
SEHEMU YA 5
ILIPOISHIA SEHEMU YA NNE : lililomtupa kando na kujibwaga chini, akitengana na bunduki yake, huku yule mwingine, akijaribu kulipokonya lile begi jeusi, toka kwenye mkono wa yule mwanamke mrembo, ambae sasa alikuwa amelishika kwa mikono miwili, na kujaribu kulitetea, huku anapiga kelele, “jamani msaada, naomba msaada” alipiga kelele yule mwanamke huku akivutana na yule jamaa, kitu ambacho hakikutumia muda mrefu, maana yule jamaa alimshinda nguvu na kumpokonya lile begi, wakati huo yule mlinzi, alionekana kutulia pale chini, amepoteza fahamu…. Endelea….
Naam kwa kawaida ungesema imetosha, lakini aikuwa hivyo, maana yule mwanamke alimwona mmoja kati ya wale vijana akimsogelea na kuinua mkono wake kwanguvu, akiwa ametanua kiganja chake na kukishusha kwa nguvu usawa wa uso wa mwanamke, yule kwa lengo la kumzaba kibao, watoto wa mjini wanasema kumtia wenge, yule binti mrembo hakuwa tayari kushuhudia lile kofi likija usoni kwake, hapo kwa uoga akafumba mbacho huku akijikunyata kwa uoga, lakini kabla mkono aujatuwa kwenye uso wake, yule mwanamke mzuri akasikia, “kwanini unataka kumpiga huyu mwanamke mzuri namna hii, yani ume mwibia alafu, bado una mpiga tena?” ilikuwa nisauti ya upole ambayo aikuwa na dalili ya utani.
Yule mwanamke ambae mwanzo alizania kuwa alie sema vile alikuwa ni yule mwizi, alie mnyang’anya begi, akafumbua macho taratibu ili kujiakikishia alicho kisikia kama kweli kinatokea aula, na ile anafumbua macho akamwona kijana mmoja ambae akuwepo miongoni mwa wale walioziba nyuso zao, akiwa ameudaka mkono wa yule jamaa alie taka kumba kibao cha usoni, huku wale jamaa wote wawili wakimshangaa kijana huyu, ambae siyo tu kuonekana mwenye mwili ulio jengeka kimisuri, ya kazi, pia mwonekano wake ni wakijiji aswaaa, “ebu niachie we fala, kwanini unaingilia inshu zisizo kuhusu” alisema yule jamaa alie shikwa mkono huku anaupapatua kwanguvu mkono wake toka kwenye mkono wa Peter, “mrudishieni huyu dada begi lake, mnamiili mizuri kabisa ya kweda kulima mashamba makubwa au kukata mkaa, na kujipatia fedha zenu, siyo kuiba” alisema Peter kwa sauti ile ile tulivu, huku anapiga hatua kumfwata yule jamaa alie shiilia begi, huku yule mwanamke mrembo akimtazama Peter kwa macho ya mshangao na kustahajabu, maana hakuamini kama msaada ume fika kwa wakati, japo hakuwa na uhakika wa asilimia zote kwamba ule msaada ungedumu mpaka anaondoka.
Lakini Peter kabla aja mfikia yule mwenye begi, akashtuka akitandikwa teke la mgongoni, huku mwenye begi akirusha mguu wake, na kwa lengo la kumkwatua gwala, ambayo atailipo mgusa mguu wake aikusababisha madhara, maana yule jamaa alijikuta akikutana na kitu mfano wa chuma, kilicho simikwa chini, na kuyumba yeye mwenyewe, huku kijana huyu, pasipo kuteteleka, akirusha konde zito, kuelekea kwa yule kijana wakwanza, ambalo lilituwa usawa wa mdomo, na kukita kwanguvu, kiasi cha kijana huyu, kuhidi mfupa wa jino, ukigusa mkono wake, maana aliunga nisha nguni na jino la yule jamaa ambae alipasuka mdomo, na kubakia kidogo kumeza jino lake alililong’oka mdomoni mwake, huku akirudi nyuma hatua kadhaa, kuona hivyo yule jamaa mwingine akavurumisha ngumi yake ambayo ilituwa kichwani, mwa Peter, na ambae aliyumba kidogo, na kugeuka kwa haraka, akamwona yule jamaa anarudha teke moja zito lililokuja usawa wakifua chake, Peter alikwepa kidogo, na kulidaka lile teka, kisha akauvuta ule mguu na kumfanya yule jamaa kupiga msamba wa bila kutegemea, kitu ambacho kilisababisha maumivu makali sana kwa jamaa yule, ambae aliachia ukulele wa nguvu, “mamaaa nakufaaaaa!!!!!” alilia yule majamaa huku anaachia lile begi, hapo yule mwenzie alie pasuliwa mdomo, akainuka alaka na kwenda kumwinua mwenzie alie kuwa ana galagala, kwa maumivu, kisha wakakimbilia kwenye gari lao na kuondoka zao.
Hapo Peter aliokota lile begi na kumsogelea yule mwanamke, ambae muda wote alikuwa amesimama kama vile sanamu, yani kwakifupi alishikwa na bumbuwazi, “pole sana dada yangu, inapaswa uwe na walinzi wengi zaidi, tena wenye uwezo wa kupambana” alisema Peter, huku anamkabidhi begi lake, na yule dada pasipo kuongea chochote akalipokea, huku anamtazama Peter kuanzia juu mpaka chini, kitendo ambacho Peter hakukielewa kilikuwa na maana gani, au pengine huyu dada alimshangaa kwa uvaaji wake wa kishamba, ambao haukutakiwa kumsogelea mwanamke kama yule maana bira ata wale majambazi walikuwa wamevaa vizuri, kuliko yeye.
Hapo Peter hakasubiri kukosolewa, akaamua kujiwai, “samahani dada, sikuwa na maana ya kukusoglea, ila nilikuwa nashida ya kuulizia Mfaranyaki ni wapi” alisema Peter, kwa sauti ya upole iliyojaa nidhamu, kitu cha ajabu yule mwanamke akujibu lolote, zaidi alibakia amekodoa macho yake kumtazama Peter, na pia akamtazama mlinzi wake ambae sasa alikuwa anaanza kujitikisa, akumjali, akamtazama tena Peter, kwa macho yale yale ya mduwao, kisha akamwona anafungua begi lake, hapo Peter akaona sasa anachukuwa simu, ili aitiwe polisi.
Peter akaona isiwe tabu, “samahani dada, kama kunajambo nimekosea” alisema Peter kwa sauti iliyojaa nidhamu, huku anainamisha kichwa cheke kwa heshima zote, na kisha akageuka na kuondoka zake, akimwacha yule mwanamke anapekuwa pekuwa kwenye begi lake, huku yule mlinzi akijiinua pale chini, na kuokota ile bunduki yake, na kumtazama yule mwanamke ambae ndie boss wake, akamwona anapekuwa pekuwa begi lake na kuibuka na noti kadhaa za elfu kumi kumi, “asante sana kaka yangu, ukiwa nashida yoyote unaweza kuja hapa kuni…” alisema yule mwanamke, huku ananyoosha mkono wenye fedha pale aliposimama Peter na kusita, baada ya kuona hapa kuwa na mtu, “ameenda wapi yule kijana” aliuliza yule mwanamke kwa mshangao, huku anatazama kushoto na kulia, kama angeweza kumwona, “kijana gani unamzungumzia boss?” aliuliza yule mlinzi, huku na yeye akitazama kushoto na kulia huku amenyoosha bunduki yake, mfano wa askari alietayari kwa mapambano, kuona kuwa mlinzi huyu hakuwa na msaada, yule mwanamke mrembo akatoa funguo na kubofya remote kwaajili ya toa lock, kisha akafungua mlango na kuingia ndani ya gari pasipo kuongea lolote, na kufunga mlango, kisha akawasha gari na kuondoka ondoa gari lake aina ya Range Rover HSE, la kisasa kabisa, na kifahari.
Huyu anaitwa Careen Martin, au mama wa dhahabu, kama wengi wanavyopenda kumwita, kutokana na maisha yake kutawaliwa na vitu vya dhahabu, mwenye miaka ishilini na sita, mwanamke ambae siyo tu ni mtoto wa tajiri mmoja mkubwa toka nchi ya kifalme ya #mbogo_land, pia ni mwana dada tajiri, ambae ni mfanyabiashara mwenye maduka makubwa ya nguo na vito vya dhahabu, na almas na madini mengine, toka nchini #mbogo_land ambayo kwa sasa inaongozwa na mfalme Elvis Mbogo wa kwanza, mtoto wa mfalme Eric, (soma umekosea lakini tamu), mwanamke ambae kiukweli, ukiachilia uzuri wake, wa asiri, kuongeza mavazi na mapambo ya thamani, ambayo katika hali ya kawaida, mavazi yake na vitu alivyo vaa kama mikufu, hearing, pete na bangiri za mikono, pasipo kusahau saa na kibanio cha nywele vyote kwa ujumla wake, ungeweza kununua gari dogo la kutembelea.
Lakini licha ya mwonekano na uzuri alionao, mwanamke huyu, hakuna alie wai kumwona akiwa na mwanaume, na kitu ambacho wafanyakazi wake waofisi zake mbali mbali, hapa mjini songea, na wale ambao anaishi nao kwenye jumba lake kubwa la kifahari, lililopo karibu na hotel kubwa ya kihistoria ya Angoniams, (ngoni armys) pengine ni kutokana na tabia yake yakuto kutaka maongezi ya mala kwa mala na mtu yoyote, ni mala chache sana ungemwona anatabasamu au kitoa kicheko afifu sana, na hapo kama siyo kuna jambo kubwa lime mpendeza, basi ata kuwa anaongea kwa njia ya simu na mmoja wa wazazi wake, walioko nchini #mbogo_land, kwa King Elvis wa kwanza, mtu pekee ambae uwa anaweza kuongea nae japo kwa sakika tano au kumi, ni mlezi wake, zaidi ya hapo, sauti yake ungeisikia wakati anatoa maagizo au kuuliza swali kuhusu report anayoitaji, akuwai kuwa na rafiki songea, awe wakike au wakiume, hakuna alie fahamu sababu ya mwanamke huyu mrembo toka #mbogo_land, kuwa na tabia kama hii.***
Naam kijana Peter alipoachana na yule mwanamke alie mwita mrembo sie ongea, alitembea taratibu kurudi kule alikotoka, ili kuwarudia wale watu aliowaona kule, akawalize, ulipo mtaa wa Zanzibar, ambako alielekezwa kuwa mke wake Sada yani mama Michael anaishi……
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU