
KIAPO CHA MASIKINI (04)

SEHEMU YA 4
ILIPOISHIA SEHEMU YA TATU : ukweli ilikuwa uzuni kubwa sana kwa wanafamilia wale, huku wazazi wa Peter wakiwa wanasikitikia fedha zilizoibiwa na Sada, huku Peter akisikitika kukimbiwa na mke wake kipenzi, yani Sada Joseph Nyoni, na baada ya hapo, Peter akaenda nyumbani kwa wakwe zake, ambao sasa aliwakuta wamelewa vibaya sana, na kama aitoshi, aliwakuta wakiwa na majirani, wakiwa wameagiza pombe zaidi, na wote wakionekana kulewa, huku wanachoma nyama ambayo ilikuwa inanukia na kutawanya harufu nzuri eneo lile la nyumbani kwa mzee Nyoni, cha kupendeza zaidi, nikwamba palikuwa na madumu mengine matatu ukiachilia lile moja la asubuhi……endelea…….
Hakika Peter akuweza ata kusogeza uso wake kwenye lile kundi la watu, ambao walikuwa wanafikia kumi kwa idadi yao, wakiwa ni wake na wanaume, “unajuwa nini bwana Nyoni, toka zamani binti yako alionekana mwenye hakiri sana, ona sasa unavyofaidi mtunda yake” alisikika mzee wakwanza kati ya wale waliokuwepo nyumbani kwa mzee Nyoni, “umeona hen mzee Ponera, yani natamani kama Sada ange kuwa binti yangu, yani kamwachia baba yake laki mbili, ili afaidi” alisifia mama mmoja mtu mzima aliekuwa miongoni mwao.
Naam hapo Peter ndipo alipogundua kuwa, Sada amegawa fedha zake kwa wazazi wake na zile zinazo nyweka pale nyumbani kwa mzee Nyoni, “unajuwa mzee Nyoni unapaswa kushukuru pia, kwakuwa binti yako amepata mwanaume wanguvu, ambae anamwezesha binti yako kuweza kukupatia fedha kama hiyo” alisema mzee mwingine ambae muda huo alikuwa ameshikilia kikombe chenye pombe ndani yake, na kukipeleka mdomoni, akaipiga funda moja, ambalo lilimfanya akunje uso, na kujishika kifua huku anampatia mtu mwingine kile kikombe, “unazani alimpatia, hapana bwana, yule kijana mwone hivi hivi, ni mshenzi kama nini, alikuwa anamnyanyasa binti yangu, mpaka ameibwa fedha na kuondoka zake” alisema mzee Nyoni kwa sauti ya majisifu iliyojaa kujiamini, na kuwafanya wenzake washangae, “weeee, usiniambie inamaana Sada ameachana na yule kijana wa mzee Jacob?” aliuliza mzee Ponera kwa mshangao, huku yeye na wenzake wote, wakimtazama mzee Nyoni kwa mshangao, “ameachana nae, sasa ameitwa na mwanaume wake wasiku nyingi, ni tajiri sana huko njini, yani Sada sasa anaenda kuwa tajiri pia” safari hii alijibu mke wa bwana Nyoni, yani mama Sada, kwa sauti iliyojaa majivuno.
Ukweli Peter akuweza kusubiri zaidi, maana akutaka kuendelea kusikiliza maongezi yale, kati ya wakwe zake na walevi wenzake, na kilicho muuma zaidi, nipale alipo gundua kuwa wakwe zake walikuwa wanafahamu kila kitu juu ya kuondoka kwa mke wake Sada, “hapana, ninaitaji kumfata mjini, lazima nitafute fedha nikamchukue mke wangu, sito msema kuhusu fedha wala kutoroka kwake, cha msingi lazima nimpate mke wangu” aliwaza Peter, ambae kiukweli hakujuwa aanzie wapi kumsaka mke wake wala ataenda vipi kule mjini, hakuwaza sehemu ya kufikia wala kinachoweza kumkuta kule mjini, lakini nilazima akamsake mke wake, amrudishe kijijini, ili waje wakumlea mtoto wao.****
Zilipita siku sita pasipo Peter kwenda shambani kwake, zaidi alifanya vibarua (kazi ndogo) kwa wakulima toka mjini, wanao miliki mashamba makubwa, akijitafutia fedha za nauri kwenda mjini kumsaka mke wake, wakati huo bahari za kutoroka kwa mkewake zilikuwa zinaanza kusambaa taratibu, huku watu wakiwa na mtazamo tofauti, wapo waliosema kuwa Peter aliyataka mwenyewe, kwa kujiingiza kwenye mausiano na Sada, waschana nao walisema afadhari Sada ameondoka pengine wao, wanaweza kupata nafasi ya kuolewa na kijana huyu, mchapa kazi, ambae awakujuwa kuwa kila jioni aliporudi toka vibaruani alienda mpaka stendi, kutazama kama mke wake alikuwa anarudi, na alipo mkosa aliuliza kwa watu waliokuwa wanashuka kwenye gari toka mjini, “samahani, ujamwona mama Michael huko mjini?” aliuliza Peter ambae toka azaliwe mjini aliwai kukanyaga mala mala mbili tu, tena akiwa na umri dogo sana, hivyo hakuwa na picha ya upana kamili wa mji wa Songea na tabia zake, “mh! sijabahatika kukutana nae” ndilo jibu alilopata mala kwa mala.
Wiki ya pili ikakatika Peter akifanya vibarua, na kukusanya kiasi fedha za kitanzania laki moja na elfu therathini, na kujiweka tayari kwa safari ya kwenda mjini kumchukuwa mke wake, ikiwa ni wiki ya pili toka mke wake huyo, aondoke pale kijijini Mwanamonga, na ndio siku ambayo alibahatika kupata tetesi, za sehemu mke wake anapoishi kule mjini, hivyo hakujari kuwa ni jioni, aka endesha baskeri yake mpaka Namtumbo, maana akukuwa na gari mida, gari utoka kijijini, saa kumi na moja alfajili, kwenda mjini, nakurudi pale kijijini, saa kumi na mbili za jioni, mpaka saa mbili za usiku, wakati mwingine zaidi ya hapo, asa kama mvua imenyesha, ndio maana Peter alilazimika kutumia baskeri mpaka Namtumbo, ambapo angeiacha kwa mtu anae mfahamu, na kupanda gari, kuelekea mjini, maana pale Namtumbo, nisehemu ambayo inapita barabara kuu itokayo songea kuelekea mikoa ya kusini mashariki mwa Tanzania, kitu ambacho kilisababisha usafiri kuwa mwingi pale Namtumbo.***
Naam saa mbili na robo za usiku, tayari Peter alikuwa amesha shuka kwenye gari, na sasa alikuwa anakatiza mitaa ya Zanzibar anaelekea upande wa soko kuu, ambayo ndiyo sehemu pekee anayo kumbuka pale mjini, ambapo amini kuwa ange ulizia na kufika mtaa wa mfaranyaki, kama alivyoelekezwa, kuwa ndio mtaa ambao mama wa mtoto wake anaishi, Peter ambae akujuwa matokeo ya ile safari yake, alitembea kwa haraka na kijibegi chake kidogo mgongoni, alichoifadhia nguo mbili, yani shati na suluali, pia alibeba mswaki, na dawa yake, japo dawa yenyewe ilikuwa inakaribia ukingoni, huku macho yake yakipata burudani kwa kuona maduka yenye vitu vizuri, ambayo yaliuzwa na waschana wazuri, huku akipishana waschana wengine nao wazuri wenye kuvalia vizuri, kuliko ata mke wake Sada, “kidogo changu vikubwa vina wenyewe” alijisemea Peter huku akiendelea na safari yake.
Lakini basi, wakati anamaliza kukatiza kwenye mtaa huu ambao uchangamfu wake ulikuwa wa iwango cha chini, na uiizidi kupungua kila aliposogea mbele, sasa alijikuta akiwa mwenywe kabisa, akatazama mbele sasa aliweza kuliona soko kuu, ilikkiwa limesha fungwa, hapo akaona kuwa mpango wake wakwanza ukakwenda vibaya kwaajili ya kuto kuzingatia muda, hivyo akageuka kutazama kwenye jengo moja kubwa, la ghorofa mbili, lenye maandishi makubwa yaliyokuwa ya wakataa, “#Mbogo_Land Sonara” ndivyo yalivyo someka, lengo lake ni kuona kama anaweza kupata mtu wakumwuliza anawezaje kufika mfaranyaki, mtaa ambao sikuzote alikuwa anausikia tu, lakini hakuwai kufika.
Nje ya jengo lile kubwa la ghorofa mbili akuweza kuona mtu yoyote zaidi ya gari magari matatu yaliyokuwa yamesimama tofauti kwa mtindo, magari mawili yali simama pamoja, kwenye sehemu maalumu ya maegesho ya jengo lile la #Mbogo_land, moja kati ya hayo mawili lilikuwa ni Range Rover HSE, rangi nyeusi, lakisasa kabisa, na gari moja aina ya IST jeupe, likiwa peke yake, lenye vioo vyeusi, vilivyo pandiswa mpaka juu, likiwa limesimama, hatua kama kumi hivi, mbele ya jengo ili, usawa wa lango la kubwa la vioo, la kuingilia kwenye jengo lile, la kisasa lililotawaliwa na vioo kwa asilimia hamsini. Huku egine yake ikiwa iana unguruma.
Peter alitamani kurudi alikotoka, kule alikowaacha watu wengi, ili aweze kuwauliza kuhusu mtaa wa mfaranyaki uliko, mfaranyaki ni sehemu ambayo ilikaliwa na mmoja wa machifu wa kingoni, miaka ya 1800, alie fahamika kwa jina la Chifu Mfaranyaki, lakini kabla bwana Peter aja anza safari ya kurudi alikotoka, mala akaona mlango wa jengo lile ule mkubwa wa vioo ukifunguliwa, hapo Peter akajuwa lazima kuna watu wata toka, nae akasimama na kutazama atakae toka, hapo akawaona watu wawili wana toka nje ya jengo lile, alikuwa ni mwanamke na mwanaume, mwanamke alikuwa ambele, akiwa amevalia suit nyeusi ya kike, ambayo ilikuwa ni suruali, iliyomshika vyema mapajani, na kutoa taswira ya umbo lake zuri la kuvutia, kama vile hips zilizo chomoka vyema, japo Peter akuona jinsi mwana dada huyo alivyo upande wa mgongoni, lakini aliweza kupata picha kamili kwa kupitia hips hizo, pia juu alivalia kikoti kidogo cheusi, cha suit, kilichoficha shati jeupe lililoonekana kidogo, akiwa amechomekea kwenye ile suruali yake, usoni alikuwa mzuri, aswaaa, siyo kwaajili ya pua yake iliyotaka kufanana na wa hindi, au macho yake makubwa kidogo, ya duara, au nyusi zake mzuri ambazo ungesema alichana kwa kitana, siyo kwaajili ya nyusi ambazo ungesema amezichonga kwa jinsi zilivyo kaa vyema, au mdomo wake mdogo, ambao ilibeba lips pana, za kuvutia, na kutamanisha kumtazama akiwa anakula au ananyinya kitu chochote kitamu, siyo kwaajili ya kidevu chake kizuri kilicho chongongoka kidogo, au shingo yake yenye pingiri kama za watoto wadogo wenye afya njema au miilimikubwa, zilizozidisha uzuri wake, au nywele ndefu, za mwanamke huyu zizofungwa kwa nyumba na kufanana kama mkia wafarasi dume, ila nazani ni kwaajili ya mwonekano wa upole wa mwanamke huyu, mrefu wa wastani, mwenye umbo zuri, yani siyo mnene sana wala siyo mwembamba, alie valia viatu vya mikanda vyenye visigizo virefu, vilivyo sababisha kuonekana kwa nyanyo zake nzuri na safi, ungesema nikiganja cha mikono anachotumia kulia chakula, na kucha zake nzuri zilizopakwa rangi kwa ufundi mkubwa, ikionyesha bendere ya nchi jirani ya #mbogo_land, na mwanaume alikuwa nyuma yake, akiwa amebeba mkoba mweusi, ambao kwa haraka haraka ungeshindwa kuuelezea kama ni wakiume au wakike, ila ulikuwa wa mfano wa bref case, mwanaume huyu alikuwa amevalia kama askari flani toka kampuni binafsi ya ulinzi, sale zake za kaki, zenye fito za njano kwenye usawa wa mkunjo wa suruali na mikono ya shati, pamoja na kofia nyeusi, aina ya barehat, (ile ya duara, isiyo na cap wala masikio, na bunduki yake kubwa begani, nazani ilikuwa ni Maker 4, mahalumu kwaajili ya uwindaji, lakini hapa inaonekana ilikuwa inatumika kwenye ulinzi.
Niwazi yule mlinzi, alikuwa anamsindikiza yule mwanamke mzuri, ambae alionekana kuwa ni boss wake, ambao sasa walikuwa wanaelekea kwenye gari moja kati ya yale mawili, kwwenye maegesho, “wanawake wote awa wazuri, kwa nini mtu anataka kumchukuwa mkewangu, tena toka kijijini” alishangaa Peter huku anasogelea kwenye lile jengo la ghorofa, huku lengo lake likiwa ni kumwai yule mlinzi, amuulize swali lake pindi atakapo agana na boss wake, na wakati Peter anatembea kusogelea upande ule, macho yake ayakuacha kumtazama yule mwanamke mrembo, na kuusanifu mwili wake, japo kimoyo moyo, alijuwa fika kuwa hakuwa na hadhi wala uwezo wa japo kuomba salamu, ya yule mwanamke, mrembo mwenye uso wa upole, kama siyo uzuni.
Naam wakati Peter anasogea huku macho yake yakiwa kwa mwanamke yule ambae sasa alikuwa amesha likaribia lile gari aina ya Range Rover HSE lakifahari, mala ghafla akaona mlango miwili ya mbele ya gari lile aina ya IST lililosimama mbele ya jengo, lile la kifahari, na wakaibuka vijana wawili walioziba nyuso zao, kwa kofia nyeusi za sox, na kwa haraka sana wakawafwata wale wale wawili, yani mwanamke mrembo na mlinzi wake, Peter alimwona yule mwanamke mrembo sana na mlinzi wake wakiwaona wale jamaa, na hapo yule mlinzi akatupa chini, begi jeusi na kujaribu kuweka sawa bunduki, huku mwanamke yule akiokota haraka begi lake, na kujaribu kutoa funguo za gari, lakini ni kama walikuwa wamesha chelewa, maana tayari wale watu wawili walisha wafikia, na kabla yule mlinzi ajakoki bunduki yake, akashtuka akipewa kode zito, la shavuni, lililomtupa kando na kujibwaga chini, akitengana na bunduki yake, huku yule mwingine, akijaribu kulipokonya lile begi jeusi, toka kwenye mkono wa yule mwanamke mrembo, ambae sasa alikuwa amelishika kwa mikono miwili, na kujaribu kulitetea, huku anapiga kelele, “jamani msaada, naomba msaada” alipiga kelele yule mwanamke huku akivutana na yule jamaa, kitu ambacho hakikutumia muda mrefu, maana yule jamaa alimshinda nguvu na kumpokonya lile begi, wakati huo yule mlinzi, alionekana kutulia pale chini, amepoteza fahamu…. Endelea kufwatilia mkasa huu

