
JOGGING MASTER (16)

JOGGING MASTER ππ16Β
(Master of Love π)
πππππππ
Nilipomuona tu Jarred nilimkimbilia na kumkumbatia bila kujali Nipo mbele ya Maombi π
“how can u hide ure feelings to a right and handsome man like Himπ u can’t ….ushamba uliniisha juu yake
“thankyou for everything Jarred’ nilimwambia
” Is my pleasure” alijibu na kunitaka nikakae
nilienda kukaa
alisalimiana na Maombi kisha akakaa kwenye kiti tukaanza stories …..
stories zilikuwa nyingi sana za hapa na pale kucheka na kuvunja mbavu mwisho alituomba twende Lunch mana muda ulikuwa ushaenda ……
tuliongozana hadi restaurant tuliagiza chakula na kuanza kula
lakin tukiwa kwenye kula simu yake ilikuwa ikiita sana na aliipuuzia…….. .simu yake iliita sana na mwisho akaomba akaipokee …..
mmh anaenda kuongea na nani ? labda mkewake ? alisema Maombi ile kauli ilimiuma mno π’ itakuwaje kama Jarred ana mke? lakin hapana hawezi kuwa na mke na akanitendea uzuri namna hii …nilijipa.moyo
Alikaa kama dakika kumi tu then akarudi pale mezani ……aliaga kuwa Kuna sehemu anatakiwa kuwahi na akaahidi angerudi jioni kutuona ….
comeooon please baki kidogo Jarred π’ nilimwambia lakini alisisitiza kuwa ni muhimu awepo huko alikoitwa……sikuwa na namna π’π’π’
Nilimsindikiza mpaka nje huku Maombi akibakia pale hotel …..
tulifika hadi kwenye gari yake …..
sikuwa na furaha kabisa π’
Ingia ndani ya gari ,alinambia nikaingia
aligeukia upande wangu na kunitizama sana ,alinitizama kwa makini mnoo
“Kuna shida?π’ nilimuuliza
“I wish u could be someone’s wife forever π, natamani uwe mke wa mtu milele …alisema
“wifey π? niliuliza kwa mshangao kidogo
“no am joking ….soma kwanza okay , zingatia masomo yako Ili wazazi wako wawe proud na wewe .alisema akitoa wallet yake na kutoa elfu 50 akanipatia …..
“Fenny please jitunze ,usishawishike na yeyote yule one day I’ll tell u something good na utafurahi alisema akiniaga ….
“see u momy” alisema na nilishuka kwenye gari aliwasha ndinga yake na kuondoka , nilibakia mimeduwaa pale pale barabarani nilitizama uelekeo lilikoelekea gari
maneno yake yalianza kuitesa akili yangu hapohapo …nilitamani angeongea maneno mengine zaidi lakin hakuwa na maneno mengi π’ …..
“I wish u could be someone’s wife” anatamani niwe mke wa mtu ,mtu yupi huyo .π€ …mmh mbona sasa hajawa open ,kwa msaada huu anaonipatia natamani afunguke anitake nikubali tu kuwa nae kwa maana nampenda sana π ,nilijisemea nikirudi kwa Maombi ……
“I feel so badπ’…napenda kuwa karibu yake muda wote…. nilimwambia Maombi bila woga wowote
“hahaha” Maombi alicheka , chunguza kwanza usije kuingia mtegoni ukaja kutolewa meno na wenye Mali yao π€£
basi bwana kesho yake asbh Jarred alikuja pale Lodge akanipatia simu nzuri Samsung Kali mnooo akasema tutakuwa tukiwasiliana na nisimpatie mtu mwingine yeyote namba yangu zaidi yake na wazazi wangu na rafiki yangu Maombi π
nilimshukuru mno kama kawaida yangu …..
basi bwana siku zilienda wiki mbili zikakatika huku tukiendelea na masomo yetu pale chuoni ….. Jarred pia hakuacha kuja kututembelea kila alipopata nafasi ……
Ilikuwa ni kawaida yake kila inapofika ijumaa anatupeleka shopping tutachagua mazaga huko hatarious mpaka tunachoka wenyewe ππ
tukitoka hapo tutaenda bitch na sehem zingine nyiingi za kuenjoy ,yaan maisha yetu yalibadilika ghafta from zero to hero ..pale chuoni tukawa ndo maslay queens ,Yan tulikuwa tunapendeza hamna mfano ππ…..
nilinenepa ,Yan ule mwili niliotoka nao Namtumbo kumbe haukuwa wangu bwana πππ mwili wangu ulikuwa mikononi mwa Jarred π€£….aisee maisha so ndo haya sasa ……
wale maroom mates wetu walikuwa wakija pale Lodge kututembelea wakawa wanabakia midomo wazi tu π€£hawaamin macho yao ….
“ni chupi tu ndo zinawapa jeuri ya pesa namna hii ?.
“hapana ni Yesu tu π …hayo ndo yalikuwa majibu ya Maombi kwa yeyote atakae muuliza kuhusu mafanikio yetuπ€£ π…..
kila siku asubuhi na mapema nilikuwa naamshwa na Jarred tunaenda zetu kule jogging π ,Yan nikawa jogging mistress π€£π€£, nikazoea kabisa Yan ,tutakimbia weee tukichoka tunaenda pale dukani kwa yule mdada tunakaa tunapata maji pale ,tukitoka hapo tunapitia restaurant jarred anapenda sana chai ya Nazi ….
Kuna restaurant moja wameshamzoea wakimuona tu wanaleta chai faster Yan π
wanamwita ” quite handsome” Yan ni jitu lizuri ambalo halipendi kuongea ongea. …. huyo ndiyo Jarred…..
Sasa siku hiyo tumetoka kukimbia tupo restaurant tulikuja kuhudumiwa na mdada mmoja hiviπ’ sitasahau hii siku
je ni kitu Gani alifanya na huyo mdada ninani ? usikose sehemu inayofuata

