
SEHEMU YA 9
ILIPOISHIA SEHEMU YA NANE : Lisaa lizima lilitumika kwa Peter kuisaka stendi, na alipoipata akachagua sehemu nzuri na kujikunyata, akitafuta usingizi, baridi ilikuwa kari kwa ile nguo yenye unyevu unyevu aliyoivaa, njaa ilimsokota, sambamba na maumivu ya mwili kwa kipigo alicho kipata, kule kwa mke wake Sada, suzani kama nita kuwa mkweli endapo nita sahau kuhusu mbu, walio jaa pale stendi, ambapo sasa palikuwa kimya kabisa, nikama uwanja wa mpira ambao hakuwa unatumika, japo palionekana watu wachache wengiwao ni wale watumiaji wa zile dawa zinazokatazwa, na magari yaliyo egeshwa kusubiri safari za kesho mapema……Endelea……
Peter Jacob hakubahatika kupata ata chembe ya usingizi, kutokana dhahama ya mbu, baridi, njaa, maumivu ya mwili na mawazo ya machungu ya kukataliwa na mke, hakufikilia kuhusu kipigo alicho kumbana nacho, “mwanangu ujawaona wanawake wote awa hapa kijijini, mpaka unaenda kujizolea mwanamke asie jiheshimu kama huyu?” Peter alikumbuka maneno ya mama yake, wakati ule anampa honyo juu ya Sada, Peter aliwaza kuhusu mwanae Michael, kwamba atamwelezaje pindi akiwa mkubwa, kuna kipindi Peter alijaribu kupotezea mawazo hayo, lakini akuweza kabisa, mawazo yale ya kuumiza moyo wake, ata alipoamua kuhesabu nyota za again, pasipo kufanikiwa kupata idadi yake, mpaka kunakucha, na watu kuanza kumiminika pale stendi kuingia kwenye magari tayari kwa safari za kwenda sehemu mbali, saa moja na robo akaliona gari toka kijijini kwao nalo likiingia.
Naam bahati nzuri, ikawa upande wa Peter, ambae alikutana na rafiki yake toka kijijini, ambae alimpatia nauri, itakayo mfikisha Namtumbo, ambako alifika mida ya saa nne, na kuchukuwa baskeri yake akaelekea kijijini mwanammonga, moja kwa moja nyumbani kwake ambako alijifungia ndani mwake, ambako alikaa siku tatu, pasipo watu kujuwa kama alisha rudi safari yake ya mjini, Peter alitumia muda mwingi kuwaza juu ya Sada, na kile kilichotokea, ata siku ya nne, akaamua kujisahaulisha kuhusu mwanamke huyo, na kutumia nguvu zake kufanya kilimo akiandaa maisha ya mwanae Micahel, hakutaka aje adhalilike kama yeye alivyo dhalilika.
Naam huo ndio ulikuwa mwanzo wa maisha mapya, kwa kijana Peter Jacob, ambae licha ya kuelekeza nguvu kwenye mashamba yake ya tumbaku na mahindi, pia alijikita kwenye kazi ndogo ndogo, (day waker) wakati mwingine tunaitaga vibarua, na kujipatia fedha ndogo ndogo za matumizi, yake na mwanae Michael, na wakati mwingine wazazi wake ambao awalikuwa wanaishi na mtoto Michael, Michael lijitaidi kumsahau mke wake mama Michael, yani Sada binti Nyoni, ambae mala kwa mala alikuwa anamkumbuka, na kuvuta tukio la kumkuta mle ndani ya kile chumba, akiwa na wale wanaume nusu uchi, hakika ilikuwa kazingumu sana kusahau, na kuondoa kumbukumbu hoyo, aliwalahumu sana wazazi wa Sada yani mzee Nyoni na mke wake, kwa kushirikiana na binti yao, kumtoroka yeye, na kwenda kuishi maisha ya ajabu kwenye nyumba ya ajabu huko mjini, akitumia hovyo fedha ambayo Peter mwenyewe aliitolea jasho jingi, kwa muda mrefu katika mazingira magumu,
Kuna wakati wazazi wa Peter waliamua enda kwa mjumbe na kumwomba waende kwa wazazi wa Sada, na mjumbe akawachukuwa wazee wawili watatu, na kwenda nyumba kwa mzee Nyoni, kwa lengo la kuwaeleza yaliyo mioyoni mwao kama wazazi, “mna mpango gani na ili swala alilo lifanya binti yenu” aliuliza mama Peter, yani mke wa mzee Jacob, siku ambayo walienda kuwaona na kuitaji kujuwa mwafaka wa swala la binti yao kutoroka na kwenda mjini, “jamani, sisi tuwajibu nini, kama ni mke tulishawapa, mnategemea sisi tungekuja kuwa saidia kumlea mke wenu asitoroke?” aliuliza mzee Ngonyani kwa sauti iliyo jaa kiburi, “lakini niwazi kabisa Sada aliwaaga wakati anaondoka” alisema mzee Jacob, ambae licha ya kushukuru Sada kujitoa katika maisha ya Peter, lakini walikuja ili kupata ushaidi na kuthibitisha kama Sada ameamua yeye mwenyewe kujiondoa kwenye ndoa, “hivi nyie mliona raha mwanangu aendelee kufubaha kwa huyo mpuuzi wenu, baada ya kwenda mjini kwa wasomi wenzake” ilikuwa ni sauti ya juu yenye nyodo na majigambo, toka kwa mama Sada, kiasi cha wale wazee wengine pamoja na mjumbe kushangaa, “ilo ndilo jibu ambalo tulikuwa tuna liitaji, siyo hapo baadae mje mjifanye hoooo! tunaomba msamaha” alisema mama Peter na kumfanya mama Sada na mume wake yani mzee Nyoni, wacheke kwanguvu, “usitegemee kuwa ilo dua la kuku lita mfikia mwewe, nyie kaeni hivyo hivyo, na msi chulie binti yetu kuwa ata patwa na mabaya” hiyo ilokuwa ni kauri ya mama Sada, “sawa sisi tumesha wasikia, na tunachowaomba wazazi wa Peter, waongeena kijana wao, ili asahau kuhusu Sada na pia kwa mzee Nyoni, na mke, hakika mlicho kifanya pamoja na binti yenu, siyo kitu kizuri kabisa, na make mkijuwa, lolote ambalo lita mkuta Sada huko mjini, akito muhusu Peter wala wazazi wake, litakuwa juu yenu” alisema mjumbe mbele ya wale wazee wengine, “kwahiyo we ulizania tuta wausisha wao, kwani wao wanausika nini na binti yetu, sisi tunachoomba wasije tena wakatufwata fwata, na kumwalibia Sada mambo yake” alisema Mzee Nyoni, na kuwafanya wale wazee pamoja na mjumbe kutikisa vichwa masikitiko, niwazi hawakupendezwa na kile walichokuwa wanakiongea mzee Nyoni na mke wake.
Maisha yaliendelea taratibu Peter akaanza kumsaahu Sada, kwamaana ya kwamba tayari alisha kubari matokeo, ya kwamba mapenzi yao yaliishia pale, hivyo hakuwa na budi kutaendelea kivyake, japo wanawake wengi waliitaji nafasi ambayo Sada aliiacha wazi, lakini Peter akutaka kujiingiza kwenye mapenzi mapema, alipanga kutafuta fedha kwa juhudi zake zote, ili ajenge nyumba nzuri ya kisasa na kuweka umeme wanguvu za jua, ili ata kama akiowa basi mke wake asije kubabaika na mwanaume mwingine mwenye maisha mazuri, kama ilivyo kuwa kwa mama Michael, ambae yote kwa yote, ni kama alisogezaga utamu, yani akufunga nae ndoa.***
Naam miezi mitatu baadae, mida ya saa mbili usiku, maeneo ya majengo karibu na mwisho wa lami, nje ya Msogeze Pub, walionekana watu wengi sana waliokuwa wamekaa kwa kuzunguka meza zao, zilizo tapakaa vinywaji na vyakula, huku wakiburudishwa na sauti kubwa ya music, ukiachilia watu waliokaa kwa pea ya wawili wawili, yani wakike na wakiume, ambao ni wazi kabisa kuwa ni wapenzi, pia walionekana waliokaa mmoja mmoja, kama siyo mwanaume alie kuwa anapata kinywaji huku anachezea simu yake, basi ni mwanamke alie kuwa anakunywa maji au soda, huku anazungusha macho kutazama huku na huko, mfano wa chui au samba aliepo kwenye mawindo.
Ilinivutia meza moja ambayo kulikuwa na wanawake wawili, ambao vichwani mwao walikuwa wamatundika kovia za nywele za bandia, ambazo mwoneknao wake aukuwa mzuri sana, kutokana na uchakavu wake, pia walikuwa wamevalia nguo ambazo ni nzuri kwa miji au mikoa yenye joto kali, lakini siyo kwa ukanda huu wa nyanda za juu kusini, ukiacha jivi brauzi, vilivyo acha mabega yao na kwapa wazi, pia walivaa vinguo vifupi na vya kubana, ambavyo viliangaza adi rangi za nguo zao za ndani, walikuwa wamekaa pamoja wana chupa zao za maji, ambayo kila walipopeleka mdomoni kuyanywa walikuwa wanakunja mdomo, mfano wa mtu anae kunywa pombe kali, bilashaka na wewe ungeshawishika kutazama chini, ambapo ungeona chupa moja ya pombe kali, ikiwa imelala chini bila kitu ndani, inamaana yale kwenye chupa hayakuwa maji, ila ni vilevi ambavyo vimewekwa ndani yake, ukiachilia vilevi na uvaaji wao pia nilivutiwa na maongezi yao, “mh! leo naona watu wamechalala, ajitokezi ata mmoja” alisema mmoja kati ya wale wanawanawake wawili, ambao mwonekano wao, ulionyesha kuwa ni dhaifu, nazani ni kutokana na pombe wanazo tumia, “tatizo Queen we nae una wasiwasi sana, hivi unakumbuka juzi tuliopoa saa sita za usiku?” aliuliza yule mwingine, “lakini leo hatuna ela kabisa, tukimaliza hizi tutakaa bila vinywaji” alisema yule alie itwa Queen, ambae kwa sasa tusingeweza kumwona dura yake, kutokana na giza la pale walipokuwa wamekaa, “sasa inabidi tunywe taratibu mpaka tuopoe” alisema yule mwingine na hapo kikapita kimya kifupi, kabla Queen ajavunja ukimya ule, “unakumbuka zamazile tunakaa bomba mbili?” aliuliza Queen, huku anaangaza macho upande wakuingilia pale msogeze pub, “yani ilikuwa raha sana, tusinge pigwa na baridi hapa, mfano raha za kule mfaranyaki kabla atujahama?” aliuliza yule mwingine, huku wanagongeana mikono, “yani we acha tu, watu tuna kunywa navichupi tu, mnatiana kwa raha zenu, siyo kwa biashara” aliongea Queen, wakionyesha kufurahia kumbu kumbu hizo, “alafu nime kumbuka hivi yule mumeo vipi ulipata habari zake tena?” aliuliza yule mwingine akionyesha kukumbuka jambo, “nasikia yupo tu, huko kijijini na maisha yake” alisema Queen kwa sauti ya kupuuzia, mfano wa mtu ambae akutaka kuendelea kuzungumzia habari ile, huku macho yake yakiwa yameilenga meza moja ambayo walikuwa wamekaa wanaume wawili, “dah! alipewa kipigo, mpaka nikajuwa tumeuwa….” alisema yule mwingine, kabla aja katizwa na Queen, “ngoja nijipitishe kwa wale jamaa” alisema Queen na kuelekea upande wa chooni, akipita mbele ya meza ile ambayo, ilikuwa na wanaume wawili, waliotandaza vinywaji mezani, ambavyo walikuwa wanavifakamia huku napiga story mbili tatu.
Queen alitembea taratibu, huku anatikisa vijikalio vyake vodogo vilivyopotea kwa ugumu wa maisha, akipita karibu kabisa na meza ile ya wale jamaa…..Endelea kufwatilia mkasa huu.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU