KIAPO CHA MASIKINI (56)

SEHEMU YA 56

ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TANO: aliuliza mmoja, na hapo mama Sada akashusha kisonjo na kutazama kule linakotokea gari, hali hiyo pia ilikuwa upande wa mbele wa nyumba, ambako mzee Nyoni akiwa na wenzake wanaendelea kuongea ili nalile juu ya maisha ya binti yake huko mjini, na wao wakaliona gari moja kubwa kiasi la mtindo wa loli, likija taratibu, upande huo, Ilikuwa hivyo kwa mzee Nyoni na mke wake ambao nikama badi walikuwa wanaendelea kusemana, juu ya kuwachekea wakina mzee Nyoni, wote walisikia ngurumo ya gari na kutazama upande wa barabara, wakaliona gari ilo likija taratibu upande wao…Endelea…

watu zaidi ya hamsini waliweza kuliona gari lile, na kila mmoja akijiuliza limefwata nini pale kijijini, au linaenda kwa mzee nani, ukiachilia watoto ambao walikuwa wanalifwata nyuma huku wakilishangilia, “gari!! gari!! gari!” maana gari kama ili alikuwai kuonekana pele kijijini, zaidi ya bus kubwa chakavu la muundo wa zamani, ambalo uja kijijini majila ya kiangazi, namala chache kipindi cha masikaa kutokana na ubovu wa barabara, na bbasihiro utoka mapema saa kumi au tisa za usiku, na kurudi saa mbili au tatu za usiku, ukiachilia ilo ni magari chavu, ambayo utumika kubeba mzao toka mashambani,kuni au tofari na vitu vingine kama hivyo,

“sasa ili loli dogo dogo limefwatani” hayo yalikuwa ni maswali ya wengi, waliokuwepo pale, ukiachilia watoto ambao awakuwa wanaelewa chochote, zaidi ya kulishangilia gari lile, ambalo lilizidi wakuduwaza watu, na kuanza kuwapa majibu, baada ya kuliona likikata kona kuingia upande wa kushoto kuifwata njia afifu inayoingia nyumbani kwa mzee Jacob, ambae ata yeye na mke wake pia walitoa macho kwa mshangao, kulishangaa gari lile kwamba pale kwao linafwata nini, au limepotea nyumba, “au Peter ndio anakuja” aliuliza mama Peter, huku yeye na mume wake wakijitaidi kukodoa macho kutazama ndani ya gari, kupitia kioo kikubwa cha mbele, pengine wange mwona Peter akiwa Michael, ndani yagari lile,

lakini awakuweza kumwona ata mmoja wanae mfahamu, zaidi ya vijana watatu, waliovalia nguo zinazo fanana, ambao sura zao ni ngeni kabisa machoni pao, “mh! kama ni yeye ata kuwa amekaa nyuma au?” aliuliza mzee Jacob, huku yeye na mke wake na wanakijiji waliokuwa wanalitazama gari lile, wakishuhudia linaegeshwa kwenye uwanja wa nyumba yam zee Jacob, na kisha wakashuka wale vijana watatu, toka kwenye gari lile, alafu mmoja kati ya vijana wale akamfwata mzee Jacob, huku akiwa ameshika kibao flani cha plastic chenye kuambatishwa karasi flani zenye maandishi, “shikamoni wazee wangu” alisalimia yule kijana, huku wenzake pia wakisalimia toka mbali, kwa heshima na tahadhima, “marahaba vijana karibu sana” aliitikia mzee Jacob, huku watu wakiendelea kuwa tazama na wale walikosa subira wakianza kusogelea eneo lile la tukio.

Unajuwa nini kilikuwa kichwa kwa mama na baba Sada, ebu sikia mawazo yao, wote wawili walikuwa wanawaza kitu kimoja, maana licha ya mioyo yao kushtuka kwa kuona gari lile linakuja nyumbani kwa mzee Jacob, lakini walipata hisia kuwa, lile gari litakuwa linepotea njia, kwamaana nigari ambalo litakuwa limebeba mizigo ambayo inatoka kwa binti yao Sada, kuja kwao, waliendelekea kutazama kule kwa mzee Jacob, na kuwaona wale vijana watatu, wanachuka toka garini, na kusalimiana na mzee Jacob, japo awakusikia maongezi ya mzee Jacob na yule kijana mwenye makablasha mkononi, lakini walihisi kinachongelewa, “samahani mzee tunaulizia kwa mzee Nyoni” hiyo ilikuwa ni hisia yam zee Nyoni, na mke wake.
Lakini ukweli ni kwamba, maongezi ya mkijana na mzee Jacob yalikuwa hivi, “asante mzee, samahani hivi hapa ni kwa mzee Jacob?” aliuliza yuke kijana, sasa kwenye jibu, ndiko mzee Nyoni na mke wake walikokuwa wanasuubiria, lakini akujibu mzee Jacob, baada yake akajibu mke wake, “ndiyo hapa hapa mwanangu, karibu sana” ndilo lilikuwa jibu harisi, tofauti na mzee Nyoni, ambae alikuwa anahisi kuwa jibu, la mama Peter, lilikuwa ni “ndiyo mimi” hapo mzee Nyoni akamwona yule kijana akitabasamu, na kumpa mkono yule mzee Jacob, na kisha mke wake, huku anaongea maneno flani, ambayo mzee Nyoni na mke wake, alitafthiri kuwa ni “hongereni sana binti yenu ni tajiri sana, na ametuagiza tuwaletee hii mizigo” ukweli mzee Nyoni akainuka ghafla kama mtu alie kalia kiti kilicho lowa, “wacha nika jionee mwenyewe” alisema mzee Nyoni kwa sauti, huku wenzake wakimtazama mzee huyu kwa mshangao, ambae walimwona akielekea kule kwa mzee Jacob, na ata mke wake alipomwona aliinuka na kumfwata mume wake, wakiungana na wenzao ambao walikuwa wanaelekea kwa mzee Jacob, kupata umbea na kujuwa nini kimeletwa na gari lile kubwa.

“hongereni sana wazee” alisema yule kijana huku anampa mkono mzee Jacob, ambae alikuwa anashangaa hongera ya nini, “tumekuja kuwafungia solar, na vifaa vingine kama vile TV redio na taa za ndani na nje, ambavyo vimenunuliwa na mkurugenzi wa #mbogo_land Sonara, bi Careen Martin” alisema yule kijana ambae pia alimpatia mkono mama Peter, “Careen ndio nani, na kwanini atununulie solar?” aliuliza mama Peter, kwa sauti ya chini iliyojaa mshaka, kwamaana akutaka watu waliokuwa wamezunguka eneo la mbele la nyumba yao wasikie, ata mzee Nyoni na mke wake pia, naa walikuwa wamesha fika na kusimama mita chache toka walipokuwepo wakina mzee Jacob, wakifwatilia maongezi yale, sambamba na watu wengine wengi, na kuhisi kuwa wale jamaa wamekosea njia.

Hapo yule kijana akashangaa kidogo, “samahani mzee, unasema umfahamu Careen, huyu mwanamke mrembo hivi tajiri” aliuliza yule kijana alie shikilia makablasha, huku wenzake wakiwa wanaanza kushusha mizogo toka kwenye gari, “mwanangu nita mfahamu vipi na mimi sina binti tajiri” alijibu mzee Jacob, nae akionyesha mshangao, hapo yule kijana akatulia kidogo, “ok! labda nielekeze kwa mzee Jacob, ambae mtoto kijana anae itwa Peter, anaishi wapi hapa kijijini?” aliuliza yule kijana “hapo mzee Jacob na mke wake wakacheka kidogo, wakisaidiwa na baadhi ya watu waliokuwepo jilani wanafwatiia mazungumzo hayo, “Peter ni mwanangu yupo huko mjini, na mjukuu wangu Michael” alijibu mama Peter, huku meno yote yakionekana kwa tabasamu, “sasa mnashindwaje kumfahamu Careen, aya basi tia sahihi hapa tuanze kazi” alisema yule kijana akiwatania wale wazee wawili, huku anampatia mzee Jacob, lile kablasha, pamoja na karamu ya wino, “kwani yeye yupo wapi, si alisema leo anakuja na huyo rafiki yake?” aliuliza mzee Jacob, huku anapokea lile kablasha na ile karamu, kisha akaanguka sahihi, ya kupokea vifaa, japo yeye akusoma neno lolote, kwenye karatasi lile, “nazani mpaka sasa watakuwa njiani, maana wamewapigia sana simu mlikuwa hampatikani” alisema yule kijana huku anapokea makaratasi yake toka kwa mzee Jacob, “nikweli simu yangu jana mama yako aliitia kwenye maji, hapa napanga niende Namtumbo nikanunue simu nyingine” alisema mzee Jacob, akimweleza yule kijana,bae alikuwa anaelekea kwenye gari kuweka yale makablasha.

Mpaka hapo tayari mzee Nyoni na mke wake, pamoja na wale majilani waliokuwa wamamsimanga mama Peter, walikuwa wamesha aanza kupata jibu, ni majibu ambayo yalizisuta nafsi zao, asa walipoanza kuona mafundi wanaanza kufunga vifaa ndani ya nyumba ya mzee Jacob, watu walizidi kuongezeka kwa mzee Jacob, ungesema ndio palikuwa na sherehe, wapo walioshindwa kusubiri, wakaamua kubeba visonjo vya komoni, na vikopo vya ulanzi, wakinywea pale pale kwa mzee Jacob, hiyo yote ni kusubiri kumwona mwanamke ambae Peter anakuja nae, mwanamke ambae amesemwa kuwa ni mzuri na tajiri. walisahau kuwa kuna sherehe kwa mzee Mangolingoli,

“baba Peter hivi anacho tufanyia Peter ni haki kweli, sasa sikututia aibu kwa huyo rafiki yake” alilalamika mama Peter, akiwa amesimama pembeni kidogo na mume wake, “kututia aibu kivipi, si alituambiwa toka juzi kuwa atakuja leo na huyo mwanamke” alisema mzee Jacob, akirudisha mpira kwa mke wake, “lakini wewe ulisema kuwa huyo mwanamke ni waovyo, na akija atafikia nae kwake” alisema mama Peter, akimshutumu mume wake, “ebu sikia mke wangu, wacha nimtafute yule kijana wa mzee Nyongopa, wachinje kuku watatu, na kuanza kuwaandaa, huku wewe unaandaa chakula haraka” alisema mzee Jacob, akitoa wazo, ambalo lilipingwa na mke wake………..……..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata