KIAPO CHA MASIKINI (61)

SEHEMU YA 61

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI: wake kwa waume, nao wakijiongeza na kujipa umuhimu, kwa kujifanya ni watu wakaribu wa familia hii, na kuja kukaa pale chini ya muembe, kwa wageni, “yani Peter unaenda mjini bila kuja kuniaga baba yako?” ungemsikia mmoja akisema hivyo, mala tu baada ya kufika pale, “yani we mtoto umenikosea sana, kwanini hukusema kama utakuja na mkwe, niwaandaie zawadi kudogo” ungemsia mama flani angesema hivyo japo yeye ni mmoja kati ya watu ambao mama Peter aliwaona wakimsimanga pale kwa Mangolingoli…..………..Endelea…
Mida hiyo, ndio wakati ambae mzee Nyoni na mke wake walipoamua kuondoka zao, wakiwa tayari wamesha pata mgao wa vinywaji vyao, yani juice na soda ya take away, ambazo walizipokea basipo kujari wanacho kisikia mioyoni mwao, maana mioyo yao ilikuwa ina wauma sana, kwa kile wanacho kishuhudia kwenye familia hii yam zee Jacob, kuanzia kijana Peter na mjukuu wao kuja wakiwa wamenawili, na kupendeza kwa sura na nguo zao, pia mwanamke ambae inasemkana kuwa ni mchumba wa Peter.

Ukweli baba na mama Peter, walikuwa na hamu ya kusukiliza kilichotokea kati yake na Sada, na yeye akiwa analijuwa ilo, na kwakuwa tayari watu walikuwa busy na vyakula na vinywaji, nae akatumia nafasi hiyo kuwa eleza kilicho tokea.***

Naam sasa Emma, alikuwa ameshaoga, anajiandaa kutoka kwenda kuweka sawa mipango ya kazi, na sasa aikuwa anamsubiri Janja, aje amchukue maana gari alikuwa nalo yeye, tayari kijana huyu, ambae makovu usoni mwake yalikuwa yanaonekana, alikuwa amesha maliza kuongeea na boss wake Kalonga, akimwelezea kuhusu Peter, kwamba leo ameenda kijijini, huku wakijuwa ndio ameenda moja kwa moja, sababu huko ndiko makazi yake, na huku mjini alikuja mala moja kwaajili ya kununua vifaa vya ujenzi, hivyo asingeweza tena kuzuwia wala kuinglia mipango ya juu ya mwana dada Careen, ambayo OCD Mwanauta alikuwa ameipa kibari cha kutendeka.

Kalonga nae alimweleza Emma, juu ya mpango mpya wakumteka mjukuu wa RCO Mlashani, “kuanzia sasa andaa vijana watatu, ambao wata mteka huyo mtoto, wakae tayari, ilinikikupa taarifa tu, unahakikisha unwapata mala moja na wanaenda eneo la tukio, hakikisha unakuwa karibu na awatumii gari linalofahamika, nita toa gari moja, tutabadiri namba za gari, watakalo tumia” alielekeza Kalinga na ndiyo sababu sasa Emma anajiandaa kutoka, kwenda kuandaa watu ambao wata tumika kwenye mpango huo.**

Peter akiwa pale chini ya mti, pamoja na Careen na wazazi wake, wakina mzee Ngongi, watu wengine wote, waliokuwepo pale chini ya mtia, alieleza kilakitu kilichotokea kati yake na Sada, kuanzia walivyo wasilina akiwa kijijini, Sada akijifanya kuwa amebadirika na anaitaji kuishi nae, walee mtoto.

Peter alieleza jinsi Sada alivyo wakuta pale mti pub, na kumpeleka kwenye hotel ya kifahali yemye gharama kubwa, kisha kuwatelekeza akiwaibia kila kitu, na yeye kunusurika kupelekwa kituo cha polisi, bada ya kusaidiwa na Careen, ambae jana usiku alikutana nae kwa mala ya pili.

Peter aliendelea kueleza jinsi alivyo kutana na tena na Sada, akiwa amepondeka usoni, na kujaribu kuzungumza nae swala la kurudi kijijini wakaanze maisha mapya, na majibu ya sada ambayo yalimsikitisha kila mtu, kama vile kusema akuwa na mtoto, kama Michael, na pia kutoa kiapo cha kwamba, awezi kurudiana na Peter, itakuwa bora akilala na mbwa, kuliko kufanya hivyo, na endapo ata kiuka na kufanya hivyo, bai ageuke kuwa kichaa.

Hakika habari ile ilimsikitisha kila mmoja, alie kuwepo maali pale, “vipi kuhusu maisha yake, ni kweli ana ghorofa huko mjini” aliuliza mzee Ngongi, “ukweli sijuwi maisha yake yalivyo huko mjini, maa nilikuutana nae pale pele njiani na kuachana nae hapo hapo” alijibu Peter, wakati akiwa amesha itimisha simulizi ile ya kuudhunisha.***

Ebu tuangazie nyumbani kwa mzee Nyoni, ambako yeye na mke wake walikuwa wamesha maliza kula wali, waliouchukuwa kwa mzee Mangolingoli, na sasa walikuwa wanakunywa pombe yao taratibu, huku wanatafakari kilicho tokea leo nyumbani kwa mzee Jacob, na kujiona kama wameumbuka sana, “kama Peter ameenda jana tu na leo amerudi akiwa hivi, basi Sada ambae ameenda muda mrefu, lazima ayakuwa tajiri, sana” alisema mama Sada, ambae mpaka sasa kinywa kilishaanza kumlewesha, kama ilivyo kwa mume wake,

“lakini kwanini yeye atutembelei wakati wenzake tuna waona kila siku wanakuja na kuwatumia fedha wazazi wao?” aliuliza mzee Jacob, ambae kwa haraka haraka, alisha aanza kutilia mashaka maisha ya binti yao huko mjini, “wala hatupaswi kumshutumu mtoto, cha msingi hapo tutafute nauri twende mjini, atuwezi kukosa wakumkopa” alisema mama Sada, ambae alimini kuwa mjini wata pata fedha nyingi kwa binti yao, ambazo watatumia kama nauri ya kurudia kijijini na ile ya kulipa deni ambalo watakuwa wameliacha kijijini, “tena tutakuja na vitu kibao, siumeona mzee Jacob, anavyo jidai” alisema mzee Nyoni, na hapo mke wake akakunja mdomo kwa chuki, ni baada ya kusikia jina la mzee Jacob,

“wameniuzi wanavyo jishaua, sasa kwataarifa yao nikirudi watajificha chooni, nitakusanya kijiji chote, alafu mwanamke mwenyewe amfikii sada ata kidogo wakauzuri” alisema mama Sada, ilibakia kidogo mzee Nyoni acheke kwa maneno ya mke wake, kumfananisha Sada na Careen, “ebutunywe zetu pombe kisha tukatafute wa kukopa ela kesho twende zetu mjini” alisema mzee Nyoni.****

Yap! saa kumi na moja za jioni, ndio mida ambayo wakina Peter waliondoka kijijini, wakiwa wamesha zunguka baadhi ya maeneo, pale kijijini, ikiwa ni pamoja na kwenda nyumbani kwa Peter, ambako Careen alisema kuna aja ya kujenga nyumba kubwa, ambayo watakuwa wanafikia kipindi wanakuja kutazama mashamba na kuamua kulala.

Waliondoka huku kila mmoja akiwa amefurahi sana, kuanzia Careen na wafanyakazi wake, ambao ndio walikuwa wageni, wao walifurahi na kwa mapokezi waliyoyapata, japo ni kijijini kwenye mazingira ya umasikini, lakini walionyeshwa ukarimu wa hali ya juu, asa uwingi wawatu waliowakuta ndio ulio wafurahisha zaidi, pia Peter na Michael, nao walifurahi sana, kila mmoja kwa sababu zake, wakati Peter akifurahi kwa jinsi mpenzi wake alivyo pokelewa na wazazi wake, na majilani, pia alifurahi kumwona mpenzi wake amefurahi pia.

wengine ni wazazi wa Peter, ambao walifurahi kuona kijana wao amempata mwanamke wa maisha yake, achana na utajiri aliokuwa nao Careen, pia uzuri na tabia njema na nidhamu ya hali ya juu ya mwanamke yule, na pia walifurahi kuona Peter, ameshajitoa kwenye mikono hatari ya Sada, mwanamke ambae amebadirika na kuwa hatari sana, mwizi mlaghai na mwongo, mwanamke ambae kijana wao Peter, alikuwa amempenda kwa moyo wake wote.

kundi jingine ni majilani na wana kijiji, ambao walitamani Peter asiondoke pale kijijini, nawao waendelee kufaidi soda na kumwona mwanamke huyu mzuri, ambae pale kijijini awajawai kumwona kwa macho, ukiachana na wale ambao waliwai kumwona mjini, kwenye maduka yake, hakika Careen aliacha gumzo pale kijijini.

Safati yao ilikuwa ni nzuri yenye furaha, kiasi cha kuiona fupi, tofauti na wakati walipokuwa wanakuja, kwa jinsi walivyo kuwa wanaongea na kucheka, wakikumbushana kuhusu mapokezi, ukweli Careen alionekana kujiachia kwa vicheko na maongezi, kiasi cha kumshanga yaya Glory na wafanyakazi wale wawili, ambao awakui kumwona Careen akiwa vile, yaya Glory alichukuwa video ya siri, na kuituma kwa mama yake Careen, yani waziri wa jinsia mama na watoto wa #mbogo_land, ambae ata kabla awajafika mjini tayari alisha piga simu.

Careen aliipokea na kuongea na mama yake huku akishindwa kufika furaha yake, “unaonekana mwenye furaha sana Careen ni mwaka watatu sasa sijawai kukuona ukiwa hivyo” alisema mama Careen, ambae aliomba mkwe wake apelekwe #Mbogo_land akasalimie na kujitambulisha, “usijari mama, juma tatu nita shughurikia vibari vya kusafiria, vya Peter na Michael, baada ya hapo jumanne tuta kuja huko” alisema Careen jambo ambalo mama yake akukubariana nalo, “hakuna aja ya kusubiri jumatatu, nitaongea na ubarozini, kesho mchana huyo Peter na Michael aende akafanya taratibu, za kupata vibari vya kuingia nchini” alisema mama yake Careen ambae alionekana kuwa na hamu ya kumwona mkwe wake.

“sawa mama nitafanya hivyo lakini itakuwa ni jumatatu, kesho nisiku ya kupumzika nyumbani” alisema Careen na mama yake akamuelewa, “ok! fanya hivyo mwanangu, nimeona ulivyo ufurahi, ni miaka mingi sana tka nikuone mwenye furaha kama hiyo, umepokelewa vizuri sana na wakwe zako huko kijijini, nao wamefurahi sana” alisema mama yake Careen, ambae pia alisisitiza jambo, ambalo lilimfanya Careen amtazame Peter, huku anatabasamu kwa aibu, “mwanangu, lakini hakikisha amfanyi chochote kabla ya ndoa, sawa mama” ………..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!