JOGGING MASTER (24)

JOGGING MASTER πŸ’žπŸ’ž 24
(Master of Love πŸ’—)
πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—
Simu yangu iliita sana sikutaka kuipokea maana nilitaka kusoma tu kwa wakati ule
basi iliita mno nikaamua kuizima kabisa
tukaendelea na discussion na Maombi pale
ila baadae moyo wangu ukawa mzito

mh huyu ninani anapiga simu namna hii

niliamua kuiwasha

please tusome kwanza achana na mambo ya simu alisema Maombi

nikaachana nayo tukasoma wee hadi saa nne hivi tukaamua kulala

nilimpigia simu Jarred na kumuuliza kuhusu Jiden akasema Yuko poa mno na anaendelea vzr kabisa
basi niliamua kuipigia na ile namba pia
lkn haikupokelewa
nikamtumia msg hello mambo nani mwenznangu ?

msg yangu haikujibiwa nikapotezea

tulilala na asbh na mapema tukawahi kujiandaa na kwenda chuoni
tukiwa njiani ile namna ulinipigia Tena

nilipokea

Hallo niliita

“wewe ndo Fanikiwa”

“ndiyo ni Mimi” na wewe ninani mwenzangu?

simu ikakatwa 😳

khe huyu vipi ninani ? nilijiuliza nikampigia Tena lakini ile namba haikupatikana Tena

nilipata hofu sana huyu ninani ?

mh nikaamua kupotezea

basi baada ya pale tulienda kula na kutembeza mzigo wetu wa chupi hostels kama kawaida
tuliuza na badae tukaona tumechoka tulirudi zetu lodge kulala …..


siku hiyo sikuwasiliana kabisa na Jarred asbh tukawahi chuoni ila tulivofika tu nilikutana na kijana mmoja hivi ambae alinichangamkia kupita kiasi

alikuwa ni kijana handsome mno mule mule mwa Jarred 🀣ila sikuwa na mpango nae kabisa

“Aaah Fanikiwa ndo unipite kama mlawi ?
alilalamika kijana yule

samahani kaka angu Mimi sikufahamu

najua ila huu ndo mwanzo wa Mimi na wewe kufahamiana Fanikiwa …..alijibalaguza nikaona anyway si mbaya kumfahamu na kujua shida yake Ninini

“Tunaweza kutoka tukapate japo breakfast ?

“hapana naenda darasani Niko bize mno

“sawa Mimi pia naenda darasani lakin baada ya kipindi naomba tuonane Fanikiwa aLisema

naomba namba yako bas

niligoma kumpa na kumwambia labda yeye ndo anipe yake …hakukataa alinipatia namba yake nikaisev na kwenda zangu darasani

kipindi kilipoisha Maombi anapenda sana discussion akabakia kudiscuss na wenzake hata hivyo alikuwa na kipindi kingine karibuni nikaona nikapate chai tu

nilipofika tu pale canteen mara paap yule mkaka huyu hapa πŸ™„πŸ™„
kajuaje kama Niko hapa huyu vipi ?
nilijiuliza nukikasirika kwann ananifatafata hovyo…..

alikaa na kuanza akijichekesha

naitwa Filbert ,akajitambulisha

“sawa jina zuri ,nilimuangalia kwa dharau sana sijui likoje

mhudumu alikuja nikamuagiza chai na chapati moja tu

“namimi naomba kama Fanikiwa πŸ™„ akasema Filbert

Kwan unataka nn kaka maana sikuelewi kabisa

Haman just friendship tu napenda compan yako ..alisema
okay but mme wangu akikukuta hapa utakuwa ugomvi

mme wako? nani Mr Jarred ? au Kuna mwingine
aliropoka nilishangaa sana kamjuaje Jarred huyu kijana πŸ™„…
“unamfahamu Jarred? nilimuuliza

aah hapa chuoni nani asiyemfahamu yule bwana πŸ™„πŸ™„
khe πŸ™„
itaendelea dears

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BIOLOGY TEACHER FULL

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL

BINTI MDUNGUAJI FULL

error: Content is protected !!