
SEHEMU YA 26
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA TANO: Yap! saa tatu na robo, Peter na Michael walikuwa ndani ya gari lilile aina Toyota V8, pamoja na wale wajumbe toka kwa Careen wakielekea maji maji shule ya msingi, karibu na Angoni armys hotel, tayari malipo yalisha fanyika kule hotelini, japo Peter hakujuwa huko anakopelekwa kuna nini kinaenda kutokea, ila kichwani mwake alikuwa amawaza kwanini Sada amemfanyia vile, “yani ameshindwa kuwaza ata kuhusu mwanae mwenyewe, hivi huyu mwanamke amekutwa na nini” aliwaza Peter akiwa namachungu makubwa sana moyoni mwake….…… Endelea…
Akishindwa kumwelewa mzazi mwenzie huyo kwa kumwibia kila kitu, yani kuanzia fedha, nguo na mpaka miswaki “yani akufikilia kuniachia ata fedha kidogo, ambayo ingeniwezesha kurudi kula na kurudia kijijini” kama unge mtazama vyema kijana huyu wakati anawaza hayo, ungeweza kuona macho yake yana jawa na machozi, kiasi cha kutaka kuchuruzikia mashavuni, kwa upande wa Michael yeye alikuwa anafurahia kupanda gari ili zuri lenye kunukia sana, na kumfanya asahau kuhusu njaa iliyokuwa inavuluga tumbo lake, “baba ili gari zuri lanani?” aliuliza Michael, alie kaa karibu na baba yake katika seat ya kati kati, “gari la shangazi yako” alijibu Peter akizuwia sauti yake isionekane kuwa yenye machungu, “utaninunulia viatu vingine baba?” aliuliza Michael na hapo Peter akakumbuka jinsi jana usiku kijana wake huyu, alivyokuwa anaomboleza mama yake asiondoke na nguo zake, “ndiyo mwanangu nitakununulia vingine vizuri” alisema Peter ambae kichwani mwake alipanga kuwa, mala tu atakapokutana na yule mwanamke asie ongea, alie msaidia jana usiku ikiwa ni mala ya pili kumsaidia, angemwomba msaada wa kurudi kijijini, nao ulikuwa ni kupata fedha kidogo, ya nauri, japo akujuwa mwanae Michael ata kula nini kwa muda ule, “kaka kwanza nikupe hongera sana, kwa kualikwa nyumbani kwa madam Careen, kila kitu kitaenda sawa, naamini kwa ulicho mtendea awezi kukuacha uende bule, lazima atasaidia pale ulipo poteza” alisema Jasmin alie kuwa amekaa seat ya abiria wa mbele.
Ukweli kwa upande wa Peter, akuona kama alitenda jambo kubwa sana kwa Careen, mwanamke mrembo kuliko wote aliowai kuwaona kwa macho yake, labda kwenye video, tena wale kutoka nchi za mbali, au aliopata kuwasoma kwenye vitabu.**
Naam Sada alitembea taratibu huku akiwa ameziba eneo la mdomo, wake alipo bomolewa jino, kwa ngumi ya Emmanuel, akuweza kutembea kwa haraka, kutokana na maumivu makali, yaliyojaa kila kona ya mwili wake, kuanzia kichwani mpaka kwenye nyayo za miguu yake, maana kipigo alicho kipata toka kwa mtu anae mwita mpenzi wake akikuwa kidogo, mpaka leo ameamua kuondoka hapa nyumbani kwake, ujuwe yame mfika shingoni, lakini uwezi kuamini, licha ya yote yaliyo mkuta lakini Sada akutaka kumfilia Peter kuwa ndie mtu sahihi kwake, na akutaka kuwaza juu ya Michael mwanae mwenyewe, kwamba yupo na hali gani baada ya kuiba fedha zote zambazo zinge wasaidia yeye na baba yake, siyo tu kutimiza malengo yao, bali ata kula na kufanya nauri ya kurudia kijijini.
Sasa basi wakati ana katiza maeneo ya majengo mwosho wa lami, ikiwa ndio anaingia mtaa wa majengo, akashangaa kuliona duka moja kunwa la vitu vya urembo, lililopo kwenye moja ya nyumba, iliyopo mbele ya barabara iendayo stendi kuu, kwenye moja ya nyumba za mtaa huu wa mwisho wa lami, zilizopo pembezoni mwa barabara, yalikuwa ni mabadiriko ya ghafla, maana sikuchache zilizopita, alipita mtaa huu na hakuweza kuona duka ili, alikumbuka fedha alizopoteza usiku wa jana, pengine zingetosha kabisa kufungua duka kama ili, au zaidi ya ili, lakini baada yake fedha zimeondoka na yeye kubakia na maumivu makali, alitamani kwenda hospital kupata japo dawa kwaajili ya pengo na maumivu ya mwili mzima, lakini akuwa na ata mia ya kununua kipande cha muogo cha kutuliza maumivu ya njaa aliyo kuwa nayo.
Sada akutaka kuwaza sana juu ya ilo, akaendelea kutembea kulipita lile duka, huku kichwani mwake akiomba itokee tena bahati ya kupata fedha kama zile, toka kwenye huyo mjinga wa wake wakijiji, ambae alimini kuwa bado atakuwa anampenda tu, “nikizipata tu! nina mwonyeshea Emma mpaka yeye mwenywe atanifwata na kuniomba msamaha, kwa alicho nifanyia” aliwaza Sada au Queen kabla ajasikia sauti ya kike ikimwita, “we da Queen, mambo” nisauti ambayo aikuwa ngeni masikioni kwa Sada, ambae aligeuka upande wa kushoto, kutazama sauti ilikotokea.
Sada alimwona Kadara akiwa amesimama kwenye valanda la lile duka la urembo, na vipodose, akimtazama kwa tabasamu la bashasha, “mh! amenituwaje wakati nimejifunika kanga namna hii, alijiuliza Sada, huku ana mtazama Kadara na kuowanisha na lile duka, maana alisha pata picha kuwa lile duka ni lakadara, sababu siku chache zilizopita alimkuta Kadara ana fanya manunuzi, kwaajili ya kufungua duka lake, akujiuliza sana, maana tayari alisha juwa kuwa lile duka ni mali ya Kadara, ambae sikuchache zilizopita, alimpa habari ya kuwa Peter alikuwa na safari ya kuja mjini, huku akimpatia namba za simu, “safu tu Kada” alijibu Sada huku kisha akataka kuendelea na safari zake, lakini Kadara akawa king’ang’anizi, “salama kweli da Queen mbona kama unaumwa?” aliuliza Kadara huku anatoka pale dukani kwake na kumsogelea Sada ambae ilimbidi asimame, kumsubiri, pengine ingekuwa bahati yake, na angepata msaada, “Emma amenipiga ata sija mkosea chochote” alisema Sada kwa sauti ya kulalamika, iliyokaribia kuangua kilio, “jamani pole ebu nione” alisema Kadara huku anamfunua usoni Sada, ambapo aliweza kujionea jinsi mwanadada huyu alivyo vimba vimba na kupasuliwa sehemu yamdomo huku pengo kubwa likionekana mdomoni mwake, “jamani kwanini amefanya hivi?” aliuliza kwa masikitiko makubwa sana, Kadara, “yani eti kosalangu ni kumwamsha apokee simu yake” alisema Sada kwa sauti inayo ambukiza uzuni na masikitiko, “pole sana da Queen sasa kwanini ujaenda hospital?” aliuliza Kadara huku anamshuka mkono Sada, na kumwongoza kuelekea pale dukani kwake, “yani hapa sina ata shilingi mbovu” alisema Sada, kwa sauti ambayo ilitosha kabisa kuwa kiombeo cha msaada, “vipi kuhusu Peter, ulimpigia?” iloswali Sada akulitegemea hivyo kiukweli hauwa amejiandaa kwa jibu la swali ilo, kwa wakati ule, “niwasilianae nae wanini mshenzi yule, sina ata mpango nae” alisema Sada kwa sauti ya kujifanya, yani ungesema kuwa nikweli akuwa amekutana nae, “lakini mbona ni kijana mzuri tu, kila mwanamke anatamani kuishi nae kule kijijini” alisema Kadara, kwa sauti ya msisitizo huku anamwachia Queen pale nje ya duka, na kuingia ndani kumtolea kiti, “umeshasema kijijini, atakuwaje bora kwangu, mwache atafute mshamba mwenzie” alisema Sada, akioyesha kuwa akuwa anatania, “lakini da Queen ni bora kuishi na mtu anaekupenda kuliko mtu anae kufanyia hivi” alisema Kadara alie toka na viti viwili ndani kimoja akakalia Sada, na kimoja akakalia yeye mwenyewe, “bora niolewe na kichaa wa mjini kuliko kurudiana na Peter, ata akiwaje, yani namchukia, namchukia sana mbwa yule” alisema Sada akijaribu kupandisha sauti, lakini akajikuta akipatwa na maumivu makali yam domo, “we da Queen usiseme hivyo jamani, unakufuru” alisihi Kadara, ambae ata mwonekano wake, ulibairika nakuwa tofauti na wakati ule anafanya kazi ya kuuza chakula pale msogeze pub, “yani na hapa Kadara, ata nikose mwanaume kabisa, na niwe na shida vipi, siwezi kurudiana na Peter, yani silipendi kama nini” kiapo cha Sadakili mshangaza sana Kadara, ambae alijiuliza sababu gani inamfanya huyu mwenzie atoe kiapo kama hiki, kwa mwanaume ambae ajamkosea lolote, “sawa wewe mwenyewe ndie unaejuwa, sasa huku unaenda wapi?” aliuliza Kadara, ambae alimwonea huruma sana huyu mwanamke mwenzie, toka kijijini kwao, “naenda kwa Rose yule rafiki yangu, na juwa Emma lazima ayaifwata tu” alisema Sada, ambae kiukweli, licha ya majigambo, yake lakini alitia huruma, “basi sawa ila ngoja nikupatie ela kidogo uende kwanza hospital” alisema Kadara huku ana inuka na kuingia ndani ya duka lake, ambako akukaa sana akatoka akiwa na noti mbili za elfu kumi kumi mkononi mwake, akamkabidhi Sada ambae aliachia tabasamu zito na kuifanya sura yake ifanane na katuni flani ya kwenye tv, “asante sana Kada, yani hapa naeda sasa hivi hospital” alisema Sada huku anainuka na bgi lake mkononi, “da Queen ungesubiri boda boda kwanza” alisema Kadara, lakini nikama Sada alikuwa na haraka sana, maana aliendelea kutembea kwa kuchumbagila, kurudi alikotoka, “nitapanda nikikutana nayo” alisema Sada, ungesema ni kweli angepanda boda boda mala tu atakapo iona, lakini ukweli ni kwamba hakuwa na mpango huo.***
Yap! huko kijijini mambo yalikuwa moto moto, ni shangwe na vifijo, kwa familia ya bwana na bibi Nyoni, ambao walitembea nyumba moja baada ya nyingine, asa kwa wale walio amini kuwa ni marafiki zao, kutangaza kilicho mtokea Peter, “kweli ujinga ni mzigo, yani yule kijana amejiendea mjini kichwa kichwa, wenzie wamesha mingiza mjini, sasa mzee Jacob anaanza kulahumu Sada” alisimulia mama Sada, kwa sauti ya shangwe kama anasimulia ugomvi wa ulevini, “masikini jamani kijana wa watu, imekuwaje tena, mpaka akaibiwa?” angeuliza mama Nakomba, kwa sauti ya masikitiko, ikionyesha anamfahamu vyema kijana Peter, kuwa ni kijana mchapa kazi mwenye nidhamu, anamweshimu kila mmoja, na mwenye kujitolea kwa kila jambo, la kijamii, “eti wanaficha, ila atakuwa amepigwa sana, yule kijana, mjini kunawenyewe yeye anaenda kichwa kichwa” alisema mama Nyoni,kwa sauti ya kejeri, mume wake akidakia, “yame mkuta, hivi sasa wazazi wake wanaenda kusaka mtoto wao kama kuku mgeni kipindi cha sikukuu” alisema mzee Nyoni, ata kama ukutaka kucheka hakika ungejikuta unacheka, na mambo yalizidi kuwa moto baada ya kuwa kuta wakina kina mzee Mbilo, wakiwa wanakunywa ulanzi, nao wakajiunga na kuanza kumwaga story ya kuibiwa kwa Peter, huku hadithi iyo iliyo buniwa vyema ikiongezewa ubunifu zaidi, kila walipozidi kulewa, “yeye aliambiwa na Sada, kwamba akifika ampokee, lakini yeye akajifanya mjanja, ndio kwanza akamkimbia mwenzie, na kujifanya mwenyeji, kilicho mkuta niaibu kwa kijiji kizima” alisimulia mama Sada, yani mke wa mzee Nyoni, huku huku mzee Nyoni mwenyewe akisakafia kwa juu, “yani leo hii ukifika mjini usije ukajitambulisha kuwa unatoka mwanamonga, utaonekana nawewe mshamba tu” watu wote waliokuwepo hapo kilabuni, saa nne hii ya asubuhi, waliangua kicheko.** …..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU