KIAPO CHA MASIKINI (01)

SEHEMU YA 1

MWANZO: Ilikuwa ni jumapili iliyochangamka, kama ambavyo ungeweza kuona nje ya eneo la kanisa katoliki, la mtakatifu Telesia lilivyofulika watu, walio gubikwa na nyuso za furaha, huku kanisa nalo likiwa limepambwa kwa mapambo mbali mbali, kwenye madirisha na milango yote ya kanisa, pia magari sita ya kifahari, yenye kupambwa mauwa na Maputo ya rangi mbali mbali, yalionekana yakiwa yamepambwa vizuri sana.
Ebu sasa tuingie ndani ya kanisa ili, ambako sasa vilisikika vinanda vizuri vyepesi, huku watu waliokuwepo mle ndani, ya kanisa, wakiwa katika hali ya utulivu, wanatazama mbele ambako walionekana maharusi wawili waliopendeza katika mavazi yao ya harusi, huku bwana harusi mwenye kuvalia suit nyeusi, akifanana kimavazi na mtoto mdogo wa kiume mwenye umri wa miaka miwili, na miezi mitatu, alie simama jirani na mtoto mdogo wa kike mwenye umri unao lingana nae.
Mala vinanda vikakoma, na utulivu ukatawala, hapo Padre akasogea mbele ya maharusi, “ikiwa matangazo matatu ya ndoa hii yalisha tangazwa na hakutokea mtu yoyote mwenye pingamizi, na sasa kabla ya kukamilisha agano ili landoa, nafasi kwa mala ya mwisho, kama kuna yeyote ambae anapingamizi kuhusu ndoa hii, ajitokeze, maana ikipita agano ili, hakuna atakae weza kuitengenisha ndoa hii, ipokuwa mungu pekee” alisema Padre, na hapo ukafwata ukimya mfupi, huku watu wakiwa na nyuso za tabasamu, niwazi hawakujuwa kinachofwata.
Lakini ghafla ukasikika ukulele toka kwenye mlango wa kuingilia ndani ya kanisa, “pingamizi!! Jamani pingamizi, naomba msaidie” ilikuwa ni sauti kali yakike iliyojaa maumivu, watu wote waigeuka kutazama kwenye ule mlango ulikotokea sauti ile, na hapo waliweza kumwona mtu ambae kila mmoja alisisimkwa na mwili kwa mwonekano wake, maana alikuwa amefungwa POP, kwenye mkono wa kulia na mguu wakushoto, pia bandage nyingine ilifungwa kichwani kwakuzunguka kichwa chote, akitembea kwa kujikongoja akisaidiwa na gongo flani la mti, lililoonekana wazi kuwa alikuwa ameliokota sehemu, niwazi mwanamke huyu, alikuwa amepatwa na hajari au kipigo toka kwa kundi la watu wabaya, “huyu ni mume alinitelekeza na kuja kuowa mwanamke mwingine” kwa kauri hiyo hapo, ukasikika mguno wa uzuni, kutoka kwa watu karibia wote mle ndani, huku wanageuka kumtazama bwana Harusi, ambae sasa alikuwa anamtazama yule mwanamke, ambae alivalia mavazi chakavu, yenye halama ya damu, iliyokauka, ambae uso wake ulionekana kupondeka pondeka, kwa kipigo au ajari aliyo ipata, ambae sasa alikuwa anazidi kulisogelea madhabauni, kwa mwendo wa kuchechemea, “naomba ndoa isifungwe, nipewe mume wangu tuondoke” alisema yule mwanamke ambae kila alipoondoka alionekana kupatwa na maumivu makali, nazani pia aliumia sehemu za mbavu.
Naam hapo Padre akamtazama bibi harusi, ambae muda wote, alikuwa ametulia, huku anamtazama yule mwanamke, kama vile alikuwa anamfahamu, na wala hakuwa na wasi wasi nae, Padre akamtazama bwana harusi, ambae kiukweli ilimuwia vigumu, kutambua alikuwa katika hali gani, maana wakati macho yake yalikuwa yana mtazama yuke mwana mke huku tabasamu likishamili usoni mwake, pia macho yake hayo hayo yalikuwa yana tililisha machozi, “kweli nimeamini KIAPO CHA FUKARA hakina nguvu” alinong’ona bwana Harusi, kwa sauti ya chini kabisa, huku akimtazama mwanamke huyu alie chakaa akizidi kusogea madhabauni.
Huyu anaitwa Peter Jacob, sijuwi ilikuwaje akamtelekeza mke wake na kuja kufunga ndoa, na sijuwi kwanini anasema kuwa kipao cha fukara hakina nguvu, basi jiandae kupata mkasa huu wa kuburudisha kuuzunisha na kufurahisha

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata