KIAPO CHA MASIKINI (21)

SEHEMU YA 21

ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI: Naam pasipo kukumbuka kuwa mala ya mwisho pochi aliliweka juu ya meza kabla ajapitiwa na usingizi, Sada ambae alijikuta kuwa yupo peke yake, akachukuwa begi lake haraka na kuondoka zake, pasipo kulikagua ndani yake… Endelea……
Sada alitembea kwa tahadhari kubwa sana katika usiku huu wa giza nene na ukimya wa ajabu, akiofia kuvamiwa na vibaka na kumpora fedha nyingi alizokuwa nazo kwenye begi, fedha ambazo na yeye alizipora kwa mume wake wa zamani, yani Peter ambae bila kujari amewacha katika matatizo makubwa yeye na mwanae wa kumzaa yani Michael, akujari watatokaje pale hotelini, na wala akutaka kujuwa huku watakayoipata baada ya kulala kwa usiku kucha pasipo kulipia gharama kubwa ya chuma walicho lalia kwa usiku mmoja, gharama yake ilikuwa ni tsh laki moja.
Sada alitembea na kutokomea uapande wa mahenge, ambako ni nyumbani kwa mpenzi wake Emma, akiwa ajuwi kuwa yajayo yanafurahisha.***
Naam saa kumi na moja na robo, ndio muda ambao mwana dada Careen alipo shtuka toka usingizini, kwanza alikumbana na maumivu ya kichwa, mfano wa mtu ambae jana alikunywa pombe nyingi sana, yani nikama alikuwa na mning’inio, Careen ambae alikuwa anakumbuka vyema kuhusu tukio la jana la kunywa maji, na kuanza kulewa ghafla, kisha kujaribu kutoroka mikononi mwa watu ambao alikuwa nao kwenye kikao, na kujikuta akiingia mikononi mwa watu ambao mpaka sasa anawafahamu kuwa ni vijana wa adui yake namba moja, yani bwana Pitus Kalonga, ambae lengo lake siyo tu kuhakikisha anaonja kitumbua cha mrembo huyu wa dhahabu, ila pia ni kuhakikisha anampra kila alicho kuwa nacho.
Lakini bahati ikawa upande wake, maana aliokolewa na na kijana ambae siyo mala yake ya kwanza kutoa msaada kama huo ambae, hapo Careen akageuka kutazama upande wake wakushoto, ambako alimwona kijana yule akiwa amekaa kwenye kochi, huku ameptiwa na usingizi, na sasa aliweza kumwona mtoto mdogo wa miaka kama miwili na kitu, akiwa amelala pembeni ya kijana yule, “mh! hivi nipo salama kweli?” alijiuliza Careen huku ana peleka mkono ndani ya shuka na kujipapasa sehemu za mbele za jinsia yake, lakini akakuta kuwa bado alikuwa na nguo zake kama alivyokuwa jana, kasoro viatu ndivyo vilivyokuwa vime vuliwa toka miguuni mwake, akatazama pembeni yake akaliona begi lake, akalichukuwa haraka na kulifungua, akaona vitu vyake vipo vyote, kuanzia fedha simu, ata funguo zote za maofisini na zagari, akafunga begi na kuinuka toka kitandani akavaa viatu vyake, na kuufwata mlango akafungua na kuondoka zake pasipo kujari muda, yeye careen alitembea kwa tahadhari kuelekea chini, ambako alilikuta gari lake lipo kama alivyo liacha, akafungua na kuingia ndani, akawasha na kuondoka zake, kueleka nyumbani, huku kichwa chake kikiendelea kumuuma japo siyo sana.***
Yap! Emmanuel ambae alikosa usingizi kutokana na maumivu ya kung’olewa jino, maumivu ya mgongo, alikuwa amabadiri milalo, juu ya kitanda chake, huku akijaribu kufanya marekebisho ya nyumba ile, kwa macho, akimkosoa fundi, na mwenye nyumba, “kama ningekuwa mimi, ningeweka kabati la ukutani pele karibu na mlango bafu, alafu hii gypsum, ninge weka ya urembo urembo” aliwaza Emmanuel Pengo, wakati mwingine akiwaza kuhusu mwanamke alikuwa anaishinae yani Queen, ambae mapaka mida hii majogoo na wika hakuwa amerudi nyumbani, “huyu Malaya amepata hizo senti zake ndio maana ame amua kunikimbia, wengoja tu, hipo siku ata jileta tu, ndipo atakapo nitambua mimi ni nani, kwausalama wake alete kwangu hizo fedha” safari hii Emmanuel aliongea kwa sauti.
Naam akiwa katika mawazo na maumivu, akaanza kusikia vishindo vya kuchovu vikitembea kwenye kolido, alipotazama saa yake ilisha timia saa kumi na moja na robo, muda ule haukuwa wa watu kwenda kazini, hivyo moja kwa moja akajuwa kuwa vishindo vile vilivyokuja na kuota mlangoni kwake, ni vya Queen, hapo akautazama mlango akitegemea kusikia mtu akibisha hodi, lakini haikuwa hivyo, baada yake aliweza kuona mlango ukishikwa kitasa chake na kunyongwa nao ukajibu kwa kufunguka, akafwatia Queen alie ingia ndani, na begi lake mkononi, huku yupo na uchovu wa ulevi wapombe, “unaweza kunieleza ulikuwa wapi we mwanamke” alisema Emma, huku anajitaidi kujikalisha kitandani, “weweeee, ebu tazama kilicho fanyika bwana, siyo unaongea ongea tu” alisema Sada yani Queen huku anarusha begi kueleka kwa Emmanule Pengo, ambae alichelewa kulidaka na kwenda kumgonga mdomoni, ambapo lilimtonesha kidonda, alishikwa na hasira kali, lakinia akavumilia, ni sababu alimini kuwa lile begi litakuwa na fedha nyingi sana ndani yake, aliishia kumtazama Sada ambae alikuwa anavua viatu na kujitupa kitandani, miguu imemchafuka kwa vumbi alilolipata kwa kutembea kwamguu, “mshenzi sijuwi amekunywa bia ngapi?” alijisemea Emma huku anafungua zip ya begi, na kuingiza mkono ndani yake kisha akaibuka na kiatu cha mtoto, akakiweka pembeni na kuingiza tena mkono, akaibuka na boxer ya mtu zima, akaiweka pembeni na kuingiza tena mkono ndani yabegi akaibuka na kijisimu chakavu cha tochi, akakitazama na kukiweka pembeni, safari hii akamua kumimina kabisa lile begi.
Naam alilikamata na kumimina kitandani, ambapo zilimiminika nguo na kiatu kimoja cha mtoto, Emma akatanua lile begi na kuchungulia ndani akuona kitu, akafungua zip za pembeni, ambako alikutana na miswaki na mafuta ya kupakaa mwili, hapo akamtazama Queen kwa jicho moja kali lililo beba uzani mkubwa wa hasira, akamwona mwana dada huyu, ambae alikuwa ananuka pombe akiwa amelala na sasa alianza kukoroma.**
Saa kumi na moja na dakika ishilini ndio muda ambao, Careen alifika nyumbani kwake, mtaa wa Angoni arms au maji maji shule, kama wengine wanavyopaita, geti lika funguliwa na gari likaingizwa ndani, ambapo alipokelewa na wafanyakazi watatu tu, ambao licha ya kusalimia ile salam yao ya utamaduni wa #mbogo_land, lakini Careen akuitikia, akaingia ndani haraka ambako alipokelewa na yaya Glory, alie msaidia kubeba begi, na kueleka flow ya pili, kwenye chumba cha mrembo huyu, “Careen imekuwaje mpaka umelala nje ya nyumba yako, nilipata wasi wasi sana?” aliuliza yaya Glory mala baada ya wawili awa kufika chumbani kwa Careen, ambae sasa alikuwa anaanza kuvua nguo zake, “yaya Glory, sijuwi nisemeje, yani ata nashindwa pakuanzia” alisema Careen, ambae sasa kichwa kilikuwa kinamuuma kwambali, maana kila dakika zilivyozidi kwenda, nivyo kichwa chake kilivyozidi kupungua maumivu.
Careen alimsimulia yaya Glory, juu ya kilicho mtokea, mwanzo mpaka mwisho, “kwanini uliondoka bila kuaga, Careen ujuwe unaitaji kuwa sahau yaliyopita na kujitaidi kufanya yanayofanana ata kwa kuigiza” alisema yaya Glory, kwa sauti ya kuelimisha na kusisitiza, “yaya najuwa nacho kifanya, maana hii ni makusudi kabisa, siyo bahati mbaya, mimi kusaidiwa na yule kijana” alisema Careen, ambae sasa aikuwa amebakia na nguo za ndani pekee, huku anachukuwa simu yake, na kubofya namba flani, ambayo aikuchelewa kupokelewa, “naam madam Careen” iliitikia sauti ya kike, iliyojaa nidhamu na heshima, “njoo haraka nyumba kubwa” alisema Careen na kukata simu, “lakini Careen kazi gani tena usiku kama huu, inakupasa upumzike kwanza, kukipammbazuka uende hospital ukafanye vipimo” alisema yaya Glory, kwa sauti ya upole na kubembeleza, “siitaji kupumzika, wakati nina mambo mengi ya kufanya” alisema Careen huku ana vaa joho mfano wa gauni, lile la kulalia, au kuendea bafuni, yaya Glory akageuka tayari kutoka nje ya chumba, na hapo Careen akawa kama emekumbuka jambo, “Glory, kabla sijaenda kazini, kuna maagizo nita kupa, hivyo tutaonana muda huo” alisema Careen, kwa sauti ambayo ilionyesha kama yupo katika hali flani ya uchangamfu, tofauti na siku zote, “sawa Careen nitakuona” alisema yaya Glory, na kutoka nje, akipishana na mwanamke mmoja mrefu alie valia suit nyeusi, ya suruali, kwamba mbali ungeweza kusema ni suit ya kiume, “salaam dada Careen” alisalimia yule mwanamke huku akiinamisha kichwa chake mkono mmoja akiuweka kichwani mwake usawa wa utosi, na mwingine kifuani, hiyo ni kwa wanawake, maana kwa wanaume mkono mmoja utosini, mkono mmoja mgongoni, “hoooo! karibu Jasmin, kuna kazi nataka unifanyie” alisema Careen japo sauti ilikuwa ya chini na tulivu, lakini Jasmin aliweza kuona tabasamu afifu usoni kwa boss wake huyu, alietoka nae #mbogo_land, ilionyesha wazi kuwa boss wake leo alikuwa na kitu cha tofauti, pengine ni kuwashinda tena wakina Kalonga na vijana wake.**
Naam Queen au sada kama tulivyozowea kumwita kule Mwana Mmonga, aliekuwa ametopea kwenye usingizi mzito anakoroma kwa raha zake, akastukia akipigwa kofi la nguvu mgongoni mwake, pah!! “mshenzi wewe umetokwa kutombw…. huko, ukaona gia ya kuingilia hapa kwangu ni kisingizo kwamba unaela” alisema Emma, na kumfanya Sada akurupuke kitandani na kumtazama Emma kwa macho ya mshangao, kama vile amwelewi anachoongea, “ela zewenyewe ziko wapi?” aliuliza Emma ambae sasa alikuwa amesimama chini akimtazama Sada aikuwa kitandani anajikuna mkogongo, kutokana na maumivu ya lile kofi, “kwani wewe ujaona pochi ya ela humo ndani ya begi?” aliuliza Queen huku anavuta begi tupu na kulijaribu kuking’uta, lakini akukuwa na kitu, akatazama nguo na viatu vilivyokuwepo pale kitandani, lakini hakukuwa na kitu, “jamani ela zikuwepo humu ndani ya….” kupewa nafasi ya kumalizia kuongea alichokusudia, alishtukia kofi zito likitua usoni kwake, pah! “mamaaaaa na kufaaaa” alipiga kelele Sada, huku akiona giza usoni mwake, “kufa tu mbwa wewe, ebu toka nje haraka, nakufuma unaongea na hawara yako, alafu unasingizia sijuwi kuna ela zikowapi sasa?” aliuliza Emma huku akimtazama Sada kwa jicho kali, lenye hasira nyingi sana, ukweli mpaka hapo Sada akuwa na ata chembe ya kilevi kichwani mwake, pombe zote zilisha mtoka, hakuelewa kilichotokea, “si….si….sijuwi, mi…mi….mmm” ukweli wasi wasi na uoga ulio mshika Sada ulizidi kumtia hasira Emmanuel Pengo mbili, ambae alirusha ngumi mzito kuelekea usoni kwa Queen ambae uoga wa kuziba uso wake ulimsaidia, na ile ngumi kwenda kukita kwenye mikono yake, japo alihisi maumivu yakipenye kwenye usowake, lakini kosa mikono ile hakika asinge tamani kwa mpasuko ambao angeupata, kwa ngumi ile nzito, ambayo aikuja pake yake ilifwatiwa na kofi la mgongoni, hapo Sada ambae anamfahamu vyema Emma, akajuwa kuwa kinachofwata nikipigo cha mbwa mwizi, lakini hakuwa na chakufanya maana hakuwa na pakwenda, kilicho bakia ni kuficha uso apigwe weeeee, mpaka hasira za Emma zitakapoisha.
Kipigo kilidumu kwa dakika tano nzima, na kuja kuisha baada ya Emma kuamua kufanya ukaguzi wa sehemu zote nyeti za Sada, ambazo yeye uzitumia kumwingilia kimwili, “bahati yako ningekuta uchafu, leo ningekuuwa” alisema Emanuel Pengo mbili, mala baada ya kumaliza ukaguzi wake, “aya niambie ilikuwaje, mpaka umepoteza fedha” alisema Emanuel, na hapo sada ambae sasa alilazimika kusimamisha kilio chake, na alimsimulia Emmanuel kila kitu, kuanzia kwenda kumchukuwa Peter na Michael pale mtini Pub, na kwenda kumtelekeza Makukimaluga chumba namba sana cha ghorofa ya tatu, na yeye kwenda kumsubiri Msogeze pub, “nimekumbuka kuna wakati niliiweka ile pochi mezani, nazani nilipolala kuna wezi wameiba” alisema Queen akionekana kukumbuka, “kumbe wewe ndie ulie mpeleka yule mjinga pale Makimakuluga, ametuaribia kila kitu yule mbwa” alisema Emmanule ambae nusu ampige tena Sada, kwa kosa alilo lifanya, “kwahiyo yule fala ndio Peter?” aliuliza Emma kwa mshangao, wa kuto kuamini, Sada akaitikia kwa kichwa, ungesema anajuwa kilicho mtokea Emma, “yani mjinga mmoja toka kijijini anakuja kuaribu inshu za watu” alisema Emma kwa hasira huku anachukuwa simu yake na kumpiga kwa Hussen…..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!