KIAPO CHA MASIKINI (62)

SEHEMU YA 62

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA MOJA: “sawa mama nitafanya hivyo lakini itakuwa ni jumatatu, kesho nisiku ya kupumzika nyumbani” alisema Careen na mama yake akamuelewa, “ok! fanya hivyo mwanangu, nimeona ulivyo ufurahi, ni miaka mingi sana tka nikuone mwenye furaha kama hiyo, umepokelewa vizuri sana na wakwe zako huko kijijini, nao wamefurahi sana” alisema mama yake Careen, ambae pia alisisitiza jambo, ambalo lilimfanya Careen amtazame Peter, huku anatabasamu kwa aibu, “mwanangu, lakini hakikisha amfanyi chochote kabla ya ndoa, sawa mama” ………..Endelea…

Ukweli mama Careen alikuwa amechelewa, maana tayari Careen alikuwa amesha onja dudu, “aya mama tutaongea baadae sasa hivi naendesha gari” alisema Careen na kukata simu, kisha kuongeza mwendo wagari kwa kukanyaga mafuta zaidi, kuelekea mjini, kichwani mwake akipanga kusherehekea jinsi alivyo pokelewa na wakwe zake.**

Wakati wakina Peter wapo njiani wamejwa na furaha, Sada alikuwa alikuwa anamalizia kujiandaa kwaajili ya kwenda kwa Kadara, ebu nikudokeze kidogo, kisa cha Sada kwenda kwa kadara jioni hii ya saa kumi na mbili kasoro.

Ilikuwa hivi, toka Emma alipoondoka asubuhi kwenda kufanya mipango ya kutafuta vijana watako usika na zoezi la kumteka mtoto wa RCO Mlashani, akurudi mpaka mida hii, na mbaya zaidi akuacha fedha yoyote, maana awakuwa na fedha ya kutosha, iliyobakia walinunua supu asubuhi, njaa ilikuwa ina mchamanda mwanadada, ndani akukuwa na ata chembe ya kitu kinachoweza kuliwa, zaidi ya kinywaji ambacho ni maji pekee, nayo alisha yanywa na kumsabishia safari za chooni mala kwa mala

hakuwa na uwezo wa kuwasiliana na Emma pengine ange mweleza maali alipo na yeye angeenda japo kupata chakula au fedha za kununulia chakula, sababu akuikalili namba yak e ya simu, maana ata angeiwasha simu ya Peter, asingeitapata namba ya Emma, na alipo muwazia rafiki yake Rose, lakini aliamini ingekuwa vigumu kumpata kwa sasa, maana lazima mida hii, atakuwa amesha ingia mtaani kusaka wanaume wakumpatia fedha, maana mwenzie bado alikuwa anaendelea na biashara hiyo, ambayo yeye alisha isahau, mala baada ya kuanza kuishi na Emma.

Baada ya kuwaza kwa muda mrefu, akamkumbuka Kadara, ambae anaweza kumpata kilahisi, pale dukani kwake, hiyo akaingia ndani haraka na kuanza kujiandaa, ambapo alitumia dakika chache sana, na kuanza safari, kuelekea majengo, akitumia njia za mkato, ambazo aliamini zingemfikisha haraka sana.***

Naam saa kumi na mbili za jioni, ilimkuta Emma akiwa eneo la manzese nyuma ya soko la wakulima, ambapo palikuwa na jengo moja kubwa chakavu, kulikuwa na vijana kadhaa waliokuwa katika mikao mbali mbali, wapo waliokuwa wameshika misokoto ya bangi, wapo waliokuwa wanajichoma sindano mwenye mishipa yao ya mikono na kuminya dawa zilizo kuwa kwenye bomba maalimu za sindano tiba, wapo waliokuwa wamesinzia huku mate yanawatoka midomoni, wapo pua waliokuwa wanaongea maongezi yao ya kawaida.

Emma yeye alikuwa amesha vuta sokonto, na kumkabidhi Janja, ambae pia alivuta kwa mikupuo miwili, isha akampatia kijana mwingine mwenye mwili mkubwa uliojengeka kimazoezi, ambae walikuwa wamekaa nae karibu, pamoja na mwingine, ambae anatimiza idadi ya kuwa walikaa wanne, “kwahiyo bro hiyo kazi inafanyika lini?” aliuliza yule alie pewa msokoto, huku anamkabidhi yule kijana wanne, “sikia Dullah, kwanza sitaki mapepe kwenye hii kazi, na mkifanikisha mnakula fedha nefu sana, cha msingi hapa tudusubiri taarifa toka kwa boss, tujuwe kazi inafanyika lini na wapi?” alisema Emma, huku anapewa tena sigara bwege toka kwa yule wanne, “kwahiyo tutakuwa mimi na Seba tu?” aliuliza Dullah, “mimi na Janja tutakuwepo, lakini atuto fanya chochote, nyie mtakuwa na gari lenu” alisema Emma na wakati huo huo simu yake ikaanza kuita.

Emma aatembeza ile sigara yenye majina mengi, kisha akaingiza mkono mfukoni, na kuitoa simu yake, akatazama jina la mpigaji, “boss huyo” alisema Emma huku anaipokea simu, “shikamoo boss” alisalimia Emma, na kuanza kuongea na boss wake, huku wenzake wakiwa awasikii kinachosemwa na upande wapili, “nimesha wapata boss….. nawaamini sana… ni Dullah, na Seba… ndiyo niwale ambao tuliwatumia kusafirisha mzigo wa mwisho… sawa …. sawa boss.. ndiyo… kwahiyo nitawafatilia toka wakiwa kanisani boss” alisikika Emma akiongea na mwisho akaagana na boss wake na kukata simu.

baada ya hapo akamtazama janja, “kaka tayari mchongo ni kesho, unaanza mida ya asubuhi, boss amepewa tarifa kuwa mke wa RCO anampango wakwenda NPF kwenye bembea za watoto, kumpeleka mjukuu wake, atatumia gari la binafsi, sasa hapo NPF ndiyo sehemu ya kwenda kumteka huyo mtoto, na yasifanyike makosa yoyote” alisema Emma, kwa sauti yenye msisitizo.
Naam baada ya kukamilisha mipango yao, Emma na Janja, wakatoka pale Manzese na kuelekea Mateka kwa boss wao Kalonga, kupeleka fedha za makusanyo, kisha wangeenda Msogeze Pub, kupata bia kadhaa, kwa fedha ambazo wao walikuwa wame zichota kwenye fedha za makusanyo, ya mauzo ya dawa za kulevya na bangi.***

Kijijini Mwanamonga, mambo yalikuwa bam bam, nikama kijiji kiliamia kwenye eneo la mbele la nyumba ya mzee Jacob, ambako sasa watu wengi walikuwa wameja, ni wakubwa wadogo, wake kwa waume watoto vijana mwaschana wavulani wababa wamama, ata watoto na wazee, pombe zilinyweka, kwa wingi, na leo akukuwa na kelele za music, kama sikunyingine inavyokuwaga, watu walikuwa wamekaa kwa utulivu, wanatazama TV ya nchi alobaini na mbili, iliyowekwa juu ya meza kubwa mbele ya kibaraza cha nyumba hii ya mzee Jacob, ambae leo kwake yeye na mke wake, nikama wamezaliwa upya.

Nakama ujuwavyo, siyo wote ambao wangeenda kwa mzee Jacob, au walifurahi kilicho mtokea mzee Jacob, ambae walitegemea ameingia kwenye matatizo baada ya kusikia kijana wao ameibiwa huko mjini, hao ndio watu walio kuwa wametulia nyumbani kwa mzee Kabwenga, wakiendelea kunywa pombe, huku wakimteta mzee Jacob, “ushamba ule, wamezuzuka naile rangi tu hakuna kitu pale, demu anasula ngumu” alisema moja kati ya wazee wale, huku wenzake wakiangua kicheko, ambacho kilikuwa na tafsiri tofauti tofauti, wapo walio sheka kama kucheka tu, kwa ile kebei ya mwenzao, lakini wao waliocheka, kwakuona mwenzao amezisiaha chuki, kiasi cha kukataa kweli ulio wazi kabisa, maana Careen ni mschana mzuri sana, “wajinga sana, yani wamejifanya kununua vijuice kwatu wote wale, usikute yule dogo pale anatumia ela zake za tumbaku, kumbe akuibiwa wala nini, alafu sisi tunajuwa yule mwanamke ndie tajiri” alisema mwingine, na wenzake wakaunga mkono, “kweli bwana, we mshamba kama yule ghafla tu, anakukokotoa chuma kizuri kama kile, wakati kuna watu wapo mjini miaka na miaka”

Wakati wanaendelea na maongezi yao, mala wakatokea mzee Nyoni na mke wake, “aya sasa kimenuka” alisema mzee Nyoni, ambae sauti yake ilionyesha wazi kuwa amelewa ibaya sana, “lete mchapo mzee mzima, kuna jipya gani tena” aliuliza mzee kabwenga huku anampatia mzee Nyoni kopo la ulanzi, “Sada ameamua kujibu mapigo” alisema mke wa mzee Nyoni, yani mama Sada,

Nae nikama mume wake, alionekana kuwa amelewa vibaya sana, wale wenzao wakashanglia kwa nguvu, “lete habari hiyoooo” ndivyo walivyo sema, “Sada ametupigia simu, amesema twende mjini, tukafaidi mapocho pocho, na kuchukuwa zawadi zetu” alisema mzee Nyoni, ukweli ata mimi ambae nilijuwa kuwa wanampango wa kutafuta nauri waende mjini, sikufikilia kama anaweza kudanganya kiasi hiki, “weeee kwahiyo mnaenda lini?” aliuliza mzee Kabwenga, kwa sauti iliyojaa shahuku,

“hapo ndipo pagumu sasa” alisema mzee Nyoni, huku yeye na mke wake wanakaa chini kwenye vumbi kabisa, “pagumu kivipi?” aliuliza mzee Kabwenga, “amesema tukope nauri, alafu yeye ata tupa fedha za kuja kulipa, yani kama ningepata nauri, ata kesho sisi tuna jihimu kuwai gari” alisema mama Sada, na hapo kabwenga, akacheka kwa furaha, “hiyo italeta heshima sana, wasijione kama mtoto wao peke yao, kwani nyie mnaitaji shilingi ngapi?” aliuliza mzee Kabwenga, “kwani nauri ya mjini ata naijuwa basi” alisema mzee Nyoni, “nauri ya kwenda mtu mmoja ni elfu mbili na mia tano, watu wawili elfu tano” alisema mzee mwingine alie kuwa amekaa pembeni, “nita wakopesha elfu tano, muende mjini najuwa sikosi zawadi” alisema mzee Kabwenga ambae hapo hapo alizama mfukoni, na kuibuka na noti kdhaa,ambazo alichambua chambua na kuibuka na elfu tano, “hii hapa” alisema Kabwenga huku anampatia mzee Nyoni, ambae aliipokea kwa heshima na tahadhima, japo alikuwa amelewa.***

Saa moja na nusu, ndiyo mida ambayo, mwana dada Sada Nyoni, alikuwa anasimama mbele ya duka la Kadara, mwanamke ambae ametoka nae kijiji kimoja, akiwa amechoka kama ametoka kupanda milima, miguu imechafuka kwa fumbi la songea, ungesema anatoka kulima.

lakini licha ya kukuta duka lipo wazi, Sada alishangaa kuona pale dukani, kuna mwanadada mwingine kabisa, na siyo Kadara kama alivyo tegemea, “mambo” alisalimia Sada kwa sauti ya kirafiki, usingeweza kuhisi kama anauchovu uliochanganyika na njaa, “poa tu karibu” aliitikia yule dada alie kuwa dukani, na kumkaribisha, niwazi alizania kuwa ni mteja, “walaa mimi siyo mteja, nimekuja kumuulizia huyu mrembo” alisema Sada kwa swaga za kimjini na kisister du, “nani dada Kadara, ameondoka jioni ya leo kwenda kijijini, kuna vitu baba yake amemtumia fedha amnunulie, ndio amevipeleka kijijini kwao” alisema yule mwanamke ambae umri wake ni mdogo kwake. ………..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!