KIAPO CHA MASIKINI (16)

SEHEMU YA 16

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TANO: lilionekana kiliingia gari moja ainaya BMW jeusi, na kusimama kwenye maegesho ya ile motel kubwa sana, hapa mjini songea, kisha wakashuka watu watatu, wawili wakiwa ni wazee wamakamo waliovalia suit zao nyeusi, na viatu vyao vyeusi, huku wakifwatiwa na mschana mmoja alie valia vizuri kabisa, huku amebeba sanduku dogo, la Ngozi, nalo jeusi, waka tembea taratibu kuingia ndani ya jingo lile la ghorofa tatu, wakionyesha walikuwa na kikao muhumu, na mtu muhimu sana…… Endelea……
Walienda moja kwa moja na kupanda ngazi mpaka ghorofa ya tatu, ambako waliingia chumba cha VIP, ambacho kilikuwa tulivu sana, ata music uliokuwa inasikika humo ulikuwa ni tulivu sana, “jamani hakuna makossa sasa kila mmoja wetu afanye kazi yake inavyo takiwa” alisema yule mschana, ambae kiukweli ungesema kuwa ndie kijakazi wao, lakini uongeaji wake ungetambua wazi kuwa ndie kiongozi wao, “sawa madam umeeleweka” walijibu wote kwa nidhamu ya hali yajuu, “hakuna ajaya kuangaika, chakufanya nyie fateni maelezo ya kwenye makaratasi, na vile mlivyelekezwa na boss” alisema tena yule mwanamke mdogo, alie valia skirt fupi nyeusi, na shati yeupe, chini alimaliza kwa viatu vyeusi vyenye visigino virefu, huku anatoa baadhi ya makaratasi na kuwapatia wale wazee wawili, nao wakapokea na kujianza kuyasoma “ndoa shaka madam” alisema mmoja wao, akimwakikishia mwanamke yule, kuwa hakuna kitakacho aribika.***
Naam sasa turudi kidogo kijijini mwanamonga, ambako mzee Jacob na mke wake walikuwa wamekaa nje ya nyumba yao, wakinywa bia zao wakichanganya ulanzi, kinywaji ambacho wamekizowea tang una tangu, huku harufu tamu ya kuku wakubanikwa, alie kuwa juu ya jiko pembeni yao ikisikika, hayo ni moja ya mambo yanayo patikana hapa kijijini wakati wa msimu wa malipo kama huu, “lakini baba Peter hivi umeshindwa kabisa kumzuwia mtoto asiende mjini kukutana na yule mwanamke?” aliuliza mama Peter yani mke wa mzee Jacob, kwa sauti ya manung’uniko, japo walikuwa kwenye starehe, “mama Peter, mwanao ni mtu mzima sasa, anajuwa lipi afanye na lipi asifanye” alisema mzee Jacob kwa sauti tulivu huku wanaendelea kupata kinywaji chao mchanganyiko, ambacho wao walinywea kwenye grass kama wafanyavyo watu wa mjini, “lakini wewe ni baba yake aijalishi anamiaka mingapi, wala anaonekanaje” alisisitiza mama Peter, huku anageuza kuku juu yajiko la mkaa, “ndiyo mke wangu, mimi nitabikia kuwa baba Peter na wewe utabakia kuwa mama Peter, lakini kuna wakati ambao mzazi uwezi kumlazimisha toto wako kufanya jambo au asifanye, hatuwezi kumshikia fimbo wala kumzaba vibao” aliffanua mzee Jacob, ufafanuzi ambao mke wake nikama aliuelewa lakini akutaka kukubaliana nao, “baba Peter unakumbuka mambo yaliyomkuta wakati ule alipo mfwata huyo mwanamk, nina wasi wasi sana juu ya ilo mume wangu, yana weza kumkuta tena, unazani yule mwanamke anawezaje kumpenda Peter ghafla namna hii?” alisema mama Peter, akieleza wasi wasi wake, “nafahamu mama Peter, lakini tungewezaje kumzuwia, cha msingi tuombe arudi salama, hayo mengine yanaweza kuwa ni mafunzo kwake” alisema mzee Jacob, akionyesha amekubariana na kitakacho tokea, “sawa yeye yamkute vipi kuhusu Michael ambe ameenda nae?” aliuliza mama Peter, nah apo mzee Jacob akatulia kidogo kama anawaza jambo flani, kisha akamtazama mke wake, “hapo nipo pagumu, na ninazidi kuwaombea uzima” alisema mzee Jacob, kwa sauti ambayo iliingiwa na simanzi kidogo, “baba Peter hapana