
SEHEMU YA 17
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA SITA: alipoingia tu wote wawili wakasimama “karibu mkurugenzi” alisema mmoja wao huku wanainamisha vichwa vyao, “asante” iliitikia Careen kwa sauti tulivu, huku na yeye akiinamisha kichwa cheke, kama watu wakwao #mbogo_land afanyavyo, kisha wakaa chini kwa kutazamana, yani wale wawili walikaa upane mmoja na Careen akaa upane wake, “samahani dada nikuhudumie tafadhari” alisema yule mwanamke……. Endelea……
Aliekuwa amevaa shati jeupe na skirt nyeusi, ungesema ni tarishi au mhudumu wa hotel ile, “hapana sitotumia kinywaji chochote” alisema yule mwanamke kwa sauti tulivu, ya upole, na wale jamaa wawili wakatazamana, huku wakizuwia mshtuko wao, huku mioyoni mwao wakijiuliza watafanyaje, ili kufanikisha jambo lao, huku mwana dada huyu ambae wakati ule walimwita madam, na yeye akiwa amesimama pembeni ya Careen ameishiwa pose, “tuna weza kuanza sasa” alisema Careen kwa sauti yake ile ile ya taratibu, huku anawatazama kwa zamu wenyeji wake, “sawa sawa, mkurugenzi, mpango ni huu hapa” alisema mmoja wao huku anafungua mkoba mweusi na kutoa karatasi, na kuiweka mezani mbele ya Careen, “nikwamba tume fungua maduka yetu Mbeya na Iringa, ni maduka ya urembo na vipodose kama yanavyo jieleza….” Alianza kueleza yule mmoja wao, nah apo Careen akamkatiza kwa kumwita yule mwanamke alie kuwa amesimama pembeni, “niletee maji tafahari” alisema Careen na Madam akaondoka zake haraka pasipo kuuliza ya mato au ya baridi.
Mwanamke huyu ambae ni kibaraka wa bwana Kalonga, alienda mpaka kwenye counter ya ukumbi wa flow ile ya tatu, na kununua maji haraka, akaomba tray, na kuweka lile chupa la maji na grass moja, kisha akatembea mpaka kwenye kolido, na kuweka chini lile Tray, alafu akaingiza mkono nani ya skrit yake kwa kupitia chini, akapeke nyua kwenye chupi na kuibuka na bimba la sindano jipya kabisa, na kijicupa flani chenye maji meume akafunga sindano kwenye bomba lake, kisha aka chima ile sindano kwenye kizibo cha ile chupa, kama wafanyavyo watabibu, na kuvuta dawa, bila kipimo, alafu akachima kwenye ile chupa na kuminya ile dawa, alafu anatoa guni maarufu kama super grue, na kuweka kiogo sana pale alipochoma, na baada yasekunde kadhaa paliacha kutoa maji, alafu akatupa vile vitu nyuma ya mlango wa ukumbi ule alafu akatoka huku ameba Tray lake lenye maji na grass juu yake, akaelekea VIP.***
Naam kijana Emanuel, akiwa anaongoza mpango wakumteka mama wa dhahabu, ili kumpora funguo za jengo lake na kuiba mzigo mpya wa vito vya dhahabu na madini mengine pamoja na kiasi kikubwa cha fedha ambazo utunzwa kwenye makabati ya chuma ndani ya ofisi ya mwanadada huyo toka #mbogo_land, alitulia kwa dakika kadhaa akisikilizia simu toka ndani ambako kikao fake kilikuwa kinaendelea, mala akapelaka uso wake kwenye meza ya pili toka pale alipokaa, na kuiona sura ya kijana mmoja, ambae alikuwa amekaa na mtoto mdogo wa miaka miwili kasoro, “mh! Janja, unamchek huyu jamaa! Hivi tuliwai kuonana nae wapi?” aliuliza Emmanul Pengo, huku akizuga kuto kumtazama kijana yule, ambae alikuwa anakunywa bia taratibu, na mwanae mdogo akinywa soda na sahani ya chipis ikiwa imeliwa nusu, “sura yake siyo ngeni, ila nahisi kama roho yangu ina mchukia flani hivi” alisema Janja, huku anamtazama yule jamaa, alie kaa na mtoto, “ata mimi sijuwi kwanini nimemfikilia vibaya huyu jamaa, ebu tu badiri uelekeo wengine waende kwenye gari mimi na wewe tupande juu, tukasikilizie mchongo” alisema Emmanuel na Janja akasimama na kupita kwenye meza waliyokaa wale wenzao, akawanong’oneza jambo, na wakainuka nakuelekea kwenye maegesho ya pale mtini pub, huku Janja na Emmanuel wakielekea upande wajengo la MAKIMAKULUGA, na kutokomea ndani ya jengo ilo wakienda kukaa kwenye ukumbi wa flow ya pili, ambako palikuwa ni sehemu tulivu yenye watu wengi sana, waliokuwa wakipata vinywaji huku wanasindikizwa na music laini kabisa, nawao wakaagiza vinywaji na kuendelea kuburudika huku masikio yao yakiwa kwenye simu ya Emmanuel, wakitarajia ujumbe toka ghorofa ya tatu, kwenye kikao cha mikataba fake.
Lakini wakati huo huo ghorofa ya tatu, bado kikao kilikuwa kinaendelea, huku wajumbe watatu wakipeana mawazo na ushuri, juu ya kufanikisha jambo lao, lakini licha ya wajumbe wawili kuendelea kupata vinywaji vyao, lakini Careen yeye akuwa bado ameyagusa yale maji aliyoletewa, kwa madai ni ya baridi na yeye alitaka yenye vugu vugu, hivyo alikuwa anayasubiri yapoe kidogo, ndipo ayanywe, akujuwa kama mschana alie simama hatua chache toka kwenye kochi alilo kaa huku anachezea simu yake, alikuwa anandika ujumbe kwenda kwa Emmanuel “bado ajayanywa maji yake, anasubiri yapungue ubaridi” ndivyo ilivyo someka hiyo sms, **
Naam muda ulikuwa umeenda sana, sasa masaa mawili yalisha katika, bado Peter akiwa na mwanae Michael, alikuwa ametulia zake pale Mtini Pub, anaendelea kupata kinywaji, huku akiwa amesha ongea na mama wa mtoto wake yani Sada, ambae alimweleza kuwa yupo njiani anamfwata, huku kichwani mwake ana waza jinsi atakavyo jiachia usiku kucha na mke wake, akila kitumbua kwa raha zake, kitumbua alicho kimiss kwa muda mrefu, pia aliwaza jinsi ambavyo ataingia na mke waki kijijini, na jinsi watu, watakavyo kuwa wanamtazama kwa jicho la wivu na mshangao, huku wazazi wake wakikubariana na maneno yake, kwamba mke wake amejilekebisha na ameamua kurudiana na yeye.
Wakati bado ana waza hayo mala akasikia simu yake, inaita akaitazama haraka sana, na kuona kuwa mpigaji ni mama Michael, akaipokea mala moja, “niambie mama Michael umesha umesha fika?” aliuliza peter kwa sauti yenye kihoro, “ndiyo nimesha fika, hooo! nimekuona na kuja” alisema Sada, na hapo Peter akatazama kushoto na kulia, huku anasimama toka kwenye kiti chake, na yeye akamwona, akiwa hatua chache karibu yake, “waooo! mume wangu jamani” alisema Sada huku ana mkumbatia Michael ambae aipatwa na msisimko wa mshawasha, japo aliziwa na aibu kwa kiwango kikubwa, maana akuwai kukumbatiana na mwanamke adharani, “mama Michael uoni watu” alisema Peter kwa sauti ya chini na hapo Sada akajifanya kuona aibu, na kumwachia na kumnyayua mwanae “jamani mwanangu Michael” alisema Sada huku ana mkiss mwane Michael aliekuwa anamtazama kwa mshangao, maaana akuwa anafahamu mama huyu, “baba Michael mmepanga kufikia wapi?” aliuliza Sada swali ambalo, lilimshangaza kidogo Michael, lakini hakushangaa sana, maana alikumbuka mazingira yale ya mwanzo aliyo mkuta nayo kule mfanyaki akajuwa ni kweli aliitaji sehemu ya kufikia, wakuwa alikuwa na uhakika wa fedha akuwa na wasi wasi, “tulikuwa tuna kusuburi wewe wenyeji wetu” alisema Peter na hapo Sada akatazama kushoto na kulia kisha akagandisha macho usawa wa jengo la MAKIMAKULUGA, huku anatabasamu, twende tuka lale paleee, itakuwa safi sana, tutaenjoy sana usiku waleo” alisema Sada huku anachukuwa begi na kulibeba, kisha akiwa amembeba Michael na begi, Sada akaongoza kuelekea kwenye jengo la MAKIMAKULUGA Motel, Peter akimfwata kwa nyuma huku akifikilia jinsi atakavyolala ghorofani kwa mala ya kwanza tena huku akila kitumbua usiku kucha.
Naam safari yao iliishia counter, yani mapokezi, ambapo palikuwa na mhudumu mmoja alie kuwa amesimama nyuma ya meza kubwa sana iliyo tengenezwa kwa mtindo wa kisasa, “nisubiri kidogo” alisema Sada, akimwambia Peter ambae alisimama pale pale alipokuwepo, ni kama hatua tano toka kwenye meza yamapokezi, huku Sada mwenyewe akisogea kwenye ile meza huku amembeba mtoto Michael.
