KIAPO CHA MASIKINI (10)

SEHEMU YA 10

ILIPOISHIA SEHEMU YA TISA : Alisema Queen kwa sauti ya kupuuzia, mfano wa mtu ambae akutaka kuendelea kuzungumzia habari ile, huku macho yake yakiwa yameilenga meza moja ambayo walikuwa wamekaa wanaume wawili, “dah! alipewa kipigo, mpaka nikajuwa tumeuwa….” alisema yule mwingine, kabla aja katizwa na Queen, “ngoja nijipitishe kwa wale jamaa” alisema Queen na kuelekea upande wa chooni, akipita mbele ya meza ile ambayo, ilikuwa na wanaume wawili, waliotandaza vinywaji mezani, ambavyo walikuwa wanavifakamia huku napiga story mbili tatu.
Queen alitembea taratibu, huku anatikisa vijikalio vyake vodogo vilivyopotea kwa ugumu wa maisha, akipita karibu kabisa na meza ile ya wale jamaa….Endelea…..
Ambao nikama alivyo tegemea waligeuka kumtazama, na yeye akajifanya kama ajawaona akaelekea zake chooni, ambako ambako hakukaa sana, akatoka na kupita tena pale pale kwa wale jamaa wawili ambao walikuwa wamesahau vinywaji vyao, kwa kumkodolea macho mwana dada Queen, ambae nikama alizidi kutembea kwa kutikisa vile vijikalio vyake kama ndimu, “hoya we mrembo, ebu njoo mala moja” hapo Queen akusubiri aitwe mala ya pili aligeuka mala moja na kutazama ilikotokea sauti ile ya kiume, “unaniita mimi anko?” aliuliza Queen kwa sauti flani hivi yenye swaga za kisister duu, “ndiyo ni wewe au hupo na mtu” aluliza mmoja wao ambae wakati anaongea ungeweza kuona pengo moja lajino mdomoni mwake, pengo ambalo ni wazi lilikuwa ni lahajari, maana juu yam domo usawa wa pengo lile, apalionekana kovu, ambalo kama siyo alipigwa basi lilikuwa nila kugongwa na kitu flani, kigumu, “wala sina mtu, nipo na rafiki yangu” alijibu Queen, na wale jamaa wakatazamana, kisha wakapeana ishala, ya kukubariana, yani walitikisa vichwa vyao juu nachini, kisha wakamtazama Queen, “vipi mnaweza kuja kujiunga na sisi tuwe pamoja usiku waleo?” aliuliza yule mwenye pengo, hapo kidogo Queen akajifanya kama ana fikilia kidogo, “mmmh! Ngoja kwanza nikaongee na mdogo wangu, maana hapa tunamsubiri dada yetu, akikubari tutakuja” alisema mwanamke huyu, alie jiita Queen na kuondoka kuelekea kwenye meza aliyo mwacha rafiki yake.
Nazani msomaji unafahamu kwamba Queen alikuwa anazuga tu, sababu walikuwa wanaitafuta sana hii nafasi, ata kule kwenye meza alikaa kama dakika mbili tu na kuwote wakainuka na kuamia kwenye meza ya wale jamaa, ambao waliwapokea kwa kugawana, Queen alienda kwayule mwenye pengo na mwenzie alienda kwa yule mwingine, “mtakunywa vinywaji gani, wakina dada” aliuliza mhudumu, ambae alikuja kuwahudumia, “mh! Queen mimi labda nile kwanza” alisema yule mwingine, hii aikuwashangaza wale jamaa, nikawaida kwa baadhi ya wanawake kusikia njaa pale anapo pata mwanaume, “agizeni wakati anaenda kuwaitia mtu wajikoni” alishauri yule mwenye pengo nao wakaagiza bia, huku wakiomba kaitiwe mtu wajikoni, ambae aliwai kabla ata ya vinywaji avijafika, “he! Mama Michael, ni wewe au nakufananisha?” ilisikika sauti ya mhudumu wachakula wakike, wa pale Msogeze pub, huku anamtazama Queen, ambae aligeuka kwa mshtuko na mshangao, kisha akamtazama alie muita, ambae ni mhudumu wa jikoni, alimkata jicho flani kali sana lililo jaa mahonyo, huku ame mkazia usoni, kiasi flani nazani yule mhudumu wa jikoni alielewa somo flani, maana anilijishtukia mwenyewe, “hooo! samahani, dada umefanana na dada mmoja hivi wa kijijini kwetu, sijuwi niwahudumie chakula gani, maana kuna…” alisema yule mhudumu wajikoni, ambae rafudhi yake ni ya kindendeule, kabira lenye makazi yake wilaya ya namtumbo, huku taja ambatanisho la horodha ya vyakula, vinavyopatikana mahali pale, wakina Queen wakataja chakula walicho itaji, kisha yule mhudumu wakike jikoni akaondoka zake, huku akipishana na mhudumu wa vinywaji alie beba bia ambazo alikuwa anazipeleka kwenye meza ya kina Queen, ambao walipewa viunywaji vyao na kaunza kunywa taratibu, wakisahau kauri zao za kwamba hawawezi kunywa bila kula, “unaitwa nani mrembo?” aliuliza yule jamaa mwenye pengo, ambae alikuwa amekaa karibu kabisa na Queen, “naitwa Queen wewe je unaitwa nani?” aliuliza Queen kwa sauti flani yenye swaga za kujisexisha, “na itwa Emma, ninafanya kazi kwenye kwa Kalo, siunamjuwa?” alisema kijana yule ambae kimwonekano ni mtu mwenye kujiweza kifedha, “namfahamu sana, si yule mzee mwenye maduka makubwa” alisema Queen, huku anaendelea kujinywea bia yake, “na wewe mbona uniambii unaitwa nani?” aliuliza yule kijana mwingine alie kaa na rafiki yake Queen, “naitwa Rose, na wewe uniambie unaitwa nani” alisema yule mwanamke pasipo swaga za kujisexisha kama Queen, “hooo! jina zuri sana, mimi naitwa Hussen, ukiona jau, unaweza kuniita Janja” alisema yule kijana mwinginea mbae uitaji ata dakika kuitambua tabia yake ya ujanja ujanja, na pengine ukorofi waghafla ghafla, “lakini bado amjatuambia nyie mnafanya kazi wapi, mnaishi wapi” aliuliza yule mwenye pengo alie jitamburisha kwa jina la Emma ikiwa ni kifupi cha Emanuel.
Kusikia swali ilo sijuwi kwanini waschana awa wawili, kila mmoja akatabasamu huku anatazama chini, kabla Queen ajajibu swali lile, “kiukweli hatuna kazi yeyo, zaidi tunaishi na dada yetu, hapo majengo mitumbani, (jina la mtaa)” alijibu Queen, na wakati huo huo wakamwona yule mhudumu, wa chakula anakuja huku amebeba sinia lenye sahani kadhaa, zilizo sheheni mapocho pocho, “hooooo! Sawa, hakuna shida yoyote, kama utakuwa mtulivu na mwaminifu” ndivyo alivyo eleza Emanuel, ambae kama umemwelewa alikuwa anamaanisha anaitaji kuwa na Queen kimapenzi, “kwahiyo unataka niwe mpenzi wako?” aliuliza Queen huku anajifanya kucheka kiaibu aibu, “yes, sina mpenzi kwa sasa nataji kuwa nawewe” alisema Emanuel, kwa sauti iliyoonyesha msisitizo kwa kile anacho kisema, “mh! sawa baby, kuhusu uaminifu wala usiofu kwanza mimi sina mwanaume, nilie kuwa nae nimeachana nae mudamrefu” alisema Queen, kwa sauti iliyopoa kidogo, ungesema kuwa alikumbuka machungu, “mh! mbona umepoa, kwani mumeo uliacha nae vipi?” aliuliza Emanuel, kwa sauti ynye shuku na shahuku.
Hapo Queen alitulia kidogo kama anapoodha machungu, ya hisitoria ya ndoa yake, “unajuwa mimi baada ya kumaliza foem four, nikalazimishwa kuolewa, na mshamba mmoja hivi huko kijijini, na mbaya zaidi ile kuolewa nae tu, akanipachika mimba, na hapo ndipo alipoanza kunipa mateso, yani baby we acha, alikuwa aninunulii chochote siyo nguo tu, ata nguo za ndani sikuwa na nunuliwa, wakati mwingine ananisingizia nime mwibia ela, hapo ataanza kunipiga weeeee, mpaka akishocha ananifukuza mimi na mtoto, kisha yeye anaenda kulala pasipo kujali mimi nitalala wapi na mtoto, mala nyingi akilewa mimi ndie ngoma yake, ananipiga mpaka anapolidhika ndio anaenda kulala, alikuwa anipi ela ya chakula, wakati mwingine ananisingizia nimemwibia ela, wakati mtu mwenyewe masiki ela zenyewe za kuokoteza, mwisho akanifukuza na mimi nikaona isiwe tabu, nikamchukuw mwanangu na kumpeleka kwa mama, alafu nikaondoka zangu kuja huku mjini kwa dada” alimaliza kusimulia Queen kwa sauti iliyojaa udhuni na machungu, kiasi cha kumsisimua kila mmoja kasoro mwenzie Rose, sijuwi sababu alikuwa anaifahamu ile story, au alikuwa anafahamu ukweli harisi, “pole sana baby, huyo jamaa nimshenzi sana, anaitaji adhabu kali sana” alisema Emmanul, kwa sauti ambayo siyo uchungu pekee ila pia ilijawa na hasira kali, tena huyo mpuuzi siku nikimwona sidhani kama atachomka akiwa anatembelea miguu yake miwili, afai kuishi” safari hii alisema Janja, kwa sauti iliyojaa hasira na machungu ya hali ya juu, “sanaaa, huyu mpuuzi anapaswa kulipia unyama alioufanya kwa mrembo wangu” alisema Emanuel, huku wakiendelea kula na kunywa, sijuwi kwanini Queen alijisikia raha sana moyoni mwake, baada ya kusikia maneno hayo ya wanaume wale wawili, wenye hasira.
Naam lisaa limoja baadae wakiwa wanaendelea kunywa, tayari wamesha maliza kula, wanaongea kwa furaha na vicheko, huku wanafanyiana michezo ya kimahaba, ungesema, ni wapenzi wa muda mrefu, mala Queen akamwona yule mhudumu wa kike wajikoni, akielekea upande wa chooni, “baby ngoja niende chooni mala moja” alisema Queen huku anainuka na kuelekea chooni, “na mimi nukapunguze maji kidogo” alisema Rose, huku anainuka na kumfwata Queen, wote wakawa wanaelekea upande wa chooni, “Queen leo umetisha, jinsi ulivyotoa historia ya huyo bwana wako wakijijini, mpaka umewajaza hasira wale mabuzi” alisema Rose, huku wanaendelea kutembea, kuelekea chooni, “wacha wa mbomoe yule mpuuzi” alisema Queen, kisha ukaita ukimya mfupi, kabla Queen ajaongea tena, “hivi Rose unamwonaje yule mpuuzi, nikweli anataka kuwa na mimi au nipombe tu zime mtuma?” aliuliza Queen huku wanaingia chooni, “weee! ata kama ni pombe we mng’ang’anie tu! maana huyo jamaa wanae mfanyia kazi ana mbumba, (fedha) nyingi sana” alisema Rose, na wakati huo huo wakamwona yule mschana mhudumu wa jikoni anatoka kwenye mmoja ya mlango wa choo, “Kadara” aliita Queen huku anamzuwia yule mwanamke alie mhudumu wa jikoni, “hoooo! kumbe kweli ni wewe dada Sada, nilizani nilikufananisha” alisema Kadara kwa sauti iliyojaa mshangao………

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata