
KIAPO CHA MASIKINI (13)

SEHEMU YA 13
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA MBILI: aka panda kitandani, ambako mwanae Michael alikuwa amesha lala muda mrefu uliopita, akaiwasha simu yake hiyo na kusubiri kwa dakika kama mbili, kabla ajasikia jumbe mbili zikiingia kwa kufwatana, akuchelewa kuzifungua jumbe zile, ambazo zilikuja kwa namba ngeni, ya kwanza kabisa ambayo ndiyo ya mwisho kutumwa, iliandikwa hivi, “basi ukiwasha simu nitafute, nimewamiss sana wewe na Michael, ujumbe ambau ulimshtua sana Peter, ambae alitazama ile sms nyingine ambayo ndiyo ilikuwa yakanza kutumwa, “mambo za kunisusa mume wangu, mimi mama Michael” hapo Peter alijikuta anaachia tabasamu pana la furaha….Endelea……
Samba na simko mwili mzima, akihisi kitu kama nyenye ana tembea kwenye kichwa wazi kilichopo ndani ya bukta yake, na kumwinua wima wima, Piter aka bofya namba ile haraka kwa aajili ya kuipiga, nayo ikaanza kuita mala moja, iliita mpaka ikakatika bila kupokelewa, akaipiga tena, lakini safari hii aikuita sana, ikakatika ikifwatiwa na sauti ya kike, “namba unayopiga inatumika kwa sasa, jaribu tena baadae” kwakuwa awakumtajia baadae ya saangapi, Peter akusubiri zaidi, akaipiga tena ile namba, huku moyoni akiwa na hamu kubwa ya kusikia sauti ya mke wake, lakini ikawa vile vile ikakata, na kufwatiwa na ile sauti ya kike kwamba simu inatumika, hapo akaona bola asubiri dakika moja kisha apige tena, lakini ata dakika aikutimia, Peter akasikia ujumbe unaingia kwenye simu yake, akaufungua haraka sana mana alijuwa fika kuwa utakuwa unatoka kwa mama Michael, “nime lala mume wangu, nitakupigia kesho mapema tunza chaji” ndivyo alivyo sema hiyo sms, ukweli Peter alifalijika sana kwa sms ile, alifurahi kwa kuona mke wake anarudisha mapenzi kwake, ukweli alitamani kumshirikisha mtu mwingine yoyote yule, ili alifahamu jambo lile, ambalo mwanzo alipanga kufanya siri, mpaka atakapo maliza ujenzi, ndipo aliweke wazi na kumrudisha mke wake, “poa mke wangu jitaidi basi hiyo kesho usisahau, maana nimekumiss sana” hiyo ni sms aliyo andika Peter, na kuituma kwa mke wake, yani Sada Nyoni, kisha akamtazama Michael alie kuwa amelala pembeni yake, pasipo kujuwa kinachoendelea kwa baba na mama yake, ambae akuwa na kumbu kumbu yoyote juu yake, “Michael sasa tunamrudisha mama yako, sasa familia itakamilika” alisema Peter huku anamtazama Michael, unajuwa kuna wakati nawaza kuwa kama Michael angekuwa macho pengine angemshauri jambo baba yake, lakini sijuwi ingewezekanaje, maana bado Michael hakuwa na uwezo wa kuchambua mambo, japo alikuwa anaweza kuongea kidogo.
Peter alilala akiwa mwenye furaha kubwa sana moyoni mwake, akuwaza mke wake aliipataje namba yake na wala akujiuliza aliambiwa nini wakati anapewa namba ile, na wala akujiuliza kwanini mke wake abadirike ghafla namna ile.***
Naam mida hii mschana mrembo Careen, alikuwa amekaa kwenye kochi kubwa zuri chumbani kwake, macho kwenye TV, mkono wa kushoto akiutumia kushika grass yenye mvinyo mweupe uliotengenezewa kwa nazi toka nchini mbogo Land, huku mkono wa kulia ukiwa umeshika simu, ambayo alikuwa anaiperuzi, “mh! hivi awa JJ Campany, wana nia ya kweli ya kufanya uwekezaji, au wana lao jambo?” alijiuliza Careen mala baada ya kukumbuka juu ya kikao ambacho alitakiwa kukifanya kwenye hotel ya Makimakuluga, kikao cha biashara, ambacho bado akuwa anajuwa wawekezaji wale wa JJ, wanataka kuwekeza kwa kiwango gani” aliwaza Careen, ni kuhusu kikao ambacho alitakiwa kukifanya na wawekezaji flani wa campuni ya JJ, waliotaka kuingia nae mkataba, wakati huo huo Careen aliakuwa anawaza namna ya kuandaa matangazo juu ya mzigo mpya wa vito vya thamani, alivyo vipokea leo hii toka nchini kwao, kutoka kwa rafiki yake wa utotoni, king Elvis 1, “safari hii nita dhamini, miss Ruvuma, itasaidia ata kutatangaza mavazi mapya na mitindo mipya ya viatu, toka chini kwetu” ndivyo alivyo waza Careen, ambae akujuwa kuwa kikao cha uwekezaji alicho alikwa, ni mtego wa kumnasa iliaibiwe funguo za ofisi na makabati ya chuma, anayo tunza fedha na vito vya thamani.****
Mida hii ya saa tatu za usiku, kwa mjini ilikuwa kama ndio saa nane mchana, maana kulikuwa kume changamka sana, asa maeneo ya kuanzia Delax Hotel, MAKIMAKULUGA Motel, Mtini pub, kushuka mpaka Msogeze Pub, kule majengo mwisho wa lami, ambapo nje ya Msogeze pub, watu walikuwa wengi wamekaa kwa kuzunguka mezao, kwa pea kuanzia wawili wawili mpaka wanne wanne, wanaume kwa wanawake.
Kwenye meza moja pembezoni mwa eneo ili, la mbele la jjengo la msogeze Pub, walikuwepo wakina Emmanuel, Sada, Rose na kijana Hussein, au Janja kama wanavyo mwita wenzake, “kaka ilidiri siyo la kukosa, lazima liende kama lilivyo pangwa, vinginevyo boss ato tuelewa” alisema Emma, akimtazama Hussein, wakati huo Sada alikuwa anatazama simu yake mala kwa mala, kuangalia kama Peter angetuma ujumbe mwingine, maana tayari alisha mweleza kuwa wata wasiliana kesho, ila akumiani kama angejibu ujumbe ule.
Nikweli mawazo yake yalikuwa sahihi, maana uliingia ujumbe kimya kimya, niwazi Sada alikuwa ameondoa sauti kwenye simu yake, hakutaka mtu mwingine agundua mawasiliano yake na Peter, Sada au Queen akaufungua mala moja, “poa mke wangu jitaidi basi hiyo kesho usisahau, maana nimekumiss sana” ulikuwa ni ule ujumbe uliotumwa na Peter, na baada ya kuusoma akaiweka simu kwenye pochi yake, “kaka kesho achomoki yule Malaya” alisema Husseni, kwa sauti ya kujiamini, huku wakiendelea kunywa bia zao, “Queen namba nisindikize chooni” alisema Rose huku anainuka toka kwenye kiti chake, na Queen nae akainuka, “usiseme nikusindikize sema twende, maana ata mimi mwenyewe ulisha nibana” alisema Queen huku akiongoza njia ya chooni, “rose unamkumbuka yule mschana aliekuwa anahudumia chakula hapa” aliuliza Sada wakiwa wanaelekea chooni, “nani yule aliekuita Sada siku ile?” aliuliza Rose, “huyo huyo, basi mwenzangu, leo si nimemkuta anafanya shoping ya nguvu, yani ya mamillioni ya fedha” alieleza Sada, ambae alimsimulia Rose, kla kitu, mpaka kuhusu Peter, kwamba anafedha nyingi na bado ana onyesha kuitaji kuwa nae, “weee! umemfanya nini kaka wawatu, yani yote yale uliyo mfanyia, nilitegemea sasa angekuwa na RB yako anakusaka kila kona, alafu unasema yupo tayari kurudiana na wewe?” aliuliza kwa mshangao Rose, wakati huo walikuwa wanaingia chooni, “unanichezea mimi wewe Peter hapa amefika” alisema Sada kwa majigambo, “ila afadhari wangu, bora urudiane na mumeo mlee mtoto wenu, mimi naona kama wakina Emma wenyewe hawana faida yoyote zaidi ya pombe” alisema Rose ambae akujuwa mwenzie anawaza nini, “nani arudiane na yule mshamba, yani hapa nitakacho mfanyia yeye mwenyewe atajuta kunifahamu” alisema Sada kwa sauti flani ambayo ungesema anatania, sijuwi kwaajili ya bia alizo kunywa ama ni nini, “jamani Sada, yani mtu amekuvumilia muda wote huo, alafu wewe unataka kumwibia ela zake tena?” aliuliza Rose kwa sauti iliyuojaa uzuni nyingi, na msikitiko yasiyo kifani, “kwanini yeye alivyo nizalisha, unajuwa mimi ningeolewa na nani?” aliuliza Sada kama mtu asie jali chochote, “yani Sada ukweli kama ningemfahamu huyo mume wako, ninge mzuwia asiendelee kuwasiliana na wewe, yani unaacha kwenda kuishi na mwanaume ambae anakupenda unapanga kumfanyia unyama , kwani kama ni gari si mtanunua wenyewe” alisema Rose kwa sauti ambayo ilionyesha wazi kuwa anamaanisha alicho kisema, lakibi kwa upande wa Sada ulikuwa ni kichekesho, maana alicheka kwanguvu, tena kwa muda mrefu, aliacha kucheka walipokuwa wanatoka, “yani wewe kwahakiri zako, maisha aya ya kukaa na mtu ambae hana mbele waa nyuma eti mume” alisema Sada akimaliza kwa kubana pua, namaongezi yao yalikoma hapo.***
Saa mbili asubuhi, ndani ya kijijini cha Mwanamonga, kijiji ambacho kilionekana kimechangamka sana, kuliko misimu mingine yoyote, asubuhi hii ungeweza kumwona Limbagile, akiwa anaenda nyumbani kwa Ponera, huku amebeba redio kuwa ya pana sonic, yenye kutumia betries nane, yenye kusikika music mkubwa sana, na anapofika nyumbani kwa Ponera, anamkuta Ponera ana piga mswaki kwamaji ya chupa toka dukani, kwamba maji ya kisima yana taiphod huku pembeni kuna redio kama ya Limbagile, nayo ina sikika music kwa sauti kubwa sana, kiasi cha kushindwa kusilizana wao kwa.
Isinge kuwa hajabu kumwona mtu akiagiza kreti la bia asubuhi hii anakuambia anazimua zile za jana, usinge shangaa kuona mtu mmoja ananunua mikate miwili kwaajili ya chai, wakati hakuwa na uwezo wa kumaliza ata mmoja, wapo walio jiona wana hakiri zaidi ni wale ambao waliezua paa za nyumba zao walizo ezeka mwaka jana, na kuezeka bati mpya, kama ambavyo walifanya msimu uliopita, zaidi ya hapo ungeweza kuona viduka vidogo vidogo kila baada ya nyumba moja au mbili, na yumba zilizobakia ungekuta vibanda ya mama lishe, ungeshangaa mwateja wanapata wapi, lakini viduka vile mwisho wake uwa ni mwisho wa msimu wa malipo.
Licha ya shamla shamla hizi kwenye kijiji cha Mwanammonga, lakini ilikuwa ni tofauti kabisa kwenye nyumba ya mzee Nyoni, ambae kiukweli hakuwa na fedha yoyote wala kuwepo kwenye orodha ya malipo ya tumbaku, siyo kwamba hakuwa na shamba, ukweli masamba alikuwa nayo, tena mengi tu! lakini alikuwa ameyakodisha, kwa wakulima toka mjini, hivyo mzee Nyoni na mke wake, yani mama Sada waliishia kuwa watazamaji tu, tofauti na msimu uliopita ambao walipewa kiasi cha fedha na binti yao, fedha alizo iba toka kwa mkwe wao Peter mtoto wa mzee Jacob, mbaya zaidi ata kile walicho kitarajia kwa binti yao kwamba ange waleteea fedha na vitu vingi toka mjini, hawakukipata, na kubakia kama wazee ambao hawakuzaa, waliishia kusikia arufi ya vyakula vitamu toka kwenye majumba ya jirani, kilicho wasaidia ni kupata nafasi ya kudowea pombe toka kwa washirika wao wa pombe, yani wakina mzee Ngongi.**
Mida hiyo mwana dada Queen alikuwa bado kitandani, yupo macho, ana mtazama mpenzi wake, Emma yani pengo, alie kuwa anavaa tayari kuelekea kwenye mipango yake, kitu ambacho hakikutumia muda mrefu, maana Emma alitumia dakika tano kumaliza kuvaa na kutoka nje ya chumba chake alichopanga pale Mahenge, na ndipo Sada alipotoa simu yake na kutafuta namba ya Peter, aliyo isave Jinga la Kijiji, ana kuipiga, lakini kwa bahati mbaya aikuwa hewani, “mjinga wewe unawezaje kuzima simu muda wote huu?” aling’aka Sada, huku anajaribu kupiga tena, ma jibu yakwa yale yale “namba ya simu unayopiga haipatikani kwa sasa” hapo Sada aliachia msonyo mkali sana, huku anaandika ujumbe kwenda kwa Jinga la kijiji, “ukiwasha simu nipigie” ndivyo alivyoandika na kuituma alafu akaiweka simu pembeni na ya mto alio ulalia, na ndio wakati alio iona simu ya mpenzi wake Emma, inamaana Emma alikuwa amesahau simu yake.
Sada akapuuzia swala ilo na kuanza kuwaza jinsi atakavyo jipatia fedha nyingi toka kwa mtu ambae ana mwita jinga la kijiji.**
Mida hiyo Peter aliamka tayari ameshaamka, na akiwa mwenye uchangamfu mkubwa, aliandaa kifungua kinywa cha mwanae, nasema hivyo sababu yeye hakuwa na hamu yakula kutokana na kumuhe muhe cha kuwasiriana na mama Michael, hivyo alimwandalia Michael chai, nae akanywa, kisha wakaondoka zao kuelekea nyumbani kwa wazazi wake, yani kwamzee Jacob na mke wake.
Na akiwa njiani, Peter akawasha simu yake ambayo aliizima toka jana usiku kwaajili ya kutunza chaji ya kuwasiliana na Sada mwanamke ambae alimchukulia kuwa bado ni mke wake, na ile anaiwasha tu akakutana na ujumbe, “ukiwasha simu nipigie” ukweli nifuraha kubwa sana ilijaa moyoni mwake, “ngoja kwanza nifike nyumbani kwa wazee kisha nimpigie, ndivyo alivyopanga Peter, ambae alifika nyumbani wazazi wake, ambao aliwakuta wanajiandaa kwenda wilayani Namtumbo, kuchukuwa malipo ya tumbaku, “vipi Peter, naona leo kama una furaha sana, vipi mambo yako yanaenda vuzuri?” aliuliza mzee Jacob, huku uso wake ukinawili kwa tabasamu la furaha, mala baada ya kusalimiana na kijana wao, maana hakuwai kumwona Peter akiwa mwenye furaha namna hii kwa muda mrefu sana, “baba, mama nimekuja na habari nje” alisema Peter na wazazi wake wakatulia kumsikiliza kijana wao ambae kiukweli ajawai kuwaletea sifa mbaya hapa kijijini, “jana nime wasiliana na mama Michael” ndivyo alivyoanza Peter au baba Michael, na kuanza kueleza jinsi alivyo pata habari, kuwa mama Michael, anamkumbuka sana, yeye na mtoto wao, na kwamba kuna dalili za wazi kabisa za kurudi nyumbani waanze maisha mapya.
Mwisho wa maelezo hayo, mzee Jacob na mke wake waligeuka kutazamana kwa macho ya mshangao, kisha wakamtazama kijana wao kwa pamoja, lakini unakumbuka kuwa wazazi wake walisema kuwa hawakutambui kuwa wewe ni mume wa binti yao, na kwamba anaishi na mwanume mwingine huko mjini?” aliuliza mama Peter, kwa sauti ambayo ni wazi ilikuwa inzuwia kitu kooni, “nakumbuka mama lakini lazima tujuwe ya kwamba mapenzi ni makubariano ya watu wawili, ukizingatia sisi tuna mtoto, ambae anatuunganisha” aliongea Peter kwa sauti ambayo ulijawa na hali mpya ya furaha, niwazi kwa wakati ule asingeweza kusikia ushauri wowote toka kwa mtu yoyote, “sawa Peter, nazani unamuda mwingi wa kulima, bado unanguvu za kuvumulia maumivu, hivyo ni juu yako, kufanya unacho jisikia kufanya, japo wahenga walisema kuwa kuchafuka ni ndiyo kujifunza, lakini pia kuna watu wanachafuka kila siku pasipo kujifunza, maana uchafu umekuwa ni tabia zao, sijajuwa wewe kwamba utakuwa unajifunza, au ndio kuchafuka iakuwa tabia yako” alisema mzee Jacob, kisha akamshika mkono mke wake na kuondoka nae kufwata barabara inayoelekea upande wa stendi, ambako kwa msimu huu wa malipo kunakuwa na piki piki nyingi sana, za kubeba abiria, kupeleka sehemu mbali mbali, yani boda boda, tayari kupanda mshikaki kuelekea wilayani, wakimwacha Peter alie mbeba mwanae Michael akiwasindikiza kwa macho, ya viulizo, kwanini wazazi wake walionekana kama wanapinga juu ya yeye kurudiana na mke wake Sada, yani mama Michael.
Peter alitulia kwa dakika kadhaa akiwaza kuhusu maneno ya baba yake, na mwonekano wa mama yake, pale alipowajulisha juu ya maamuzi yake kuhusu Sada, na ndipo alipokumbuka kuwa kuna kitu amesahau, akachukuwa simu yake na kumpigia Sada, ambae nikama alikuwa anaisubiria kwa hamu ile simu, mana aliipokea mala moja, “niambie mume wangu, yani nime furahi kusikia sauti yako” ilikuwa ni sauti tamu yakubembeleza toka upande wapili wa simu ile, sauti ambayo ilimsisimua kijana Peter, ambae alitabasamu kwa furaha, “unajuwa siamini kama wewe ndie yule mke wangu” alisema Peter kwa sauti iliyojaa furaha na kuto kuamini.**
Naam Emanuel au Pengo kama alivyo itwa kutokana na pengo la jino alilotolewa kwa ngumi, miezi kadhaa iliyopita, alipokuwa anaingia kwenye gari akakumbuka kuwa amesahau simu yake chumbani hivyo akashuka toka kwenye gari, na kurudi ndani, akatembea kwa haraka kusogela mlango, lakini ile anafika kwenye mlango na kutaka kushika kitasa afungue, akasikia sauti ya mpenzi wake Sada toka ndani ya kile chumba chake alichopanga, “yani mume wangu nina kukumbuka kila siku mpaka namani nije huko kijijini lakini sijuwi kama bado umenikasirikia, au umenisamehe” Emma alimsikia Sada akiongea kwa sauti ya kubembeleza ambayo yeye aliisikiaga miezi mingi iliyopita, ukweli moyo wake ulilipuka vibaya sana, akajwa na wivu mkali sana, “inamaana huyu Malaya ananisaliti, na anamwanaume mwingine, tena anambembeleza namna hii” aliwaza Emma au pengo huku moyo wake ukipatwa na machungu ya kiwango cha juu sana, “ila baby, wala usijari, ngoja nipige mswaki, nioge, alafu nitakupigia sawa mume wangu?” alisema Sada na hapo nazani, alikata simu, “atanitambua huyu mshenzi” alisema hivyo Emma, huku ana usukuma ule mlango na kuingia ndani, na kumkuta Sada akiwa ametoa macho kwa mshangao……….

