
KIAPO CHA MASIKINI (59)

SEHEMU YA 59
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA NANE: Taratibu mzee Nyoni akaanza kuhisi miguu inakosa nguvu, baada ya kuona lile gari lina kata kona kuja kwa mzee Jacob, “jamani na ili nalo linakuja kwake tena?” aliuliza kwa sauti iliyo jawa na mshangao wa kukata tamaa…..………..Endelea…
Huku yeye na mke wake, wana litazama lile gari kwa umakini sana, ilikuweza kuona waliokaa kwenye seat ya mbele, ambapo walifanikiwa kuwaona watu wawili, mabao kwa haraka haraka, awakuweza kuwa tambua.
Siyo mzee Nyoni peke yake alie shangaa juu ya gari lile ni watu wote walilitazama gari, akiwemo mama Peter na mume wake, ambao waliacha shughuri zao, na kulisogelea gari lile lililokuwa linakuja kwa mwendo wa taratibu, huku kila mmoja akiwa na hamu ya kuona wakinani watashuka toka ndani yagari, ilo ambalo kutokana na mwendo wake, ni wazi dereva ana abiria wake, walikuwa wanashangaa kitu flani.****
Yap! OCD mwanauta, akiia nyumbani kwake, hapa kwenye makazi maalumu ya kamanda wa polisi wilaya, amejipumzisha huku anavuta muda, wakwenda kukagua nyumba yake ya kisasa, inayo jengwa kwa msaada wa bwana Kalonga, ambae muda wote amekaa hapa anawaza juu ya kuitajika kwake pale kituoni, jana asubuhi, na baadae kutumwa askari wakamkamate, ukweli swala ilolilimvuruga sana OCD, ambae anatumia nguvu zake zote kumlinda Kalonga, ambae ni mfadhiri wake mkubwa sana, ndie alie mfanikisha kununua gari lake moja aina ya Toyota Raum, na saa anamsaidia kujenga nyumba.
Wakati Mwanauta anawaza hayo, mala akasikia simu yake inaita, akaichukuwa toka mezani na kutazama jina mpigaji, akajikuta anatabsamu mwenyewe, huku anaipokea, “habari za leo kaka, yani nilikuwa nakufikilia sasa hivi” alisalimia Mwanauta kwa sauti ya uchangamfu, “kaka nazani mawazo yetu yalikuwa sawa, maana toka usiku tulipoachana, nikaanza kuwaza juu ya swala la jana, kuitwa na yule bwsana mdogo, na mabaya zaidi nafika pale eti naambiwa niende zangu, unazani kulikuwa na nini pale” huyo alikuwa ni Kalonga.
Ukweli maongezi na swali yao ayakuweza kupata majibu, maana OCD Mwanauta akufanya uchunguzi juu ya swala ilo, “ilo swala inabidi nilifwatilie na kulikomeshe kabisa, maana mpaka sasa ajaniambia chochote” alisema Mwanauta kabla ya kukata simu, wakikubariana wawasiliane mala baada ya kupata jibu.
Naam baada ya kukata simu, hapo hapo Mwanauta akampigia OC CID, ambae akuchelewa kuipokea, “habari za leo afande” alisalimia OC CID, “salama kaka, hivi nasikia jana mlimwita Kalonga, vipi kuna kosa alilifanya?” aliuliza Mwanauta kwa namna ya kawaida kabisa ambayo usingeweza kuzania kuwa kuna jambo anachunguza, “hakuna kosa, ila lilikuwa ni agizo la RCO, ambae baadae akasema tumwachie” alijibu OC CID, na hapo tayari Mwnauta alikuwa amesha pata jibu kilahisi sana, “kwahiyo akusema wanamwitia nini, maana mimi akunieleza chochote?” aliuliza Mwanauta, “kwakweli afande akunieleza chochote, ila nazani kuna tuhuma juu yake na wanajaribu kupata uhakika” alijibu tena OC CID, “ok! basi wakati mwingine naomba unijulishe inapotokea swala kama ilo” alisema Mwanauta, kabla ya kukata simu.
Hapo Mwanauta alitulia kwa dakika akadhaa akijaribu kupambanua majibu ya OC CID, “niwazi kabisa kuna kitu kinaandaliwa juu ya Kalonga, maana RCO, ndie anae chunguza kesi za Kalonga” aliwaza Mwanauta, ambae anafahamu jinsi Kalonga anavyo chunguzwa, na yeye ndie mtu pekee anae msaidia kuondoka na mitego ya polisi, akitumia madaraka ya ukuu wapolisi wilaya, hapa inabidi kifanyike kitu, ili kumwepusha huyu jamaa, na kile kinachopangwa juu yake” aliwaza Kalonga, ambae anajuwa fika kuwa endapo ata luhusu Kalonga akamatwe na ushahidi, kutamwondolea nafasi ya kujipatia fedha, na vitu mbali mbali, zinazo msaidia katika mambo yake mbali mbali, ikiwa na starehe anazo kula yeye na familia yake, “inakuwaje RCO asinijulishe mimi OCD na kwenda kumtuma OC CID?” ilo ndilo swali ambalo lilikosa jibu kwa Mwanauta.
Mwanauta baada ya kuwaza kwa muda kidogo, nakupata wazo la kumshawishi RCO kulegeza upelelezi wake, akampigia simu Kalonga na kumtaka wakutane ili wapange njia sahihi ya kumnyamazisha RCO Mlashani.****
Nikweli, ndani yagari wote wanne, kasoro Michael aliekuwa anafurahi kwa kuona amesha fika kwa babu yake, walikuwa wametoa macho, wanashangaa uwingi wa watu, pale kwa mzee Jacob, lakini ushangaaji wao ulikuwa na mitazamo tofauti, wakati Peter yeye anajiuliza kulikuwa na jambo gani kubwa, lililokusanya watu pale nyumbani kwao, maana kama ni kushangaa gari lile lawafanyakazi wa kampuni ya umeme wajua, ambalo wamepishana mitachache nje ya kijiji, wangekuwa watoto tu sehemu ile, sasa inakuwaje wamekusanyika watu walika lote, kwa jinsia zote.
Careen yaya na wafanyakazi wale wawili, wao walikuwa wanawaza mambo mengine kabisa, yani wao walihisi kuwa mkusanyiko ule ulikuwa ni kwaajiliyao, ni baada ya kusikia kuwa Peter anakuja na mwanamke wake, yani Careen, ambae alisimamisha gari, na kumtazama Peter, “Peter hukuniambia kama kutakuwa na watu wengi hivi” alisema Careen huku ana achia tabasamu pana ambalo, labda Peter na asinge lishangaa, ila yaya Glory na wale wafanya kazi walishangaa, kwa tabasamu lile la Careen, Peter mwenye, alitabasamu bila kusema chochote, wakati huo careen alikuwa anatzama mbele, na kumwona mama Peter, akiwa ameambatana na wanawake akadhaa wanasogelea gari, “Peter huyu wambele ni mama yake Hen, naona mmefanana sana” alisema Careen ambae alikuwa amepatia kwa kumwonyesha mama Peter, “ndiyo yeye” alisema Peter, huku anajiandaa kufungua mlango, tayari kutoka nje ya gari, “Careen kumbuka” alisema yaya Glory, wakati Careen nae anatoa mkanda wa kiti (seat belt) tayari kushuka toka kwenye gari.****
Emma alijiinua kitandani, akiwa mwenye njaa kali sana, huku kichwa chake kikiwa akieleweki kwa mning’inio (hang over), mdomo wake ukiwa unatamani supu ya yenye pili pili nyingi na limao nyingi sana, ila kwa upande wa afya yake alikuwa amesha pata unafuu kwa kiasi kikubwa sana, ata maumivu alikuwa anayasikia kwambali sana, ni mpaka ayajiguse sehemu usika.
Ile anatazama vyema anamwona Queen amekaa kwenye kingo ya kitanda, akionekana mweka mawazo mengi sana, “we vipi mbona kama unamawazo mengi” aliuliza Emma Pengo, huku anainuka na kujitazama eneo la kinena ambalo lilikuwa na uchafu mwingi wa kinyesi, “walaaaa mimi nawaza namna ya kwenda gengeni kununua vitafunwa” alisema Sada, ambae mjini wanamwita Queen huku nayeye anainuka na kumpatia ndoo yenye maji mpenzi wake, “kuna ela humo kwenye suruali, kachukue supu” alisema Emma ambae sasa alikuwa anaandaa sabuni na mswaki.
Baada ya kumaliza kuandalia mswaki na sabuni tayari kuelekea bafuni, Emma akakumbuka jambo, ni baada ya kuiona simu ikiwa imetenganishwa na betrie yake, “hivi nani alikupigia simu wakati ule?” aliuliza Emma, “mama alipiga, amesema anasikia kuwa Peter leo anaenda kijijini” alisema Sada kama ambae akutaka kuzungumzia swala lile, “inamaana sikuzote hizi alikuwepo hapa mjini?” aliulzia Peter kwa mshangao, huku anweka vitu vyake chini na kuchukuwa simu yake, kwa lengo la kumpigia boss wake, akiwa na lengo la kumjulisha kuwa Peter amesha enda kijiji kwao.***
Naam sasa huku kijijini, ebu tutumie macho ya mama baba Sada, kungalia tukio la kukaribisha wageni, baba na mama Sada, ambao walikuwa wamesimama wanalitazama gari, huku mzee Nyoni ameshikilia dumu mbili za pombe, na mke wake alie kuwsa amebeba sufuria dogo la wali mgongoni mwake, waliweza kuona milango ya gari inafunguliwa, wakashuka watu kadhaa, ambao baadae walifahamu kuwa idaidi yao walikuwa ni sita, walio valia vizuri na kupendeza, lakini awakumtambua ata mmoja, siyo wale wanawake wala yule kijana na mtoto, alie wavutia zaidi ni mwanamke mzuri kuliko uzuri wenyewe, alie shuka upande wa kulia wa gari seat za mbele.
“ebwana eeee, zinga la demu, amekuja kufanya nini huku” ilisikika sauti ya kijana mmoja aliekuwa amesimama jilani na wazee awa, yani mama na baba Sada, huku wakimtazama Careen alie kuwa anashuka toka kwenye gari, upande waliokuwapo wao, yani upande wa kulia seat ya mbele, ambayo ndiyo seat ya dereva.
Nazani akuna aja ya kuelezea uvaaji na mwonekano wa mschana huyu, maana kwa sasa sisi wote tunaufahamu, sasa vuta picha jinsi wakina mzee Nyoni walivyo mwona akishuka toka kwenye gari, sambamba na wafanyakazi wake mmoja akiwa ameshika Michael, na mmoja alie kuwa na yaya Glory, wakimfwata Careen, aalie kuwa anazunguka gari, wakimfwata Peter, alie kuwa anasalimiana na mama yake, ambae pia anaonekana kutoa macho kwa mshangao pale anapo mwona Careen.
Siyo kwamba anamfahamu, hapana ila ukweli nikwamba Careen ni mzuri jamani, yani licha kuwepo kwa wageni watatu wakike, lakini yeye na wenzake walimtazama Caree, ambae uzuri wake usingeweza kutumia kurasa moja kuuelezea, pengine nusu ya hadithi jii ingetumika kuelezea uzuri wake, kiasi cha kwamba, siyo mama Peter peke yake ata baba Peter, mzee Nyoni na mke wake, na watu wote waliokuwepo pale awakufikilia kama Peter ana weza kuwa anafahamiana na mwanamke huyu ambae licha ya uzuri wake, anaonekana wazi kuwa ni tajiri, pia ata wale waschana wawili, ukiacha yaya Glory, ambae ni mtu mzima, akuna ata mmoja mwenye ambae Peter anaweza kuwa na uwezo wakuwa nae. …..………..l