Peter alie kuwa anashangaa shangaa madhari ya mle ndani, ambapo watu walikuwa wanaingia nakutoka, huku baadhi yao wakiwa wawili wawili yani mwanamke na mwanaume, na wengine wakiwa wamelewa, pia aliweza kumwona mama wa mtoto wake aliekuwa anaongea na yule mhudumu wa wamapokezi yani alie shughurikia maswala ya vyumba, ni maongezi yaliyo chukuwa dakika kumi nzima, Sada akionekana kumwelewesha jambo dada yule mhudumu wa vyumba, mpaka akamkubaria na kumpatia funguo, kisha Sada akamfwata Peter pale aliposimama, “aya twende zetu, nimechukuwa chumba namba saba cha ghorofa ya tatu, au upendi ghorofani” alisema Sada huku anaongoza kuzifwata ngazi, za kupandia ghorofani, “kwanini nisipende na hivi sijawai kulala ghorofani” alisema Peter kwa sauti iliyojaa utani na wote wakacheka kidogo, huku Sada moyoni mwake akijisemea, “we jichekeshe tu, leo hakuna rangi utaacha kuiona, sisi tuna tafuta ela wewe una leta mchezo” hivyo ndivyo alivyo jisemea Sada moyoni mwake huku wanapandisha ngazi.***
Emanuel akiwa gorofa ya pili, alipokea ujumbe toka wenye kikao Fake, akaufungua nakuusoma, “pumbavu kwanini ayanywi hayo maji?” alisema Emmanuel kwa sauti ya chini, iliyojaa hasira na chuki, huku anatazama saa ya kwenye simu yake, “tulia kaka, kwanza huku anakojipeleka ni kuzuri zaidi, maana giza ndio linazidi kutanda” alisema Hussein, kisha akainua chupa yake ya bia na kuiweka mdomoni, na kuigugumia, na kuirudisha chupa mezani, “saa moja na robo sasa, muda unazidi kwenda yule demu saa mbili uwa ni lazima awe amesha fika nyumbani kwake, unazani tuta mpata sasa” alisema Emmanuel, kwa sauti ambayo ilionyesha yupo tayari kufanya chochote, ilimatokeo yawe ya kumpendeza boss wao Kalonga, boss mimi nakuambia ilo wala usiwe na shaka nalo, akikwepa dawa, tuna mnasa kwenye gari lake” alisema Hussein, na hapo kidogo kama vile Emmauel, akaonekana kuelewa somo, “hapo Janja umesema kitu” alisema Emmanuel kwa sauti yenye matumaini,***
Yap! Sada aliwaongoza mzazi mwenzie na mwanae alie mbeba yani Michael, mpaka kwenye chumba namba saba, cha ghorofa ya tatu, chumba ambacho kilimshangaza na kumvutia sana Peter, kutokana na uzuri wake, yani kitanda kizuri, kilichotandikwa vizuri, pia meza nzuri dogo ya kioo, na kochi dogo la watu wawili, zaidi kilicho mchanganya, screen ya television iliyotundukwa ukutani, “ile inafanya kazi kweli?” aliuliza Peter kwa mshangao, huku anaonyesha ile tv ukutani, “yani hapo niwewe tu, kubadirisha chanel, ukitaka mpira ukitaka movie za kibongo au za ngumi, yani niwewe tu” alisema Sada huku anamweka Michael chini, na kuchukuwa remote nakuiwasha TV, nayo ikawaka na kuanza kuonyesha, “dah! mjini raha sana, leo nitafaidi sana” alisema Peter huku meno yote nje kwa tabasamu, “kesho utanipeleka nikanunue kama hii” alisema Peter huku anakaa kwenye kochi, kwa kulijaribu kama lingeweza kumuimili, Michael nae nikama alikuwa anasubiri baba akae ndipo na yeye apande kwenye kochi, “alafu baba Michael nime kumbuka, unajuwa huku uwa kuna maelekezo, wanayaweka” alisema Sada huku anachukuwa karatasi flani lilijaradiwa kwa karatasi ya prastic inayo angaza, yenye maandishi yaliyoandikwa kwa mistari kama kumi hivi, yakitanguliwa na kichwa cha habari notes, “kwanza ona hapa” alisema Sada huku anamwonyesha pita mstari wa nne, “uaribifu wa vifaa na vitu vya humu ndani utalipia mwenyewe” alisoma Peter kwa sauti, “alafu ona hii namba saba” alisema Sada, na Peter akatupia macho kwenye mstari huo, “kama una mali yoyote au kitu cha thamani, kama fedha kuanzia laki mbili, unashauriwa kuleta kwenye uongozi, ili kuifadhiwa ni kwa usalama wako maana vikiibiwa hotel aito usika kwa upotevu huo” alisoma Peter kwa sauti na kumtazama Sada kwa macho ya uoga, “kweli Sada mjini kuna wezi sana, sasa inabidi uwapelekee ilibegi wakaifadhi” alisema Peter, huku akilitazama begi ambalo bado lilikuwa mikononi kwa mama wa mtoto wake…..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU