
JOGGING MASTER (15)

JOGGING MASTER ππ15
(Master of Love π)
ππππππππ
Mungu upo ,Mungu upo sana upo baba Nimeuona ukuu wako baba alisema baba huku mama akilia pembeni πππ
Nilishindwa kuvumilia nilikata simu na kuendelea kulia …
“comeooon Fanikiwa please usilie huu si wakati wa machozi ….nyakati mbaya zilishapita tazama ni wakati wa furaha na kutabasamu Tena……. alisema Maombi alinikumbatia na nikahisi unafuu kidogo moyoni mwangu …..
Alinisindikiza mpaka chuoni nikasajili course zote na kila deni lililokuwepo pale nika clear βοΈ…..yule cashier sasa akabakia kunishangaa tu π³ haelewi nimetoa wapi pesa yote hiyo ya kulipia madeni yote ….
“Wewe si tulikufukuza juzi imekuwaje Leo ume clear ada ya miaka yote mitatu π³ aliuliza yule mhasibu wa chuo
“Siyo Mimi ni Mungu ndo kanilipia ,nilimjibu nikiondoka zangu ….akaishiwa pozi na kunikidolea macho tu π …..
“Sasa rafk angu nisikilize , Jarred ametulipia hotel tuishi huko mpaka pale tutakapomaliza chuo vipi si umekubali tukaishi wote kipenzi changu ? Nilimuuliza Maombi
“Siwezi kukataa π€£ na unalijia Hilo na unajua kuwa nakupenda sana na siwezi kukaa mbali na wewe Fanikiwa πNilimkumbatia na kumuuliza vipi ule mzigo wa chupi umefika ?
Akasema mzigo upo hostel Cha kufanya tuendeleze tulipoishia ππππila Maombi ππ
Basi tulienda hostel tukachukua mzigo wetu kama kawa kama dawa tukaaanza kutembeza pale pale hostel…vile tuna nyota Kali ya biashara tuliuza balaa …yaan ndani ya masaa machache tayari dozen nne kwa siku moja zimekata π³π₯
Yaan biashara ilikuwa tamu ilikuwa ni baraka juu ya baraka nyakati za huzuni zikaishia pale pale …..tulikusanya pesa siku hiyo tukapitia hostel Maombi akawaaga wale roommate wake π€£
we Maombi unaenda wapi umeshapata wanaume Nini mbona unaondoka na mabegi ? mmoja wa roommate wake alimuulizaπ
nimepata mwanaume wa kweli naye ni Yesu kristo mwana wa Mungu π€£π€£π€£ila Maombi π π hahaha
wale wadada wakavunja mbavu kwa kucheka
haooo tukaita zetu tax tukapanda ,yan jeuri ya pesa mpaka tax tukapanda hahaha ilikuwa hot sana ….
Tulifika hadi kule hotel tukaweka mizigo yetu tukooga na kupumzika kidogo story zikaanza …..
Simain kama naishi huku paradise ,jamani Jogging master amekuna wakati sahihi kabisa ..alisema Maombi
.yaan mm naona kama Niko kwenye njozi isiyoisha naona kabisa huyu siyo mtu ni malaika katumwa na Mungu …..
wakati tulipiga story Ile simu ya mezani iliita
nilipokea faster ……
“fungua mlango tafadhali ,sauti ya kike ilisema .
nilienda kufungua na kulikuwa na mhudumu akiwa na mabegi makubwa ya nguo ,
“your order from Jarred alisema yule mdada
nilimpokea yule mhudumu aliaga na kuondoka …….
Maombi alibakia kakodoa tu macho haelewi Yan π
tulianza kufungua begi moja baada ya lingine …..
la kwanza tulilofungua juu lilikuwa na ujumbe
“for You Fenny”π
tukafungua la pili nalo liliandikwa
“for you prayers ( Maombi) “π
yaan tulikuwa so excited tukarukiana na kukumbatiana pale kwa furaha
zile begi zilijaa nguo π yaan na vile tulikuwa tunaendana miili ,zilikuwa nguo Kali mnooo πππ
tulifurahi mpaka tukachanganyikiwa ππππ
nilichukua kisimu Cha Maombi na kumpigia Jarred kumshukuru malaika Yule wa Nuru na matumaini
chaajabu simu iliitia mlangoni ππ
kumbe alikuwa keshafika pale mlangoni
ππππ
itaendelea dears

