KIAPO CHA MASIKINI (23)

SEHEMU YA 23

ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA MBILI: “lakini tungempa muda iliafanye mawasiliano na ndugu zake” alisema mwingine na yule mwenye kimbele mbele, ambae alikuwa ni mfanyakazi wa hotel mwenye jinsia ya kiume akadakia, “bwana ee mimi nimesha piga simu polisi, wapo njiani wanakuja” alisema yule jamaa na akati huo huo wakasikia ngurumo ya gari likiingia kwa kasi ya hajabu pale Hotelini, na kufunga brake za ghafla, kusotesha tairi zake kwafujo, “tena haoooo! wamesha ingia”……Endelea…
Alisema yule mhudumu ambae, unaweza kusema kuwa ategemei kama hipo siku na yeye atakuja kupata shida yoyote, “hivi we Beka, nani alikuambia upige simu bwana, ilibidi kwanza tumpe nafasi ya kuwasiliana na zaidi na ndugu zake” alisema mmoja wa wahudumu mwenye jinsia ya kike, “atujuwa mwenyewe bwana, polisi nako ni sehemu anaweza kuomba kuwasiliana na ndugu zake, vile vile” alisema Bakari, na baadhi ya wenzie wakamuunga mkono, “ata tia hakiri, sikunyingine akija mjini, atakuja kwa heshima” alisema mwenzie, ambae kichwa chake nikama kime zidi ukubwa hivi, na wsakati huo huo wakaingia polisi watatu, ukweli Peter akajiona mwenye bahati mbaya, na kwama la kwanza anaenda kulala kituo cha polisi, ilo siyo tatizo kwake tatizo ni mwanae Michael ata mwacha na nani, au na yeye taenda kulala kituo cha pilisi.
Naam baada ya pilisi kuongia tu, wakaitaji maelezo ya tukio, hapo siyo manager wala yule dada wa mapokezi, alie anza kutoa maelezo, ni yule kijana alie fahamika kwa jina la Bakari, ndie alikimbilia kutoa maelezo. **
Naam ebu turudi kijijini mwanammonga, nyumbani kwa mzee Jacob, mambo yalikuwa moto, mambo yalikuwa changanyikeni, ni mala baada ya simu ya mzee Jacob, kuzima chaji, kabla aja maliza kuongea na kijana wake Peter, ambae alimweleza kuwa anaitaji msaada kwamaana yupo kwenye matatizo makubwa, tena ameibiwa simu, ikiwa ni neno la kwanza kulisikia, “mume wangu twende mjini tuka mfwate Peter” alisema mama Peter, ambae alikuwa amechanganyikiwa zaidi kuliko mume wake, “lakini mke wangu, mjini ni kubwa sana unazani tutampataje?” aliuliza mzee Jacob, ambae pia allishtushwa na simu ya mwanae, “nilijuwa tu, akikutana na huyu mwanamke lazima yatokee yakutokea” alilalamika mama Peter, “lakini mama Peter, unajuwaje kama ni Sada ndie alie sababisha hayo yote, pengine ni watu wengine ndio wamemwibia” alisema mzee Jacob, lakini mama Peter akukubariana na mumewe, “unazani ni nani mwingine zaidi yake, ni huyo huyo mshenzi, safari hii na mfunga, awezi kumfanyia hivi mwanangu, na kama amelisha uchafu, atanijuwa mimi ni nani” alisema mama Peter ambae hasira yake ilikuwa kubwa sana.
Naam baada ya majadiriano marefu, mwisho wake wakakubariana waelekee mjini, ambako watajuwa huko huko pakuanzia kumtafuta kijana wao.**
Kijana Hussein au dogo Janja, kama walivyozowea kumwita watu wake wakaribu, na wanao mfahamu, mida hii alikuwa karibu kabisa na lango la kuingilia kwenye jengo kubwa la hotel kubwa ya kitajiri ya MAKIMAKULUGA, pamoja na wenzake wawili, wakifwatilia tukio la kijana alie washambulia jana usiku, akionekana anadaiwa fedha ya kodi ya chumba, alicho lala usiku wa jana hapa Makimakuluga, “huyu fala kweli, aliwezaje kulala hapa tena ghorofa ya tatu VIP, wakati hana ata senti moja” alisema Janja, huu wakitazama kule ndani ambako sasa polisi walikuwa wanapewa maelezo juu ya kilicho tokea, “kwahiyo kijana ulijuwa hapa wanalala bule, kwanini unachezea biashara ya watu” aliuliza mmoja kati ya polisi watatu waliokuwepo pale mapokezi, “kaka polisi, hapa mimi nililetwa, na sikujuwa kama pana lipiwa fedha nyingi kiasi hiki” alisema Peter, huku wakina Janja wakifwatilia tukio na maongezi, “uliletwa na nani na yupo wapi, na hizo fedha zako zipo wapi?” aliuliza yule polisi mwenye cheo cha koplo, na Peter akaanza kueleza jinsi ilivyokuwa, mpaka anamaliza kuna baadhi ya watu walisikitika sana, ila polisi na watu wengine akiwepo Bakari, awakusikitika ata kidogo, ndio kwanza Bakari alikuwa anacheka, “hapa ndiyo mjini kaka, sisi tunachotaka nifedha ya watu” alisema Bakari, na wakati huo huo, kuna gari jingine dogo aina ya Toyota V8 jeusi, liliingia kwenye viunga vya hotel, na kusimama, kisha wakashuka watu watatu, kati yao kulikuwa na mwanaume mmoja na wanawake wawili, Jasmini akiwa ni mmoja kati ya wale wanawake wawili, wote walikuwa wamevalia suit nyeusi, zilizo wapendeza kweli kweli, huku ndani yagari akibakia dereva peke yake.
Watu wale watatu waliingia moja kwa moja ndani, na kuishia pale mapokezi, ambapo palikuwa na watu wengi pamoja na polisi, “bwana Peter hiyo siyo shauri letu, kinachotakiwa ni wewe kulipa fedha ya watu, vinginevyo tuondoke kuelekea kituoni, alisema yule koplo wa polisi, huku anatoa pingu kiunoni, tayari kuvisha Peter, hakuna ata mmoja alie mjari Michael ambae sasa alianza kuhisi kunachotaka kumtokea baba yake, nikwamba baba yake huyo, yupo kwenye matatizo, “salaam waungwana” alisalimia Jasmini, huku yeye na wenzake wawili wakiinamisha kichwa kwa hesima, hakuna alie washangaa, sababu salamu hii inafahamika, ni ya watu toka #mbogo_land, “salamaa wahesimiwa, poleni kwa usumbufu, kuna watu wanadharau sana, inabidi aende akajifunzie huko polisi” alisema manager, huku anawasogelea wale wageni wenye suit nyeusi, “poleni sana, ila sisi ni wafanyakazi toka #mbogo_land sonara, tume tumwa na madam Careen kuwafwata wageni wake, walifikia chumba namba saba, cha ghorofa ya tatu” alisema Jasmin, wakati huo tayari Peter alikuwa amesha vishwa pingu, kwenye mikono yake, na wanaanza kumkokote kumpeleka kwenye gari, huku mwanae Michael, alikuwa ameng’ang’ania mguu huku anaanza kupolomosha kilio, “mgeni wa namba saba, ebu kwanza” alisema muhudumu kwa sauti ya mshangao kidogo, huku anamtazama mhudumu wa vyumba, ambae pia alitakiwa kuambatana na polisi, waliokuwa wanatoka nje na Peter, “eti Suzi, chumba na saba cha ghorofa ya tatu, sindio alilala huyo jamaa?” aliuliza manager, kwa sauti ya chini, na yule mhudumu alieitwa Suzy, ambae alisimama na kugeuka, akamtazama manager wake, “ndiyo ni yeye, kwani kuna nini?” aliuliza yule mhudumu, “awa ni watu toka #mbogo_land, wametumwa kuja kumchukuwa” alisema manager, kwa sauti ya chini, nikama awakutaka watu wengine wasikie, huku sauti zao zikiwa zimejaa mishangao, kwanza Suzy aligeuka na kumtazama Jasmini, kisha na kisha wenzake, yani yule mwanaume na mwanamke, ambao uvaaji wao, na mwonekano wako, aukufana na kumwulizia kijana toka kijijini alie tapeliwa mjini, “kwani wamesema, wanamtaka wa nini?” aliuliza Suzy, kwa sauti ile ile ya chini, wakati yule polisi Koplo, aliekuwa anasaidia kumtoa nje Peter, alisimama na kuwatazama, “manager inabidi tuongozane, wewe na mhudumu alie mhudumia huyu mtuhumiwa” alisema yule polisi, alie onekana kuwa haraka sana, “sawa mweshimiwa, lakini nazani kama vile kuna watu tunapaswa kuongea nao kidogo” alisema manager, na yule polisi, alisogea pale waliposimama wao, “mzee awa ni watu toka ofisi za #mbogo_land, wamemfwata huyo jamaa, wanasema ni mgeni wa boss wao” alisema Manager, na polisi yule akamtazama manager kwa mshangao, “unamaanisha ni mgeni wa boss wao Careen?” aliuliza koplo wa polisi, huku Suzi nae akishangaa, wakati huo Bakari na baadhi ya wahudumu wengine wakisogea pale waliposimama wao, “ndiyo ni mgeni wa boss wetu, je kuna tatizo juu yake?” aliuliza Jasmini ambae aliona kama vile kunajambo wanajaribu kuwaficha, polisi manager na wenzake wakatazamana, kwa macho ya mashaka, na mshangao, “we dada una uhakika kama yeye ndie mgeni wa yule mama wa dhahabu, au mmemfananisha, kwani alilala chumb anamba ngapi?” aliuliza Bakari ambae alionyesha kuto kuami, na kumdharau sana Peter, “ndiyo kaka yangu, boss wangu anamgeni hapa, alilala chumba namba saba ghorofa ya tatu, yupo na mtoto mdogo” alifafanua Jasmin, kwa sauti ya upole, Bakari akatoa macho kwa mshangao,”aiwezekanani, lazima mtakuwa mme changanya, kama vipi wakamtoe huko huko kituoni” alisema Bakari, ungesema alikuwa na ugomvi mkubwa na Michael………

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!