
SEHEMU YA 11
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI : “wacha wa mbomoe yule mpuuzi” alisema Queen, kisha ukaita ukimya mfupi, kabla Queen ajaongea tena, “hivi Rose unamwonaje yule mpuuzi, nikweli anataka kuwa na mimi au nipombe tu zime mtuma?” aliuliza Queen huku wanaingia chooni, “weee! ata kama ni pombe we mng’ang’anie tu! maana huyo jamaa wanae mfanyia kazi ana mbumba, (fedha) nyingi sana” alisema Rose, na wakati huo huo wakamwona yule mschana mhudumu wa jikoni anatoka kwenye mmoja ya mlango wa choo, “Kadara” aliita Queen huku anamzuwia yule mwanamke alie mhudumu wa jikoni, “hoooo! kumbe kweli ni wewe dada Sada, nilizani nilikufananisha” alisema Kadara kwa sauti iliyojaa mshangao………Endelea
Wakati huo Rose, ambae akushangaa lolote, alikuwa anaingia chooni, akiwaacha Queen na Kadara waongea, “nimimi huyu huyu, vipi wewe umekuja lini huku mjini?” aliuliza Queen ambae nikweli mama Michael au Sada kama tulivyoona akiitwa, “na siku tatu sasa hapa mjini, amenileta dada joy, yeye yupo kwenye ile bar karibu na sokoni” alisema Kadara, akionyesha kumfurahia Queen ya ni Sada, “sasa sikiliza Kada, ukikutana na mtu huku mjini, usimwite hovyo hovyo, wenzako tunamajina yetu huku, na pia atutaki kujulikana tulipotokea wala maisha yetu ya nyuma” alisema Queen kwa sauti ya chini, yenye kuonya, na kutaadharisha, “sawa dada Sada, sasa hivi unaitwa nani?” aliuliza Kada, ambae kirefu chake ni Kadara kwa maana ya mschana mdogo, akiwa mkubwa uitwa mdara, “naitwa Queen, we ukiniona popote niite hivyo” alisema Queen ambae aliitwa mama Michale, ambae kiukweli alionakana kuwa ni mwanamke anaishi kwa kutegemea mwili wake, asa sehemu yake nyeti, “sawa wala usiwe na wasi wasi dada Queen” alisema Kadara huku akicheka kidogo, na wakati wanaachana, Kadara akauliza “sasa dada Queen, lini unataenda kumtazama mwanao Michael, maana amekuwa mkubwa siku hizi” alisema yule mhudumu wa jikoni, “achana nao kwanza tule bata huku mjini, we mwenyewe simeona” alisema Queen kwa sauti ambayo ukiachana na ulevi, pia ilijaa majingambo na majisifu, “mwimwenzio nitaenda msimu wa malipo ya tumbaku, kunakuwaga naela nyingi sana kule” alisema Kadara, huku anaondoka zake, kuelekea nje ya choo.
Naam baada ya kutoka chooni walirudi na kujiunga na wapenzi wao, kisha wakaendelea na starehe zao, “sasa mke wangu, leo si tuna lala wote siyo” aluliza Emanuel, kwa sauti ya chini iliyo tulia, huku akimtazama usoni, mwanadada Queen au Sada kama ambavyo sisi tuna mfahamu, “niwewe tu baby, mimi ni mali yako” alisema Queen, kwa sauti flani ya kujisexisha, huku ana jifanya kuona aibu flani, “hapo ume nena, na leo isiwe mwisho, mimi na wewe sikuzote, au unasemaje?” alisema Emanie, ambae masaa mawili mbele, masaa mawili baadae aliiwaongoeza wenzake, kuelekea kwenye Toyota IST, safari ya mahenge C, ambako ni kwenye makazi ya vijana awa wawili.
Emmanuel Msengi ni kijana mtihifu wa bwana Kalonga, akiwa ni kijana mwaminifu na mtiifu namba moja katika shughuri haramu zote za bwana Kalo, ni kijana ambae miezi kadhaa iliyopita alipoteza jino lake kwa ngumi toka kwenye mkono wa kijana mmoja msahamba mshamba toka kijijini, akiwa anajaribu kupora begi, toka kwa mwanadada mrembo Careen.
Emanuel au Emma kama anavyopenda aitwe, ukiachilia kutumwa kazi za kiarifu na boss wake huyo bwana Kalonga, pia kijana huyu, alikuwa anatumika sana katika kazi za hatari kama vile kuiba kwenye majumba makubwa, maduka na ofisi ndogo ndogo za huduma za kifedha, za maitandao ya simu, nawakati wingine kufanya mauwaji kwa maadui wa boss wake yani bwana Pitus Kalonga, au Kalo kama walivyokuwa wanamwita marafiki zake, naposema maadui ni kwamba, mala nyingi walikuwa ni watu ambao amezulumiana nao katika iashara haramu ya dawa za kulevya, au anaitajikupora malizao ambao lazima auwe ndio azipate, na ata sasa anamtumia kijana huyu huyu Pengo, kumsumbua mwana dada Careen ili kulipata penzi lake, au kumfanyia kitu ambacho kitausuuza moyo wake, na kuondoa machungu ya dharau alizo letewa na mschana huyu tajiri.
Nauo ndio ulikuwa mwanzo maisha ya mapenzi kati ya Emmanuel na mwana dada Sada, au Queen kama alivyojiita huku mjini likiwa ni jina la mauzo, urafiki wao ulikuwa ni mzuri kwao maana kiukweli waliendana kwa mambo mengi sana, ikiwa tabia mpya ya utaperi na uongo, ambayo Emmanuel alikuwa nayo na sasa alikuwa anamfundisha Sada kuwa na roho ngumu, na kuto kuona huruma kwa mtu yoyote pale anapoitaji kitu, “nakuaidi mke wangu, boss akifanikiwa mpango wake mkubwa amesema ata nipatia fedha ndefu sana ambayo nitakufungulia duka kubwa la nguo zakike” moja ya ahadi za Emma, ambazo zilimfanya Sada azidi kumpenda kumng’ang’ania Emma, huku akimini kuwa hipo siku atakuwa na biashara yake ambayo itamfanya anunue gari lake “yani nitaenda mwanammoga na kusimama nje ya zile mbavu za mbwa za Peter na hicho kifaranga chake, alafu wakitoka nje kushangaa gari, naondoa kwa nguvu nawatimulia vumbi” alisema Sada siku moja akiwa anaongea na Kadara yule mschana mhudumu wa vyakula pale Msongeze Pub, “basi hapo Peter itamuuma sana, ila bora umchukue mwanao Michael nae aje kula raha” alishauri yule mschana mhudumu wa chakula, ambae ametoka nae kijiji kimoja, ushauri ambao ilidharauliwa vibaya mno na Sada, “mh! kaache kajifunze kulima uko na baba yake, kaje kufanya nini huku, si kata niwekea usiku tu huku” alisema Sada, katika maongezi hayo yaliyokuwa yanafanyika ndani ya vyoo vya wanawake, pale msogeze pub ambako, Sada na mwanaume wake walikuwa ndio sehemu yao kubwa ya kupatia chakula cha jioni, na pombe, wawili awa walipeana namba za simu, kwa ahadi ya kwamba watakuwa wanaendelea kuwasiliana, japo aikuwa kama hivyo, maana kila mmoja alikuwa na mishe mishe zake.***
Miezi sita baadae Peter alipata malipo ya awamu ya pili, ya tumbaku alizouza msimu uliopita, million tatu na laki tano, ambayo niwazi kabisa isinge weza kutimiza malengo yake aliyo jiwekea mwanzo na kushindwa kuyatekeleza baada ya Sada kumwibia fedha na kukimbilia mjini, hivyo aliifadhi fedha alizopata, ili asubiri na msimu wa mwaka huu, akishalipwa ajenge nyumba yake na kununua baadhi ya dhana za kilimo, ambazo zinge msaidia katika kilimo chake.
Wakati huo tayari mtoto Michael alikuwa amesha zowea maisha bila mama, alikuwa ni mwenye furaha na amani, siku za jumapili, au msimu ambao shuguri za kilimo zilikuwa zime pungua, Peter alikuwa anamchukuwa Michael na kushinda nae nyumbani, na sasa alijitaidi kumnunulia nguo na viatu vizuri, pamoja naviti vizuri ambavyo daima watoto upenda kuchezea, kwa kifupi aliamishia mapenzu yote kwa wmanae huyu,m na sasa alikuwa anawaogopa wanawake kama kaa la moto.***
Siku tano kabla Peter ajaenda kuchukuwa fedha zake za malipo ya tumbaku, siku hiyo alimchuuwa mwanae Michael na kwenda nae Namtumbo mjini, kwaajili ya kufanya manunuzi madogo madogo, ikiwa pamoja na nguo nzuri kwaajili yake na mwanae, ambae sasa alikuwa na miaka miwili, na wakati wakiwa mtaa wa Luwinga, madukani, wanaunua baadhi ya vitu walivyo kusudia, ikiwa ni maandalizi ya safari ya mjini, ambayo walipanga, kwenda mjini songea, mala baada ya malipo, ilikununua vitu vingi ikiwa na vifaa vya ujenzi wa nyumba yao mpya, pamoja na vitu vya ndani na vifaa kwaajili ya vifaa vya umeme wa jua, hakika kijana Peter Jacob, alipania kubadiri maisha yake na kuyafanya bora zaidi.
Sasa basi wakati flani ananunua kiatu kizuri kwaajili mwanae Michael, mala aka“shem… shem…” ilisikika sauti ya kike toka mita chache nyuma yake, lakini Peter alijisumbua ata kugeuka au kuifwatilia hiyo sauti, akaendelea kufanya malipo ya kiatu kizuri cha mwanae, ni kweli Peter hakuwa na muda wa kuifwatilia sauto hiyo sababu siyo tu kutokuwa na vigezo vya kuitwa shemeji, pia kijina huyu, ata wakati akiwa na mke wake Sada, hakukuwa na mtu yoyote alie wai kumwita shemeji, sasa leo atokee wapi, Peter aliingiza mkono mfukoni, na kutoa kitita cha fedha, alafu akachomoa noti mbili za elfu kumi kumi, na kumpatia muuzaji, na wakati anakabidhiwa chenji na kiatu, akashtuka akiguswa begani, mguso ulioambatana na sauti ile ile ya kike, “shemeji mambo?” Peter aligeuka kumtazama huyo mwanamke anaemwita shemeji, “hooo! Kadara mambo vipi?” alisalimia Peter kwa uchangamfu, ukweli nisiku nyingi zilikuwa zimepita bila kumwona mwana dada huyu, ambae ni mmoja kati ya waschana ambao waliekea mjini na kupotelea huko, pasipo watu huku kijijini kujuwa wanakazi gani huko mjini.
Naam hapo mschana huyu ambae anaitwa Kadara, akaanza kuongea kama ile mashine ya kushonea nguo, “safi tu shem, za masiku…. Hii jamani Michael amekuwa mkubwa… niamkie mwanangu….. jamani shem umezidi kupendeza….. vipi lakini Sada unawasiliana nae, maana anakukumbuka sana” kadara aliongea maneno mengi mfululizo, pasipo kutoa nafasi ya kupatiwa majibu, ukweli Peter alijikuta anasisimshwa na habari ile, iliyomhusu mke wake wa zamani, ambae alimtoroka na kukimbilia mjini, hapo hapo akajikuta anatamani kukutana na mwanamke huyo, ambae baada ya muda mrefu leo hii ameambiwa kuwa anamkumbuka, “hapana sijawasiliana nae nina mwaka sasa maana sina……” alijibu Peter, huku anamtazama Kadara ambae alionekana kuwa alikuwa safarini, kama siyo anaingia pale namtumbo basi ndio alikuwa anaondoka, na kabla ajamaliza kujibu, tayari Kadara alisha dakia, “jamani shemeji vibaya hivyo, Sada wenzako anakukumbuka kila siku wewe na Michael, au auna namba yake, ngoja basi nikupatie namba yangu, sifuri saba nne mbili mbili…” alisema Kadara, kwa haraka, na kumaliza kutaja namba, kabla ata Peter ajatoa simu mfukoni, “samahani shemeji nitajie tena hizo namba” alisema Peter huku anaweka sawa simu yake tayari kupokea namba za simu, “kumbe ujaandika basi ebu nipatie namba yako, nitakupigia mimi” alisema Kadara ambae kiukweli ata mwonekano wake, ulikuwa ni mzuri na wakisasa tofauti na miezi kadhaa nyuma, wakati anatoka kijijini Mwanammonga, alisema Kadara huku anafungua pochi yake na kutoa simu yake ya tachi, kuanaza kuandika amba iliyokuwa inatajwa na Peter, “nitakupigia shemu, lakini kwanini umekaa tu huku jikjinin wakati unmake mzuri anakulilia huko mjini, au umesha owa mwanamke mwingine” alisema Kadara, wakati anasave namba ya shemeji yake huyu, yani Peter, ambae niwazi alionekana kupendezwa na taarifa zile za Kadara, “hapana sijaowa” alijibu Peter, kwa haraka sana, kabla ajamyajia namba zake za simu, “hii namba hipo whatsapp?” aliuliza Kadara huku anasave namba kwenye simu yake ya kisasa, wakati anaona vyema kabisa simu ya Peter ni ndogo ambayo aina uwezo wa kutumikisha mitandao ya kijamii, wenyewe wanaita kitochi, “hapana kisimu chenyewe siunakiona” alijibu Peter, kwa sauti yenye aibu kidogo, ambae aliongezea kuwa, “ila kesho week ijao nitaenda mjini, nita nunua simu kubwa” alisema Peter kama vile anajitetea, “basi wala usijari mimi leo ndio naondoka kuelekea mjini, ukija unitafute sawa?” alisema Kadara huku wakati wanaagana na Kadara akaelekea stendi ya bus, akimwacha Peter pamoja na mwanae Michael, wakisimama huku wakimsindikiza kwa macho Kadara, huku Peter moyoni mwake akiwa mwenye furaha kubwa, kusikia kuwa Sada anawakumbuka yeye na Michael, walimtazama mpaka alipotokomea zake, kisha Peter akamtazama mwanae Michael, “mwanangu sasa tunaenda kumrudisha mama yako, ametambua makosa yake, na sasa anatukumbuka sana” alisema Peter huku anamnyayua mwanae, na kuchukuwa mfuko wa vitu alivyonunua wakaanza safari ya manunuzi, Michael ambae akuwa anatambua kuhusu mtu anae itwa mama, alikodoa macho yake akimtazama baba yake, ambakiukweli hakujuwa kuwa kinachofwata mbele nizaidi ya burudani kwake. ………
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU