KIAPO CHA MASIKINI (03)

SEHEMU YA 3

ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI: Wazazi wa Sada hawakuwa na pinga mizi, tena walifurahi sana, kwa kuona kuwa binti yao ameokota dodo chini ya mpera, maana akuwa na sifa za kuolewa na kijana mchapa kazi kama Peter, ambae kila mzazi angependa binti yake aolewe nae, kikwazo kilikuwa upande wa wazazi wa Peter, asa mama yake, ambae alipinga vikari Peter, kumuoa Sada, ambae kiukweli, alikuwa na sifa mbaya sana, pale kijijini, lakini kwa kuzingatia ujauzito aliokuwa nao Sada, nauo ndio ulikuwa mwanzo wa wawili awa kuanza kuishi pamoja, kama mke na mume kwenye kibanda kidogo, cha udongo kilichoezekwa kwa bati chakavu…endelea…..
Kipindi chote cha ujauzito Sada alikuwa mtulivu katika penzi lake na Peter, huku Peter akifanya kila analoweza ilikuakikisha mke wake anapata anacho itaji, ikiwa ni milo mitatu, chakura bora kwa mama mjamzito, pamoja na mavazi mazuri ya kupendeza, hakika Sada alijiona kama vile amechelewa sana kuingia kwenye maisha ya Peter, maana sasa alianza kupendeza na kunawili, akafanana na wonekano wa wanawake wa mjini, ambao alikuwa anatamani kila siku kuwa kama wao, alijisikia raha sana, maana kwa miaka minne ambayo Sada alikuwa mjini akisoma, alipenda sana kuwa kama wakina mama wale, na kuifanya kuwa ndoto yake kwenda kuishi mjini, huku akitaka kufanana na wanafunzi waliotokea pale mjini, kitendo kilicho mpelekea kujiingiza katika mausiano holela ya kipenzi, akitafuta fedha ndogo ndogo, za kumsaidia kununua nguo za kisasa ambazo, zingamfanya na yeye aonekane wa mjini, hakika ilikuwa hakiri ya kitoto, ambayo aliachana nayo, baada ya kumaliza shule na kurudi kijiji.
Maisha yalikuwa ya furaha muda wote wa ujauzito ata Sada alipojifungua, mume wake alimpatia zawadi ya simu nzuri ya kisasa, yenyeuwezo wa kutumikisha mitandao ya kijamii, huku yeye akibakia na simu yake ndogo maarufu kama kitochi, unaweza kujiuliza walikuwa wanachaji wapi simu zao wakati walikuwa wanaishi kwenye kijiji ambacho hakikuwa na umeme, ukweli ni kwamba pale kijijini kulikuwa na maduka matatu ambayo yalikuwa na umeme unaotumia nguvu za miali ya jua, hivyo wanakijiji walio bahatika kuwa na simu walikuwa wanachaji hapo, ni pamoja na wakina Peter na mke wake.
Mwaka mmoja baada ya kuzaliwa kwa mtoto Michael, mambo yalianza kubadirika ndani ya nyumba hii ya bwana Peter, ugomvi mdogo mdogo na mke wake aukupungua ndani ya nyumba yao, mfano mmoja kati ya ugomvi wao ulikuwa ni kuhusu kujenga nyumba kubwa na nzuri, kama Peter asingetoa maelezo mazuri kuhusu mipango yake nazani wangeachana, “mke wangu tumeuza tumbaku, nyingi mwaka huu, naimani kuwa tutapata fedha nyingi sana, msimu wa malipo, tuta jenga nyumba na kurekebisha baadhi ya mambo ambayo tunaitaji kurekebisha” Sada alimewelewa Peter na kutulia kwa muda mfupi kabla aujaibuka mgogoro mwingine, ambao ulisababishwa na mawasiliano ya mala kwa mala kwa njia ya mitandao ya kijamii, yaliyofanywa na mke wake, asa nyakati za kulala, huku mama Michael akiwa mkali sana pale Michael alipo itaji kutazama baadhi ya burudani kwenye simu ya mke wake, walikuwa wanafanya hivyo hapo mwanzo, “siununue simu yako bwana, we ulisikia wapi simu wanapeana” alikosoa Sada, ambae muda wote alionekana akipokea na kutuma ujumbe.
Kuna siku Peter akiwa anatoka kushukuwa simu dukani, ilikokuwa inachajiwa, akajaribu kuifungua simu ya mke wake, ambako alikutana na neno la siri, lililomzuwia kuitumia simu ile, kitu hicho kilimpa mawazo sana Peter ambae alianza kuhisi kuwa mke wake anambo flani yasiri anayafanya, hivyo akapanga kumchunguza mke wake, lakini akajipa moyo kuwa yalikuwa ni mawazo potofu.**
Ebu tuachane na historia fupi ya wawili awa, na tuja siku hii ya mvua kali, ambayo Peter aliondoka mapema kuwai shambani akimwacha mke wake na mtoto wa Michael akiwa amesha timiza mwaka na nusu, na nisiku nne toka kijana Peter atoke namtumbo na mke wake bi Sada nyoni, kupokea malipo ya mauzo ya tumbaku aliyoiuza toka mwezi wa saba, ambapo alilipwa million saba, na laki nane, ikiwa ni malipo ya awamu ya kwanza akibakisha million tatu na laki tano za awamu ya pili ambayo alitegemea kuipata miezi sita baadae.
Mvua iliendelea kuchamanda kwanguvu, Peter hakuwa na wasi wasi juu ya mahali ambako mke wake alipokuwepo, alimini kuwa pengine alikuwa ameenda kuschukuwa simu na mvua ikamkutia huko au alikuwa amepitia kwa wazazi wake, hivyo anasubiri mvua ipungue ndipo arudi nyumbani, japo alishangazwa na tabia ya kumwacha mwanae mdogo pale nyumbani, aikuwa tabia yake hapo mwanzo.
Mvua ilikoma saa nne kasoro, Peter akatarajia kumwona mke wake muda wowote kuanzia saa nne hiyo, lakini aikuwa hivyo, maana masaa mawili yalikatika pasipo kumwona mke wake wala dalili ya mke wake kurudi, hakuwa na wasi wasi wowote, juu ya uwepo wa mke wake, maana nguo zake na baadhi ya vitu vyake vilionekana mle ndani, kasoro zimu yake, Peter ambae alikuwa anampenda sana mke wake, akafunua funua masufuria me ndani ambako hakukuwa na dalili ya kupokwa kwa jioni ile, zaidi ya samaki ambao walibakia baada ya kuliwa mchana.
Peter akaingia kwenye kibarua kizito cha kuwasha moto, na kuanza kupika ugari, ambapo alitumia nusu saa tu kukamisha mapishi yake, na kumsaidia mwanae Michael kula ambae alishaachaga kunyonya, miezi miwili iliyopita, mpaka wanamaliza kula na kuamua kulala, mama Michael hakuwa amerudi.
Kama peter aliweza kupata usingizi, basi ni kwamuda mfupi sana, maana usiku ule alilala kiwa na mwazo mengi sana, juu ya sehemu aliko mke wake usiku ule, hakuwaza kama atakuwa na mwanaume mwingine wanapeana ufundi wa kitandani, ila aliwaza kuwa kama kuna lolote baya limemkuta mke wake, ata kulipokucha aliamka mapema na kwenda kwa wakwe zake, kuuliza kama mke wake alilala kule, “wewe ndie mwenye mke, sisi tuta juwaje alipo” jibu la mama Sada lilimshtua kidogo Peter, maana lilikuwa jibu la kijeuri, ambalo lilitoka bila wasi wasi wowote, na mbaya zaidi akumfikilia wala kutaka kujuwa habari za mjukuu wake, huku mzee Nyoni, ambae alikuwa anaingia pale nyumbani, huku amebeba mfuko wenye nyama, pamoja na dumu la lita tano lenye pombe halamu ya gongo, ambae akutaka kujuwa nini kinachoongelewa, na wakina Peter na mke wake pengine alisha juwa, kilichomleta Peter, yeye aliondoka zake na kuingia ndani.
Peter akiwa na mwanae Michael wakaondoka kuelekea nyumbani kwa mzee Jacob, yani baba yake Peter, ambako alieleza kilicho mtokea na kueleza majibu ya mama Sada yalivyo kuwa, “watakuwa wanajuwa binti yao yupo wapi, we nenda nyumbani, mpaka mchana utakuwa umesha juwa mke wako yupo wapi” alisema mama yake Peter, ambae alisisitiza kuwa, endapo, Peter akama angekuwa msikivu walipo mweleza kuhusu tabia mbaya za Sada basi yasinge mtokea yanayo mtokea, “lakini mama atakama alikuwa hivyo, kwa sasa amebadirika” alitetea Peter na kumshangaza baba yake ambae alikuwa ametulia pasipo kuongea jambo lolote, “sawa lakini kumbuka kuwa kichaa hasiria uwa haponi, ila anatulia kwa muda tu” alisema mama Peter, ambae alibakia na mjukuu wake Michael, ili kumpa nafasi Peter kwenda kufanya shughuri zake ambazo alipanga kuzifanya leo, ikiwa ni pamoja na kwenda wilani na mtumbo, kununua vifaa vya ujenzi, kwa lengo la kuanza ujenzi wa nyumba kubwa ambayo alipanga kuijenga, mala baada ya malipo ya awali kufanyika.
Nusu saa baadae tayari Peter alikuwa amesha peleka simu na kuiacha dukani kwaajili ya kuichaji, na tayari alisha fika nyumbani na kuoga kisha akavaa tayari kwa kuelekea mjini Namtumbo, ukweli aliuzunika sana maana alipenda kama mke wake angekuwepo maana wangeweza kumbeba mtoto wao Michael, ambapo licha ya kufanya manunuzi ya vifaa vya ujenzi, pia wangefanya manunuzi binafsi ya nguo zao na viatu, maana utokea mala mbili tu kwa mwaka kupata fedha za pamoja kama hivi, na mida hiyo, tayari ilisha timia saa nne ya asubuhi, wakati huu, wasi wasi ulisha aanza kumwingia Peter, aliamini lazima kungekuwa na tatizo, maana asinge weza kumwacha Michael kwa muda mrefu kama vile, lakini licha ya yote akaamua kupiga moyo konde, na kuendelea na mipango yake.
Peter alifunua godoro lake na kuuona mtungi, kama ule wakuifadhia maji, ulio funikwa kwa kwa kipande cha mfuniko wa bati, akainua chaga na kuweka pembeni, kisha akazamaisha mkono ndani ya mtungi ule mkuwa wastani, uliotengenezwa kwa udongo wa mfinyanzi, na hapo ungeweza kumwona Michael akitoa macho kwa mshangao, niwazi mkono wake aukugusa kitu alitarajia, zaidi mkono uliibuka na kipande cha katasi, ambacho alikiweka pembeni na kuingiza tena mkono ndani ya mtungi ule, lakini hali ilikuwa ni ile ile, safari hii aliibuka na kipande cha line ya simu, ambayo alipoitazama vizuri aligundua kuwa ni line ya simu ya mke wake, hivyo akagundua kuwa ata kile kipande cha karatasi kita kuwa kimewekwa na mke wake, hivyo aka kichukuwa na kukisoma kidogo, “baba Michael huna haja ya kunitafuta, wala kuniwazia, mimi nimesha chukuwa malipo yangu kwa kukuzalia, na muda ulio nipotezea, na sasa ninaenda zangu mjini kutafuta maiusha mengine, maisha ya kijijini siyawezi, usinihesabu kama mkewako tena, line ya simu hipo humo humo kwenye mtungi, hivyo mimi na wewe hatuna mawasiliano, na wala usjaribu kunitafuta” hapo Peter alijihisi pumzi zinakata, huku jasho jembamba likimchuluzika toka kichwani mwake, na kushukia pembeni mwa kichwa chake usawa wa mashavu, “Sadaaaa, nimekukosea nini lakini” alinong’ona Peter kwa sauti ya chini kabisa huku akikaa kwenye kingo ya kitanda na kujishika kichwani, huku akiinamisha kichwa chini, akionyesha ni mwenye maumivu makali moyoni mwake.
Ungesema kuwa Peter alikuwa anaumia juu ya fedha zake, lakini uwezi amini kuwa, Peter alikuwa anaumia juu ya mke wake, ambae alikuwa anampenda kuliko mwanamke mwingine yoyote ambae alishawai kutembea nae, nikweli alisha wai kutembea na wanawake kadhaa akiwa shuleni, lakini kwa Sada alikuwa amezama mazima, “hapana Sada uwezi kunikimbia kama hivi, kama ni mjini ungeniambia tuamie wote” alisema Peter ambae licha ya usbabi wake, lakini alikuwa ametepeta kama mtoto.
Hatua ya kwanza ambayo aliichukuwa Peter ambae hakuwa na ata fedha ndogo ndani mwake, ni kwenda kwa baba na mama yake, ambao aliwaeleza kila kitu, kama kilivyotokea, ukweli ilikuwa uzuni kubwa sana kwa wanafamilia wale, huku wazazi wa Peter wakiwa wanasikitikia fedha zilizoibiwa na Sada, huku Peter akisikitika kukimbiwa na mke wake kipenzi, yani Sada Joseph Nyoni, na baada ya hapo, Peter akaenda nyumbani kwa wakwe zake, ambao sasa aliwakuta wamelewa vibaya sana, na kama aitoshi, aliwakuta wakiwa na majirani, wakiwa wameagiza pombe zaidi, na wote wakionekana kulewa, huku wanachoma nyama ambayo ilikuwa inanukia na kutawanya harufu nzuri eneo lile la nyumbani kwa mzee Nyoni, cha kupendeza zaidi, nikwamba palikuwa na madumu mengine matatu ukiachilia lile moja la asubuhi.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!