KIAPO CHA MASIKINI (25)

SEHEMU YA 25

ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA NNE: Naam mtaa wa Zanzibar mbele ya jengo kubwa la biashara la #mbogo_land, sonara, palionekana kujaliwa na watu wengi sana waliokuwa wanaingia na kutoka ndani ya jengo ilo kubwa la ghorofa mbili, kufanya manunuzi yao, ndani ya jengo ili kulikuwa na watu wengi sana, toka sehemu mbali mbali, wakifanya manunuzi yao, wapo waliokuwa na familia zao, yani baba mama na watoto, au mke na mume, wachumba au marafiki, pia wapo waliokuwepo mama mtoto, baba na kijana wake, ikiachilia hao, pia walikuwepo waliokuja hapa wakiwa mmoja mmoja. ……… Endelea…
Kwa upande wa wafanyakazi wa duka ili ambalo lile kusanya maduka mengi ya aina mbali mbali yanayo milikiwa na mwana dada Careen mama wa dhahabu, leo walishangaa kwa jinsi boss wao, alivyokuwa anaongea nao kwa katika hali ya kawaida, kama siku nyingine ambapo ageongea neno moja kisha akaitaji jibu na ikawa mwisho wa maongezi, lakini kitu cha ajabu leo yeye Careen aliweza kuanzisha maongezi yeye maongezi, “Jenny unaonaje maendelea ya biashara msimu huu?” aliuliza Careen kwa sauti tulivu, pasipo kutabasamu wala kuonyesha dalili ya uchangamfu, “inaenda vizuri kwakweli, naona kila siku wateja wanaongezeka” angejibu mfanyakazi anaeitwa Jenny, “vipi kuna ulazima wa kuongeza wafanyakazi wengine?” aliuliza Careen ambae licha ya utulivu, aliokuwa nao, lakini kwa awa wanao mfahamu waliweza kuhisi furaha aliyo kuwa nayo, furaha ambayo awakuelewa inesababishwa na nini, “sidhani kama kuna uitaji huo boss, naona tuliopo tuna tosha kabisa” alisema Jenny, na siyo Jenny pake yake alie ongea nae, wapo wengine pia alio ongea nao, na wakashangaa Careen, ambae mala kwa mala alikuwa anawasiliana na baadhi ya wafanyakazi wake, akiulizia mwenendo wa maagizo aliyo yatoa asubuhi.
Lakini licha ya hayo yote kuna wakati mwanamke huyu, ambae ukimwona unaweza kujiuliza kwanini akugombea umiss, pengine angeshinda taji la dunia, alikuwa ana tulia juu ya kitichake kizuri cha kuzunguka, akionekana kuwaza jambo, ni picha ya kijana yule alie msaidia jana usiku, jinsi alivyo pambana na wale vijana wawili, ambao alijuwa fika kuwa wametumwa na bwana Kalonga, ambao aliwapiga vibaya sana, na vijana wale kukimbia zao, kisha kijana yule kuokota mkoba wake na kumnyayua yeye.
Sasa kitendo kile cha kunyayuliwa ndio kilicho mfanya Careem akumbuke sana tukio lile, maana kila lipokumbuka kitendo kile alihisi mwili wake ukishikwa na msisimko wa ajabu, na kutamani kama kile kiti chake cha ofisi, ndiyo kinge kuwa mikono ya yule kijana, ambae mpaka sasa ajafahamu kama amesha patikana au la, ni kijana ambae aliwai kumsaidia hapo mwanzo, na akutaka chochote toka kwake, “ni mawazo gani haya?” alijiuliza Careen huku akijaribu kusimama toka kwenye kiti na kutembea mpaka kwenye dirisha kubwa la kioo, akachungulia nje na kuona jinsi wateja wake walivyo kuwa wanaingia na kutoka pale dukani kwake, huku mawazo juu ya kijana yule msaidiaji yaking’ang’ania kichwani mwake, akavuta picha ya kijana yule akiwa amevalia nguo za aina mbali mbali na kunyoa nywele zake vizuri, pamoja na viatu vizuri, siyo yeye tu aliwaza pia juu ya yule mtoto alie mwona amelala kwenye kochi, “yule ni mume wamtu, je mke wake yupo wapi?” alijiuliza Careen, huku anatoka dirishani na kusogea kwenye kioo kibwa cha mle ofisini mwake, akajitazama kuanzia juu mpaka chini, na kama kawaida yake, alikuwa amepndeza kweli kweli, kwa gauni lake refu, la kijani, na mauwa mekundu, “lakini yeye ajatamani kuwa karibu yangu kama wengine?” alijiuliza Careen ambae mwanaume wakwanza kumpenda aliowa mwanamke meingine, nae ni kiongozi wa #mbogo_land, yani king_elvis wakwanza.
Wsakati anawaza hayo, mala akasikia simu yake inaita, akaifwata na kuitazama, akaona ninamba ngeni, ndiyo ilikuwa inapiga, akajuwa ni mambo ya kibiashara, akajiweka sawa na kuipokea mala moja, “Mbogo Sonara, Careen naongea nikusaidie tafadhari, aliongea Careen kwa sauti tulivu, “hiyo sauti inafaa sana chumbani, ila napenda kukuambia, ila ya jana usiku ni salamu, tu, siyo kwamba nilishindwa kutia mikononi, ila sikupanga iwe hivyo, na huyo mbwa wako unae mtegemea jiandae kuokota mwili wake, siku chache zijazo” ilikuwa ni sauti nzito ya kiume toka upande wapili wasimu, mapigo ya moyo ya Careen yakashtuka na kuanza kwenda mbio, huku akijuwa kuwa tayari amesha mwingiza kwenye matatizo kijana wawatu, “tafadhari yule kijana ausiki kwa lolote alicho kifanya ni kutoa msaada kwangu, vita ni ya mimi na wewe, naomba usimdhuru kwa lolote” alisema Careen kwa sauti ya kuomboleza, hapo kikafwatia kicheko, cha kuchukiza toka upande wapili wa simu, yani kwa bwana Kalonga, “kumbe kuna watu una wajari siyo, sasa ukitaka yule fala, nimwache tukubaliane jambo” alisema Kalonga kwa, kwa sauti nzito yenye kujaa tamaa, sijuwi ni kwanini, lakini Careen alijikuta anatamani kufanya lolote ili kumsaidia kijana yule, “jambo gani nikufanyie, nipo tayari kukupatia kiasi chochote cha fedha lakini usimdhuru kijana wawatu” alisema Careen alieonekana kujawa na uoga mwingi, “kama hupo tayari kweli, basi leo utakuwa mgeni wangu, tukutane njia panda ya mji mwema, utanikuta hapo kwaajili ya kwenda sehemu ambayo tutaonge kwa usiku mzima, usiku wenye furaha” alisema Kalonga kwa sauti kavu nzito ya kujiamini.
Kwanza kilipita kimya kifupi, kama vile Careen anawaza jambo, alikumbuka jinsi Kijana yule shupavu, mrefu kidogo, mwenye umbo lenye kuvu, na kifua kipana, na mikono inayo imili, jinsi alivyo watandika vijana wawili wa Kalonga, kisha kachezesha mdomo kidogo, ikiwa ni ishala yake ya kutabasamu, ukibahatika kuliona tabasamu ilo mwaka huu, basi ungeweza kuliona tena mwakani au mwaka baada ya mwakani, tarehe kama hizi, “unajingine ilo limekataliwa” alisema Careen kwa sauti tulivu, soyo kama ile ya mwanzo iliyojaa wasi wasi na uoga, “pengine unaona kitumbua chako ni bora zaidi kuliko uhai wa mtu siyo?” aliuliza Kalonga, kwa sauti nzito yenye kitisho, “labda turekebishe kidogo bwana Kalonga, siyo tu uhai wa mtu, ata kwa gharama ya uhai wangu mwenyewe, sito kuluhusu ata kinganja cha mkono wako kiguse bega langu, na usipige tena simu, labda kama utakuwa na jipya zaidi ya ujinga wako” alisema Careen na kukata simu, kisha akatulia kwa sekunde kadhaa, huku akijishangaa kwaujasili wa ghafla alio upata, akajikuta anajitabasamulia mwenyewe.***
Yap! mida hii ndiyo mida ambayo Sada au Queen alishtuka toka usingizi, baada ya kumshtuliwa na simu ya Emanuel iliyokuwa inaita, huku maumivu ya mwili yakiwa yame utawara mwili wake, kitokana na kipigo kilicho mkuta mapema leo, akamtazama Emma ambae alikuwa bado amelala fofo, akainuka na kuichukuwa simu ile kisha akamsogelea Emanule, ambae alisha mkataza upokea simu yake, “Emma…. Emma…. we Emma, amka simu yako inaita” alisema Sada alie simama pembeni ya kitanda, lakini Emmanuel alionekana kuendelea kukoroma, ndipo alipo amua kumtikisa kwa kumshika kwenye sehemu za mgongo, ambao ulikuwa juu, “we! Emma simu yako inait….” doooo! ukweli nikwamba Sada au Queen akumaliza kusema neno lake, maana Emanuel alikurupuka, huku anaachia yowe zito, “haaaaaa unaniumiza we Malaya” neno ilo halikutoka bule, lilitoka na ngumi mzito ya kushtukiza ambayo ilituwa usoni kwa Sada na kukita kwenye mdomo wa Sada, ambae aliachia simu ikianguka na kudaka mdomo wake, huku akishinda kupiga kelele yoyote, kutokana na damu kujaa mdomoni, huku Sada huyo huyo akihisi kitu kigumu kikiwa mdomoni mwake, akakitemea mkononi, na kuona kuwa ni jino lake mwenyewe, “pumbavu kwanini umeangusha simu yangu ona ilivyo pasuka” alisema Emmanuel huku anainuka na kutandika tena kofi la usoni sana, ambae sasa aliweza kuachia kelele za kilio, “kama unipendi uniambie tu, siyo kunipiga hivi, ulinikuta na masha yangu siwezi kukosa kwapakuishi mimi” alisema Sada huku anaangua kili, na hapo akazinuliwa teke zito, ambalo katika kujaribu kulikwepa, nalo likatua ubavuni na kumtupa pembeni na kumwangusha chini, “mshenzi nini, ebu toka ndani mwangu” alisema Emmanuel huku anaendelea kumshushia kipigo.
Ukweli aipendezi ata kusimulia, maana kilicho mkuta shemeji yetu, ambae ndugu yetu Peter anaweweseka juu yake, tena usiku na mchana, yani Sada alianza kuweka vitu vyake kwenye begi, aliloliiba toka kwa Peter, huku anashushiwa kipigo cha mbwa mwizi, alie kula mboga pekee ya wageni, kipigo ambacho akikuchagua sehemu ya kutua katika mwili wa Sada, ambae alilia mpaka akachoka, na kipigo kilichodumu kwa dakika saba, kilikoma baada ya Emma kuhisi maumivu makali kwenye mgongo wake, ni kutokana na kipigo cha jana usiku, Sada alikusanya nguo zake na zile za wakina Peter na Michael, bila kusahau simu chakavu ya Peter, ambayo alikuwa ameizima, kisha akaondoka zake kuelekea majengo kwa Rose.***
Yap! saa tatu na robo, Peter na Michael walikuwa ndani ya gari lilile aina Toyota V8, pamoja na wale wajumbe toka kwa Careen wakielekea maji maji shule ya msingi, karibu na Angoni armys hotel, tayari malipo yalisha fanyika kule hotelini, japo Peter hakujuwa huko anakopelekwa kuna nini kinaenda kutokea, ila kichwani mwake alikuwa amawaza kwanini Sada amemfanyia vile, “yani ameshindwa kuwaza ata kuhusu mwanae mwenyewe, hivi huyu mwanamke amekutwa na nini” aliwaza Peter akiwa namachungu makubwa sana moyoni mwake….……
MWISHO SEASON ONE

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!