
SEHEMU YA 18
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA SABA: Peter akatupia macho kwenye mstari huo, “kama una mali yoyote au kitu cha thamani, kama fedha kuanzia laki mbili, unashauriwa kuleta kwenye uongozi, ili kuifadhiwa ni kwa usalama wako maana vikiibiwa hotel aito usika kwa upotevu huo” alisoma Peter kwa sauti na kumtazama Sada kwa macho ya uoga, “kweli Sada mjini kuna wezi sana, sasa inabidi uwapelekee ilibegi wakaifadhi” alisema Peter, huku akilitazama begi ambalo bado lilikuwa mikononi kwa mama wa mtoto wake.. Endelea……
Yani bi Sada Nyoni, au mama Michael, “sawa alafu mume wangu, utaniazima simu yako niwapigie, kule nyumbani, niwajulishe kuwa nitalala huku, simu yangu imesha dakika” alisema Sada, kwa sauti ya kubembeleza na kushawishi, “hoo sawa akuna shida” alijibu Peter huku anatoa simu, na kumpatia Sada, mke wake wa zamani yani mama wa mtoto wake, ambae huku mjini anaitwa Queen.
Baada ya hapo Sada alimwelekeza Peter namna ya kubadiri chanel za tv, kisha akaaga kwa Peter “sasa mume wangu wacha nikakabidhi mzigo kwanza” alisema Sada hukuanaufwata mlango nakutoka nje ya chumba kile akiwa na begi la Peter lenye fedha zote, na nguo chache za Peter mwenyewe na Michael mwanae, akimwacha Peter ana anajiweka sawa pale juu ya kochi alipokaa na mwanae wakijielekeza kwenye TV, wakitazama na kujaribu kubadiri chanel, “baba baba nguo zangu” alisema Michael mala baada ya mama yake kutoka nje, “acha ushamba mwanangu, hapa mjini, nguo zako utazipata kesho” alisema Peter, huku ananyoosha remote mbele na kubofya, “asiporudi” aliuongea Michael kwa sauti ya kitoto sana, safari hii Peter akacheka kidogo, “we mshamba kweli Michael, yani umeshindwa kumkumbuka huyu ndio mama yako, lazima atarudi tu, leo tunalala nae hapa hapa” alisema Peter kwa sauti ambayo ilionyesha wazi ni kiasi gani alikuwa na furaha na amani, lakini jibu lile alikusaidia kumtuliza Michael, ambae alikuwa anawaza juu ya viatu vyake, na nguo mpya aliyo nunuliwa na baba yake siku tatu zilizo pita, japo alikaa kimya lakini moyoni alitia shaka kwa yule mama alieondoka na begi lao walilotoka nalo kijiji.
Kimya kikatawara macho yao kwenye TV, mala mlango uka funguliwa tena, wote wawili wakatazama mlangoni, kuona alie ingia, hapo wakamwona mama Michael ambae sisi tunamfahamu kama Queen akiingia na begi lake mkononi, nilisahau baba Michael, utaki kuagiza bia au soda, au ata maji, maana kushuka shuka kule chini nitaona kazi, nataka nikiingia nime ingia” alisema Sada kwa sauti iliyojawa na upendo wa hali ya juu sana, “hoooo! ikweli hivi na wewe bado unakunywa bia?” aliuliza Peter huku anaingiza mkono mfukoni, na kutoka na kifungu cha fedha kama cha laki mbili hivi, “nakunywa mume wangu, tena umenikumbusha inabidi nikatafute chakula kabisa, pia nikalipie chumba” alisema Sada huku anachukuwa zile fedha mkononi kwa Peter, ambae sasa alikuwa anaanza kuhesabu zikazotosha kumpatia kwa matumizi, lakini zilipochukuliwa zote, Peter ambae alikuwa na furaha ya kukutana tena na mke wake, akuonyesha kujari, akatulia akimwacha mke wake anatoka nje ya chumba huku na yeye anageukia TV, “baba ela” alisikika Michael kwa Kiswahili hake cha kitoto, lakini baba yake ambae ni Peter akumjari kabisa, Michael hakuwa na lakufanya akabakia anautazama ule mlango aliotokea yule mwanamke ambae ameambiwa ni mama yake, kwamacho ya udhuni kabisa, nazani kama angekuwa nauwezo wa kuongea vyema na baba yake, lazima angemweleza kitu anacho kihisi.***
Naam tukiwa kule kule ghorofa ya tatu, sasa twende kule VIP, ambako kikao kilikuwa kina endelea, na sasa nikama kilikuwa kina karibia ukingoni, bado Careen hakuwa amekunywa maji kwenye chupa yake, “nazani mpango wenu umekaa vizuri, na tunaweza kuuanza mala moja” alisema Careen huku anachukuwa chupa yake ya maji na kuigusa kidogo kama imepoa, wote waka watatu viroho vikaanza kuwaenda mbio, “yah! tunakuhakikishia kuwa mala baada ya kufika tu, tutaanza mchakato wa kuleta fedha kwaajili ya mzigo wa kuanzia” alisema mmoja wa wale jamaa wawili waliokuwa wamekaa kwenye makochi, “namimi sito waangusha maana ninamzigo mpya ambao bado aujaanza kuuzwa, japo niliwashauri mngeanza na vitu vya zamani, ili kuvutia wateja kwa wenu wapya” alisema Careen ambae sasa alifungua maji na kuyanywa, mkupuo mmoja na kuweka mezani, kisha akachukuwa baadhi ya karatasi na kuziweka kwenye begi lake kisha akalifunga na kuchukuwa tena maji akayanywa, kama mwanzo, na kuiweka chupa mezani, na hapo akatulia kidogo maana kama vile kuna kitu alikihisi usoni mwake, nikama macho yake yalianza kupoteza nguvu, “ilo ni wazo zuri pia tutalifanyia kazi” alijibu mmoja kati ya wale wawili, lakini Careen hakusikiliza tena, hapo mawazo yake yalikuwa katika maji aliyo kunywa ambayo yalimpelekea kuanza kuona kichwa kina kuwa kizito, akachukuwa simu yake na kutazama saa, ilikuwa ni saa mbili kasoro dakika kumi, “sahamani jamani muda wangu umeisha” alisema Careen huku anaweka simu yake kwenye begi, na kuinuka, kisha akaanza kutembea kwa umakini mkubwa, akutaka wale jamaa zake wagundue kuwa dawa zimeshaanza kumlevya, akutaka kusubiri jibu toka kwa wale jamaa, “safari nje boss, tutawasiliana” alisema mmoja kati ya wale jamaa huku wanasimama tayari kutoka nje ya ukumbi ule wa VIP, lakini yule mwanamke alie jifanya mhudumu akawaonyesha ishala ya kuwa waulie kwenye makochi, huku yeye anatoa simu yake na kupiga namba ya Emanuel, ambae akuchelewa kuipokea, “anakuja huyo muwaini kwenye korido, tayari amesha kunywa maji” ndivyo alivyosema yule mwanamke na kukata simu.
Nikweli Careen alikuwa katika hali ambayo aliishangaa sana, ali ya ulevi dakika chache baada ya kunywa maji, alihisi yae maji yale aliyokunywa ndiyo yalikuwa na kilevi, lakini akujuwa kilevi kiliwekwaje, maana maji yalikuwa yamefungwa kwa upya wake, na kama kweli kuna watu wameweka dawa kwenye yale maji, basi hawana nia njema na yeye, niwazi wanaitaji kumwibia kila alihokuwa nacho kama siyo kumbaka, nivitu muhimu kwake, kuanzia bikira yake aliyo kuwa amemtunzia mwanaume ambae ameowa mwanamke mwingine yani mfalme wa nchi yao, Elvis Mbogo, na pia vitu vilivyopo kwenye begi, ambayo ni funguo za ofisi na makabati ya chuma ambayo utunzia vito vya thamani na mamillioni ya fedha ambayo mala nyingi usafirisha kila jumamosi kupeleka nchini kwao #Mbogo_land kingdom, hivyo basi ata hiki kikao kilikuwa fake, ni njia ya kumwingiza kwenye mtego, na mtu pekee anae weza kufanya hivi ni Kalonga pekee.***
Yap! Baada ya kuchukuwa begi lenye nguo na fedha, pamoja na simu na fedha za baba wa mtoto wake, Sada alitoka shuka mpaka flow ya chini, na wakati anakatiza mbele ya counter inayosimamiwa na mhudumu wa vyumba, akaitwa, “samahani dada namba uje mala moja, “ alikuwa ni mhudumu wa vyumba ni yule alie ongea nae wakati ule wanaingia, nae akaenda haraka” naomba uniandikie majina yenu, alisema yule dada huku anamsogezea kitabu cha kuandika maji wageni, pamoja na kalamu juu yake, “hoooo! nilisahau” alisema Sada huku anachukuwa kalamu ya wino juu ya kitabu kile, na kuanza kuandika.
Hakika yule dada mhudumu angejuwa kilichoandikwa, ndani ya daftari au kitabu kile cha wageni kuwa ni jina fake, sijuwi kama ange mwacha salama huyu mwanamke, “Tito Kikoto” ndilo jina alilo andika Sada, kishakarudisha peni na daftari kwa mwenyewe, “kuhusu malipo ndio umesema baadae?” aliuliza yule mhudumu huku anapokea kile kitabu, “ndiyo wala usiwe na wasi wasi, maana tutakaa hapa kwa siku tatu” alisema Sada kwa kujiachia na kujiamini kweli kweli, huku ananyakuwa begi lake na kuondoka zake, tayari alikuwa na laki mbili mkononi, na simu ya mumewe, ukiachilia million kadhaa ndani ya begi, “mh! watu wenyewe wanaonekana wa kawaida, lakini wana lala VIP, chumba laki moja” aliwaza dada wa mapokezi, huku akimtazama Sada au Queen aliekuwa anapotelea nje ya jengo lile kubwa.***
Emmauel na Hussein baada ya kupokea simu toka ghorofa ya tatu, waliinuka haraka, na kuelekea koridoni, huku Emmanuela napiga simu kwa wenzao waliopo chini kwenye maegesho ya magari, “jiandaeni tayari mchezo umeshaanza” alisema Emanuel na kukata simu, huku wanazifwata ngazi za kwenda ghorofa ya tatu, “Hussein hakuna makosa, tunaondoka na huyu mwanamke kama tulikuwanae, chamsingi nikwamba, tunatakiwa kuficha sura ya huyu mwanamke siunajuwa anavyo fahamika” alisema Emmanuel ambae yeye pamoja na Hussein, walikuwa wamesha zifikia ngazi na wanaanza kupanda, kwenda juu.***
Nusu saa ilishapita bila Peter kumwona Sada akirudi, ndani ya chumba namba saba cha ghorofa ya tatu, lakini akajipa moyo kuwa muda wowote atamwona mke wake huyo akirudi mle chumbani lakini zika pita dakika kumi pasipo kumwona Sada, aka mtazama mwanae Michael , akamwona tayari amesha lala, na kujiegemeza kwenye kochi, “au bado anatafuta chakula, aliwaza Peter akijipapasa mfukoni mwake, kwa lengo la kuchukuwa simu na kumpigia mke wake, lakini akuipata simu, na hapo ndipo alipokumbuka kuwa simu alitoka nayo Sada, hapo akainuka na kuufwata mlango akimwacha Michael juu ya kochi amesha topea kwenye usingizi, alipoufikia mlango akaufungua na kuchungulia nje, alicho kiona kilimshangaza kidogo, na kumfanya asahau kwa muda kuhusu mke wake.**
Naam huko kijijini, mama Peter yani mke wa mzee Jacob, licha ya kunywa bia nyingi akichanganya na ulanzi, ambao ulimlewesha sana mama huyu, lakini bado alikuwa anawaza juu ya mwanae na mjukuu wake, “baba Peter, sijuwi huko mjini jamani kama kuna usalama kweli” nikama mama huyu alikuwa anaweweseka, muda wote, akiwa na mume wake, “we jiweweseshe tu! mwenzio anakula raha tu! huko mjini, na huyu mwanamke wake” mala zote mzee Jacob alitoa jibu ilo, huku na yeye akijaribu kumtafakari kijana wake huyo wa pekee, “lakini huyu Peter, hii hakiri amelithi kwa babu yangu yupi, au kwenu mama Peter, sisi kwetu hatuna hakiri za hivi” alisema mzee Jacob, “hapana siyo kwetu, huyu atakuwa amelithi kwa yule babu yako mzaa bibi yenu wa litora, alie lishwa limbwata la Nyasa kwa wa Manda” alisema mama Peter, akimaliza na kicheko kikubwa, “mhhhh! Siyo kwa limbwata lile mama Peter, ebu temea mate chini, unajuwa yule mzee alikula limbwa lahajabu sana” alisema mzee Jacob nae akiunga kucheka, kama mke wake.
Walipomaliza kucheka kikapita kimya kifupi huku wakiendelea kunywa pombe yao, kabla mama Peter ajavunja ukimya, “baba Peter mimi na wazo” alisema mama Peter kwa sauti ambayo haikuwa na dalili ya utani ata kidogo, “hupi huo mke wangu?” aliuliza baba Peter huku anatega macho na masikio kwa mke wake, “hapa tuchague moja, akirudi toka mjini, tumpeleke kanisani akaombewe, au tumpeleke kwa mganga akatolewe imbwata, au tuitishe ngoma ya mandulu (mizumi ya wafu) tuiombe imsaidie” alisema mama Peter pasipo kuwa na utani ata kidogo, “umeongea point, lakini sasa kwa ujinga wa Peter naona tufanye hayo yote kwa pamoja ndio ata chomoka kwenye ili” alisema baba Peter, kisha akaachia kicheko cha nguvu, “we mzee kweli zamwamwa, yani mimi naongea cha maana, wewe unaleta utani” alilalamika mama Peter, “sasa we unazani amelogwa yule, siutawasumbua marehemu wawatu tu! kwaajili ya mpuuzi, we ngoja arudi toka huko mjini, lazima zita mkaa, kwa kitu ambacho kita mkuta” alisema mzee Jacob, na kumfanya mke wake ashindwe kukasirika, na kubakia anatabasamu huku anamtazama mume wake wa macho ya nusu hasira nusu tabasamu.***
Naam mwanadada mrembo sana Careen au mama wa dhahabu, baada ya kutoka kwenye chumba cha VIP, walichokuwa wanafanyanjia kikao na wale wawekezaji, alizidi kuona miguu yake inakuwa mizito, mfano wa mtu alie kunywa pombe nyingi sana, huku macho yake yakizidi kupunguza nuru, na kumfanya punguze uwezo wa kuona mbali, njia pekee ambayo aliifikilia njia mbayo inge mweka salama, na kujiokoa toka kwenye mikono ya watu waliofanya hivi, ni yeye kujitaidi kutembea mpaka kwenye gari lake, ili akajifungie ndani, mpaka pale atakapo pata nafuu au uwezo wa kupiga simu, ilikupata msaada, Careen alijitaidi huku ameshikilia mkoba wake, ambao nisawa na ofisi nzima ambayo inamweka hapa Tanzania, koba ambao alikuwa na uofia kuwa, ni moja ya vitu ambavyo vilikuwa vinawindwa na watu ambao waliomwekea dawa za kulevya kwenye maji, na kila alipozidi kutembea ndivyo alipoona nguvu zina zidi kupungua mwilini mwake, ata hivyo akazidi kujikongoja kwenye kolido refu, kuelekea kwenye ngazi za kushukia ghorofa ya pili, ambayo akujuwa ataifikia saangapi kwa mwendo aliokuwa anatembea, japo tumaini lake lilikuwa ni kufika chini na kuelekea kwenye maegesho ya magari, na pengine, kujifungia ndani ya gari lake.
Lakini akufanikiwa ata kuzifikia ngazi zile, maana wakati anaendelea kujikongoja, ghafla akawaona vijana wawili wakiibuka kwenye korido, toka kwenye ngazi, wakija upande wake kwa speed kali huku macho yao wameyaelekeza kwake, vijana ambao mwanadada huyu, aliwakumbuka mala moja, kuwa ni vijana wa bwana Kalonga… Endelea……
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU