu yoote kwa usiku huo ilikuwa imejazwa na picha ya yule mkaka ,kila nilisinzia tu huyu hapa ….naamka nakumywa maji nikilala tu huyu hapa …alooh ni mchawi au 😒

niliamka nikaomba Mungu anisaidie taswira ya yule mtu itoweke kabisa kichwani kwangu lakini wapiiii …….

Alooh usingizi ulikuwa wa kudonoa sana na kulipokucha sasa ilikuwa ni jumatatu tulivuuuu kabisaaa πŸ˜‚ndo ile siku ya kulipia hostels ,ada na kuangalia majina ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ

Moyo ulikuwa mbio sanaaaaaa niliamka tu na kwenda kuharisha πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Nina preshaaaaaaa tena ya Hali ya juuu πŸ™ŒπŸ™Œ

Cha kwanza ilikuwa ni kushika simu na kumpigia baba…..

“Haloo baba Leo ndo tunalipia hostels kwa semister ni laki na sabini na Sina hata mia hapa nilipo na majina ndo yanatoka Leo niombeeni ndugu zangu nipate mkopo πŸ₯²πŸ₯²……

Baba alisema maneno haya

“Mwanangu Nipo Kijiji Cha jirani imebidi tumchinje mbuzi tumuuze kama nyama kwa wanakijiji ili nipate pesa kwa uharaka zaidi 😒😒naomba Leo tu mpaka jion nitakuwa na pesa ya kukutumia Niko nahangaika majumbani mwa watu kutembeza nyama mwanangu 😭😭
itaendelea dears

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

KIAPO CHA MASIKINI FULL

LOML | Love Of My Life FULL

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL