KIAPO CHA MASIKINI (58)

SEHEMU YA 58

ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA SABA: asije kuwa baba yake Peter, ametumia simu nyingine, aliwaza Sada, huku anaitazama ile simu ambayo ilikuwa inaendelea kuita,”wacha niipokee, kama niyeye naikata, alafu naizima kabisa” aliwaza Sada kisha akaipokea, “hallow we Sada, mbona mizigo yenyewe aijafika mpaka saa hizi?” ilikuwa ni sauti ya mama yake ambae alionekana kuwa na Jazba, “we mama mbona msumbufu hivi, sinimekuambia usubiri” alisema Sada, na kutaka kukata simu, “sawa ya nasubiri, aya sasa niambie eti hii simu ni ya baba Michael” aliuliza mama yake, swali ambalo lilimshtua sana…………..Endelea…

Hapo Sada akaona niwazi baba Peter, yani mzee Jacob, ndie atakae kuwa ameeleza habari ya simu hii ya Peter, “nani kakuambia hii simu ni ya Peter?” Sada alijifanya kushangaa, “hii namba ya Peter, hipo kwenye simu ya mama Semeni, anasema hii namba ni ya Peter” kusikia hivyo Sada akakata haraka ile simu, “kum.. make, huyu mama Semeni mshenzi sana, kilicho mchokonoa kuhusu simu nini?” alisema Sada na wakati huo huo simu ikaita tena, akaitazama kwa sekunde kadhaa, akitafuta jibu la kumpatia mama yake, ili kuweka sawa hisia zake, juu ya simu ile, na alipo pata wazo akaipokea, “eti Sada hii namba si ya Peter ya ile simu yake iliyo ibiwa…” safari hii aikuwa sauti ya mama yake, ilikuwa ni sauti ya mama Semeni, hapo Sada akaikata na kuitoa betri kabisa, kisha arushia mezani, “huyu nyoko anakimbele mbele, akafirw…huko” alisema Sada, huku anashika shuka lake na kuendelea kufikicha.****

Naam baada ya mama Semeni kukatiwa simu na Sada, wote watatu walishikwa na mshangao na kuhisi kuwa, kuna mashaka juu ya uwepo wa simu ya Peter mikononi kwa Sada, “mama Kachiki, twende tumalizie kuingiza chakula ndani, ili tuka jiandae” alisema mama Semeni huku anaweka simu yake kibindoni, nakuanza kutembea, kuelekea jungu lilipo, akifwatiwa na mama Kachiki, huku wakimwacha mama Sada akiwa amesimama anajisuta mwenyewe, “kweli sasa nimeumbuka, hivi kwanini Sada angesema kuwa Peter simu ameisahau simu yake pale kwake, alipoondoka bila kuaga” aliwaza mama Sada, humu roho inamuuma sana, “ebu ona wenzetu mtoto wao amewaletea solar kubwa, hakuna kama hiyo hapa kijijini” aliwaza mama Sada, huku ana geuka kutazama kule kwa mzee Jacob, ambako sasa mafundi walikuwa wamesha maliza kufunga zile panel juu ya paa ya nyumba, na sasa wanalizia kufunga taa za nje, “siwezi kuendelea kukaa hapa” aliwaza mama Sada, huku naanza kutembea kuondoka eneo ili.

Lakini anapiga hatua chache kisha anasimama na kuwatazama wakina mama Kachiki, ambao walikuwa wanapotelea ndani, na sufuria kubwa la chakula, alafu akatazama upande wa mbele ambako kulikuwa na pipa la pombe ya komoni, akatabasamu, na kuanza kutembea kurudi alikotoka, akiulenga mlango wa upande jikoni, wa nyumba ya Mangolingoli, akipishana na wakina mama kadhaa waliokuwa wanaenda kujiandaa kwaajili ya kuanza ratiba ya sherehe, wakiwepo wakina mama Semeni na mama Kachiki.**

Tubakie huku huku kijijini, tunaelekea nyumbani kwa mzee Jacob, tuna mwona mzee Nyoni akiwa amekaa kionyonge sana katikati ya kundi la watu ambao walikuwa wajaa kwenye viunga vya nyumba ya mzee Jaacob, wakishuhudia zoezi la ufungaji wa solar, ambalo sasa lilikuwa linaitimishwa, kwa mafundi kuunganisha redio na TV, na baadae kuaga, tayari kwa kuondoka, huku upande wajikoni, mapishi yalikuwa yanaendelea, huku wanawake kadhaa wakijitokeza kusaidia kupika, wakati huo vijana watatu wakimalizia kuandaa bata, na kumuweka jikoni.

“jamani si mngekaa kidogo, msubiri chakula” alisema mama Peter kwa sauti iliyojaa ukarimu, wakati mafundi walipokuwa wanaaga, ili waondoke zao, “asante mama, ila tunatakiwa kuwai mjini, maana kuna oder nyingi sana, ambazo azijafanyiwa kazi, hii yenyewe ilibidi isubiri, sema tume kuja kwa heshima ya Careen” alisema mmoja wawale mafundi, yule alie shika makablasha hapo mwanzo, ambae alionekana kuwa ndie kiongozi wao.

Kwa kauri hiyo iliwafanya mama Peter na baba Peter, waongeze hamu ya kumwona huyo Careen, yani watu watoke mjini, kuja kufunga Solar kijijini, kwa heshima ya mtu mmoja tu, tena ni mwanamke ambae yupo karibu na kijana wao Peter, wakidai ni marafiki, japo huyu fundi alisema wanamwonekano wa kuwa ni wapenzi, “sawa jamani, karibu tena, mkikutananao waambieni tuna wasubiri kwa hamu” alisema mama Peter, ambae aliwapatia zawadi chache za shambam zilizokuwepo pale nyumbani, kama vile mihogo iazi itamu na ndizi, kisha wale maundi wa kampuni ile binafsi ya umeme wa jua, wakaondoka zao, wakiwaacha wenyeji wao wanaendelwea na maandalizi ya kupokea ugeni.
Wakati huo huo baadhi ya watu, ambao hapo mwanzo awakuwepo maeneo yale, waliokuwa wanakuja kwenye sherehe, ambao sasa walikuwa wanakuja kwenye sherehe, ila walipoona kuna mkusanyiko wawatu pale kwa mzee Jacob, walichepuka na kuja kuona kunanini, walicho kutana nacho kiliwafanya wajikute wanakaa pale pale, na kuendelea kushangaa kitu ambacho kilisha pita, maana sasa waliweza kuona mataa makubwa yaliyofungwa nje kila kona ya nyumba ile, huku dish la kampuni flan ya televishen, na kufanya pale kijijini kuwa na TV mbili, moja ikiwa ya kijana mmoja anae tumia kuonyesha mechi za mpira wa miguu na filamu mbali mbali, ambapo ungeingia kwa kiinglio, cha tsh mia tano, kwa mechi au filam moja, na nyingine ya pili ndiyo hii aliyoletewa mzee Jacob, ambae kiukweli licha ya kikabidhiwa remote control, lakini siyo tu kutumia, ila hapo kabla mzee Jacob akuwai kugusa kifaa hiki.

Kama iliyo kawaida watoto walikimbiza gari lililokuwa lina ondoka, uku wakipishana na watu wengine waliokuwa naingia kwa mzee Jacob kushangaa, na kama kawaida ya watu wale waliokuja kuona kinachoendelea, wapo walipo pongeza kutoka moyoni, wapo walipongeza usoni, huku moyoni wakichukia, pia wapo walio ponda wazi wazi, wakidai ni kuchezea fedha, mana solar ndogo kama zao zingetosha kabisa, kuwasha taa, “ebu ona mtu amefunga na kudishi, yani atazame yeye na mkewake tu, si ushamba huo, wenzao wananunua kwaajili ya biashara” hizo ni kauri za watu wenye kijiroho flani cha wivu, na licha ya kuwaza na kuongea yote hayo, lakini vichwani mwao walikuwa wanajiuliza, Peter amewezaje kununua vitu vyote ile, wakati inasemekana kuwa ameibiwa kila kitu, huko mjini, na wazazi wake awakufanikiwa kumwona, “sasa fedha amezipata wapi” ilo swali liliwasumbua vichwa vyao.

Watu walizidi kuongezeka nyumbani kwa mzee Jacob, ijana kwa wazee, watoto ndiyo usiseme, wake kwa waume, pombe zilitolewa nyumbani kwa mzee Mangolingoli, ambako palikuwa na watu wachache sana, na kuletwa nyumbani kwa Jacob, na watu wakaendele kunywa, swala lile liliwashtua na kuwaogopesha mzee Jacob na mke wake, wakichelea mambo mawili, moja ikiwa ni ambao walimwomba kijana mmoja atangaze juu ya uwepo wa sherehe nyumbani kwa mzee Mangolingoli, lakini yangazo lile alikusaidia kitu, ata Mangoli ngoli alipoona juhudi za jilani yake za kuwakumbusha watu juu ya shrehe nyumbani kwake, zikishindikana, akamfwata jilani yake huyo, na kumweleza kuwa, amesha ongea na wausika ambao ni wanachama, watakao enda kupeleka majamanda, kisha wata juwa jinsi ya kuwapatia watu chakula.

Yap! mzee Nyoni, akiwa ametulia anakwenye kundi la watu washangaaji, roho yake ilikuwa ina mchonyota kwa kile alichokuwa anakiona, mbele ya usawa wa macho yake, huku kichwani mwake akiwa amesha poteza kiasi kidogo cha ulevi alicho kunywa kwa Mangolingoli, akiwaza jambo flani, lililo iumiza zaidi roho yake, “kama Peter amefikia kwa Sada, na akuwa na kitu chochote, inamaana ata hivi vitu vyote amenunuliwa na Sada” ndivyo alivyokuwa anaamini mzee Nyoni, ukweli aipaswi kucheka anacho waza mzee Nyoni, “isije kuwa Sada amesema tugawane, alafu huyu mshenzi ameamua kujilimbikizia vyote, mbona ni vitu vingi sana” aliendelea kuwaza mzee Nyoni, huku akimtazama mzee Jacob kwa jicho la hasira, pale anapomwona akiwa katika pilika pilika za maandalizi, ya sehemu ambayo wageni wake wata fikia, yani chini ya mwembe mkubwa pembeni ya nyumba yake, ambapo palikuwa pame weka mikeka minne chini, na viti kazaa na meza ndogo iliyo tandikwa vizuri.

Mzee Nyoni ambae alikuwa anamsubiri kwa hamu mke wake, ili amletee majibu ya simu aliyoenda kupiga, aliendelea kuwaza na kuhisia juu ya kinachoendelea, “nita mbaini tu! wacha nitafute nauri niende mjini, kama akisema mizigo yetu ndiyo hii, basi huyu mshenzi ata nitambua” aliwaza mzee Nyoni na wakati huo hyo akashtuka akiguswa bega, “aya tuondoke tuka tulie nyumbani hapa tufai hapa” ilikuwa ni sauti ya mke wake, yani mama Sada, sambamba na arufu nzuri ya chakula.

Akageuka kumtazama, akamwona mama Sada akiwa amebeba kitu flani cha duara, mfano wa sufuria, kwa kufunga na kanga mgongoni kwake, kama vile amabeba mtoto, “nisaidie ilo moja twende nyumbani” alisema mama Sada, huku akionyesha chini, na mume wake akifwata mkono wa mke wake, akaona madumu mawili, ya pombe aina ya komoni, “hapo umecheza mama sada, ndiomaana nina kukubari” alisema mzee Nyoni, huku anainama na kuchukuwa dumu zote mbili, tofauti na mke wake alivyosema, “tena hapa nimeshabeba chakula kabisaaaa, na minyama kibao” alisema mama Sada kwa sauti ya chini, huku wanatembea kwakujipenyeza penyeza kwenye makundi ya watu, kuondoka eneo lile, huku baadhi ya watu wakiwatazama kwa macho ya kujiuliza, “hivi awa sindio walisema Peter amefikia kwa Sada” akukuwa na mtu wakuwapa jibu.

Lakini kabla mama na baba Sada awajafika mbali, ghafla wakasikia kelele za watu, “gari! gari! gari!” hapo nawao wakageuka kutazama upande wa barabara, na macho yao yaka liona gari dogo zuri, ambalo awakulijuwa jina lake, kama ambavyo mimi na wewe tuna lifahamu kuwa ni Land rover discovery, tena la kisasa, hapo mzee Nyoni na mke wake wakatazamana kwasekunde kadhaa, kabla mzee Nyoni ajaslopoka kwa sauti, “huyooooo ameshafika” unajuwa alimaanisha nini mzee huyu, walimaanisha kuwa ni binti yao Sada, ndie alie kuwa amefika, “ungejuwa ata usingesema, ebu tuone kwanza” alisema mama Sada, huku wakisimama na kutulia kulitazama lile gari, lililokuwa linakuja taratibu, upande huo.

Taratibu mzee Nyoni akaanza kuhisi miguu inakosa nguvu, baada ya kuona lile gari lina kata kona kuja kwa mzee Jacob, “jamani na ili nalo linakuja kwake tena?” aliuliza kwa sauti iliyo jawa na mshangao wa kukata tamaa…..………..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!