KATOTO KA FORM ONE 🔞 (22)

SEHEMU YA 22
Bila kuongea chochote, Nurat alitoka mbio kuelekea chumbani huku moyo ukimdunda sana.

“Mungu wangu!!! Ndo nimefanya nini?” aliongea kwa hasira na aibu “Mimi nilijua yupo Ommy jamani kaaah!” alizidi kusema huku akiwa ameweka viganja vyake mdomoni kwa aibu “Sasa atanionaje?” aliwaza

Wakati anawaza hayo, pia Baba Denis naye alikuwa akiwaza yake “Huyu ntoto ni shetani au?” alijisemea huku akiwa emeshika tama “Kwanini anafanya hivi huku ndani? Au anampenda Omary? Hapa lazima kuna siri” alitafakari kisha akainuka ili aende chumbani kukaa na mkewe

Ghafla kabla hajaondoka alisikia hatua zikija sebuleni, akageuka na kukuta Winnie. Alipomaliza aligeuza shingo na kuendelea na safari yake lakini hakufika mbali akapata wazo na kumuita
“Winifrida” alisema mzee huyo

“Abee” Binti alisema huku akiibinya midomo kwa ndani na kufanya mashavu yabonyee “Shikamoo baba”

“Marahaba, samahani kwanini huendagi ibadani?”

“Aam….mh aah” alianza kupata kigugumizi ndipo mzee akajikoholesha.

“Anyway, unaonekana hauna sababu ya msingi ila jitahidi uwe unahudhuria” alisema mzee huyo

“Sawa baba”

“Samahani kuna kitu nataka unieleze kwa kina” alisema Mzee

“Kitu gani baba?” aliuliza

Mzee alishusha sauti na kuweza kuongea bila mtu mwingine kusikia
“Hivi Nurat na Omary wana mahusiano gani?” aliuliza

“Heeeh” Winnie alishangaa na kushika kiuno halafu akacheka kwa nguvu

“Ssssh” mzee alimzima “Tumia sauti ndogo”

Sasa kumbuka Winnie ana bifu na Nurat hivyo aliitumia ile fursa vizuri
“Sawa, acha nikueleze…..huyu Nurat muda mrefu yuko katika Mahusiano na Ommy…..mbaya zaidi pia yuko na Denis, anawachanganya” aliamua kumwaga mchele

“Jesus!!!” Mzee alishtuka

“Ndio hivyo, hapa hatoweza kufaulu kwani kwanza ana simu kubwa nimekuta akiwatumia picha za uchi wanaume mtandaoni?”

“Winifrida……are you serious?”

“Yes”

“Kwanini hukusema?”

“Sikupata nafasi ya kusema” alisema na kuondoka zake, lakini alimuacha mzee mdomo wazi anashangaa

Mzee alipagawa ikabidi aende chumbani kujadili na mkewe…..JE ITAKUWAJE? WATAMNYANG’ANYA SIMU?
USIKOSE

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!