mimi nampigia simu Peter nimwambie aache kukutana na huyo mwanamke, yani roho yangu inasita kabisaaaaa” alisema mama Peter huku anachukuwa simu yake, na kupiga namba ya Peter, lakini jibu alilopata ni kwamba, “simu unayopiga aipatikani, kwasasa jaribu tena baadae” mama Peter alikata simu, na kupiga tena, jibu likawa lile lile, “unaona mpaka sasa hapatikani, sijuwi kime mkuta nini” alilalamika mama Peter huku anasaka namba ya mzee Nyoni, na kuipiga, nayo ikaanza kita, “unampigia nani sasa, siumesema kuwa namba yake aipatikani?” aliuliza mzeee Jacob, lakini mke wake akujibu kitu, mpaka simu ilipopokelewa “shikamoo mzee Nyoni” alisalimia mama Peter ambae kiukweli ni mogo kiumri kwa mzee Nyoni, yani baba yake Sada, “marahaba mama Peter yani hapa umeniwai, nilipanga nikupigie baadae maana kesho tulipanga tuje huko kwenu, ukichukulia sasa Watoto wamepata tena” alisikika mzee Nyoni kwa sauti iliyochangamka kweli kweli, “sikia mzee Nyoni, na kumbuka ulisha sema kuwa mwanao ameenda mjini kwa mwanaume wake mwingine, sasa inakuwaje unasema wamepatana?” aliuliza mama Peter kwa sauti tulivu yenye kushushua, “haaa! Unajuwaaa, hayo ni mambo ya vijana, naona tuwaachie wenyewe, maana mapenzi ayaingiliwi” alisema mzee Nyoni na wakati huo huo akasikika mke wake akiuliza, “kwani mwane tulimfunga Kamba bwana, siameenda mwenyewe kwa Sada” kauri hiyo ilimchukiza na kumuumiza sana mama Peter, ambae alipata hasira za ghafla, “unasikia maneno ya mkeo, sasa nawaomba mpige simu kwa binti yenu, mumweleze ole wake afanye chochote kibaya kwa mwanangu, safari hii sitoacha lipite, nitahakikisha anaozea jela” alisema mama Peter kabla ya kukata simu, “vipi naona mnazukiana?” aliuliza mzee Jacob, kwa sauti iliyojaa utani, “hawanijuwi awa safari hii nitafunga mtu, eti anasema awaja mfunga Kamba, amejipelaka mwenyewe” alisema mama Peter kwa sauti ambayo bado ilikuwa imejawa hasira, “kunywa bia mke wangu, tusubiri matokeo, unapatwa na pressure bule bule” alisema mzee Jacob, akimalizia kwa kicheko.**
Dakika kumi sasa zilikuwa zimekatika, toka Peter na mwanae Michael wafike mtini pub, na kukaa kwenye meza moja ya wazi, ambayo waliletewa kila walicho itaji na kuwekewa juu yake, ikiwa nipamoja na bia moja ya baridi, soda na chips ya mayai na nyama za kuchoma, tayai walisha omba wachajiwe simu yao kwaajili ya kuwasiliana na mwenyeji wao, mazingira yalimkumbusha mbali sana bwana Peter, asa alipowaona wanawake waliovalia nguo fupi zilizoacha wazi baadhi ya sehemu zao nyeti, ambao walionekana wazi kuwa wanafanya biashara flani, isiyo halali, kitu kilicho mkumbusha siku ambayo alifika kwenye ile nyumba chakavu, kule mfaranyaki, alipokuwa anaishi mke wake sada, ila akutaka sana kukumbuka jambool, sababu tayari lilisha pita na amesha sameheana na mke wake, na wanatarajia kuanza Maisha mapya, alicho jari Peter nikwamba, usiku wale atafaidi kitumbua cha mkewe alicho kikosa kwa muda mrefu sana, napengine kesho angerudi na mke wake nyumbani kwao, kijijini mwanamonga.
Naam wakati Peter ana waza hayo, mala akawaona vijana watano wanaingia maali pale, na kugawana meza mbili, kisha wakaagiza bia na kuendelea kunywa, kilicho mvutia Peter ni mmoja kati ya vijana wale, ambae alikuja na kukaa meza ya pili toka kwenye meza aliyokaa yeye na mtoto wake Michael, kijana ambae alipomwona alimkumbuka mala moja, kuwa ni mmoja kati ya wale vijana wawili, ambao aliwai kuwatandika miezi kadhaa iliyopita, walipojaribu kumwibia mwanadada mmoja mzuri sana, kule mtaa wa Zanzibar.
Lakini ata hivyo Peter hakumjari akumjari sana, yule jamaa na wenzake, akaendelea kunywa bia yake taratibu, huku mwanae Michael akila chips na kushushia soda, huku akiwatazama wale jamaa kwa macho ya tahadhari kubwa, maana alimini wale jamaa ni wezi na akizubaa tu, wanaweza kumwibia fedha zake, “hoya Janja leo tusifanye kosa, leo lazima tumbananishe” alisema yule jamaa akimweleza mwenzie, huku wanakunywa pombe kali walizo agiza wakati huo, “lakini kaka mtu siyo shati, unajuwaje pengine anaweza kuja na walinzi” alisema yule mwingine, kwa sauti yenye kutilia shaka, kwa kile wanacho kingoja, nah apo nipo Peter alipoanza kuwa tilia shaka, maana ata mkao wao ulikuwa wa kutawanyika na wale wenzao watatu, ambao kiukweli, walikaa kama vile hawajafika pamoja maali pale, una wasi wasi gani Janja, akiingia ndani wata mlewesha, hivyo sisi tuta mdakia ndani, na kutoka nae kama mtu mwingine wa kawaia, hakiwa ajitambui, ata kama atakuja na walinzi awatoweza kumtambua” alisema yule jamaa ambae Peter alikuwa ana mkumbuka kwa jinsi alivyo mtandika ngumu yam domo na kumtoa jino, ambalo mpaka sasa lilionyesha alama ya wazi kabisa ya pengo, lililo onekana kila alipoongea, pia kovu la mpasuko juu ya mdomo wake.
Naam niwazi kabisa kabisa watu awa walikuwa katika mpango wao wa wizi, tena walikusuia kumteka mtu mwenye fedha na uwezo mkubwa sana, maana walizungumzia anaweza kuwa na walinzi, na moja kwa moja unaweza kutambua kuwa mtu mwenye uwezo wa kuwa na walinzi binafsi ni mtu mwenye uwezo kifedha, “huyoooo! anaingia wapigie simu ndani wakae tayari” alisema yule kijana alie itwa Janja, na wote wakageuka kutazama upande wa maegesho ya MAKIMAKULUGA, siyo wale wawili tu, ata wale wenzako wakatazama pia, na Peter nae akavutiwa kufanya hivyo, nae akatazama upande ule, nah apo ndipo alipo liona gari aina ya Range rover, likiingia pale magegesho na kusimama, kisha akashuka mwanadada mrembo sana, alievalia gauni refu jekundu lenye mauwa ya brue na kijani, na viatu vyekundu vyenye visigino virefu, mkononi mwake akiwa ameshikilia begi dogo jeusi la Ngozi, “yes leo amekwisha, mpuuzi huyu” alisema yule mwenye pengo ambae sisi tunamfahamu kama Emmanuel, huku anatoa sim una kubofya namba flani, na kuweka simu sikioni, akaisikilizia sekunde kadhaa kabla ajaanza kuongea, “kaeni tayari anakuja huyo, hakikisheni amfanyi makosa” aliongea yule jamaa huku anatazama kule kwenye maegesho, ambako alionekana yule mwanamke mrembo, ambae Peter nae alimkumbuka kuwa ni yule mwanamke asie ongea, ambae ambae licha ya kumsaidia siku ile akuisikia sauti yake, zaidi ni kwamba alitaka kumpatia fedha, na yeye alizikataa, ni mwanamke ambae sikuile vijana awa awa walijaribu kumvamia.
Ukweli Peter hakuwa na mpango wa kuingilia jambo lile maana ukiachilia tabia ya mwanamke yule ya bila kuongea pia aliona kuwa kundi la leo lilikuwa ni kubwa sana, hofu ilimtawala uchungu wa kuona yule dada anaibiwa ukamshika, hakutaka kuendelea kutazama jambo lile, likitokea huku anashuudia, “bora niondoke hapa” aliwaza Peter, huku anageuka kumtazama mhudumu ambae alimwomba akamchajie simu, “naomba unisaidie simu nazani itakuwa imepata chaji kidogo” alisema Peter mala baada ya yule mhudumu kuja mezani kwake, huku mwanamke mrembo sana akitembea taratibu kwa mwendo wa kuhesabu, kueleka kwenye mlango wah ii motel kubwa ya MAKIMAKULUGA, “asawa ngoja nikakuletee, vipi bia tuongeze?” aliuliza yule mwanamke mhudumu huku anatikisa chupa ya bia iliyopo mezani, “hiyo bado aijaisha” alisema Peter, ambae alipaga kuwasiliana na Sada yani mama Michael ili amweleze wakutane wapi na yeye aondoke zake mahali hapa.****
Sada au Queen akiwa amesha maliza kuoga na kuvalia vyema kwaajili ya kumsubiri mpenzi wake watoke kwa matembezi kama ilivyo kawaida yao, huku akiwa amesha kata tamaa ya kukutana na Peter, alishaanza kupata wasi wasi wa kupokea kipigo kingine mala Emanuel akapoona kuwa mpango wake ulikuwa fake, “leo nimeumbuka” aliwaza Sada, huku anajikuta anazidi kumchukia, Peter, ambae aliona kuwa ni sababu ya Maisha yake kuwa magumu, kwa vipigo na wasi wasi, japo vipigo alisha pokea mala kadhaa kwa sababu mbali, ikiwa pamoja na ulevi wa Emanul.
Lakini wakati Sada anawaza hayo, mala akasikia simu yake ikianza kuita, akaichukuwa haraka na kuitazama, “Jinga la Kijiji” ndiyo ilivyosomeka jina la mpigaji, hapo akaachia zinga la tabasamu, kabla aja bofya kitufe cha kupokelea, “hallow mume wangu, hupo wapi jamani” ilikuwa ni sauti ya kulalamika iliyojaa mahaba ya bandia, “tumefika mjini muda mrefu, sema chaji iliniishia, ndio nimeomba wanichajie ilinikupigie” ilisikika suti ya Peter upande wapili wa simu, “jamani mume wangu, yani nilikuwa na hofu, nikajuwa umeshatekwa na mashangingi” aliongea kwa namna ambayo ungesema kuwa alikuwa na wivu kweli kweli, “siwezi kufaya hivyo wewe mwenyewe unanaifahamu vizuri” alisema Peter kwa sauti tulivu, ya mume kwa mke anae mpenda kweli kweli, “nasikia sauti ya kama hupo bar, hupo wapi sasa hivi?” aliuliza Sada ambae sasa alikuwa anapiga hesabu za kwenda kuvuna fedha kwa Peter yani baba wa mtoto wake, “nipo hapaaaaaa, panaitwaaaaaa mtini pub, karibu nah ii ghorofa kubwa ya ghorofa tatu” alisema Peter, na hapo Sada akasisitiza kuwa amkute hapo hapo asiondoke, kwamba yeye yupo njiani anakuja.
Naam baada ya kukata simu Sada akatabasamu peke yake, “sasa je, cha mtu akieni bule, ninahaki ya kula fedha zako, wewe si umenizalisha” ndivyo alivyo jisemea Sada, huku anachukuwa mkoba wake mdogo na kutoka nje ya chumba kile, ikionyesha kuwa safari ilikuwa imeanza.**
Naam mwana dada wa dhahabu, kama watuwegine wanavyo penda kumwita yani Careen mrembo Tajiri toka nchi ya kifalme ya #mbogo_land, alitembea taratibu kupandisha ngazi za kwenda ghorofa ya tatu ya hii hotel kubwa sana, ya MAKIMAKULUGA, begi lake dogo mkononi, njiani akipishana na watu kadhaa waliokuwa wanamkodolea macho ya mshangao, ni kwaajili ya uzuri wake, maana mwada dada huyu, ata ungekaa nae mwaka mzima usingeweza kumzowea, na kumwona wakawaida, hakika ni mzuri na wakushangaza, kuna wakati akikutazama unaweza kujikuta unaitikia, ukijuwa amekuita.
Na Careen alipofika ghorofa ya tatu, akapokelewa na mwanamke mmoja, ambae niwazi kuwa alikuwa anamsubiria yeye, “karibu dada wegeni wako wapo huku VIP, alisema yule mwanamke mwenye kuvalia shati jeupe na skert nyeusi, hapo Careen aliitikia kwa kichwa kukubariana nae, alafu akaelekea kule alikoelekezwa, huku yule mwanamke akiongoza mbele, ambako ambako aliwakuta wanaume wawili watu wazima, wakiwa na vinywaji vyao mezani, na alipoingia tu wote wawili wakasimama “karibu mkurugenzi” alisema mmoja wao huku wanainamisha vichwa vyao, “asante” iliitikia Careen kwa sauti tulivu, huku na yeye akiinamisha kichwa cheke, kama watu wakwao #mbogo_land afanyavyo, kisha wakaa chini kwa kutazamana, yani wale wawili walikaa upane mmoja na Careen akaa upane wake, “samahani dada nikuhudumie tafadhari” alisema yule mwanamke…….

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!