
SEHEMU YA 2
ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA: Naam hapo Padre akamtazama bibi harusi, ambae muda wote, alikuwa ametulia, huku anamtazama yule mwanamke, kama vile alikuwa anamfahamu, na wala hakuwa na wasi wasi nae, Padre akamtazama bwana harusi, ambae kiukweli ilimuwia vigumu, kutambua alikuwa katika hali gani, maana wakati macho yake yalikuwa yana mtazama yuke mwana mke huku tabasamu likishamili usoni mwake, pia macho yake hayo hayo yalikuwa yana tililisha machozi, “kweli nimeamini KIAPO CHA FUKARA hakina nguvu” alinong’ona bwana Harusi, kwa sauti ya chini kabisa, huku akimtazama mwanamke huyu alie chakaa akizidi kusogea madhabauni….ENDELEA….
Kanisa lilizizima kwa mshangao na taharuki, kwa kile walicho kiona, ambacho nikitu adimu sana kutokea, yani kuwekewa pingamizi katika ufungaji wa ndoa, waliomfahamu bwana harusi yani Peter Jacob, walishangaa sana, kusikia kuwa alitelekeza mke na kujakuowa mwanamke mwingine, minong’ono ilitawara ndani ya kanisa, watu wakiulizana kulikoni, aikujarisha kama mtu unae mwuliza unamfahamu au mme kutana na nae mle mle ndani ya kanisa, lakini hakuna alie onekana kuwa jibu sahihi, la kwanini bwana harusi alimkimbia mwanamke huyu, ambae anaonekana kuwa katika wakati mgumu sana, na kwenda kufunga ndoa na mwanamke huyu mrembo mwenye sifa za kuitwa mzuri, ambae sasa alikuwa simama nae madhabauni, ambae pia alionekana kumtazama mwanamke mlalamikaji, bila wasi wasi wowote wala dalili ya mshangao, ilo pia lili washangaza watu waliokuwepo mle kanisani, maana walitegemea kuona pengine akiangua kilio au kuanguka na kuzimia kabisa.
Naam wasaidi na wafanyakazi wa kanisa, walimsaidia mwanamke yule alie onekana wazi kuwa alikutwa dhahama siku chache zilizopita, dhama ambayo watu wengi walihisi kuwa ni mkong’oto kutoka kwa bwana Harusi, yani Peter, walimpeleka mbele kabisa ya kanisa, yani karibu na pale walipokuwa wamesimama maharusi na wasimamizi wao, wale watoto wadogo wawili, ambao mikononi mwao walikuwa wameshikilia maua pamoja na Padre ya ni kasisi, ambae ni kama bado alikuwa katika msahangao, “nina pingamizi padre, huyu Peter ni mume wangu, tuna mtoto mmoja, naomba usifungishe hii ndoa” alisema yule mwanamke, na hapo bwana na bibi harusi wakatazamana, pasipo kusema lolote, alafu Peter akamtazama yule mwanamke ambae alikuwa amesimama karibu kabisa na paroko, yani Padre, “Sada unaona aitoshi na sasa unaisaka roho yangu?” aliuliza Peter ambae bado macho yalikuwa yana tililika kwa uchache machoni mwake, kabla yule mwanamke aja jibu, alie tajwa kwa jina la Sada aja jibu, padre aka mwuliza Peter kwa mshangao, “Peter unamfahamu huyu mwanamke, na anacho sema ni kweli?” swali la Padre ni miongoni mwa maswali ambayo ylitawara vichwa vya watu wengi pale ndani, hivyo wakatulia kusubiri jibu.***
Miaka miwili iliyopita, juma mosi moja ya mwezi wa kumi na mbili, siku tatu kabla ya mwaka mpya Saa moja na nusu usiku wingu zito lilikuwa limetanda nakusababisha giza kuwa nene sana, upepo ulikuwa unavuma kwa nguvu, ukiambatana na mvua kali, ambayo ilikuwa inayumbisha miti ya miembe, na misuku, na kudosha matunda ya miti hiyo pasipo kujali kama ni mabivu au mabichi, na kilomita moja, nje ya kijiji cha Mwanammonga, mwanamonga kama unavyoweza kutamka, kilichopo nje kabisa ya wilaya ya namtumbo, ndani ya msitu, pembezoni mwa milima ya Ngooko, alionekana kijana mmoja aliekuwa anajitaidi kukimbiza baiskeri yake, kuelekea kilipo kijiji, cha mwanamonga, kwenye kitako cha nyuma cha baiskeri akiwa amefunga jembe, na mihogo kadhaa mikubwa, baskaeri chakavu ilikuwa ikipiga kelele kwa msagano wa vyuma vyake, vilivyokosa kilainishi, japo msimu huu, alipanga kutumia baadhi ya fedha alizopata kwenye malipo ya tumbaku kuirekebisha baskeri yake, ambayo nimsaada mkubwa kwake na familia yake ya mama na mtoto mmoja, na ndio usafiri ambao unamsaidia kulifikia shamba lake la ekari tano, lililopo umbali wa kilomita nane toka kijijini.
Hakika kilicho saidia ni uenyeji, na ufahamu wa kila sehemu ya njia hii afifu, maana kwa giza lililo kuwa limetanda, hakika asifika mbali angekuwa amesha vamia miti na majabari makubwa yam awe yaliyo tanda pembezoni kwa jikinjia hiki, maana mwendo wake ulikuwa mkali sana, shati lake lililo chanika na kupoteza rangi harisia kwa uchafu na uchakavu, lilipepea nyuma yake, na kuwa na bendera.
Dakika saba baadae tayari kijana huyu, alikuwa amesha anza kuziona nyumba za kijiji chao, akazidi kunyonga pedeli za baiskeri hii chakavu, ungesema ndio anaanza safari yake, mwa nguvu na speed aliyo kuwa akitumia, usinge fikilia kuwa kijumba chake cha udongo kilikuwa mita mia mbili tu, toka pale alipokuwepo, yani mwanzo kabisa mwa kijiji, upande huu wa njia za kwenda mashambani.
Kijiji kilikuwa kimefunikwa na giza nene, mvua ndio kwanza iilikuwa kama ndio inaanza upya, ilikuwa ina nyesha kwanguvu, ardhi ilikuwa imeshiba maji na kuanza kuya tapika, yakaonekana yakitembea kwa kasi kwenye mifereji yake, ikibeba baadhi ya vitu vilivyo sahaulika nje, mfano vyombo vya kupikia na nguo zilizo anikwa, hakuna mtu alie onekana akizagaa nje ya nymba yoyote pale kijijini, kwa kuofia mvua hii kubwa ambayo matonye yake ungezania kuwa ni mawe madogo madogo, yalitiliishwa toka mawinguni.
Mpanda baskeri alisimamisha baskeri yake nje ya kijumba kimoja kidogo cha udongo, kilicho gubikwa na giza nene nje na ndani, kijumba ambacho alikiacha saa kumi na moja alfajili, wakati anawai shambani, shamba ambalo lipo kilo mita nane toka pale kijijini, giza lile liliashilia kuwa ndani hakukuwa na mtu, lakini mawazo yake hayakuwa sahihi, maana wakati anafungua jembe na mihogo nyuma ya baskeri, akasikia kilio cha mtoto toka ndani ya kibanda kile kibanda, kijana akashatuka na kuacha kile alichokuwa anakifanya, akausukuma mlango dhaifu wa kibanda kile na kuingia ndani, ambako alikutana na giza nene, sambamba na kilio mfululizo cha mtoto, “nyama za Michael baba yupo hapa, nyamaza mwanangu” alisema kijana huyu, huku ana papasa upande wa kulia ndani ya kibanda kile, na kwakuwa alikuwa alikuwa anamfahamu vyema mle ndani, ambako ni chumba kimoja, akuchukuwa muda mrefu kuipata meza, ambayo aliipapasa kwa sekunde chache na kuibuka na simu ndogo, akajaribu kuiwasha, lakini aikuwaka akumbuka kuwa wakati anaondoka asubuhi, ilikuwa na chaji ndogo sana, wakati huo bado Michel alikuwa anaangua kilio, kijana huyu akasogea kwenye dirisha lililozibwa na vipande vya mabati chakavu, na kupapasa kidogo akaibuka na kiberiti, kisha akakiwasha na kwenda kuwasha kibatari, ambacho kiliondoa giza mle ndani na kuweka nuru katika macho yao, wote wawili ambao sasa waliweza kuonana, “Michael mama yupo wapi?” aliuliza kijana huyu, huku anamsogelea mtoto, mwenye mwaka na miezi sita, alie kuwa kwenye kitanda kidogo cha mbao, akionyesha kuwa alikuwa ametoka kuamka, mtoto Michael akujibu kitu zaidi ya kushangaa, “na kijana huyu nikama aka kumbuka kuwa mwanae asinge weza kumjibu lolote, maana licha ya kutoka kuamka, pia akuwa na uwezo wa kuelewa mama yake yupo wapi kwa muda ule.
Naam kijana huyu anaitwa Peter Jacob, kijana mchapa kazi mwenye nguvu, heshima na upendo, kwa kila mmoja, pale kijijini, tofauti na vijana wengine, Peter alitumia muda mwingi shambani, kufanya shuguri za kilimo, mabinti wengi walipenda kuishi nae kutokana na uchapa kazi wa kijana huyu, mwenye mwili uliojengeka kimazoezi, kutokana na kazi ngumu, na sura ya upole, ambae mwaka mmoja ulio pita baada ya kumaliza masomo yake ya kidato cha nne alikutana na Sada Nyoni, ambae pia alikuwa ametoka kumaliza kidato cha nne, miezi michache iliyopita, ukweli ni kwamba, Sada kipindi hicho alikuwa ni mschana pekee pale kijijini, alie onekana ni bora zaidi kuliko mabinti zote, na alikuwa mfano bora kwa wa wanafunzi wote walio maliza darasa la saba katika shule ya msingi Mwanamonga, maana yeye ndie alie kuwa mwanafunzi wa kwanza kufauru, na kuchaguliwa kwenda kusoma secondary ya serikali, ya waschana huko songea mjini, huku wenzie akiwepo Peter walienda kujiunga kwenye shule ya Nandungutu, inayo milikiwa na jumuhiya ya wazazi wa mkoa wa ruvuma, iliyopo wilaya ile ile ya Namtumbo, huku mwenzao Sada alienda mjini, ambako alifanikiwa kumaliza masomo yake na kuja kijijini kusubiria matokeo yake.
Kipindi anasubiria matokeo ya mitihani, ambayo siyo tu wazazi wake ata ndugu jamaa na marafiki waliamini ange fauru, ndipo ilipo bainika tabia yake ya kuwa mwepesi wa kutoa kitumbua chake kwa wanaume wenye uitaji, akuchagua mke wamtu wala umri, yeye alicho tazama nni kwamba anapewa fedha aliyo aidiwa na mwanaume huyo, na ukweli akuweza kudumu na mwanaume yoyote alie tembea nae, leo ungemweona yupo na huyu, na kesho angekuwa yule, na keshokutwa mwingine, bahati nzuri wanaume nao walimzowea na hawakuoneana wivu, ata muda ambao amatokeo yalitoka ni mwanafunzi mmoja tu kati ya kumi na mbili wa kijiji kile, walio maliza sekondari mwaka ule, ndie alie fauru kwa alama ndogo ya division four ya ishilini na tisa, huku wengine wote wakipata division ziro, jambo ambalo liliwashangaza sana watu, ambao walitegemea kuwa Sada angefauru, na kuendelea masomo yake ya kidato cha tano na sita.
Kitendo hichi kilikuwa kichochezi kikubwa kwa Sada, kuendelea kugawa sukari pale kijijini, na vijiji vya jirani, na aikuchukuwa muda mrefu watu kumdharau na kuanza kumkwepa, kiasi cha kuanza kuchakaa na kuonekana kituko, pengine Jacob hakulitambua ilo, kutokana na kutumia muda mwingi kushinda shambani, ikiwa ni maisha aliyo jichagulia, na ata siku aliyokutana na Sada, binti wa mzee Nyoni, ambae alionyesha wazi kuitaji ifadhi ya kijana huyu mchapa kazi, na yeye Peter baada kuona dalili hizo, akajielezea kuitaji penzi la Sada, ambae kama ilivyo kawaida yake akuruka kiunzi ata kimoja, na kujikuta wakiingia kwenye penzi, ambalo miezi mitati baadae lilileta matunda, ya ujauzito, na kuamua kuliweka wazi penzi lao, kwa kuwajulisha wazazi wao, na kuwaeleza kuwa wameamua kuishi pamoja.
Wazazi wa Sada hawakuwa na pinga mizi, tena walifurahi sana, kwa kuona kuwa binti yao ameokota dodo chini ya mpera, maana akuwa na sifa za kuolewa na kijana mchapa kazi kama Peter, ambae kila mzazi angependa binti yake aolewe nae, kikwazo kilikuwa upande wa wazazi wa Peter, asa mama yake, ambae alipinga vikari Peter, kumuoa Sada, ambae kiukweli, alikuwa na sifa mbaya sana, pale kijijini, lakini kwa kuzingatia ujauzito aliokuwa nao Sada, nauo ndio ulikuwa mwanzo wa wawili awa kuanza kuishi pamoja, kama mke na mume kwenye kibanda kidogo, cha udongo kilichoezekwa kwa bati chakavu…endelea…..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU