
SEHEMU YA 60
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TISA: Siyo kwamba anamfahamu, hapana ila ukweli nikwamba Careen ni mzuri jamani, yani licha kuwepo kwa wageni watatu wakike, lakini yeye na wenzake walimtazama Caree, ambae uzuri wake usingeweza kutumia kurasa moja kuuelezea, pengine nusu ya hadithi jii ingetumika kuelezea uzuri wake, kiasi cha kwamba, siyo mama Peter peke yake ata baba Peter, mzee Nyoni na mke wake, na watu wote waliokuwepo pale awakufikilia kama Peter ana weza kuwa anafahamiana na mwanamke huyu ambae licha ya uzuri wake, anaonekana wazi kuwa ni tajiri, pia ata wale waschana wawili, ukiacha yaya Glory, ambae ni mtu mzima, akuna ata mmoja mwenye ambae Peter anaweza kuwa na uwezo wakuwa nae. …..………..Endelea…
Lakini kabla ajapata jibu, anashangaa kumwona yule mwanamke mrembo sana, akija mbele yake kwa heshima na adabu, huku suo wake ukionyesha utulivu na nidhamu iliyochanganyika na uoga flani, hapo mama Peter akajuwa kinacho fwata ni kupeana mikono, lakini akashangaa kuona yule mschana mrembo sana, na wale wengine, wakiiinamisha vichwa vyao kwanidhamu ya hali ya juu, huku wakiweka mikono yake kifuani, salaaam mama mpendwa, mzazi wa mchumba wangu” ilikuwa ni sauti tulivu na iliyo jaa unyenyekevu mkubwa, ya mwana dada Careen.
Siyo mama Peter peke yake alie shangaa, ni watu wote, waliokuwepo pale, kuanzia baba Peter ya ni mzee Jacob, na wengine wote wakubwa kwa wadogo, wake kwa waume, na mzee Nyoni na mke wake, “ina maanisha nini, hiii?” aliuliza mama Sada kwa sauti ya mshangao, huku amekodoa macho kwa mshangai wa hali ya juu, “yani huyo unae mwona, ni mwanamke ni mchumba wa Peter” alijibu mwanamke mmoja alie kuwa amesimama karibu, “mh!” mama Sada yani mke wa mzee Nyoni aliishia kuguna tu, na kuendelea kukodoa macho, kushuhudia tukio lile la kukaribishaji.
Ambapo sasa walionekana wale wanawake wanne, walioinamisha ichwa chini mbele ya mama Peter, wakiwa wametulia mbele yake, huku mama Peter akimtazama Peter kwa shamshangao, ni kama alikuwa anauliza afanyaje, kufwatia ile salam, Peter akaomwonyesha ishala mama yake kwa namna ya kuitikia, “salaam wageni wangu wapendwa, karibuni sana” alisema mama Peter, kwa sauti ya ukarimu, nao wakainua vichwa vyao, na Careen akamtazama Peter ambae sasa alikuwa na Michael kisha akamshika mkono, na Peter akaanza kuelekea chini ya mti wa muembe ambao ulionekana wazi kuwa umeandaliwa kwaajili yao.
Kila mmoja alimshuhudia Peter, akiwa amemshika mkono Careen na kuanza kutembea taratibu kuelekea chini ya muembe, huku Peter akimwona baba, amesimama mita kadhaa mbele yake, anamsubiri, huku tabasamu lime tawara usoni mwake, nikama macho yake yalikuwa yanasema, umenitoa aibu kijana wangu, wakati huo tayari mtoto Michael alisha chomoka mbio kumfwata babu yake mzee Jacob,
Huku Careen ambae akuwa na wazo kuwa alie simama mbele yao ni baba mkwe, alikuwa anapagawa na shangwe na vigeregere, za watu waliokuwa wamesimama pande zote mbili, yani kushoto na kulia, wakishangilia ujio wa kijana mwenzao alie semekana kuwa ametapanya mali za makahaba huko mjini, uzalendo unamshinda Careen na yeye anawapungia mkono, wanakijiji awa, ambao anaamini walikuwepo pale kwaajili ya kumpoea yeye, na mpenzi wake Peter, ila kusema ukweli nikwamba, chanzo cha ujio wawatu wale ni sherehe ya Mangolingoli, waka vutiwa na gari la Solar, na mwisho wakajikuta wamanshangalia mwana dada mrembo ambae amekuja na Peter, ambae ndie yeye Careen mama wa dhahabu.
Kitu kilicho mfurahaisha Careen nikitendo cha wanakiji nao kupunga mkono kwanguvu, sambamba na shangwendermo na vifijo, pale walipoona yeye amewapungia, siyo yeye peke yake ata yaya Glory na wale wafanyakazi nao walishangazwa na tukio lile, ambalo waliamua kuchukuwa picha kwa mtindo wa video, wakitumia simu zao.****
Naam swala la jana la RCO, kumtumia OC CID kumwita Pitus Kalonga kituoni, lilimuumiza sana kichwa, OCD Alphonce Mwanauta, “inamaana RCO anaamua kufanya mambo kimya kimya bila kunijulisha sasa, au ameshtuka kuwa nausika?” alijiuliza yeye mwenyewe bwana Mwanauta, ambae mida hii alikuwa njiani anaelekea Mateka nyumbani kwa Kalonga ambako walipanga wakaonane, “hapana inabidi kumzima mala moja, tena siyo kwa njia ya kubembeleza, maana yule awezi kuchukua chochote juu ya ili” aliwaza Mwanauta, ambae anajuwa fika kuwa Mlashani, ni afisa mtihifu na mwaminifu wa ngazi zajuu wa jeshi la polisi, ambae kuchukuwa rushwa kwake ni mwiko, na isitoshe uwa ajawai kushindwa kukamilisha kazi alivyo tumwa na jeshi la polisi, tofauti na wale wakina Kiangarame, Kidubo na wengine wakina Kachinga, “sijuwi huyu IGP anawezaje kuleta mijitu kama hii huku, nakuacha kuwaleta wenye shida na fedha” aliwaza Mwanauta ambae sasa alikuwa anaimamisha gari nje ya nyumba ya Kalonga na kushuka toka kwenye gari, akikaribishwa na Kalonga mwenyewe.
Moja kwa moja wakaelekea kwenye chumba cha siri, ambacho Kalonga utumia kwa maongezi na wageni kama awa, wanao zungumzia biashara zake haramu, “kaka huu mchezo, nimeutilia mashaka makubwa sana, na inabidi tuupatie ufumbuzi wa haraka sana” alisema Mwanauta, huku wanapata grass ya pombe kali, kama ilivyokawaida yao, kila wanapokutana, “vipi kama nikimtafuta na kumpatia chochote, au ukienda wewe ukamshawishi?” aliuliza Kalonga, ambae kiukweli fedha imemsaidia mpaka leo ajaingia ndani ya kuta nene za gereza, “mh! tena ilo usjaribu kabsa, bora angekuwa ajakabidhiwa ili jukumu, lakini kwasasa hii kesi hipo mikononi mwake, uwa akubari kuaribu sifa yake” alisema Mwanauta kwa msisitizo.
Naam wawili awa wakatulia kwa sekunde kadhaa, wakijaribu kuwaza ili na lile, kuona watafanyaje ili kumtuliaza Mlashani, kabla Mwanauta ajaibuka na wazo flani, “sikia Kalonga, akuna mtu anaweza kuitanguliza serikali kuliko familia yake, huyu inabidi tumpe onyo kupitia mjukuu wake, wakike, anampenda sana, awezi kuendelea kuwa na kiburi kama tukifanya hivyo” alisema Mwanauta, “tutaafanyaje kaka ebu nifafanulie, “sikia fanya juu chini, kuanzia leo, mpaka juma tatu, uwe umesha mteka huyo mjukuu wake, na njia ya kumteka ifanywe kama imefanywa na watekaji Professinonal, kumfanya yeye ajuwe kuwa ana cheza na watu hatari, alafu baada ya hapo, ata pigiwa simu kupewa honyo kali, ikiwa simu ya mwisho kati ya tatu, ambazo atapigiwa siku ya mpango, alafu simu inazimwa na mtoto anaachiwa, mpaka hapo atakuwa amesha jifunza jambo, ata ukimshawishi kupokea fedha azidi kulegea itawezekana” alisema Mwanauta na Kalonga akakubariana nae moja kwa moja juu ya mpango huo.
Baada ya hapo wakaanza kupanga mipango juu ya utekelezaji, huku Mwanauta akiaidi kuweka mtu wakaribu ambae ata kuwa anafwatilia kwa karibu mwenendo wa RCO, wakati wote wa tukio, “wacha niwasiliane na Emma tupate kijana wa kufwatilia ratiba ya familia, ili tujuwe tuna mnasa vipi?” alisema Kalonga, wazo ambalo lilipingwa na Mwanauta, “hapana hiyo kazi niachie mimi, nitajuwa nifanya nini, wewe andaa vijana wako watakae mteka” alisema Mwanauta ambae alikuwa na uhakika wa kupata ratiba ya RCO na familia yake kwa kutumia Dereva wake, ambae angemwuliza kiujanja. “vipi kuhusu yule kijana alie haribu mpango wako, umesha juwa anapatikana wap?” aliuliza Mwanauta, na kuwa kama amemkumbusha Kalonga, “hooo inabidi niwasiliane na Emma nijuwe amefikia wapi” alisema Kalonga, ambae alipokamata simu yake, akaona ilikuwa inaita kimya kimya, maana alikuwa ameondoa sauti, tena huyooo anapiga” alisema Kalonga huku anatabasamu.***
Yap! tayari mzee Jacob alisha salimia na Careen mkwe wake, kwa mtindo ule ule wa heshima na tahadhima, ukiwa ni utaratibu wa wamanchi wa #mbpgp_land, huku akishangaa mabadriko ya kijana wake, na mjukuu wake, ambao kiukweli walionekana kama wamezaliwa mjini, na wamekulia mjini, tayari mizigo ilisha shushwa toka kwenye gari, na vijana ambao walikuwa wanasaidia kuandaa bata pale kwa mzee Jacob, na sasa wageni wote watano, yani Careen Peter Michael na wale wakina yaya Glory, walikuwa wamekaa kwenye sehemu waliyokuwa wameandaliwa, yani pale chini ya mti wa muembe, pamoja na mzee Jacob, na bahadhi ya wazee walio kuja muda mfupi uliopita, yani Ngongi na Njogopa.
Japo mwanzo wale waschana wawili na yaya Glory, walitaka kujitenga kuwaachia Careen na Peter ile sehemu, ili wao wausike kwenye kuwahudumia, lakini Peter alizuwia na kumweleza Careen kuwa kila kitu mama yake ata simamia, na kwamba wote wanatakiwa kuwa kama wageni, na wakae pale ambapo baadhi ya watu walikuwa wamesimama pembeni yao wakiwazunguka, kwa kuwashangaa, kiasi cha kumuwia vigumu mama Peter na wanawake wengine kuandaa chakula.
Ulifanyika utambulisho lathmi kwa wazazi wa wote waliokuwepo jilani, Peter alieleza uhusiano wake na Careen, na kuaidi kuwa watatoa taarifa zaidi, pale watakapo itaji kukamilisha taratibu za uchumba na ndoa.
Ilikuwa ni furaha na furaja kubwa moyoni mwa Careen, kuona watu wengi wakiupokea ujio wao, ni wazi walikuwa wameukubari uhusiano wao, na kuubariki, “peter kuna naona watu wanakunywa local beer pekee, vipi kwa awa wasio kunywa pombe wameandaliwa nini?” aliuliza Careen kwa sauti ya chini, huku wakipata soda ambazo waliletewa baada ya kutaja vinywaji wanavyo tumia, “mh! sidhani kama wamwefanya hivyo maana huku soda ni gharama kuliko hizo pombe” alisema Peter, na na hapo Careen akuona kama ni jambo jema kuwaacha wana kijiji wengine bila vinywaji, hapo akatoa fedha ikanunuliewe vinywaji vya aina zote, kuanzia soda juice na bia.
Walijitokeza vijana ambao walienda kukusanya inywaji vyote, kwenye maduka ya pale kijijini, na kuleta eneo la tukio, ambapo sasa vyakula vya kwenye sherehe ya mzee Mangolingoli, vilisha letwa kwa wale watu waliokuwa wamejaa pale kwa mzee Jacob, na kuanza kula huku wakigaiwa vinywaji, “baba tumejalibu sana kukupigia simu, lakini upatikani, simu yako inatatizo?” aliuliza Peter, na mzee Jacob ya ni baba yake, aieleza jinsi mke wake alivyo itumbukiza simu kwenye maji, kwa bahati mbaya, “basi kesho jumapili, wakati tunaenda kutembea, tutapitia kununua simu, kwaajili ya baba na mama” alisema Careen.
Na hapo aliwafanya wazee awa wawili, yani baba na mama Peter, waonyeshe meno yote therasini na mbili, ya mtu mzima, kwa vicheko vya furaha, walivyokuwa nayo, “asante mama ubarikiwe sana” walijibu wazazi awa, huku wazee wanzao wakina Ngongi, waliokuwa wanajinywea bia taratibu, wakishuhudia na kusikiliza, huku wazee wangine, wake kwa waume, nao wakijiongeza na kujipa umuhimu, kwa kujifanya ni watu wakaribu wa familia hii, na kuja kukaa pale chini ya muembe, kwa wageni, “yani Peter unaenda mjini bila kuja kuniaga baba yako?” ungemsikia mmoja akisema hivyo, mala tu baada ya kufika pale, “yani we mtoto umenikosea sana, kwanini hukusema kama utakuja na mkwe, niwaandaie zawadi kudogo” ungemsia mama flani angesema hivyo japo yeye ni mmoja kati ya watu ambao mama Peter aliwaona wakimsimanga pale kwa Mangolingoli…..………..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU