KATOTO KA FORM ONE 🔞
SEHEMU YA 29
“Ngo ngo ngo ngo…” Sauti ya mlango ukigongwa ilisikika usiku saa sita katika chumba cha Denis.
Denis alikuwa hajasinzia bado, alikuwa anacheza na simu yake. Alishtuka
“Nani??” Aliuliza
“Fungua, mi Nu….” sauti ilisikika ikiwa ni ya kunong’oneza
“Mh, kuna nini?” Aliuliza Denis huku akishuka kitandani na kuangalia boxer yake imetuna
“Njoo….! Please fungua kwanza”
Denis hakuwa na kipingamizi, alijuaga huyo mtoto anampenda hivyo kwa akili zake za usiku alijua kabisa ameletewa kitumbua.
Alisogea mlangoni na kufungua halafu akatazama kweli ni nurati, ila siku ile hakuwa na khanga moko, alikuwa na track suti.
“Kaka Denis” Alisema huku akiingia ndani na kurudishia mlango
“Nini?”
“Nimechoka” Alisema binti
“Kwanini?”
“Naondoka kwenu mama ananitesa, nataka simu yangu mi nirudi kwetu”
“Kwa hiyo unanieleza kama nani?” Aliuliza
“Naomba uniibie simu hiyo, ipo kule chumbani kwa mama please nisaidie niondoke” alisema binti na kumkumbatia Denis huku machozi yakimtoka “Nisaidie please, mi nitakupa” alisema mtoto wa kike
“Nipe kwanza” Alisema Denis
“No mpaka uniletee, ukiileta tu, nataka tutafute mahali nikakupe usiku mzima”
“Mh kweli?” aliuliza
“Ndio”
“Sawa kesho wakienda kanisani tu napita nayo”
“Sawa usinidanganye sawa?” aliuliza na kumtazama usoni Denis akatikisa kichwa, kukubali.
Nuu alinyanyua visigino na kumbusu mdomoni halafu akamuachia na kuondoka zake
*
Asubuhi na mapema mama Denis aliamka na kujiandaa kwa ajili ya kwenda ibadani. Ilikuwa saa 11.
Ba Denis naye aliamka akawa ameishika ile simu ya Nurat akaitazama kwa muda mrefu halafu akatoa betri na kuweka Memory kadi akanakili vitu vyote vilivyokuwepo kisha akatoa memory kadi yake na kuiweka kwenye begi kisha akarudisha simu pale pale ilipokuwa.
Baada ya dakika kadhaa tu mama alirudi mzee naye akaenda kuoga. Baada ya kuoga alijiandaa vyema ili waweze kuondoka kwenda ibadani.
Walitoka wote wawili baada tu ya kutoa maelekezo kwa msichana wa kazi kitu cha kufanya.
Kwa bahati mbaya baba alikuwa mtu wa mwisho kufunga mlango akawa amesahau ufunguo kwenye kitasa ukining’inia kisha akatoka na kupanda gari yake na mkewe kuelekea kanisani.
Walipofika kama meta 60 hivi, mzee alianza kupata maumivu makali ya tumbo, tumbo lilimsumbua sana akawa anajisikia kuhara.
“Aiiiiii…..Mungu wangu…….aiseee!!!” alisema baada ya kupaki gari na kujishika katika tumbo lake, “Mke wangu auwii”
“Nini tena ba Denis?” Aliuliza mama yule
“Turudi!!!” Alisema huku akijisokota na kulishika tumbo
“Tatizo nini?”
“Tumbo linanisumbua najisikia kuendesha!!” alisema
“Shindwa katika Jina la Yesu huyo ni shetani hataki ukasali” alisema mama yule
“Haaaaah” mzee alifungua mlango wa gari na kuondoka akikimbia kurudi nyumbani ili akapate huduma chooni
“Unaenda wapi sasa?”
“Nisubiri au tangulia nitakuja na pikipiki mke wangu” Alisema mzee huku akikimbia sana
“Mh” mama aliguna, hakujua imekuwaje mtu kuumwa ghafla, ilibidi amsubiri
Mzee alikimbia akaingia hadi chooni na kujifungia, hakuna mtu aliyejua kama karudi.
Muda huo huo, Denis alitoka chumbani kuelekea chooni ile anapita mlangoni kwa mzee, ufunguo unaning’inia
“Eeh!!!” alishtuka kidogo “Wamesahau ufunguo?” alijiuliza na kuita “Mama……mama……Baba…..baba?” Alisema Denis
Baba Denis aliisikia sauti hii lakini hakuitika akiwa chooni. Denis akasogea na kuchungulia nje gari haipo akajua wameondoka na wamesahau ufunguo.
“Daaah” alisema kwa furaha na kufungua ule mlango akazama ndani na kwenda kuchungulia ndani.
Hakuchukua muda katika upekuzi wake aliipata simu
“Huyu mwanaume haji? Mi naenda mwenyewe mfyuuu!” Mama alisema kwa hasira na kuwasha gari anataka aondoke.
Ghafla alipata kumbukumbu kwamba Winnie alimpa onyo kuwa mumewe yuko hatarini kutekwa na Nurat hivyo awe makini.
Aligeuza gari kama mshale akijua ni michezo inachezwa na mumewe ili amsaliti
*
Denis naye alikuwa anatoka katika chumba cha Mama yake akiwa na simu mkononi ya Nurat ameshaipata anampelekea kwa shangwe.
Ghafla bin voo…. Mzee akatokea chooni na kumbamba akiwa anafunga mlango na simu mkononi
“Eh….eh……eh…….Denis” Alisema kwa hasira baba Denis
“Baba…..”
“Huko chumbani kwangu umetoka kufanya nini?” Aliuliza kwa hasira zaidii
“Ah…..ii nilik……..Nilikuwa……nilikuwa naangalia kama mmesahau…..ku….ku”
“Na hicho ulichoshika mkononi nini?” aliuliza na kumsogelea akamshika mkononi kuna simu “Hii simu si ile ya……eh? Hii si ya Nurat hii?” Aliongea kwa sauti ya juu hadi Nurat akashtuka na kutoka chumbani akaenda mpaka pale kwenye korido.
Ba Denis alimpora Denis ile simu
“Samaha…..” Alisema
“Hii simu tumemnyang’anya mwanafunzi halafu wewe unaleta mapenzi unaenda kumchukulia ili aendelee kuharibika?” Aliuliza mzee kwa hasira “Huu ndo ujinga mnaoufanya ndo maana hamtaki kwenda ibadani sio?” Aliuliza
“No…..baba…..”
Ghafla mama naye akafika, mzee kumuona aliipiga ile simu chini PAAAAAH ikapasukia kule
“Mungu wangu…..Jamani simu yangu….!” Nurat alisema kwa uchungu huku macho yakimtoka
“Pumbavu nyie” alifoka
“Nini tena mume wangu?” Mama aliuliza
“Si hawa watoto nakuta eti Denis anaiba Simu akampatie Nurat wakati sisi tumeichukua sio wajinga” Alisema mzee yule na kumgeukia Nurat, nurat haamini kilichotokea, simu imepasuliwa.
Aliketi chini puu akiwa amelegea kwa kukata tamaa. Kilichomsubirisha pale nyumbani siku zote ni ile simu, aliamini akiipata anaondoka.
Mzee alimfuata na kuchuchumaa akamfokea
“Uache ujinga unapaswa usome, kama hautaki ondoka urudi kwenu sihitaji uharibikie kwangu….mpumbavu wewe” alisema mzee na kumtikisa Nurat kwa Nguvu akiwa amemshika begani halafu akamtazama usoni binti analia.
Baba Denis alimkonyeza binti mara mbili na kumbinya mkononi halafu akainuka kwa hasira na kutoka nje
Mkewe alimfuata wakaenda Kanisani
JE ITAKUWAJE? USIKOSE SEHEMU YA 30
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU