
KIAPO CHA MASIKINI (08)

SEHEMU YA 8
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABA : Miezi michache iliyopita, akajitokeza mzee mmoja tajiri, anaeitwa Pitus Kalonga, ambae hakuna anae juwa chanzo cha utajiri wake, maana ukiachilia, maduka matatu cha viatu vya mtumba, alikuwa na duka la vifaa vya michezo, lakini visingeweza kumpatia fedha na gari la kifahari alilo kuwa analiendesha…… Endelea………
Yeye alianza kwa kujifanya mteja, wa dukani kwa Careen, alipozoeleka akanza kutoa offer mbali mbali, asa panapotokea sherehe flani, ata ya kitaifa ya huko kwao, mbogo land, mfano siku za uhuru, au sherehe zozote za kitaifa, yeye ange jifanya kutoa chakura na vinywaji, na zawadi kibao kwa Careen na wafanyakazi wake, lakini bahati mbaya akuweza kumshawishi Careen ata kutabasamu, ndipo alipo amua kuonyesha makucha yake, kwa kuomba penzi la mwanamke huyu, ambae siyo kwamba alimkataa, ila pia akumkubari.
Alichokifanya Careen ni kuwaeleza wazazi wake, “mama kuna mwanaume anaonyesha ananipenda, sijuwi unaweza kunisaidia kumtazama” alisema Careen, akimweleza mama yakem ambae alimwambia atume picha ya kijana huyo na majina yake, kwa haraka haraka unaweza kusema aliomba kutazamiwa kwenye tunguri, lakini hapana, unaweza kuelewa wiki moja mbele, siku ambayo Careen alipewa majibu yake, ambayo yalionyesha kuwa bwana Pitus Kalonga, mume wa mke mmoja, na baba wa watoto sita, watatu wandani ya ndoa wengine kila mmoja na mama yakje, kuwa ni mshukiwa wa matukio kadhaa ya urifu, wa wizi wa kutumia nguvu, anae jimilikisha kikundi kidogo cha waarifu anaowatumia kuiba kwenye mabenk na maduka makubwa, huku akiwa ni msafirishaji na muuzaji wa madawa ya kulevya, “na pia alisha shiriki kwenye matukio kadhaa ya utapeli, uanza kwa kujifanya rafiki na kuoa vijizawadi mbali mbali, mwisho utekeleza tukio la wizi kwa njia moja wapo, kama siyo utapeli, basi kuja kuvunja, sehemu usika, na ndio kitu ambacho alitaka kukifanya kwa Careen.
Ugomvi wao ulianza siku ambayo Kalonga alienda kukumbushia ombi lake kwa mwanadada Careen, ambae kwa sauti ya upole kabisa, alimwuliza, “mzee Kalonga, unalengo gani na mimi endapo nita kubari ombi lako?” swali ilo uwa alimshindi mwanaume yoyote, ndio maana Kalonga aliachia tabasamu pana huku anachezea ndevu zake, “lengo langu ni kukuoa Careen unazani nina taboa ya kuchezea wanawake, na hakika sito kuumiza kabisa, wala kuchezea hisia zako” alieleza Kalonga, huku anakenua meno yake, kwa tabasamu la kuchukiza, vile Careen alikuwa analiona mala baada ya kupata report ya mzee huyu, “eti unioe unamaana nikawe mke wapili?” aliuliza Careen kwa sauti iiyojaa mshangao, na hapo akamwona Kalonga akishtuka kwa mshangao, “nani kakuambia nina mke.. namaanisha kwamba nilisha achana nae kitambo sana.. yani…yani sina mke” alisema bwana Kalonga, kwa sauti ya kubabaika, “mh! mzee unajuwa umri wako auendani na mambo unayofanya?” aliuliza Careen kwa sauti tulivu, huku akimtazama usoni mzee Kalonga, “mambo gani Careen, mbona sikuelewi?” aliuliza Kalonga, huku akijaribu kuchekesha, “mzee Kalonga, unazani nilahisi hivyo kumdanganya mtu kama mimi, una mke na watoto sita, watoto watatu umezaa mke wako, na watatu umezaa na wanawake tofauti, ni mshukiwa wakesi za uharifi, yani wizi wa utaperi na ujambazi, pia upo kwenye mpango wa kunitaperi” alisema Careen, jibu ambalo, lilimsstua Kalonga ambae akujuwa wala kufahamu, chanzo cha habari cha Careen, “hooooo! utabiri mzuri, nazani nivyema ukajiandaa kwa kinachofwata, uwa sishindwa kufanya kile ninachofanya” alisema Kalonga, akiamini kuwa Careen amaeishisi kama siyo kuambiwa na mtuambae akuwa na uhakika na habari anazo zitoa, maana likuwa anajuwa kuwa, kwa jinsi alivyo pangilia mambo yake, haku na mtu ambae ana weza kugundua mambo yake ambayo ata polisi wamekosa ushahidi mala kadhaa, pale walipojaribu kumfikisha mahakamani.
Hapo Kalonga akainuka na kuondoka zake, kutoka nje ya ofisi, ya mwana dada huyu mrembo alafu tajiri, ambae akujibu lolote zaidi ya kumtazama kwa macho yasiyo na tabasamu wala chuki, endapo unge ya tazama vizuri ungesema kuwa yalikuwa yame jaa dharau, alimtazama Kalonga mpaka alipotokomea zake nje ya ofisi.
Naam baada ya siku kadhaa Careen akapokea simu kwa namba mpya, kwenye simu yake binafsi, ambayo ni watu wachache sana walibahatika kuipata ile namba, na isitoshe Careen akuwa na tamaduni yakuwasiliana na watu wengi ata wafanya biashara, maana tayari kuna watu walikuwa na kazi hiyo ya kupokea nakuweka oda, yani kuongea na wateja wananunuzi na wauzaji, “Careen nakupa siku tatu kunipa jibu langu, vinginevyo sibiri uone kitakacho tokea” ilikuwa ni sauti ambayo Careen akutumia muda mrefu kuitambua, kuwa ni sauti ya bwana Pitus Kalonga, hapo Careen akakata simu na kuiweka juu ya meza, akichukulia kuwa ni maneno ya mkosaji.
Lakini siku baada ya wiki moja ndipo Careen alipoona kuwa, bwana Kalonga akuwa anatania, na kwamba alicho kiongea alimaanisha, maana jioni ya siku hiyo wakati akiwa njiani anaelekea nyumbani kwake, akashtuka kuwa kuna gari aina ya Toyota IST lina mfwatilia, kila anakokwenda, akulijari sana, ila baada ya kukata mitaa miwili mitatu, na kuliona bado lina mfwata ndipo alipo gundua kuwa gari lile lina mfwata yeye, hapo Careen akaongeza mwendo kufwata barabara ya viwandani, mpaka alipofika kwenye makutano ya barabara ya zimani moto na matarawe, yani pale SODECO, akaikunja kona moja matata sana, kuifwata barabara ya kushoto, na sasa akawa anapita pembeni ya uzio wa waya wa makazi ya polisi, na upende wa kulia kulikuwa na ukuta mkubwa wa uwanja wa zimani moto, uliopakana na uwanja wa maji maji, na lipofika sehemu ya kuingilia kituo cha polisi cha wila, akakata kona kushoto, na kuingia kwenye kituo cha polisi cha wilaya, na kwenda kusimama mbele ya jengo ilo la kituo cha polisi, hapo kwa haraka sana Careen akashuka toka kwenye gari, na kuingia ndani ya kituo hicho cha polisi, ambako alikutana na polisi wawili wakiume, ambao walimpokea kwa mshangao mkubwa, wakionekana wanastaajabu kwa uzuri wa mwanamke huyu, ambae aliingia kwa pupa mle ndani, “polisi kuna majambazi wananifwata, nendeni mkawakamate” alisema kwa sauti ya uoga yenye pupa, mschana yule huku akionyesha nje, lakini nikama wale polisi awakumsikia wala kumwelewa, maana bado walikuwa wamekodoa macho wanamtazama mwanadada wadhahabu, ambae siyo kwamba walikuwa hawamfahamu, hapana, walikuwa wanamfahamu vyema kabisa, kuwa ni mmiliki wa #mbogo_land Sonara, “nyie mapolisi, mbona mimi nawaambia alafu bado mmekaa tu, kuna mtu anafwata toka ofisini kwangu naomba mka mkamate” alisema tena Careen safari hii ikiwa ni zamu yake kuwashangaa polisi wale, ambao nikama walikulupuka toka usingizini, “gari namba ngapi na aina gani?” aliuliza mmoja kati ya polisi wale, mwenye cheo cha tepe mbili mfano wa V, kwenye bega lake la kulia, huku anachukuwa karamu ya wino na karatsi tupu, “sija likalili namba ila ni Toyota IST, rangi ya silver” alielezea Careen, na yule jamaa akaacha kuandika na kumtazama Careen, huku anainuka, lipowapi ilo gari unalosema” aliuliza yule mwenye tepe mbili, na kuanza kutoka nyuma ya counter, akifwatiwa na mwenzie, ambae hakuwa na alama yoyote begani mwake, na Careen nae akaliunga, walipofika nje ya kituo wakatazama barabara kuu, “lile pale unaona limesimama pale” alisema Careen ambae huku anaonyesha lile gari, dogo aina ya Toyota IST, ambalo nikama dereva wake aligundua kuwa anatazamwa yeye, maana aliondoa gari taratibu, kueleka upande wa mjini, na kufanya namba za gari upande wanyuma kuonekana.
Nikama wale polisi walishtuka kidogo baada ya kuliona lile gari, kisha wakatazamana, alafu wakaepana ishala ya siri ya kumya kimya, “wasi wasi wako tu, lile gari lina inshu nyingine kabisa, wala hakuwa ana kufwatilia wewe” alisema yule polisi mwenye tepe begani kwake, huku anarudi ndani, akifwatiwa na mwenzie, ambae aligeua nyuma kila baada ya hatua kadhaa, kutazama mgongo wa mschana huyu, mrembo ambae siku zote walikuwa wanamwona kwambali, ambae sasa alikuwa amesimama anatafakari jibu la polisi awa, na baada ya sekunde kadhaa akaondoka zake, bila kuaga, akiacha mmoja kati ya wale polisi akitoa simu yake na kupiga sehemu.
Careen alienda moja kwa moja mpaka nyumbani kwake, kule angoniams, ambako akukaa muda mrefu kabla ajapokea ujumbe wa simu, toka kwenye namba ile ile iliyo mpigia siku kadhaa zilizopita na kumpa onyo, yani ya Kalonga, “umesha ambiwa kuwa wasi wasi wako, hapo inamaana kuwa polisi hawana msaada na wewe, sasa sijuwi sasa utakimbilia wapi?” ujumbe huo ulimtia hofu kubwa Careeen, ambae alizidi kukosa amani katika maisha yake, kwamaana kwamba ata polisi walikuwa wanashilikiana na Kalonga, na wasingeweza kufanya lolote, katika kumzuwia, Careen aliwasiliana na wazazi wake, na kuwaleza kilicho tokea, nao walimweleza kuwa, aondoe wasi wasi, pengine nikweli ilo gari lilikuwa katika mienendo yake, na haikuwa likimfwata yeye.
Sasa basi leo ikiwa zimepita week mbili, ndipo likamtokea tukio lakuvamiwa na wale vijana wawili, waliotumia gari lile lile aina ya Toyota IST, na kusaidiwa na kijana mwenye mwonekano wa kutoka kijijini, ambae akutaka kupokea chochote toka kwake.**
Naam Peter alishtuka akiwa kwenye sehemu finyu, yenye maji yaliyotoa arufu mbaya, giza lilikuwa limetanda, kuonyesha kwamba ulikuwa usiku mkubwa sana, kwambali alisikia maumivu kichwani mwake, akainuka na kujikagua, hakuwa na simu wala kiasi cha fedha kama laki moja na efu kumi, alizo kuwa nazo, akaliona begi lake pemmbeni ya ule mtaro, likiwa wazi huku nguo na baadhi ya vitu vyake kama mswaki na dawa, vikiwa vime tawanyika, na vingine kuingia mtaroni kwenye maji machafu, “aiwezekani Sada uniache mimi na kuwafwata hao wezi” alinong’ona Peter mtoto wa mzee Jacob, huku anatazama kushoto na kulia pengine angeweza kuona alama yoyote ambayo inge mtambulisha kuwa yupo sehemu gani, ili aweze kurudi kumchukuwa mke wake, lakini hakuambulia chochote.
Hapo Peter alaanza kutembea kutafuta sehemua mbayo anaweza kuikumbuka na nakuweza kuelekea mfaranyaki, lakini baada ya kutembea kwa mita kama mia moja, akatokea kwenyenjia aliyotumia kuingilia ingilia mtaa wa vandu, hivyo akaamua kuifwata ile njia, mpaka alipolifikia lile duka la yule mzee, na kuingia kwenye ule uchochoro, wa kuifwata nyumba kubwa ya zamani, huku kichwani mwake akipanga kuwa akiwakuta wale jamaa, lazima apigane kutetea ndoa yake, akujari matusi ya mke wake, wala jeuri na kipigo alichopokea toka kwa mwanamke huyu, ambae sasa alionekana kuchanganyikiwa kabisa.
Yap, Peter alifanikiwa kufika kwenye ile nyumba ambayo sasa ilikuwa kimya kabisa, akaanza kutembea kwenye kolido, huku akijikumbusha kile chumba ambacho alimkuta mke wake, na bahati nzuri kwake alifanikiwa kuipata na alikuta mlango ukiwa wazi, na taa inawaka ndani yake, lakini bahati mbaya kwake, hakukuta kitu chochote mle ndani, wala dalili ya kwamba kuna mtu anatarajia kulala mle ndani, inamaana walikuwa wamesha ondoka, nazani ni baada ya kujiona wamefanya tukio, ambalo walilihisi kuwa ni mauwaji.
Peter hakuwa na la kufanya, zaidi ya kutafuta uwezekano wakurudi nyumbani, yani kijijini mwanamonga, uchaguzi wakwanza ulikuwa ni kutembea kwa mguu kilomita sabini na mbili yani mpaka namtumbo, ambapo angeikuta baskeri yake na kuelekea kijijini kwao mwanamonga, wazo jingine ni kuwai stendi, ambako ange tazama kama angeweza kukutana na watu toka jijini kwao angewaazima nauri ambayo ingemsaidia kufika kijijini kwao, Peter akachagua wazo la pili, kwamba akalale pale stendi, ambapo gari toka kijijini kwao linge mkuta na yeye angeweza kukopa fedha au pengine angeongea na kodakta, wa gari lile, amsaidie lift, na ange mlipa fedha yake pindi angeipata.
Lisaa lizima lilitumika kwa Peter kuisaka stendi, na alipoipata akachagua sehemu nzuri na kujikunyata, akitafuta usingizi, baridi ilikuwa kari kwa ile nguo yenye unyevu unyevu aliyoivaa, njaa ilimsokota, sambamba na maumivu ya mwili kwa kipigo alicho kipata, kule kwa mke wake Sada, suzani kama nita kuwa mkweli endapo nita sahau kuhusu mbu, walio jaa pale stendi, ambapo sasa palikuwa kimya kabisa, nikama uwanja wa mpira ambao hakuwa unatumika, japo palionekana watu wachache wengiwao ni wale watumiaji wa zile dawa zinazokatazwa, na magari yaliyo egeshwa kusubiri safari za kesho mapema.

